Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Maruzuku katika Kata ya Mnyamani Buguruni Manispaa ya Ilala, kupitia
Chama cha Wananchi (CUF), Jabiri Sanze (kulia), akimkabidhi sare za
shule mtoto, Hamad Ali Dar es Salaamleo, ambaye ataanza darasa la kwanza
mwezi huu. Serikali ya mtaa huo imetoa sare za shule, daftari na
penseli kwa watoto 200 watakaoanza darasa la kwanza mwaka huu wa 2017.
Katikati ni mama wa mtoto huyo, Farida Rashid.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt.Ali Mohamed Shein
akikata Utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Msikiti,
Masjid Muhammad (S.A.W) uliojengwa na Kampuni ya Al-Buwardy
huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa Kaskazini Unguja
leo Desemba 30, 2016. Wanaoshuhudia ni, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja
Mhe,Vuai Mwinyi Mohamed na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman (kushoto). (PICHA NA IKULU YA
ZANZIBAR)
Rais akifunua kitambaa kuzindua msikiti huo
Rais, akipokelewa wakati akiwasili kwenye ufunguzi huo
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt.Ali Mohamed Shein
(kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Vuai Mwinyi
Mohamed wakati alipowasili katika ufunguzi wa msikiti, Masjid Muhammad (S.A.W)
huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa kaskazini Unguja
leo Desemba 30, 2016. Msikiti huo umejengwa chini ya usimamizi wa Bw,Yakoub
Othman mwakilishi wa Kampuni ya Al-Buwardy Tanzania.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
(kulia) akisalimiana na Bw.Samir Ayoub mmoja wa wanafamilia ya Yakoub Othman,
msimamizi wa ujenzi wa msikiti huo.
Sheikh
Otman Maalim alipokuwa akitoa mawaidha baada ya ufunguzi wa Msikiti
Masjid Muhammad (S.A.W)
Rais akihutubia waumini baada ya ufunguzi huo
Waumini waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa msikiti huo
Ni wakati wa sala
Rais wa Russia, Vladimir Putin
Hata
hivyo Russia imekanusha kuhusika kwa namna yoyote na tuhuma hizo na kuita tuhuma
hizo hazina ushahidi.
Wizara
ya Mambo ya Nje ya Marekani, imetangaza wanadiplomasia 35 wa Russia kutoka mji
mkuu Washington na ubalozi mdogo wa Russia mjini San Francisco kuwa watu hao na
familia zao hawatambuliwi na kupewa saa 72 wawe wamefungasha virago na kuondoka
nchini humo.
Kremlin imesema haitalipiza kisasi na haina mpango wa kuwafurusha wanadiplomasia 31 wa Marekani walio kwenye miji ya Moscow na
Saint
Petersburg
No comments:
Post a Comment