Rais Dkt
John Pombe Magufuli akikagua pembe za ndovu 50 zilizokamatwa katika operesheni
maalum ya
kusaka
majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na
Utalii (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam leo Oktoba 29, 2016
Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi baada ya kukagua akikagua pembe za ndovu 50 zilizokamatwa katika operesheni maalum ya ya kusaka majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam leo Oktoba 29, 2016
R
DTB YAZINDUA TAWI LA 26 BARABARA YA MWAI KIBAKI, MBEZI CHINI, JIJINI DAR ES SALAAM
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Benjamin Sitta, akikata utepe katika
uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya Diamond Trust lililopo barabara ya
Mwai Kibaki, Mbezi Chini Jijini Dar es salaam, kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa benki hiyo Viju Cherian na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha
Fedha Joseph Mabusi na Meneja wa Tawi hilo Msingo Kimune wakishuhudia.
Tawi hilo ni tawi la 12 jijini Dar es Salaam na ni tawi la 26 nchini
Tanzania.(picha na Mpiga picha wetu)
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Benjamin Sitta akiongea na wageni
waalikwa kwenye uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya Diamond Trust
lililopo barabara ya Mwai Kibaki, Mbezi Chini jijini Dar es salaam, Tawi
hilo ni tawi la 12 jijini Dar es Salaam na ni tawi la 26 nchini
Tanzania. (picha na Mpiga picha wetu)
<!--[if gte mso 9]>
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe, Mkuu wa
Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu na viongozi wa ngazi ya Chama cha
Mapinduzi CCM Wilaya ya Ikungi wakitazama namna wakimbiaji wanavyowasili katika
uwanja wa shule ya Sekondari Ikungi
Wananchi wakifatilia kwa makini Ikungi Half Marathon katika
maeneo yao vijiji vyao
Washiriki wa Ikungi Half Marathon wakianza kukimbia Riadha
katika Kijiji cha Kimbwi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu kulia akisistiza jambo wakati akizungumza na washiriki
wa Ikungi Half Marathon kulia kwake ni MathiasCanal Mwandishi wa Habari
wa mtandao wa Www.wazo-huru.blogspot.com
Afisa Michezo Wilaya ya Ikungi Aboubakary Kisuda akizungumza na awashiriki wa Ikungi Half Marathon kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu
Washiriki wa Ikungi Half Marathon wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu
Na Mathias Canal, Singida
Mashindano ya kuibua vipaji vya
wafukuza upepo kwa mbio ndefu Ikungi Half Marathon yanayotaraji kufika ukomo
jumamosi hii Octoba 29, 2016 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Ikungi
ambapo Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe anatarajiwa kuwa mgeni
Rasmi katika mashindano hayo.
Vijana takribani 60 shupavu
waliochomoza kwenye mchujo wa ngazi ya Vijiji, Kata na Tarafa wataingia
barabarani kuisaka ama heshima ya ushindi au ushiriki kwa ngazi ya Wilaya huku
wengine waliokosa nafasi katika awamu hii kusubiri awamu ijayo katika
mashindano ya Full Marathon yatakayofanyika Mwaka 2017.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu amezungumza na washiriki wote wa mbio hizo ambapo amewapongeza
kwa kujitokeza kwa wingi jambo ambalo linaonyesha kuwa mchezo huo una wahitaji
wengi.
Mtaturu amesema kuwa mashindano haya
ya Ikungi Half Marathon yanafanyika kwa mara ya kwanza na yatakuwa endelevu
ambapo mwakani yatafanyika pia mashindano yam bio ndefu yatakayojulikana kama Ikungi
Marathon 2017.
Dc Mtaturu alisema kuwa Dhamira ya
kuanzishwa kwa mashindano haya ni kuibua vipaji kwa vijana na kuviendeleza,
Kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa vijana na kuwaandaa vijana katika
Wilaya hii kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.
Mashindano ya mbio ndefu yenye
umbali wa kilomita 21 yatahusisha vijana wenye umri wa kuanzia miaka 17 hadi 30
waishio Wilayani Ikungi na yanatarajiwa kufanyika kila mwaka ili kuinua hamasa
ya Mchezo wa riadha huku yakiambatana na mbio fupi za mita 100, mita 400
na mita 800.
Mashindano haya yalianza Septemba 3,
2016 kwa ngazi ya Vijiji, Octoba Mosi yalifanyika kwa ngazi ya Kata, ambapo
mchujo wa ngazi ya Tarafa imemalizika Octoba 15, 2016 na hatimaye kupisha
mchuano wa Kiwilaya.
Mashindano haya yatatoa fursa kwa vijana kuonyesha uwezo wao
wa kucheza na miguu kwa kasi ya ushindani kwa maana ya manufaa ya pesa lakini
pia itaimarisha ajira kupitia chama cha Riadha mkoa wa Singida na Taifa kwa
ujumla lakini pia kuwaondoa vijana wengi katika mawazo ovu ya kushinda vijiweni
badala yake kujitokeza kwa ajili ya kujihusisha na Kilimo pamoja na ufugaji.
Dc Mtaturu
amewasihi washiriki wote kukimbia kwa kutumia muda mzuri ili iwe taswira ya
rekodi nzuri katika ukimbiaji jambo litakalokifanya chama cha cha Riadha Taifa
kuchagua vipaji vitakavyoendelezwa
No comments:
Post a Comment