Pages

Thursday, December 29, 2016

MBUNGE MWAMOTO ACHANGIA MILIONI 20 MIRADI YA MAENDELEO KILOLO

mot
Mbunge  wa  jimbo la Kilolo Venance  Mwamoto  wa tatu  kulia  akiongozana na kamati  yake ya mfuko  wa   jimbo  kukagua  miradi  ya kimaendeleo na  kuchangia  miradi  hiyo pichani ni  jengo la maabara ambalo limekwama  kuendelea  katika  shule ya  Sekodari Ipeta
Mbunge  Mwamoto  akitazama  shughuli  za ujenzi wa  vyoo katika  shule ya Msingi Iramba
Mbunge wa   kilolo Venance  Mwamoto  akikagua ujenzi wa choo  cha wanafunzi  shule ya Msingi Iramba  jana wakati wa  ziara  yake  ya ukaguzi  wa miradi  mbali mbali  jimboni  humo
Mwamoto  akikagua  ujenzi  wa kituo cha  Afya Ukumbi
Shimo  la choo  shule ya Sekondari Ipeta
Vyumba  vya madarasa  shule ya msingi Italula
Vyoo  vya zamani  vya  wanafunzi  shule ya Msingi Kidabaga
Ujenzi  wa  vyoo  vya kisasa  shule ya Msingi Kidabaga  ukiendelea
Majengo  ya  shule ya Msingi  Kidabaga
Nyumba  ya  mwalimu Kidabaga  shule ya Msingi
Maabara  ya  shule ya sekondari Ipeta  ikiwa  imesimama  ujenzi  wake
Choo  cha mwalimu  mkuu  shule ya Msingi Mdeke  Kilolo
Na  MatukiodaimaBlog
MBUNGE
wa  jimbo  la  Kilolo mkoani Iringa  Venance Mwamoto amechangia   zaidi
ya Tsh milioni 20 kwa  ajili ya   kukamilisha miradi  mbaali  mbali  ya
kimaendeleo  ikiwemo  ya  ujenzi  wa  vyoo vya  wanafunzi ,madarasa
,nyumba  za walimu na Zahanati  katika jimboni hilo  huku akiwataka
viongozi  wa  serikali za  vijiji  na kata   kuhakikisha   wanakamilisha
ujenzi  huo kwa wakati na  ubora .
Pamoja
na kuwataka   viongozi hao  kusimamia ujenzi   huo amesema atachukua
hatua  kali  kwa  kiongozi  yeyote  wa serikali ya  kijiji ama kata
ambaye atatafuna  fedha   hizo   za ukamilishaji  wa miradi hiyo ya
kimaendeleo jimboni   humo.
Mbunge
huyo  aliyasema   hayo  jana  wakati  alipofanya  ziara  ukaguzi  wa
miradi  9  inayoendelea  kwa  nguvu  za  wananchi  na Halmashauri  ya
wilaya   ya  Kilolo na  kueleza  kuvutiwa na  miradi  hiyo japo
kunahitajika  msukumo  wa haraka  katika umaliziaji  wa miradi   hiyo
hasa ile  ya vyoo vya  wanafunzi ili kuwawezesha  wanafunzi hao  pindi
shule  zinapofunguliwa kuwa na vyoo bora.
Alisema
kutokana na  hali ya  hewa  kuwa mbaya  kwa  mvua  kuchelewa  kunyesha
katika  maeneo  mbali mbali ya  wilaya ya  Kilolo tofauti na miaka
mingine ameona ni  vema   kuwapunguzia makali ya michango wananchi
wake  na badala  yake  sehemu ya  michango  ambayo  walipaswa
kuchangia  ili  kukamilisha miradi  hiyo  kuibeba  yeye  kupitia  mfuko
wa  jimbo kwa  kuchangia fedha  hizo.
Kwani
alisema ni rahisi  kwa wananchi  kuchangia  nguvu  zao  kwa
kushirikia  katika  ujenzi  huo  wa miradi  hiyo  kuliko kushiriki
