Pages

Friday, October 28, 2016

DR. JAKAYA KIKWETE, FORMER PRESIDENT AND CHANCELLOR OF THE UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM ADDRESSES THE 55TH ANNIVERSARY OF UDSM




Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu, Vicent Magere akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati) kufungua mkutano wa kamati hiyo wenye lengo la kujadili pamoja na kuweka mkakati wa kukabiliana na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu nchini. Kushoto ni Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara hiyo kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. (PICHA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI).



NA FELIX MWAGARA, MOHA
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya amewataka wajumbe wa Kamati ya Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu kuweka mikakati imara ya kupambana na wahalifu wa biashara hiyo nchini.
Akizungumza kabla ya kufungua mkutano wa wajumbe hao wenye lengo la kujadili na kutengeneza mkakati wa kukabiliana na biashara hiyo, Balozi Simba alisema biashara hiyo imekuwa ikiongezeka duniani na wahalifu wakipata faida ya mabilioni ya fedha kutokana na wahanga, wengi wao wakiwa ni watoto, ambao huporwa utu na uhuru wao.
“Inawezekana wengi wetu hatujakutana na aina hii ya uhalifu, lakini unatokea kila siku duniani kote, na nchi yetu ni mojawapo kati ya nchi zinazoathirika na tatizo la biashara hii haramu,” alisema Balozi Simba na kufafanua;
“Tanzania ni chanzo, njia ya kupitia na pia hupokea wahanga wa biashara hii haramu. Wahanga hawa husafirishwa kutoka maeneo ya vijijini kwenda mijini hapa nchini, wengine husafirishwa kwenda Ulaya, Marekani, Asia na nchi za Kiarabu kama vile Oman na Dubai.”
Alisema watu hao hudanganywa kwa ahadi za kupata ajira nzuri au nafasi za elimu, lakini mwisho wake huishia kunyonywa, kuwa watumwa wa ndani na kufanyishwa kazi kwa nguvu.
Hata hivyo, Simba alisema katika hatua ya kupambana na biashara hii haramu, mwaka 2008 ilitunga sheria ya kudhibiti biashara hiyo hapa nchini, na mwaka 2015 walikamilisha kazi ya kuandaa Kanuni za kutekeleza sheria hii. Aliongeza kuwa, sheria hii ndiyo ilipelekea kuundwa kwa Kamati na Sekretariet ya kupambana na biashara hiyo haramu ya usafirishaji binadamu.
“Na leo Kamati na Sekretarieti mnakutana hapa kwa lengo hilo la msingi, kwamba mnafanya tathmini ya utendaji wenu tangu mwaka 2012 hadi sasa ili kubaini wapi mlifanya vizuri na wapi hamkupata mafanikio mliotarajia. Tathmini hii itawawezesha kuweka mikakati thabiti ya kuzuia na kupambana na tatizo hili hapa nchini,” alisema Balozi Simba.
Simba alisema anajua wana mafanikio mengi ambayo Kamati hiyo wameyapata katika utendaji wao tangu kuanzishwa ikiwemo baadhi yake ni pamoja na kuandaa Kanuni za sheria ya kupambana na biashara haramu ya usafirishaji binadamu, kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kupambana na biashara hiyo na kuimarika ushirikiano wa kiutendaji baina yao na idara zingine za serikali, pamoja na Mashirikia yasio ya kiserikali na ya Kimataifa mfano Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Wahamaji (IOM).
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu, Vicent Magere, alisema kikao hicho kinawahusisha Wajumbe wa Kamati na Sekretarieti kutoka Bara na Visiwani ambapo wanakutana kwa mujibu wa sheria ambapo wanapaswa kukutana mara tatu au nne kwa mwaka.
“Lengo la kukutana ni kufanya tathmini ya utendaji ili kubaini ni wapi tulifanya vizuri na wapi hatukufanya vizuri. Kikao hiki pia kinatupatia fursa ya kupanga mikakati ya utendaji ili hatimaye tuweze kuboresha zaidi utendaji wetu,” alisema Magere.

Naibu Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu, John Makuri akizungumza katika kikao hicho.
Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella, akiwasilisha mada juu ya Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu na juhudi zilizofanywa na serikali hadi kufikia sasa
Picha ya pamoja

Wachezaji wa Timu ya Azam Fc wakiwa uwanjani Kaitaba hii leo jioni wakijifua, Tayari kwa mchezo wao na Wenyeji wao Kagera Sugar.
Kipa wa Timu ya Azam FC "Wanalambalamba", Aeshi Manula akiwa na Mwalimu wake.(PICHA NA FAUSTIN RUTA)


Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu 2016/17, raundi ya 12 inaendelea keshokwa michezo sita ambako mabingwa watetezi Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba ulioko Bukoba mkoani Kagera.
Jijini Dar es Salaam, katika Uwanja wa Uhuru African Lyon itakuwa mwenyeji wa Mbeya City ya Mbeya ilihali Mwadui ya Shinyanga itasafiri hadi Mtwara kucheza na Ndanda Fc kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona wakati Stand United itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye mchezo utaofanyika Uwanja wa Manungu, ulioko Turiani – Mvomero.
Majimaji itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa Majimaji huko Songea. Michezo yote mitano hapo juu itaanza saa 10.00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki lakini mchezo kati ya Azam FC na JKT Ruvu itaanza saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam huko Chamazi-Mbagala Dar es Salaam.
BEKI mahiri wa kulia wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Shomari Kapombe Baada ya kukosa mechi kama sita alionekana kama bado anaugulia jeraha lililomfanya afanye mazoezi mepesi na akiwa peke yake katika Uwanja wa Kaitaba leo. Jumapili itakuwa ni zamu ya kinara wa ligi hiyo, Simba ambayo itaikaribisha Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Tanzania Prisons itapambana na Mbao FC kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Michezo yote ya Dar es Salaam, mfumo wa kuingia utabaki kuwa ni uleule wa kutumia kadi za Selcom kununua tiketi za kielekroniki. Viingilio kwenye mechi za Uwanja wa Uhuru ni Sh 30,000 kwa Jukwaa Kuu (VIP-A), VIP-B na C Sh 20,000 na mzunguko ni Sh 5,000 wakati Kiingilio Uwanja wa Azam ni Sh 10,000 kwa VIP na Mzunguko ni Sh 3,000.


