Pages

Thursday, October 27, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AAGANA NA MFALME WA MOROCCO MOHAMED VI KATKA UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kumuaga Mfalme wa Morocco Mohamed VI wakati akipunga mkono kwenye ndege yake taryari kwa kuanza safari ya kuelekea nyumbani katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam Oktoba 27, 2016. (PICHA NA IKULU).


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mfalme wa Morocco Mohamed VI mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi  jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mfalme wa Morocco Mohamed VI kabla ya kuagana nae katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mfalme wa Morocco Mohamed VI wakiangalia bendi ya matarumbeta iliyokuwa ikitumbuiza katika ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.

AKAUNTI ZA LAKE FM MWANZA NA WAFANYAKAZI WAKE ZATOWEKA HEWANI.

Ikiwa yamebaki masaa machache kuelekea kwenye show ya Usiku wa Mshike Mshike iliyoandaliwa na Lake Fm redio ya Jijini Mwanza, akaunti ya Instagram ya redio hiyo imevamiwa na watu wanaosadikika kuwa ni wahuni wa mtandaoni.

"Siku hizi mitandao ya kijamii ina nguvu sana hususani kwenye kusambaza habari, hivyo nadhani wameamua kuingilia akaunti yetu baada ya kuona namna ambavyo tunaitangaza show ya Usiku wa Mshike Mshike inayofanyika leo". Uongozi wa Lake Fm umefafanua na kuongeza;

"Tunapenda kuwaambia Wananzengo wetu kwamba show hiyo itafanyika kama kawaida na tayari Khadija Omar Kopa amewasili Jijini Mwanza kwa ajili ya kuwapa burudani hivyo wasishtuke kutoona posts zetu kwenye mtandao wa Instagram kwani tunapatikana Facebook na Twitter @lakefmmwanza".

Mbali na akaunti ya redio kuibiwa, pia akaunti za Instagram za wafanyakazi wa redio hiyo pamoja na wasikilizaji wake waliokuwa wakipost kuhusu show ya Mshike Mshike zimeibiwa.

Show ya Mshike Mshike inafanyika leo alhamisi Oktoba 27,2016 katika kiwanja cha nyumbani Villa Park Rerort kuanzia saa moja jioni kwa kiingilio cha shilingi 7,000 kabla ya saa tano usiku na shilingi elfu kumi baada ya saa tano usiku ambapo bendi ya Ogopa Kopa Classic pamoja na wasanii mbalimbali akiwemo Fatina Khamis kutoka bendi ya Big Star watakuwepo.
Na BMG
Bonyeza HAPA Kujua Zaidi


Baadhi ya Wasanii wa kundi la  Dar Creators
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwenye tamasha la muziki wa asili lililopewa jina ’Marahaba Swahili Music Festival’ lililofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Biafra na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa Jiji la Dar waliopata burudani mbalimbali za muziki wa ngoma za asili na nyimbo mbalimbali zilizoimbwa (Live).

Mmoja wa Waratibu wa tamasha hilo,Karola Kinasha alieleza lengo lake ni kukuza vipaji vya wasanii chipukizi wanaoimba na kupiga vyombo mbalimbali vya muziki wa asili,na piia kuutangaza muziki wetu wa asili.

Mwenye kanga ni mwanamuziki kutoka visiwa vya Mayotte aliyepanda jukwaani akisindikizwa na wanafunzi wa muziki wa kituo cha Music mayday

Mwanamuziki kutoka katika viziwa vya Mayotte akipiga gitaa akishirikiana na wanamuziki kutoka chuo cha muziki cha Music May Day.





