Pages

Sunday, October 30, 2016

BENKI KUU YA TANZANIA (BoT) YACHUKUA USIMAMIZI WA BENKI YA TWIGA BAADA YA KUFILISIKA

 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jioni hii kuhusu kuchukuliwa kwa benki hiyo ambayo ilikuwa ikimilikiwa na serikali kwa asilimia 100.
 Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mabenki, Kenedy Nyoni (kushoto), akichangia jambo kwenye mkutano huo. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu, Profesa Beno Ndulu.
 Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Victoria  Msina (kulia), akimkaribisha Gavana Beno Ndulu kuzungumza na wanahabari. Wa pili kutoka kulia ni Kaimu Katibu wa Benki, Mustafa Ismail.
 Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
 Wapiga picha wakiwa kazini.
Taswira ya ukumbi huo wakati wa mkutano.

Na Dotto Mwaibale

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imechukua usimamizi wa Benki ya Twiga 9Twiga Bancop Limited) kuanzia Oktoba 2016 imefahamika.

Hayo yamebainishwa na Gavana wa Tanzania, Profesa Beno Ndulu Dar es Salaam leo jioni wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu hatua hiyo ya kuchukuliwa kwa benki hiyo ambayo serikali ilikuwa ikiimiliki kwa asilimia 100.

"Kwa mamlaka iliyopewa benki kuu chini ya kifungu cha Sheria namba 56 (1) (g) (i) na 56 (2) (a)-(d) cha Sheria ya mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 benki kuu ya Tanzania imeamua kuchukua usimamizi wa benki hiyo kuanzia tarehe 28 Oktoba 2016" alisema Ndulu.

Alisema uamuzi huo umechukuliwa baada ya kubaini kuwa benki hiyo ina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 20016 na kanuni zake.

Alisema upungufu huo wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na pia kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki hiyo kutahatarisha usalama wa amana za wateja wake.

Profesa Ndulu alisema kutokana na uamuzio huo Benki Kuu ya Tanzania  imeisimamisha Bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa benki hiyo na imemteua Meneja Msimamizi ambaye atakuwa na jukumu la kusimamia shughuli za benki ya Twiga kwa kipindi ambacho itakuwa chini ya usimamizi wa benki kuu.

Alisema pia Umma unaarifiwa kuwa katika kipindi kinachokadiriwa kufikia wiki moja kuanzia siku ya taarifa hii, shughuli za utoaji wa huduma za kibenki za benki hiyo zitasimama ili kutoa nafasi kwa ajili ya kupanga taratibu za uendeshaji wa benki hiyo.

Alisema Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.

WAZIRI ASIYEKUWA NA WIZARA MAALUM ZANZIBAR AKABIDHI MSAADA WA VYAKULA NA MATUNDA HOSPITALI YA MENTAL KIDONGOCHEKUNDU ZANZIBAR

Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum Zanzibar Mhe Juma Ali Khatib akikabidhi msaada wa Matunda na Vyakula kwa Hospitali ya Mental Kidongochekundu Zanzibar akipokea msaada huo Daktari Mkuu wa Hospitali hiyo Bi Zainab Kassim. hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hospitali hiyo huko Mental.
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Zanzibar Mhe Juma Ali Khatib akisalimiana na Mgaga Mkuu wa Hospitali ya Mental Kidongochekundu Zanzibar Bi Ruzuna Mohammed,wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo wa Matunda kwa ajili ya Wagonjwa wanaopata tiba katika hospitali hiyo. Kuu Zanzibar. 
Mhe Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum Zanzibar Mhe Juma Ali Khatib, akizungumza na Viongozi baada ya kukabidhi msaada huo nac kuwataka Wananchi na Wafanyabiashara kujitokeza kusaidia Wagonjwa wa akili ili kusisikia wako katika mazingira mazuri na kupota misaada mbalimbali inayohitajika kwao na kwa jamii. 
Imeandaliwa na OthmanMapara. Zanzinews.com
Mobile 0777424152.   

