Wafanyakazi wa kampuni ya bia
ya TBL wakionyesha kwa waandishi wa habari chupa mpya ya Chibuku Super
ya Ml 500 wakati wa hfla fupi ya uzinduzi iliyofanyika jijini Mwanza
leo
Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya
TBL wakijipongeza, wakati wa hafla ya kuitambulisha chupa mpya ya
Chibuku Super ya Ml 500 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika
jijini Mwanza leo.
Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya
TBL wakionja Chibuku super ya Ml 500 wakati wa hfla fupi ya uzinduzi
iliyofanyika jijini Mwanza leo.
Meneja Masoko wa TBL Group Oscar
Shelukindo,akizungumza na waandisi wa kuhusiana na muonekano mpya wa
chupa ya Chibuku Super ya Ml 500 wakati wa hafla fupi iliyofanyika
jijini Mwanza leo. kulia ni Meneja Kiwanda cha Chibuku Super Mwanza
Herbert Ilembo.
Kampuni ya TBL Group, leo
imezindua Chibuku Super kwenye chupa ya bia ya ml 500, huku ikitoa wito
kwa watanzania kutumia vinywaji vinavyozalishwa hapa nchini ili kujenga
uchumi wa taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika hafla ya
uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa kiwanda kilichopo eneo la
Pasiansi Mwanza , Meneja Masoko wa TBL Group, Bw. Oscar Shelukindo
alisema uzinduzi wa bia hiyo ya Chibuku Super” kwenye chupa ya glasi
inayorudishwa (Returnable) unatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika
soko la Bia hapa nchini.
“Leo ni siku ya furaha kubwa
sana kwetu TBL na kwa watumiaji wote wa Bia yetu hi ya asili , kwani
tumeweza kuzindua Bia hii imetengenezwa kwa utaalamu wa hali ya juu na
kwa kutumia mitambo ya kisasa kabisa, hivyo kuwahakikishia wanywaji
Ubora wa hali ya juu, ina ujazo wa nusu lita na itauzwa kwa bei ya
shilingi 700/- tu, kwa chupa na 14,000 kwa kreti,’’ alisema.
Akiizungumzia bia hiyo Shelukindo
alisema inatengenezwa kwa kutumia malighafi za hapa nyumbani, ikiwemo
nafaka ya mahindi na mtama bora toka kwenye ardhi ya Tanzania na hivyo
kutoa kila sababu kwa watanzania kujivunia kinywaji chenye asili ya
taifa lao.
“Chibuku Super ina kilevi cha
asilimia 4, kinachomfanya mtumiaji aweze kuitumia kwa muda mrefu akiwa
na marafiki, lakini pia inampa lishe nzuri kutokana na virutubisho
vinavyopatikana katika nafaka zinazotumika kutengeneza bia hii,’’
aliongeza
Akizungumzia juu ya usambazaji wa
Bia hiyo, meneja mauzo wa TBL Bw. Fred Kazindogo alisema baada ya
uzinduzi huo itaanza kupatikana Desemba 2 mwaka huu kwa wasambazaji
wakubwa na katika baa mbalimbali na sehemu nyinginezo zinazouza vileo.
Alisema kwa kuanzia Bia hiyo
itaanza kupatikana katika mikoa 15 ikiwemo Mwanza, Kagera, Mara,
Shinyanga, Geita, Tabora, Singida, Kigoma, Simiyu, manyara ,
Kilimanjaro, Arusha, Katavi, Mbeya na Rukwa.
“Na kwa wauzaji wa jumla,
tunatarajia watahamasika kuuza bia ya Chibuku Super kwani ina faida
nzuri na inadumu kwa miezi 4 kwenye soko, muda ambao ni mrefu sana
kulinganisha na products zetu nyingine,’’alisema
No comments:
Post a Comment