Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu
Tanzania Bibi Joyce Fissoo (Wa kwanza kushoto ) akizungumza na uongozi
wa East Afrika Televisheni na East Afrika Radio alipotembelea vituo
hivyo Novemba 2 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Mkuu
wa vipindi vya EATV Bi Lydia Igarabuza.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu
Tanzania Bibi Joyce Fissoo (Kushoto ) akifanya mahojiano na
watangazaji wa EA Radio alipotembelea vituo hivyo Novemba 2 mwaka huu
Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu
Tanzania Bibi Joyce Fissoo (Kushoto ) akifanya mahojiano na
watangazaji wa EATV alipotembelea vituo hivyo Novemba 2 mwaka huu
Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa vipindi vya East Afrika
Televisheni Bi Lydia Igarabuza (wa kwana kulia) akimueleza jambo
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo (wa kwanza
kushoto) wakati alipotembelea kituo hicho Novemba 2 mwaka huu Jijini
Dar es Salaam.
………………………………………………………..
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzania Bibi Joyce Fissoo amewashauri wasanii wa filamu nchini
kujiendeleza kielimu ili kuongeza weledi na kutengeneza filamu zenye
ubora.
Akiongea na uongozi wa Kituo
cha Radio na Televisheni cha East Afrika leo Jijini Dar es Salaam
Katibu Mtendaji huyo amesema kuwa chombo hicho kina nafasi kubwa ya
kutoa elimu kwa wasanii hususani namna ya kuandaa Filamu zenye bora
kwa kuwa wako mstari wa mbele katika kuonyesha kazi za tasnia hiyo.
“Kituo chenu kina nafasi kubwa
zaidi ya kushawishi wasanii kutengeneza filamu bora kwa kuwa mmekuwa
mkiwapatia fursa ya kutangaza filamu hizo pamoja na kuzionyesha ndani na
nje ya nchi hivyo ni muhimu kuwakumbusha kuzingatia ubora wa filamu
.”Alisema Bibi Joyce.
Aidha ameongeza kuwa vyombo vya
Habari ni nguzo muhimu katika kuendeleza tasnia ya filamu hapa nchini
hivyo ni budi kwa wasanii kuhakikisha wanatengeneza Filamu bora ambazo
zitapata nafasi ya kuonyeshwa katika vyombo hivyo kwa maendeleo yao
wenyewe na Taifa kwa ujumla.
Naye Mkuu wa vipindi vya
televisheni wa East Afrika Bi Lydia Igarabuza ameipongeza Bodi ya
Filamu kwa kufanya maboresho katika tasnia ya Filamu nchini na
kuishauri kutoa elimu zaidi kwa wasanii katika kufuata Sheria ya
Filamu na michezo ya kuigiza kabla ya kutengeneza filamu zao.
“Naipongeza Bodi ya Filamu kwa
juhudi mnazofanya katika kuboresha tasnia hii na msichoke kutoa elimu
hiyo kwani wasanii wetu bado wanahitaji elimu ya filamu na sheria zake
kwa ujumla.Alisema Bi Lydia.
Bodi ya Filamu imejidhatiti
katika kuhakikisha tasnia ya Filamu inakuwa kwa kutengeneza bidhaa bora
ambapo imekuwa ikitoa mafunzo kuwajengea uwezo wanatasnia hao .
WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AZINDUA BODI YA HOSPITALI YA MNAZIMMOJA
Waziri wa Afya Zanzibar Mahmuod
Thabit Kombo akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mnazimmoja
katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika Wizara ya Afya Mjini
Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Mahmuod
Thabit Kombo katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya
Mnazi baada ya kuizindua rasmi Bodi hiyo, wa kwanza (kushoto) Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Jama Malik Akili na (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi
Dkt. Abdulwakil Idrissa Abdulwakil.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
…………………………………………………………………………………
Na Ramadhani Ali-Maelezo Zanzibar .
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit
Kombo amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka matarajio
makubwa kwa Bodi ya Hospitali ya Mnazi mmoja katika kufanikisha azma ya
kuwa Taasisi yenye mfumo wa kujitegemea baada ya Baraza la Wawakilishi
kupitisha Sheria ya kuanzishwa taasisi hiyo.
Amesema Bodi hiyo inayoongozwa na
Mwenyekiti mzoefu wa masuala ya Afya Zanzibar Dkt. Abdulwakil Idrissa
Abdulwakil inahitaji mashirikiano ya karibu ya wafanyakazi wa Hospitali
hiyo na wananchi katika Kuleta mabadiliko hayo.
Waziri Mahmoud ameeleza hayo
Ofisini kwake Mnazimmoja alipokuwa akizindua Bodi ya Ushauri ya
Hospitali ya Mnazi mmoja ambayo lengo lake kuu ni kuifanya Hospitali
hiyo kufikia kuwa ya rufaa inayoshughulikia maradhi maalum
yaliyoshindikana katika vituo vya afya na Hospitali za kawaida.
