Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya
Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (katikati) akibonyeza kitufe
kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G inayotolewa
na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za
teknolojia ya Mawasiliano. Kulia ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL,
Bw. Waziri Waziri Kindamba na Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Tanzania, Bruth
Zhang (kushoto) wakishuhudia.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya
Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (katikati) akipiga makofi pamoja
na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Waziri Kindamba (kulia)
na Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Tanzania, Bruth Zhang (kushoto) mara baada
ya uzinduzi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya
Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za teknolojia ya
Mawasiliano.
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Waziri Kindamba akizungumza
katika hafla ya uzinduzi rasmi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G
inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika
huduma za teknolojia ya Mawasiliano. Hafla hiyo ilifanyika jana katika
Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.ILIVYOKUWA KWENYE USIKU WA MSHIKE MSHIKE NA KHADIJA OMAR KOPA JIJINI MWANZA.
Malikia
wa Taarabu Afrika Mashariki na Kati, Khadija Omar Kopa, akitoa burudani
kwa wakazi wa Jiji la Mwanza usiku wa kuamkia leo ndani ya Villa Park
Resort kwenye show ya Usiku wa Mshike Mshike iliyoandaliwa na 102.5 Lake
Fm Mwanza.
Na BMG
Na BMG
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
BENKI YA POSTA YAJENGA CHOO CHA SH.MILIONI 14.5 SHULE YA MSINGI PANDE JIJINI TANGA
Meneja
Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves
Moses akizundua Jengo jipya la Choo cha Shule ya Msingi Pande ambalo
wamelijenga.
Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses pamoja na wageni wengine wakipiga makofi mara baada ya kulizundua jengo hilo
Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses kulia akipongezwa na mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Pande,Mathias Anthony mara baada ya kuzindua Jengo la Choo
Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses pamoja na wageni wengine wakipiga makofi mara baada ya kulizundua jengo hilo
Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses kulia akipongezwa na mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Pande,Mathias Anthony mara baada ya kuzindua Jengo la Choo
BALOZI SEIF AFUNGUA MKUTANO WA KIKANDA WA KIMATAIFA WA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA, ZANZIBAR
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa pili kutoka kulia
akiwa pamoja na Viongozi waandamizi kabla ya kuufungua Mkutano wa
Kikanda wa Kimataifa wa Siku Mbili unaohusiana na Sekta ya Mafuta na
Gesi asilia ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi na kufanyika katika
Ukumbi wa Hoteli ya Park Hyatt Mjini Zanzibar.
Baadhi
ya washiriki wa Mkutano wa Kikanda wa Kimataifa wa Siku Mbili
unaohusiana na Sekta ya Mafuta na Gesi asilia wakimsikiliza Balozi Seif
wakati akiufungua Mkutano huo.
UJERUMANI WAIPIGA JEKI SAUTI ZA BUSARA 2017
Mwenyekiti
wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Ndg Simai Mohammed Said
akitiliana saini ya Makubaliano ya kusaidia Tamasha la Sauti za Busara
Zanzibar na Balozi wa Ujerumani Tanzania Balozi Egon Kochanke, Ujerumani
imekubali kuchangia €5000 sawa na shilingi za Kitanzania milioni
12,hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Park
Hyyat Shangani Zanzibar leo. Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar
hufanyika kila mwaka katika mwezi wa Febuary na kuhudhuriwa na Wageni
mbalimbali wanaotembelea Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said,
akibadilishana mkataba na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Balozi
Egon Kochanke, baada kumaliza kutiliana saini ya makubaliano ya
kuchangia Tamasha hilo kwa mwaka 2017, hafla hiyo imefanyika katika
Ukumbi wa Hoteli ya Park Hyyat Shangani Zanzibar, leo mchana. Kwa hisani ya ZanziNews
No comments:
Post a Comment