Sehemu ya vijana hao wasomi 53 wakichota maji ili kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Vijana wasomi 53 wa grupu la Whatsapp la WAZALENDO wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani, umbali wa kilomita 151 kutoka Dar es salaam, na kilomita 53 kutoka makao makuu ya Wilaya. 
Leo wamekutwa wakifanya kazi hiyo nzito huku wakihamasika kwa nyimbo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga (wa pili kulia). Vijana hao, 14 wakiwa wanawake na 39 wanaume, walikubaliana kupiga kambi shuleni hapo toka Septemba 27, 2016  na kufanya kazi hiyo ya kujitolea na bila malipo kwa moyo mmoja na kufanikiwa kufyatua matofali hayo. Kambi hiyo inatarajiwa kufungwa kesho Jumamosi Oktoba 29, 2016 na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako
 Mmoja wa vijana hao wasomi akielekea kazini
  Sehemu ya vijana hao wasomi 53 wakichota maji ili kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Sehemu ya vijana hao wasomi 53 wakichota maji ili kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Sehemu ya vijana hao wasomi 53 wakichota maji ili kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Sehemu ya vijana hao wasomi 53 wakichota maji ili kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akielekeza vijana sehemu ya kuweka matofali 
 Kazi ikiendelea
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akiwa katika picha ya pamoja  na vijana hao wasomi 53 baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akipungia pamoja  na vijana hao wasomi 53 baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akitoa maelekezo kwa vijana hao wasomi 53 baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakiwa bwenini
 Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakiwa bwenini ambako kuna uhaba wa nafasi kiasi cha kurundikana namna hiyo
 Huko jikoni msosi unaandaliwa
 Wanafunzi wa shule hiyo wakijipanga kupata chakula cha mchana
 Wanafunzi wanapata chakula na matunda kila mlo
 Mojawapo ya nyumba chache za walimu ambamo wanakaa walimu saba
 Walimu sita kati ya saba wanaoishi kwenye nyumba hiyo
 Nishati mbadala ya solar itumiwayo na walimu hao saba
 Wanafunzi wakipata mlo wa mchana
 Vijana wasomi wanawake wanalala hapa 
 Sehemu ya vijana hao 14 wanawake wakipumzika baada ya kazi nzito
 Pamoja na kufyatua matofali baadhi ya vijana hao wasomi ambao ni walimu walikuwa wakiingia darasani kufundisha. Hapa mwalimu akiandaa kipindi baada ya kufyatua matofali
 Mwalimu akiandaa kipindi
 Sehemu ya vijana hao
 Jiwe la msingi
 Nje ya darasa
 Mandhari ya sehemu ya shule hiyo
 Bweni la vijana wasomi wanaume
 Pamoja na kazi nzito ya kufyatua matofali vijana hawa wazalendo wana nyuso za furaha na kuridhika kwa kujitolea kwao
 "....HAPA KAZI TU!" anasema kijana huyu mzalendo
 Furaha ya kumaliza kazi kwa mafanikio
 Kijana mzalendo Petro Mgoti (suruali ya njano) alikuwa katika ziara ya mafunzo ya wiki sita nchini Ujerumani, na aliporejea nyumbani alienda moja kwa moja kujiunga na wenzie huko Mkuranga.
 Furaha ya ushindi
 Utamu wa uzalendo ni kufanya kazi na kufurahi kwa pamoja
 Vijana mapumzikoni
  Jengo la darasa la maabara ambalo sasa hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
  Darasa la maabara ambalo sasa hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
  Darasa la maabara ambalo sasa hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
 Bweni kwa ajili ya wanafunzi ndani ya darasa la maabara
 Kila sehemu ya stoo ya darasa la maabara  hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
 Stoo ya darasa la maabara  hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
 Darasa la maabara ambalo sasa hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
 Hayo matofali ni alama ya kuwa upande huo wa mbele ni wa Msikiti kwa ajili ya walimu na wanafunzi wa Kiislamu. Wakristo na waumini wa madhehebu mengine hutumia madarasa
 Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakielekea bwenini
 Baada ya kazi na msosi sasa ni wakati wa kuimba wimbo wa kambi
 Wimbo wa kambi ukiimbwa na kuchezwa kwa furaha
 Kijana akishukuru kwa kuhitimishwa kwa kazi hiyo
 Mmoja wa vijana hao akishukuru Mungu kwa kumaliza kazi salama
 Sehemu ya vijana hao
 Vijana wakiwa katika kikao kidogo cha kuhitimisha kazi
  Kijana mzalendo Petro Mgoti (suruali ya njano) akisema machache. Yeye alikuwa katika ziara ya mafunzo ya wiki sita nchini Ujerumani, na aliporejea nyumbani alienda moja kwa moja kujiunga na wenzie huko Mkuranga.
 Baada ya kazi nzito Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akijiunga kupata msosi na  vijana hao wasomi 53 baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
Vijana hao wasomi 53 wakipata msosi baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.

Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akizungumza na wakulima wa Bonde la Mto Katengela Kijiji cha Kinonko Wilayani humo wakati wa ziara yake.
 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akilima moja ya shamba la mkulima.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewaomba wakulima wa Bonde la Mto Katengela Kijiji cha Kinonko Wilayani Kakonko kulima mazao yao kwa misimu miwili ya Kiangazi na masika kitaalamu zaidi na kujiunga kwenye vyama vya ushirika.

Ndagala pia amewataka wakulima hao kuacha tabia ya kuuza mazao yote kutokana na hali ya hewa ya mwaka huu inayoweza kupelekea maeneo mengi kukosa chakula.

Akizungumza na wakulima wa Bonde la Mto katengera jana wakati wa ziara yake , vijiji vya Kinonko,Nyamibuye na Rumashi,  Ndagala alisema wakulima wengi wamekuwa na tabia ya kuuza mazao yote na kupelekea kubaki wakilia njaa baada ya mazao yao waliyo lima kuisha ,pia wakulima wanatakiwa kuunda vikindi vya ushirika vitakavyo wasaidia kupata mikopo,pembejeo na masoko yatakayo wasaidia kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu.

Alisema Wakulima wakiweza kulima misimu yote miwili ya Kiangazi na masika bonde hilo linauwezo wa kuhidumia wananchi wote wa Kakonko kutokana na mkulima mmoja katika hekali moja anauwezo wa kuzalisha gunia tatu za mpunga kwa msimu mmoja wa mavuno na hali inayo weza kuikomboa wilaya hiyo isikumbwe na janga la njaa.

Aidha Ndagala amewaomba maafisa kilimo wa Wilaya hiyo kuwawezesha wakulima kulima kwa misimu miwili na kuwapa mbinu za kulima kitaalamu kwa kutumia pembejeo zinazotolewa na Serikali ilikuweza kupata Mazao mengi na  kuweka tahadhali kutokana na hali ya hewa inayo weza kupelekea ukosefu wa mvua.

"Niwaombe wananchi kwa mwaka huu mlime mazao yanayo weza kustahimili ukame kama Vile mihogo, mtama na viazi na yale yanayo stawi haraka kutokana na mabadiliko ya tabia ya Nchi yaliyojitokeza hali inaweza kusababisha mwaka huu chakula kika kosekana kabisa pia mjenge tabia ya kuhifadhi chakula msikiuze chote tusije tukaanza kuomba misaada wakati uwezo wa kuhifadhi chakula tynao",alisema Ndagala.

Kwa upande wake Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko,Muhdin Alfani alisema  bonde hilo lina zaidi ya kilomita 29 na linawakulima 310 na mradi wa kukamilisha ujenzi wa bonde hilo la umwagiliaji ni shilingi milioni 312 na kila hekari moja inazalisha gunia 18 kwa msimu mmoja wa kilimo.

Alisema lengo la Halmashauri kuanzisha mradi huo ni kuwasaidia wananchi wa Wilaya hiyo kulima na kupata mazao ya kutosha yatakayo wasaidia kuilisha wilaya na Nchi jirani ya Burundi ambayo inategemea chakula kingi kutoka kwa Watanzania katika masoko ya ujirani mwema na kuweza kuiongezea serikali pato la taifa.

Nao baadhi ya wakulima wa bonde hilo,Issa Masumo na Shedrack Milembe  wameiomba Halmashauri hiyo kuwawezesha kupata masoko na kupangiwa bei maalumu itakayo wasaidia kuepukana na unyanyasaji wa Wafanya biashara wanaokuja kununua mpunga na kuwapunja wakulima na kukosa haki yao ya msingi wao kama wakulima.

No comments:

Post a Comment