UONGOZI wa kampuni ya DIRA NEWSPAPER COMPANY LTD wachapishaji wa gazeti DIRA YA MTANZANIA unamwomba radhi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa nchi na jeshi la wananchi wa Tanzania kwa ujumla kwa habari iliyochapishwa kwa bahati mbaya katika gazeti letu;  toleo Na.424 la Juni,20-26 ,2016 iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “KIFARU CHA KIVITA CHA JWTZ CHAIBWA”.</ span>
Tunapenda kueleza kwa masikitiko kuwa habari hiyo ilichapishwa kwa bahati mbaya baada ya mtayarishaji wa kurasa (graphic designer) kuipanga habari ambayo ilikuwa haijakamilika kiuchunguzi na kuiacha iliyotakiwa ichapishwe siku hiyo.
Tunapenda JWTZ na watanzania wote kwa ujumla kuwa wafahamu kuwa gazeti la DIRA YA MTANZANIA halikulenga kuchafua Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama ambavyo baadhi ya watu walivyofikiria. </ span>
Tunafahamu mchango mkubwa wa jeshi la wananchi wa Tanzania kwa taifa letu na namna jeshi hilo linavyoshirikiana kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari hasa utoaji wa taarifa mbalimbali na kamwe jeshi hili tokea kuanzishwa kwake halijawahi kukwaruzana na vyombo vya habari jambo ambalo ni heshima kubwa kwetu na taifa kwa ujumla.</ div>
Hivyo uongozi wa gazeti hili umeonelea kuomba radhi kwa Mkuu wa majeshi (CDF), askari wote wa JWTZ na watanzania wote walioshitushwa na habari hiyo na hasa mkuu wa kikosi cha 83 KJ cha Kiluvya mkoani Pwani ambaye kikosi chake kilitajwa kama chanzo cha habari hiyo.
Na tunaomba ifahamike kuwa tumeomba radhi kwa ridhaa yetu na tunaamini kuwa “kuomba radhi” ni kitendo cha kiungwana kwa utamaduni wa waafrika na hasa watanzania tuliokulia katika misingi ya amani, upendo na utulivu na pia tunaamini kuomba kwetu radhi kutazidisha mahusiano mema na ya karibu kati yetu na JWTZ.
Tunatanguliza shukrani zetu.</ div>
Musiba Esaba …………………………..</ div>
Meneja utawala na Fedha.

RPC Salome Kaganda

Na Dotto Mwaibale

WAMILIKI wa magari wametakiwa kuchukua tahadhari ya kuzima na kufunga milango magari yao pale wanaposimama kwa dharura kupata mahitaji mbalimbali ili kuyanusuru kuibwa.

Mwito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Salome Kaganda wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu tukio la kuibwa kwa gari la Kapteni Innocent Dallu maeneo ya Mbezi Juu huku akiwemo mtoto wake Lightness.

"Napenda kutumia fursa hii kuwaomba wamiliki wa vyombo vya moto kuchukua tahadhari ya kuzima magari yao na kufunga milango wanaposimama maeneo yoyote kupata mahitaji yao kwani si rahisi kumbaini mhalifu kwani wapo kila sehemu" alisema Kaganda.

Alisema katika tukio la kuibwa kwa gari la kampteni Dallu alikuwa amesimama maeneo ya Mbezi Juu bila ya kulizima akinunua mahitaji ambapo walitokea vijana wakaondoka na gari hilo aina ya Toyota Harrier baada ya kumtelemsha mmoja wa watoto aliyekuwemo ndani ya gari hilo aitwaye Philip huku wakiondoka na mdogo wake Lightness.

Alisema watuhumiwa hao walimtelekeza mtoto huyo maeneo ya Golden Bridge katika baa moja na kisha kuondoka na gari hilo ambalo lilipatikana baada kukamatwa na polisi Kiwangwa mkoani Pwani ambapo  kijana mmoja Ezekiel Daud anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.

Alisema ni vizuri wamiliki wa magari kuzingatia jambo hilo ili kuepusha matukio kama hayo ambayo yanapoteza muda mwingi wa kuyatafuta kwani tukio kama hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Kinondoni ambapo wahalifu waliweza kuiba gari aina ya Noah lililosimamishwa bila ya kuzimwa na kuondoka nalo na alijapatikana mpaka leo hii.


