“ Wizara ya Afya inapenda kutoa ufafanuzi kufuatia barua ya mwezi Novemba, 2016 iliyotumwa kwenda kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na ambayo inazunguka kwenye mitandao ya kijamii.
Lengo la barua hiyo lilikuwa ni kutoa ushauri kwa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) juu ya wanafunzi ambao walitakiwa kuendelea na mafunzo ngazi nyingine baada ya kufaulu mitihani yao, na kuchelea kuendelea na hatua nyingine kwa kuwa majibu ya mitihani yao yalikuwa hayajatoka”.
Mwamwaja amebainisha kuwa, Kupitia taarifa hii wangependa kuwataarifu kwamba mitihani ya wanafunzi hao imeanza kusahihishwa toka tarehe 5 Desemba 2016. Hivyo, ushauri uliotolewa katika barua ile kwa sasa utakuwa umepitwa na wakati na majibu ya mitihani hiyo yanatarajiwa kutoka katikati ya mwezi Januari 2017.
Aidha vyeti vya wahitimu wa marudio “supplementary” na wa mwezi April orodha na matokeo yao yaliwasilishwa NACTE kwa ajili ya utayarishaji wa vyeti. ilieleza Mwamwaja.
No comments:
Post a Comment