Kipa wa Azam Fc


Mashabiki jukwaa kuu wakiwachabo Wachezaji wa Azam Fc kwenye Uwanja wa Kaitaba hii leo


Wakimsikiliza kwa Makini Kocha wao

Shabiki mkubwa na Mpenzi wa Timu ya Azam Fc Ally Kulialia nae alikuwepo Uwanjani hapo



Mwalimu wa Makipa(kulia) wa Azam Fc

Kipa wa Timu ya Azam FC "Wanalambalamba", Aeshi Manula

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,Prof Faustine Bee (kushoto) akimuongoza Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge kuelekea katika chanz cha Mkashilingi kilichopo wilyani Hai kwa ajili ya uzinduzi, kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).Joyce Msiru.
Waziri wa Maji na Uwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akizungumza wakati wa uzinduzi wa chanzo cha maji cha Mkashilingi kilichopo  wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi huo wakimsilikiliza Waziri wa Maji na Umwagiliaji (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa chanzo cha Mkashilingi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiki akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akimueleza jambo Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge mara baada ya kujionea chanzo cha maji cha Mkashilingi.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akiwasili atika chanzo kingine cha Kaloleni kwa ajili ya uzinduzi rasmi ,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru.
Chanzo cha Maji cha Kaloleni.
Chumba maalumu kwa ajili ya matibabu ya maji.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Joyce Msiru akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa chanzo cha maji cha Kaloleni.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akizindua mradi wa maji wa Kaloleni.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Gerson Lwenge akiotesha mti katika chanzo cha maji cha Kaloleni mjini Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiki akiotesha mti katika chanzo cha maji cha Kaloleni.
Mwenyekiti wa Bodiya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Prof Faustine Bee akiotesha mti katika chanzo hicho.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa MAzingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akiotesha mti katika chanzo cha maji cha Kaloleni.
Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba akiotesha mti katika chanzo cha maji cha Kaloleni. 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Malikia wa Taarabu Afrika Mashariki na Kati, Khadija Omar Kopa, akitoa burudani kwa wakazi wa Jiji la Mwanza usiku wa kuamkia leo ndani ya Villa Park Resort kwenye show ya Usiku wa Mshike Mshike iliyoandaliwa na 102.5 Lake Fm Mwanza.
Na BMG
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Wananzengo wakifurahia burudani iliyotolewa kwenye Usiku wa Mshike Mshike na 102.5 Lake Fm
Timu ya Uongozi na Wafanyakazi wa 102.5 Lake Fm Mwanza pia ilitambulishwa kwa Wananzengo kwenye show hiyo
Timu ya Uongozi na Wafanyakazi wa 102.5 Lake Fm Mwanza pia ilitambulishwa kwa Wananzengo kwenye show hiyo
Wananzengo kutoka 102.5 Lake Fm Mwanza
Timu ya Uongozi na Wafanyakazi wa 102.5 Lake Fm Mwanza pia ikijitambulisha kwa Wananzengo kwenye show hiyo
Madjz wa 102.5 Lake Fm, Dj Hcue (katikati), Dj KFlip (kushoto) na Dj Dhifa (kulia)
Dj Dhifa
Dj KFlip (kushoto) na Dj Hcue
Khadija Omar Kopa akihojiwa na wanahabari baada ya show
Hakika 102.5 Lake Fm Mwanza ni Raha ya Rock City na ni Redio ya Wananzengo. Kaa tayari kwa show ijayo.
Bonyeza HAPA Kwa Taarifa Zaidi

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Mhe. Vesa Viitaniem (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa .
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Mhe. Vesa Viitaniem (kushoto) masuala mbali mbali ya uwekezaji,elimu na uwezeshaji Ikulu jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Mhe. Vesa Viitaniem (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam.
                          ............................................................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wawekezaji kutoka nchi ya Finland kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya nishati katika kipindi hiki wakati ambapo taifa la Tanzania linaelekea katika uchumi wa viwanda.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Vesa Viitaniem
Makamu wa Rais amesema kuwa mkakati wa sasa wa Serikali ni kuhakikisha taifa linajitosheleza ipasavyo katika nishati ya umeme hatua ambayo itasaidia wawekezaji wengi kutoka mataifa mbalimbali Duniani kuja kuwekeza nchini kutokana na nchi kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika utakaotumika katika viwanda vitakavyojengwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Makamu wa Rais pia ameishukuru Serikali ya Finland kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na kuwezesha makundi mbalimbali ya kijamii hapa nchini ikiwemo ya wanawake,yatima na vijana.
Makamu wa Rais amemweleza Balozi huyo kuwa kwa sasa jitihada kubwa za Serikali ya awamu ya Tano zimeelekezwa katika uimarishaji wa miundombinu ikiwemo reli, bandari na barabara ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kote nchini.

Kwa upande wake, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Vesa Viitaniem amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa nchi ya Finland itaendelea kushirikiana na Serikali katika kusaidia uimarishaji wa huduma bora kwa wananchi ikiwemo kuwezesha wajasiriamali ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Finland yamewezesha Watanzania zaidi ya 500 kuishi nchini humo kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo za kimasomo.
Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Vesa Viitaniem aliongozana na Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment