MWENYEKITI wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare
akionyesha baadhi ya hati ambazo alipatiwa na halmashari kwa ajili ya
kumtambulisha kuwa kiwanja ni chake sasa hivi kiwancha hicho kinataka
kunyang’anywa na halmashauri ya Wilaya ya Monduli
Wananchi wakiwa wamesimama na mabango yaonayoonyesha unyanyasaji wanao fanyiwa na halmashauri hiyo
wamama wa kijiji cha Lendikinya wakiwa wamekaa kwa huzuni katika mkutano wa hadhara
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare akiongea katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Lendikinya
Mwana kijiji Amina Longitoti akiwa anatoa kero yake katika mkutano huo |
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya
Monduli wameitupia lawama halmashauri ya wilaya hiyo na kusema kuwa
inachochea migogoro ya ardhi na kuwanyima baadhi ya wananchi amani ya
kukaa katika vijiji vyao
Hayo wamesema jana wakati walipokuwa
wakifanya mkutano wa adhara uliofanyika katika kijiji cha Lendikinya
kilichopo ndaniya halmashauri ya Monduli mkutano ambao uliohudhuriwa
na vijana wa jamii ya Kimasai (morani) na wazee wa mila (Laigwanani)
zaidi ya 300, kueleza ardhi ya kijiji hicho inayotaka kunyang’anywa na
halmashauri hiyo,ambapo walisema kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na uongozi
huu mpya wa halmashauri ambao unaongozwa na chadema kwani katika kipindi
kilichopita walikuwa hawanyanyaswi wala awafukuzwi katika maeneo yao
ambayo walikuwa wanaishi tangu enzi za mababu zao .
Mmoja wawananchi hao
aliyejitambulisha kwa jina la Songoyo Ole Matata alisema kuwa uongozi
wa halmashauri hiyo umekuwa ukiwasumbua na kuwafukuza katika maeneo hayo
ambayo ,walikaa tangu enzi za mababu wao,huku akibainisha kuwa pamoja
na kuwa wanafukuzwa lakini sio wananchi wote bali uongozi huo unafukuza
wananchi kulingana na chama ambacho anatokea.
“Tumekuja apa siku nyingi lakini
tunashangazwa hatujawai kufukuzwa ila tangu halmashauri hii ichukuliwe
na chadema tumekuwa tunanyanyaswa sana haswa sisi tunaotoka na
tunajilikana ni wanachama wa chama cha mapinduzi,nasema hivyo kwa sababu
hata sisi tunaolalamika ambao tumeambiwa tumevamia msitu ni wanachama
waCCM hamna mwanachama hata mmoja wa CHADEMA ambaye amefatwa akaambiwa
amevamia msitu ,mimi mwenyewe pembeni yangu nimepakana na aliyekuwa
waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa katika maeneo hay o hayo kunashamba la
Askofu Laizer lakini hao hawajaambiwa wamevamia misitu waondoke ila
sisi ambao ni wanachama wa CCM ndio tunaambiwa tumevamia msitu kwakweli
hii sio haki kabisa tunamuomba Rais wetu magufuli aje atusaidie maana
tunanyanyaswa sana”alisema Amina Longitoti
Akiogea katika mkutano huo
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani
Arusha, Loota Sanare alisema kuwa halmashauri ya wilaya hiyo
inayoongozwa na Chadema, inachochea migogoro ya ardhi na chama chao
hakitakaa kimya kwa hilo.
Alisema vijana wa kimorani,
Laigwanani na watu wengine akiwemo yeye mwenyewe Sanare, wanamiliki
ardhi iliyopo katika kijiji hicho kwa kufuata michakato yote ya kisheria
na hatimaye kupata hati ya kumiliki ardhi hivyo anashangazwa na
kusikitishwa na kauli ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Monduli, Isack Joseph kutangaza baadhi ya watu kuwa wanamiliki ardhi
katika msitu huo kinyume cha sheria.
Alisema CCM haitavumilia uchochezi
unaofanywa na baadhi ya viongozi wa halmashauri kwa maslahi binafsi na
hatakuwa tayari kuona wananchi wananyanyaswa kwa sababu ya maslayi ya
mtu binafsi .
“mimi nilipata shamba hilo kama
mwananchi wa kijiji hicho na sikuchukuwa shamba hilo kama kiongozi wa
CCM hivyo nashangaa sana kwa kitendo cha kuingiza chama katika mambo
yangu binafsi kimenisikitisha sana na kwakweli sita vumilia kabisa na
kingine kinachonishangaza sio mimi tu au sisi tu ndio tunamashamba au
tunamiliki ardhi katika kijiji hichi kwani hata Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Chadema, Edward Lowassa (Waziri Mkuu mstaafu) ana ekari za kutosha
katika eneo hili pamoja na diwani wa Monduli Juu na wengine walioko
ndani ya Chadema lakini nashangaa wote amna aliyeambawa amevamia ila ni
sisi tu “alisema Sanare.
Kwa upande mwananchi mungine
aliyejitambulisha kwa jina la Olais Taiyai alisema kuwa ubaguzi na
uchochezi uliopo ndani ya halmashauri hiyo unapaswa kupigwa vita na
hautavumilika hata kidogo kwani sio jambo jema linalofanywa na viongozi
hao na kuomba serikali kuingilia kati swala hili kwani wananchi hao
wanateseka na hawana pa kwenda iwapo wataendelea kufukuzwa katika
viwanja vyao
Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya
Wilaya ya Monduli, Amani Ole Silanga, aliwataka wanakijiji kuwa na
subira, kwani huo ni upepo mchafu unaovuma kupitia
No comments:
Post a Comment