Klabu
ya Real Madrid ilipewa takriban pauni milioni 250 na klabu ya China
ambayo haikutajwa jina ili kumnunua nyota wake Cristiano Ronaldo
kulingana na ajenti wake Jorge Mendes.
Amesema kuwa nahodha huyo wa
Portugal mwenye umri wa miaka 31 hana haja na mpango huo ambao
ulishirikisha mshahara wa kila mwaka wa pauni milioni 85.
Ronaldo alisema kuwa anaweza
kucheza kwa miaka mingine 10 mnamo mwezi Novemba baada ya kuandikisha
mkataba mpya na Real Madrid hadi Juni 2021.
”Soko la China ni soko jipya.wanaweza kuwanunua wachezaji wengi, lakini haiwezekani kumnunua Ronaldo”, alisema Mendes.
”Cristiano ndio mchezaji bora duniani, ni kawaida kupata maombi”, aliongezea raia huyo wa Ureno.
Chini ya ombi hilo analodai
Mendes, Ronaldo angepokea kitita cha pauni milioni 1.6 kwa wiki ikiwa ni
mara tatu ya zaidi ya kitita cha uhamisho wa pauni milioni 89
zilizogharimu uhamisho wa Paul Pogba kutoka Juventus kuelekea Manchester
United.
Mendes aliambia Sky Italia: Klabu
ya China imetoa pauni milioni 257 kwa Real Madrid na zaidi ya Yuro
milioni 100 kila mwaka kwa Ronaldo.
”Lakini fedha sio kila kitu.Klabu hiyo ya Uhispania ndio maisha yake”.
Hatua hiyo inajiri baada ya klabu
ya Shanghai Shenhua kutoka China kuthibitisha kwamba imemsajili
aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez kutoka klabu ya
Boca Juniors.
Shanghai inayofunzwa na aliyekuwa
mkufunzi wa Brighton Gus Poyet ,wameripotiwa kukubali uhamisho wa pauni
milioni 40 mbali na mshahara wa zaidi ya pauni milioni 310,000 kwa wiki.
No comments:
Post a Comment