Mradi wa uboreshaji wa huduma ya majisafi katika Kijiji cha Kasapo, Kata ya Mkuyuni, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Rasilimali za Maji na
Umwagiliaji wa Misri, Prof. Dkt. Mohammed Abdel Aty na Waziri wa Maji na
Umwagiliaji nchini, Inj. Gerson Lwenge, pamoja na Balozi wa Misri
nchini, Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi
wa Rasilimali za Maji, Grace Nsanya mara baada ya kuzindua mradi wa
maji wa visima 30 kwa ajili ya uboreshaji wa huduma ya majisafi kwa
wilaya za Same, Mwanga, Kiteto, Bariadi na Itilima.
Waziri wa Rasilimali za Maji na
Umwagiliaji wa Misri, Prof. Dkt. Mohammed Abdel Aty na Waziri wa Maji na
Umwagiliaji nchini Inj. Gerson Lwenge, wakifungua maji yaliyotokana na
moja ya visima 8 vilichochimbwa mkoani Kilimanjaro katika Kijiji cha
Kasapo, Kata ya Mkuyuni, Wilayani Same.
Waziri wa Rasilimali za Maji na
Umwagiliaji wa Misri, Prof. Dkt. Mohammed Abdel Aty na Waziri wa Maji na
Umwagiliaji nchini, Inj. Gerson Lwenge wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Mecky Sadick na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule.
Waziri wa Rasilimali za Maji na
Umwagiliaji wa Misri, Prof. Dkt. Mohammed Abdel Aty akijaza ndoo ya maji
kwa ajili ya kumtwisha mkazi wa Kijiji cha na Waziri wa Maji na
Umwagiliaji nchini, Mhandisi Gerson Lwenge akiangalia, kuashiria
uzinduzi na makabidhiano ya mradi wa maji wa visima 30 kwa ajili ya
uboreshaji wa huduma ya majisafi uliotekelezwa kwa ushirikiano wa
Serikali ya Tanzania na Misri katika wilaya kame za Same, Mwanga,
Kiteto, Bariadi na Itilima wa mradi huo wa maji.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Inj. Gerson Lwenge akiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji
na Umwagiliaji (katikati), Inj. Emmanuel Kalobelo na Mkurugenzi wa
Rasilimali za Maji, Hamza Sadiki katika hafla ya uzinduzi na
makabidhiano ya mradi wa maji wa visima 30 kwa ajili ya uboreshaji wa
huduma ya majisafi kwa wilaya za Same, Mwanga, Kiteto, Bariadi na
Itilima.
No comments:
Post a Comment