“Tunawataka wananchi kutoa
ushirikiano kwa kuvitumia vituo vya afya vilivyo karibu nao,
vinavyofikia 142, na kuiacha taasisi mpya ya Mnazi mmoja kushughulia
magonjwa makubwa,”alisisitiza Waziri wa Afya.
Ameitaka Bodi kuishauri
Serikali njia bora za kuchangia matibabu katika maeneo maalum kwa vile
Sera ya Serikali bado ni kuendelea kutoa matibabu bila malipo kwa
wananchi.
Waziri wa Afya amewaeleza wajumbe
wa Bodi hiyo kuwa Hospitali ya Mnazi mmoja inarasilimali kubwa ya
kuaminiwa na wananchi wengi wa Zanzibar na linapotokea tatizo lolote
huwa ni la nchi nzima hivyo suala la kuongeza ufanisi lina umuhimu
mkubwa.
Amesema hivi karibuni Hospitali
hiyo itafunga majengo mengine mawili mapya ambayo yanavifaa vya kisasa
hivyo wafanyakazi watapaswa kuwa waangalifu na kuacha kufanyakazi kwa
mazoea.
Amewataka viongozi wa sehemu zote
za Hospitali ya Mnazimmoja kuwasimamia wafanyakazi walio chini yao na
kuiunga mkono Bodi katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili
Hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt.
Abdulwakil Idrissa Abdulwakil amesema jukumu walilopewa na Serikali ni
kubwa lakini kwa kutumia utaalamu wa wajumbe wa Bodi hiyo watajitahidi
kuhakikisha malengo yaliyowekwa ya kuifanya Hospitali ya Mnazimmoja kuwa
ya kujitegemea linafikiwa.
Hata hivyo amewaomba viongozi wa
Wizara na wafanyakazi wa Hospitali ya Mnazimmoja kuwapa ushirikiano na
watakuwa tayari kupokea ushauri utakaosaidia kufikia malengo
yaliyopangwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.
Juma Malik Akili amewaeleza wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mnazi mmoja
kuwa Wizara itaendelea kusimamia sera lakini Bodi ndio yenye jukumu la
kushauri maendeleo ya taaisi hiyo.
DKT MGWATU APONGEZA UTENDAJI KAZI WA TEMESA LINDi
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme – TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (kulia) akiongea na Meneja wa TEMESA
Lindi Mhandisi Grayson Maleko (kushoto) alipotembelea kituoni hapo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme – TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (katikati) akiongea na Mafundi wa
TEMESA Lindi walioko kwenye mafunzo ya vitendo, alipotembelea kituoni
hapo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto w) akiongea na watumishi
wa Karakana ya TEMESA Lindi, alipotembelea kituoni hapo mapema.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu akiangalia eneo litakalojengwa
gati kwa ajili ya Kivuko cha Lindi Kitundamkoani Lindi.
Picha Zote na Theresia Mwami TEMESA Lindi
…………………………………………………………..
Na Theresia Mwami TEMESA Lindi
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme Tanzania – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amepongeza utaratibu
unaotumika katika kituo cha TEMESA Lindi na karakana zake kwa kuratibu
vizuri kazi za kila siku.
“Nawapongeza sana kwa utendaji
wenu wa kazi kwa kuweka utaratibu wa kufuatilia kila kazi inayofanywa na
wafanyakazi wa kituo” alisema Dkt. Mgwatu.
Dkt Mgwatu amemuagiza Meneja wa
TEMESA Mkoa wa Lindi Mhandisi Greyson Maleko kuhakikisha kuwa magari
yote ya Serikali mkoani Lindi yanafanyiwa matengenezo katika karakana ya
TEMESA iliyopo mkoani humo.
Dkt. Mgwatu amemtaka Meneja huyo
kuhakikisha anakusanya madeni yote wanayodai kwenye Taasisi, Halmashauri
na Idara mbalimbali za Serikali kutokana na matengenezo ya magari na
mitambo, sambamba na kulipa madeni yote wanayodaiwa na wazabuni kwa
kipindi cha Julai-Septemba, 2016.
Kwa upande wake Meneja wa TEMESA
Lindi alisema kuwa changamoto kubwa inayokabili kituo hicho ni uwepo wa
madeni makubwa wanayodai kwenye Taasisi na Halmashauri mbali mbali za
serikali zilizopo Mkoani Lindi kutokana na matengenezo ya magari na
mitambo lakini wanajitaidi kuendelea kufanya kazi kwa ustadi na
kujituma.
Katika hatua nyingine Dkt. Mgwatu alitembelea eneo litakalojengwa gati kwa ajili ya kivuko kutoka Lindi hadi Kitunda.
Dkt. Mgwatu yupo katika ziara ya
kikazi kutembelea mikoa ya Lindi na Mtwara ili kujionea hali ya Vituo
katika mikoa hiyo pamoja na utendaji kazi wake.
No comments:
Post a Comment