Mbunge
wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amekabidhiwa visima Vitatu
vyenye thamani ya Shilingi Milioni 48.5 toka kwa Shirika lisilo la
kiserikali toka Nchini Omani linaitwa kwa TUELEKEZANE PEPONI chini ya Afisa Mtendaji wake Nasr Al Jahdhamy.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi visima hivyo Mbunge huyo alisema kuwa , shida ya
maji ndani ya Halmashauri ya chalinze imekuwa kubwa na kueleza kuwa kazi
iliyofanyika kufanikisha ujenzi wa visima hivyo ni kubwa ili kusaidia
tatizo hilo kwa kipindi hiki wakati wakisubiri kukamilika kwa ujenzi wa
mradi wa kutoa maji mto wami.
“Nimeona
nifanye kazi ya kutengeneza visima ili kupunguza ukali wa uhaba wa maji
kwani matengenezo ya mradi wa wami bado yanaendelea kuchimbwa kwa
visima hivi si ishara kuwa ule mradi wa maji ambao tuliongea kuwa
umekufa mradi wa wami utakapokamilika tunataraji utawanufaisha wananchi
wengi wa jimbo letu.”alisema Ridhiwani
Aidha
visima hivyo vitatu vimekabidhiwa katika kijiji cha matipwili , shule
ya sekondari ya matipwili na kijiji cha Gongo ambavyo vinaendelea
kujengwa na vinataraji kukamilika mapema ndani ya wiki ijayo.
Naye
Bwana Naseer aliahidi kuendelea kumsaidia Mbunge kufikia malengo yake
ya kusaidia kutatua changamoto zinazokabili nyimbo hilo,na kuongeza kuwa
atasaidia kuchimba visima vingine kumi katika Halmashauri hiyo na
kusaidia michezo.
No comments:
Post a Comment