Mwenyekiti
wa kampuni ya Uwekezaji wa Taifa (NICOl) Bw. Gideon Kaunda kulia
akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam mara
baada ya kupata uongozi mpya wa kampuni hiyo ulioteuliwa rasmi hivi
karibuni na bodi ya NICOL kushoto ni Mtendaji Mkuu Bw. Adam Wamunza.
Picha Na Ally Daud-Maelezo
………………………………………………………………………
Na Ally Daud-MAELEZO
Kampuni inayojihusisha na
uwekezaji nchini (NICOL) imejidhatiti kuendeleza uwekezaji wa hisa
nchini ili kukuza uwekezaji wa ndani na kuleta ushindani kwa wawekezaji
ndani na nje .
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa
kampuni ya Uwekezaji wa Taifa (NICOl) Bw. Gideon Kaunda wakati wa
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
“Sasa tunahitaji kuendeleza
uwekezaji wa ndani katika hisa na hivi karibuni tumenunua hisa ili
kukuza uwekezaji na kuleta ushindani kwa wawekezaji wa nje katika soko
huria” alisema Bw. Kaunda.
Aidha Bw. Kaunda amesema kuwa
wamejipanga kuhakikisha wanapata wawekezaji wa ndani ili kukuza uchumi
wa nchi pamoja na kuweza kuleta ushindani .
Mbali na hayo Bw. Kaunda amesema
kuwa wanataraijia kuwekeza kwenye sekta zote za uchumi kama mazao ya
biashara ikiwamo korosho,gesi, mafuta pamoja na madini ili kuweza
kutangaza bidhaa za Tanzania kwenye soko la nje.
Aidha Bw. Kaunda aliwataka
wawekezaji wote wa ndani na wa nje kushirikiana na NICOL katika shughuli
za uwekezaji hasa wa mazao ya biashara ili kuipeleka Tanzania katika
soko la kimataifa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijach
No comments:
Post a Comment