Pages

Thursday, November 3, 2016

PSPF YAONGEZA WANACHAMA WAPYA 50,185 KWA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA CHA UTAWALA WA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI.




NA TIGANYA VINCENT-MAELEZO- DAR ES SALAAM
Novemba 5, mwaka huu ni mwaka mmoja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alioapishwa kuwa kiongozi  na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa nchi hii.
Katika kipindi cha mwaka mmoja cha utawala wa Rais Magufuli nchini, Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa upande wake umesaidia Watanzania wanaopata huduma za Jamii kupitia PSPF kuongezeka kutoka 394,494 hadi kufikia 444,679 ikiwa ni sehemu ya utekeleza wa agizo lake.
Hatua hii ya PSPF imelenga kutekeza agizo na kutimiza ahadi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyokuwa akitoa ya kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wanufaika na huduma za Hifadhi za Jamii ikiwemo huduma za Bima za afya wakati wa kampeni na baada ya kuingia madarakani.
Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka mmoja kwa upande wa Mfuko wa PSPF iliyotolewa na Costantina Martin kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF ,idadi hiyo hii inajumuisha Watanzania walio katika sekta rasmi na isiyo rasmi nchini.
Kundi hili kubwa lilikuwa limesaulika kujumuishwa katika hifadhi ya jamii , lakini baada ya Mhe. Rais Magufuli kulizungumzia katika kampeni zake hivi sasa mwamko wa kujiunga na hifadhi ya jamii umeongezeka na PSPF imeanza kulitekeleza agizo hilo kwa kuwahamasisha wananchi waliopo katika sekta isiyo rasmi na sekta rasmi kuchangia na kujiunga katika Bima ya Afya.
Katika kuhakikisha kuwa azma hiyo inatimizwa tayari PSPF imeingia makubaliano na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) kwa lengo la kufikisha huduma za afya kwa watanzania wengi ambao wapo katika sekta isyo rasmi na hivyo kujenga jamii yenye afya bora inayochangia katika ujenzi wa nchi.
Chini ya makubaliano yanawasaidia wanachama wa PSPF walio katika Mpango wa Uchangiaji wa Hiari kuweza kupata ya tiba kupitia NHIF kwa gharama ya shilingi 76,800/- kwa mwaka katika hospitali mbalimbali ziliingia makubaliano na Mfuko huo wa Bima ya Afya.
Mpango huo wa PSPF unaounga mkono juhudi za Rais Magufuli  za kutaka kuhakikisha kuwa wananchi wengi wanapata huduma na matibabu nchi nzima kwenye vituo vyote vilivyosajiliwa na NHIF kuanzia Zahanati hadi Hospitali ya Taifa kwa gharama nafuu.
Hivi sasa huduma hiyo ya PSPF kuwadhamini wananchama wake kwa ajili ya kupata matibabu imesaidia watanzania wengi sana kunufaika na huduma hii husasan katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Magufuli.
Akifungua rasmi Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Rais Magufuli alisema kuwa dhamira ya kujenga uchumi wa kisasa na suala la kupambana na umaskini linakwenda sambamba na kuwa na wananchi wenye afya bora.
Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya kwa kuhamasisha wananchi wengi wanajiunga na Bima ya Afya.
Katika kutekeleza hilo PSPF kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) imeshawafikia Watanzania 2,710 walio katika sekta isiyo rasmi kuanza  kunufaika na huduma za Afya kupitia PSPF.
Mbali na sekta ya afya , katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Magufuli PSPF kwa upande wake imesaidia kuhakikisha kuwa Tanznaia inakuwa Nchi ya Viwanda kwa lengo la kutoa ajira kwa Watanzania walio wengi.
Viwanda hivyo ambavyo PSPF imewekeza ni pamoja na 21st Century cha Morogoro, Saruji Tanga.
Martin ameongeza kuwa hivi sasa PSPF imejipanga kuwekeza katika Kituo cha Biashara cha Kurasini (Kurasini Logistic Center) kwa lengo la kuchochea uwekezaji wa viwanda na kutoa ajira kwa wananchi.
Viwanda vingine ambavyo PSPF imejipanga kuwekeza ni kile cha Nguo cha Urafiki, Morogoro Canvas Mill na Kiwanda cha Viatu Karanga kilichopo Moshi.
Hatua hiyo iliyoanza kutekelezwa na PSPF ni sehemu utekelezaji hotuba ya Mhe. Rais Magufuli wakati anafungua rasmi Bunge 11 mjini Dodoma mwishoni mwa mwaka jana ambapo alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaweka mkazo katika ujenzi wa viwanda ili mwaka 2020 idadi ya ajira itokanayo na viwanda ifikie asilimia 40 ya ajira zote hapa nchini.
PSPF ilianzishwa kwa sheria ya Mafao ya Hitimisho la Kazi kwa Watumishi wa Umma namba 2 ya mwaka 199 . sura ya 371 na inatoa huduma za Hifadhi ya Jamii katika Mapngo wa lazimana wa hiyari.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mwakilishi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird Ikulu jijini Dar es Salaam

Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akisalimiana na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Profesa Karoli Njau, wakati wa ziara ya balozi huyo chuoni hapo.
Pichani juu na chini ni Balozi wa Umoja wa nchi za Ulaya EU kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akihutubia wanafunzi wa vyuo mbalimbali katika ukumbi Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela ambapo alifanya ziara ya kutembelea Chuo jijini Arusha.(Picha na Ferdinand Shayo).

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Profesa Karoli Njau akifafanua jambo katika ziara ya Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki, Roeland Van De Geer alipotembelea chuo hicho.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akisalimiana na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Profesa Karoli Njau, wakati wa ziara ya balozi huyo chuoni hapo.
Picha ya pamoja ya washiriki wa semina ya malengo ya dunia ya Umoja wa Mataifa katika Chuo cha Nelson Mandela wakiwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki, Roeland Van De Geer.
Picha ya pamoja ya washiriki wa semina ya malengo ya dunia ya Umoja wa Mataifa katika Chuo cha Nelson Mandela jijini Arusha.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Profesa Karoli Njau (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu (wa pili kushoto) na Amon Manyama (kushoto).

 Ofisa mkuu wa Biashara wa Tigo Shavkat Berdiev (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Kampuni ya Simu ya Tigo kuja na vifurushi vipya vya intaneti ;Mega Mix'. Kulia ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.
 Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.




 Na Dotto Mwaibale

Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imetangaza kuanzishwa kwa  ofa ya MEGA MIX ambayo itakuwa inatoa vifurushi vya intaneti ambayo vitawazawadia wateja dakika za ziada kwa ajili ya kupiga simu. Ofa  hii itawapatia wateja  urahisi wa kutumia vifurushi hivi vipya kupitia kifaa chochote kinachotumia intaneti  zikiwemo simu za mkononi  na modemu. 
Akitangaza vifurushi vya Mega Mix kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo Ofisa mkuu wa Biashara wa Tigo Shavkat Berdiev alivielezea vifurushi hivyo  kama “hatua moja mbele ya mabadiliko katika soko  inayotoa   vifurushi sahihi zaidi: ikiwa ni suluhisho kwa watumiaji wote wa data ndani ya sekta ya mawasiliano ya simu nchini Tanzania.”
 Shavkat  aliongeza, “Wateja wetu hivi sasa  wana uhuru wa kuchagua  kutoka katika simu zao  kifurushi chochote wanachokitaka kikiwa na dakika za ziada  zitakazo wawezesha kuunganishwa na wapendwa wao  wakati tunapoukaribisha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.”
 Aliendelea kusema, “Kwa vifurushi vipya wateja wanaweza kuhabarishwa kwa wakati katika mtiririko wa  kuunganishwa  na  wenzi wao na kuwa bega kwa bega na yanayotokea  sehemu mbalimbali duniani. Vifurushi hivi vipya vinaendelea kuonesha jinsi Tigo ilivyojikita katika kuboresha mabadiliko katika mtindo wa maisha ya kidijitali na inavyoongoza katika kutoa  teknolojia ya kisasa pamoja na ubunifu  kwa wateja wetu.
“Wateja wetu vilevile wanaweza kuzipata taarifa za kidunia, kutafuta  kupitia Google, kusikiliza muziki, kuangalia video, kupakua na hata  kutiririsha sinema. Hii ni kwa sababu  tumeunda vifurushi hivi  kwa kuzingatia mahitaji ya kipekee ya wateja  wetu  kwa kufanya uwepo urahisi katika kuchagua  kutoka  katika kifurushi kimoja  kwenda kingine kutegemeana na hali ya kifedha ya wateja.”
Aidha Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga alisema, “Kutokana na teknolojia ya 4G LTE kupatikana  kwa hivi sasa katika miji 20 vifurushi vya  Mega Mix  kunafungua enzi mpya za kufikia intaneti kusiko na ushindani, ambako kutaondoa vikwazo  na kuwawezesha watumiaji  kuona mengi, kusikia zaidi na hatimaye  kupata yaliyo mazuri katika maisha.”
Mpinga aliongeza, “Mteja anachotakiwa kukifanya ili kupata  vifurushi vya Mega Mix ni kupiga  *148*00#  halafu chagua, ‘Vifurushi vya intaneti.”


WAKATI Bunge la Tanzania wiki hii linatarajiwa kujadili na kupitisha muswada wa habari, Shirika la Umoja wa mataifa la Elimu, sayansi na Utamaduni (UNESCO) limehadharisha juu ya uwapo wa sheria zinazotishia uhuru wa vyombo vya habari.

Akizungumza katika kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, Mkuu wa idara ya mawasiliano na habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania, Christophe Legay alisema katika utekelezaji wa maendeleo endelevu sekta ya habari ni muhimu na hivyo watendaji wake wanatakiwa kuwekewa mazingira huru ya kiutendaji.

Serikali ya Tanzania imepeleka muswada wa habari ambao unalalamikiwa na wadau wa habari kwamba haukupatiwa muda wa kutosha wa kujadiliwa na kuondolewa kwa vipengele ambavyo vinawanyima waandishi wa habari uwezo wa kuandika.
Mkuu wa idara ya mawasiliano na habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania, Christophe Legay akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Aidha ndani ya muswada huo imeelezwa na Jukwaa la Wahariri kwamba kuna vipengele ambavyo vinakwamisha umahiri wa uandishi na uchunguzi kama kufutiwa kwa leseni na kuuzwa kwa mitambo kutokana na makosa mbalimbali ambayo yamegeuzwa ya jinai.

Aidha wadau hao wanasema kwamba serikali imejitengenezea nafasi ya kuwa na nguvu kubwa ya kudhibiti habari kupitia Kurugenzi ya Maelezo na Waziri mwenyewe huku Bodi iliyopangwa kuwa huru ikionekana kwamba haina nguvu zakutosha.

Akizungumza haja ya mazingira rafiki Legay alisisitiza kuwaTaifa linastahili kuhakikisha kwamba kumewekwa mazingira rafiki ya upatikanaji wa habari na kwamba kila mwananchi anapata haki yake ya kupata, kusambaza habari kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa na sheria zinazohusu habari za taifa.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Jamal Zuberi akizungumza akifungua kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Alisema ingawa haki ya kupata habari imeelezwa waziwazi katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vifungu 18 na 21 mambo yanayojitokeza sasa katika sheria za habari nchini Tanzania yanatishia haki hiyo, kutokana na sheria hizo kuonekana kubana uchakataji wa habari. Akitolea mfano wa sheria ya huduma ya habari ya mwaka 2016.

Alisema katika mkakati wa utekelezaji wa malengo endelevu ya dunia kuna mpango mkakati wa kulinda waandishi wa habari na upatikanaji wa habari kama ilivyoelezwa katika lengo namba 16, kifungu kidogo cha 10.

Alisema kwa sasa dunia inakabiliwa na tishio kubwa la upatikanaji wa habari kutokana na vitisho vinavyowekwa kwa waandishi wa habari ikiwa na pamoja na kuuawa, kutiwa kizuini au kupotea bila kujulikana.

Alisema katika muongo mmoja uliopita waandishi 827 waliuawa na kwamba ni asilimia 7 tu ya mauaji hayo yalipatiwa ufumbuzi. Aidha alisema mwaka jana ulikuwa mwaka mbaya zaidi kwa waandishi wa habari, huku waandishi 16 pekee wakiuawa katika bara la Afrika.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa akijadili rasimu ya mkakati wa mpango wa usalama wa waandishi wa habari wakati wa kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Alisema kitendo cha kuwadhibiti waandishi wa habari kunaashiria udhibiti wa upatikanaji wa habari huru ambao ndio msingi wa demokrasia na maendeleo ya jamii.

Aliitaka jamii kuhakikisha kwamba inakaa pamoja na kuona haja ya kulinda uhuru wa habari ikiwa na pamoja na kuwalinda wachakataji habari ili kila mtu anayetaka kupata habari aweze kuipata na kuitumia kwa maendeleo yake, jamii na taifa.

Akimkariri Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova, mkuu huyo wa mawasiliano alisema kwamba ukatili na vitendo vinavyoshabihiana navyo dhidi ya waandishi wa habari ni kinyume na uhuru na haki ya upatikanaji wa habari na wanaofanya mambo hayo wanatishia utawala bora wa kisheria na kusababisha utoaji habari usiokamili kwa hofu ya udhibiti na matokeo yake jamii nzima inapotoka na kuhangaika. Leo hii tunahitaji dhamira mpya ya kuhakikisha kwamba tunatengeneza mazingira salama na rafiki kwa waandishi wa habari.

UNESCO ni mdau mkubwa wa habari nchini Tanzania na katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ilikumbushia kazi inayofanya pamoja na wadau wengine wa habari wakiongozwa na Tanzania Human Rights Defenders Coalition kutengeneza mpango kazi wa ushawishi wa namna bora ya kuchakata na kufanyakazi ya uandishi wa habari nchini Tanzania.
Mdau wa tasnia ya habari, Kenneth Simbaya akiwasilisha fursa na changamoto walizokumbana nazo wakati wa uandaaji wa rasimu ya mkakati wa mpango wa usalama wa waandishi wa habari katika kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Kutokana na mkakati huo mwaka jana kuliundwa kikosi kazi cha kuangalia usalama wa waandishi wa habari na taarifa inatarajiwa kutolewa wakati wowote kuanzia sasa namna bora ya kuwawezesha waandishi wa habari kufanyakazi kwa usalama.

Naye msemaji wa serikali ya Tanzania akizungumza Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Jamal Zuberi akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel katika tukio hilo alitoa wito kwa taasisi zisizo za kiserikali, taasisi za sheria na vyombo vya habari kuhakikisha kwamba mazingira ya kufanyia kazi waandishi wa habari ni salama na haki za upatikanaji wa habari haudhibitiwi.

Alisema ili kuwezesha hali hiyo serikali imepeleka muswada wa waandishi wa habari bungeni na pia ikiwa kama moja ya nchi iliotia saini mikataba ya kimataifa kuhusu upatikanaji wa habari serikali itafanyakazi kwa pamoja na wadau kuhakikisha kwamba waandishi wa habari wanapata mazingira rafiki na salama ya kufanyia kazi.
Mmoja wadau wa masuala ya sheria akizungumza jambo katika kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria kutoka Nola, James Marenga akifafanua jambo wakati wa kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Jamal Zuberi (kushoto) akiwa na wadau wa tasnia ya habari wakati wa kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Wadau wa tasnia ya habari na masuala ya Sheria walioshiriki kwenye kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Washiriki wakitazama moja ya video ya shuhuda inayozungumzia usalama wa waandishi wa habari wakati wa uchaguzi wakati wa kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.


 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu aliyesimama akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi
 Madiwani, na Wakuu wa Idara na Vitengo wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu walengwa wa Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi
 Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Juma Mwanga, na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka
 Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu mradi huo
Madiwani,Wakuu wa Idara na Vitengo wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi

Na Mathias Canal, Singida

Shirika la Health Actions Promotion Association (HAPA) la Mkoani Singida kwa ushirikiano na Shirika la The Foundation For Civil Society la Jijini Dar es salaam linatarajia kuendesha mradi wa miaka mitatu kwa vijiji vyote vya Wilaya ya Ikungi kwa lengo la kuijengea jamii uwezo na mbinu shirikishi kama fursa na vikwazo katika maendeleo.

Mradi huo utaanza na Vijiji 10 vya majaribio (Pilot Villages) kutoka katika kata nne na kila kata itakuwa na Vijiji ama viwili ama Vitatu ambapo uchaguzi wa Vijiji hivyo vya majaribio umezuingatia utayari wa jamii husika katika shughuli za maendeleo pamoja na gharama za uendeshaji wa mradi ili kupata matokeo chanya kwa uendelezaji wa mradi husika.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa Uongozi wa Wilaya hiyo unaendelea kushirikisha wadau mbalimbali katika kusaidia kutekeleza shughuli za maendeleo, kwani kwa uhabarisho wa mafunzo ya kujenga uwezo wa jamii na Halmashauri yataendelea katika kuimarisha juhudi za Wilaya zinazoendelea kuchukuliwa katika kutekeleza miradi ya maendeleo pia itakuwa ni fursa kwa jamii kuwa na Uwezo na Nyenzo muhimu katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ufanisi.

Amesema kuwa Wilaya ya Ikungi inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kujiletea maendeleo ambapo endapo zitapatiwa upembuzi yakinifu zitapunguza kadhia zinazowakumba wananchi ambapo amezitaja changamoto hizo ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Vituo vya Afya na Zahanati (Kata na Vijiji) ambapo kwa sasa Wilaya ina vituo 39 tu vya kutolea huduma za Afya ambapo upungufu ni Asilimia 60, Ujenzi na Uboreshaji wa miundombinu ya shule za msingi ambapo kuna nyumba za walimu 387 ambapo upungufu ni nyumba 854, Ujenzi na Uboreshaji wa majosho na mifugo kwani kwa sasa yapo majosho 30 huku kati ya hayo majosho 20 ni mabovu.

Dc Mtaturu alisema kuwa Zipo Asasi mbalimbali ambazo zimesajiliwa kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi lakini zimegeuka na kuwa Asasi zinazofanya kazi za kisiasa tofauti na usajili wao ambapo amesema serikali haitasita kuzichukulia hatua ikiwemo kuzifuta Asasi hizo ili ziache kupotosha wananchi.

Dc Mtaturu alisema kuwa Mradi huo unaotolewa na Shirika la HAPA ni lazima uzingatie matakwa ya kutoa elimu kwa wananchi ili wafahamu kuwa wana nafasi kubwa ya kufanikisha maendeleo yao katika jamii hivyo waache kupotoshwa na baadhi ya wanasiasa kuwa maendeleo yataletwa na serikali pekee.

Msimamizi wa Mradi wa HAPA Noel Makyao amewataja walengwa wa Mradi huo kuwa ni wananchi wote wa kijiji cha Mradi wa majaribio, Wawakilishi 100 kutoka kila kijiji ambao watachaguliwa ili kuendesha zoezi la kutengeneza bajeti ya mpango wa kila mradi ulioibuliwa na jamii kwa siku tatu mfululizo na watu mashuhuri, wakuu wa madhehebu ya dini na makundi mengine wapatao 20.

Alisema kuwa Jumla ya gharama zote za kutekeleza mradi wa mbinu shirikishi ya kujenga uwezo wa jamii katika kuibua, Kupanga, Kutekeleza na kupima matokeo ya Mradi katika vijiji kumi vya majaribio kwa robo mbili zitakuwa shilingi milioni hamsini (50,000,000/=).

Makyao alisema katika awamu hii ya vijiji kumi vya majaribio jumla ya watu wapatao 25,511 watafikiwa kati ya lengo la watu 25,334 zaidi ya watu 177 ya walengwa wa mradi.

 Wachezaji wa timu za Ruvu Shooting wenye jezi rangi ya bluu na wa African Lyon wakiwa wamelala chini ikiwa ni kujihami na makundi ya nyuki ambayo yalikuwa yanapita uwanjani hapo hivyo wachezaji, waamuzi na mabenchi ya wachezaji wa akiba wote walilazimika kulala chini ikiwa ni kujinusuru kutokana na hali hiyo. Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Shooting iliibuka na ushndi wa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji mwenye nguvu za miguu Issa Kanduru kunako dakika ya 19.
 'Ni kama wanasema 'Nyuki hao bado wapo tuendelee kujificha chini ya viti"

 Watu wazima chini ya viti 'Chezea nyuki wewe'
 

No comments:

Post a Comment