Pages

Thursday, November 24, 2016

KATIBU MKUU (SEKTA YA UJENZI) ATEMBELEA UJENZI WA JENGO LA TATU LA ABIRIA (TERMINAL III), JIJINI DAR ES SALAAM

uje1
Mkurugenzi wa Mradi wa jengo la tatu la abiria (Terminal III), kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Eng. Mohammed Milanga, akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (kushoto), alipokagua maendeleo ya mradi huo.
uje2
Meneja Mradi wa BAM International ya Uholanzi, Erick Van Zuthem, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (kulia), alipokagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria (Terminal III), jijini Dar es Salaam.
uje3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Mradi wa jengo la tatu la abiria (Terminal III), kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Eng. Mohammed Milanga, alipokuwa akikagua mradi huo, jijini Dar es Salaam.
uje4
Mkurugenzi wa Mradi wa jengo la tatu la abiria (Terminal III), kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Eng. Mohammed Milanga, akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo upande wa kushukia abiria kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (kushoto), alipokagua maendeleo ya mradi huo.
uje5
Mafundi wa umeme wakiendelea na kazi ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria (Terminal III), jijini Dar es Salaam. Jengo hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua ndege 21 kwa wakati mmoja na abiria milioni 6.
uje6
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, akifurahi jambo na Mkurugenzi wa Mradi wa jengo la tatu la abiria (Terminal III), kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Eng. Mohammed Milanga, alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria (Terminal III), jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment