Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na Balozi wa Uingereza
nchini, Sara Cooke (kulia) masuala
mbalimbali ya ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania. Mazungumzo hayo
yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo Novemba 28,
2016.
NA
FELIX MWAGARA- MOHA
WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Balozi wa
Uingereza nchini, Sara Cooke na kumuakikishia ushirikiano zaidi kati ya Wizara
yake na Ubalozi huo nchini.
Mazungumzo
hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es
Salaam leo ambayo yalijadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa ushirikiano
kati ya Wizara na ofisi ya Balozi huyo nchini.
Waziri
Mwigulu alimuakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuwa salama kwa
kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja
na wageni wote waishio nchini.
“Mheshimiwa
Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na
karibu sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla
tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Mwigulu.
Hata
hivyo, Balozi Sara alimshukuru Waziri Mwigulu kwa mazungumzo waliyoyafanya na
kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Uingereza na Tanzania.
Pia
kikao hicho kiliudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest
Rwegasira pamoja na Naibu Balozi wa nchi hiyo, Matt Sutherland.
Balozi
wa Uingereza nchini, Sara Cooke (wapili kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati), kuhusiana na masuala
mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo
yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto
ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali
Projest Rwegasira, na kulia ni Naibu Balozi wa nchi hiyo, Matt Sutherland
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimshukuru Balozi wa
Uingereza nchini, Sara Cooke, mara baada ya kumaliza mazungumzo yao
yaliyofanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Balozi huyo
alimtembelea Waziri huyo kwa lengo ya kujadiliana masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akiagana na Balozi wa
Uingereza nchini, Sara Cooke nje ya jengo la Wizara hiyo, mara baada ya
kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es
Salaam leo. Balozi huyo alimtembelea Waziri huyo kwa lengo ya kujadiliana
masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza. Kulia ni Naibu
Balozi wa nchi hiyo, Matt Sutherland
No comments:
Post a Comment