kutoa  fedha jambo  ambalo kwa wananchi hao  ni  sawa na  kuwatesa
kutokana na  wengi   wao  waliuwa  wakiishi  kwa kutegemea  kilimo na
hadi   sasa matumaini ya  kupata fedha  kwa njia ya  kilimo yametoweka
baada ya  mvua  kushindwa  kunyesha  .
“Ninawaombeni
sana  wananchi wangu  kwa sasa  ninyi  mshiriki  zaidi  katika
maendeleo  kwa   kuchangia  nguvu  zenu  na mimi niwaunge  mkono kwa
kuchangia  fedha  ili  kuifanya  miradi hii ikamilike  kwa  wakati”
Hata
hivyo  alisema  kuna baadhi  ya maeneo wananchi  wanachangamoto  kubwa
ya  barabara hasa  zile  zilizopo  chini ya  Halmashauri  kuwa
barabara   hizo  zitafanyiwa matengenezo na  ile  ya Tanrod kutoka makao
makuu ya wilaya ya  Kilolo  hadi Ndiwili mpakani  mwa jimbo  la
Kalenga  inaanza kujengwa  kwa  kiwango  cha lami  mapema mwakani  na
kuwa kuanzia January  ujenzi   huo  utaanza kwani  barabara   hiyo  ipo
katika  ilani ya uchaguzi  ya CCM.
Mbunge
Mwamoto  alisema  kuwa kwa suala la  ujenzi  wa Zahanati na vituo  vya
afya  wananchi wamejitahidi  kwa maeneo mbali mbali aliyopita  kukagua
ujenzi  umefikia  hatua  nzuri  na  kutolea mfano ujenzi  wa Zahanati
ya Masege  ambao jengo  lake   bado  kuezekwa na  nyumba  ya mganga
ipo  katika  hatua  ya  kuanza  kupandisha  kuta kuwa kukamilika kwa
Zanahati   hiyo  kutawawezesha  wananchi  hao  ambao  walikuwa
wakilazimika  kufuata matibabu Kibengu na  Usokami  wilaya ya  Mufindi
wataweza  kutibiwa katika Zanahati   hiyo.
Alisema
katika ziara  yake  hiyo aliyoambatana na  wajumbe  wa mfuko  wa jimbo
kupitia  fedha  za  mfuko wa   jimbo   Kijiji cha Mdeke ambako kuna
ujenzi  wa vyoo  vya  wanafunzi  amechangia  Tsh milioni 1 na kwenye
ujenzi wa  nyumba ya  mwalimu  amechangia  Tsh milioni 2 ,  sekondari
ya Ipeta kwa  ajili ya  ujenzi  wa vyoo  vya  wanafunzi  amechangia
Tsh  milioni 2, shule ya Msingi Kidabaga amechangia Tsh  milioni  3 kwa
ajili ya vyoo na nyumba  ya  mwalimu ,Wangama  amechangia  Tsh milioni 1
kwa  ajili ya ukarabati  wa madarasa ,Kitongoji  cha Ifiga amechangia
Tsh milioni 1 kwa  ajili ya  kuanzisha mkondo  B wakati ujenzi  wa
Zahanati na nyumba ya  Mganga  Masege amechangia  Tsh milioni 5
Mbunge
Mwamoto  alisema ujenzi  wa  kituo  cha Afya  Ukumbi amechangia  Tsh
milioni 2 na katika  ujenzi  huo nguvu  za  wananchi  ni Tsh milioni 35
na Halmashauri ni Tsh  milioni 10    huku  ujenzi  wa vyumba
vyamadarasa  shule ya  Msingi  Italula amechangia Tsh  milioni 2  hata
hivyo  alisema atafanya  ziara  ya ukaguzi  na uchangiaji  wa miradi
ya  maendeleo  katika  jimbo zima ili  kupitia mfuko  huo  wa  jimbo
miradi yote  iweze kupata  mgao   huo.

No comments:

Post a Comment