DC Kilolo Asaia Abdalaha akifafanua jambo |
Mwenyekiti wa Halmashauari ya Kilolo akifugua kikao kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kilolo |
Baraza la madiwani Kilolo |
BAADA
ya mradi wa maji Ipalamwa kujengwa chini ya kiwango kwa bomba
kupasuka ovyo kabla ya mradi kukabidhiwa ,baraza la madiwani la
Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa limempa muda wa
wiki mbili mkandarasi wa kampuni ya Norcom Ltd kukamilisha mradi wa
maji wa Ipalamwa kwa ubora unaotakiwa zinginevyo mkataba wake
utavunjwa.
Huku
mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalaha akiagiza Halmashauri hiyo
kutomlipa fedha yeyote mkandarasi huyo hadi hapo atakapokamilisha
mradi kwa kiwango kinachotakiwa vinginevyo kama kuna pesa alilipwa
awali basi pindi mkataba wake utakapovunjwa atapaswa kuzirudisha
fedha hizo.
Wakitoa
maadhimio hayo katika kikao cha baraza la madiwani
kilichofanyika juzi katika ukumbi wa Halmashauri ya Kilolo na
kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Kilolo ,madiwani hao walisema
kuwa wamechoshwa na mkandarasi huyo kuendelea kuchelewesha mradi
huo wa maji na kuwa sasa wanaona suala hilo la kero ya maji
kijiji cha Ipalamwa lifike mwisho kwa kumpa muda wa mwisho kwa
ajili ya kukamilisha mradi huo .
Mhandisi
wa maji wa wilaya ya Kilolo Enock Basyagile akijibu hoja za
baraza la madiwani juu ya ucheleweshwaji wa mradi huo alisema
kuwa sababu ya kuchelewa kwa kazi hiyo ni kutokana na kukosekana
kwa fedha kati ya Halmashauri na mkandarasi ila kwa sasa fedha
zimeingia na mchakato wa kufanya kazi hiyo kwa kununua vifaa
vya mradi huo ikiwa ni pamoja na mchakato wa malipo kwa mkandarasi
huyo.
Mkuu
wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah alisema hakubaliani na uamuzi
wa mhandisi wa maji wilaya kutenga fedha ama kufanya mchakato
wa malipo ya Tsh milioni 19 kwa mkandarasi huyo aliyejenga mradi
huo chini ya kiwango ila alitegemea kuona mkandarasi huyo
anachukuliwa hatua kwa kufanya kazi chini ya kiwango.
”
Sikubaliani hata kidogo na uamuzi wa kumlipa fedha mkandarasi
huyo ama Halmashauri kununua mabomba kwa ajili ya kukarabati mradi
ambao haujakabidhiwa kwa wananchi …..naagiza mkandarasi huyo afanye
kazi hiyo kwa gharama zake na asilipwe pesa yoyote hadi mradi
utakapokabidhiwa “
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Kilolo Bw Vellance Kihwaga alisema sababu kubwa
ya mradi huo kuendelea kusumbua kwa mabomba kupasuka ni baada
ya mkandarasi huyo kwenda kinyume na mkataba wa kazi hiyo kwa
kuweza mabomba membamba zaidi kuliko nguvu ya maji hivyo pindi
maji yakifunguliwa mabomba hayo hupasuka .
Alisema
kutokana na ubovu huo wa mabomba kamati ya fedha ilifanya ziara
ya ukaguzi wa mradi huo toka mwaka jana na kumwagiza mkandarasi
huyo kufanya marekebisho kwa kutoka mabomba yote yasiyo na ubora
na kufunga mabomba yenye ubora na alikubali kuifanya kazi hiyo
ndani ya wiki mmoja na kamati ilimpa mwezi mmoja ila hadi sasa ni
zaidi ya miezi 4 kazi hiyo haijafanyika .
Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Kilolo Bw Aloyce Kwezi alisema kuwa
mkanadarasi huyo bado hajalipwa fedha yoyote na kuwa Halmashauri
haitamlipa fedha hadi hapo mradi utakapokamilika na anapaswa
kufanya kazi hiyo kwa gharama zake na iwapo atashindwa kwa muda
uliotolewa basi halmashauri itavunja mkataba huo.
Wakati
huo huo serikali ya wilaya ya Kilolo imepiga marufuku wageni
kuingia katika vijiji ama kata na kuendesha miradi mbali mbali
pasipo kushiriisha viongozi wa ngazi zote za vijiji ama Halmashauri .
No comments:
Post a Comment