Baada ya kukamilisha zoezi la Uchambuzi wa maombi ya Mikopo 88,163 yaliyopokelewa hadi kufikia tarehe 11 Agosti, 2016. Jumla ya Wanafunzi wapya 20,183 wamepangiwa Mikopo. Upangaji huu umezingatia vigezo vilivyomo katika mwongozo wa  utoaji wa mikopo uliopitishwa na Bodi ya wakurgezi na kuidhinishwa na wizaya ya elimu sayannsi na teknoloji. Vigezo hivyo ni pamoja na:
 I. Vipaumbele vya  kitaifa vinavyoendana na Mpango  wa Maendeleo  wa Taifa wa Miaka mitano, Dira ya Taifa ya  Maendeleo 2025 na Mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji  ya kitaifa katika fani za kipaumbele ambazo ni;
• Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
• Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
• Uhandisi wa  Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia,
• Sayansi Asilia, na
• Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.
i. Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji  maalum kama vile ulemavu na uyatima
ii. Uhitaji wa waombaji wanaotoka katika familia zenye hali duni ya kimaisha
o Wadahiliwa yatima waliopata mkopo                                                 873
o Wadahiliwa wenye ulemavu wa  viungo                                             118
o Wadahiliwa  wahitaji wenye  mzazi mmoja                                      3,448
o Wadahiliwa wahitaji waliofadhiliwa na taasisis mbali mbali                     87
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma  kozi  za kipaumbele                      6,159
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine                                  9,867
Jumla                                                                                             20,183
Kiasi cha Fedha zinazohitajika
Bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya ukopeshaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ni shilingi bilioni 483, kwa ajili ya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 25,717, na wanaoendelea na masomo wapatao 93, 295.
Hatua zinazofuata
I. Wanufaika wote wanaopungukiwa na sifa watachunguzwa kwa ajili ya kurekebishiwa au kuondolewa katika unufaika wa mkopo
II. Waombaji waliwasilisha taarifa zenye upungufu, taarifa zao zitahakikiwa, na wakibainika kuwasilisha taarifa za uongo watachukuiwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufutiwa mikopo yao
III. Wanufaika wote watatakiwa kuhuisha taarifa kwa kujaza dodoso. Taarifa za ziada za kiuchumi za wazazi au walezi wao zitatumika kutanua uhalisia. Wale watakaokutwa na hadhi zisizo stahili, watapoteza sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi watakachokuwa wamepokea tayari.
IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
S
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu akipokea Luninga kutoka kwa Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Bw Gao Wei wakati wa makabidhiano ya. Vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kutoka Ubalozi wa China  nchini kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara hiyo , kulia ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa  Bibi Leah Kihimbi


Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu, (katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya Vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kutoka Ubalozi wa China  nchini kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara hiyo ,kushoto ni Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China Bw.Gao Wei, na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa  Bibi Leah Kihimbi.

NA SHAMIMU NYAKI-WHUSM.
UBALOZI wa China nchini umeipatia Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo vifaa vya ofisi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 ikiwa ni kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Serikali hizo mbili.
Hatua hiyo imekuja ikiwa na lengo la kusaidia katika kukuza na kuendeleza sekta ya sanaa ambayo katika mpango wa miaka mitano ya maendeleo ya Serikiali inatakiwa kuongeza ajira pamoja na pato la taifa kupitia kazi mbalimbali za sanaa.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo  leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu aliushukuru  Ubalozi huo kwa mchango wao wa kuhakikisha sekta ya sanaa inakuwa na kuleta mabadiliko nchini.
 “Tunashukuru Ubalozi wa China kwa kutupatia vifaa hivi ambavyo vitasaidia sana utendaji katika Sekta ya Sanaa ambayo inaendelea kukua kwa kasi hapa chini na kusaidia kuimarisha ushirikiano mzuri baina ya Serikali yetu na China”Alisema Bw. Petro Lyatuu.
Naye Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi huo Bw Gao Wei amesema kwamba China itaendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara katika kuendeleza Sanaa kwa kutoa misaada mbalimbali  kwa kadri itakavyohitajika.
“Tutaendelea na ushirikiano  huu sio tu kwa kutoa msaada wa vifaa bali pia kubadilishana uzoefu na taaluma ya Sanaa ili Sekta hii ikue na kuheshimika na kutambulika rasmi kama ajira ”Alisema Bw Gao.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi Leah Kihimbi amesema kuwa vifaa hivyo vitaimarisha utendaji kazi wa Sekta ya Sanaa ukizingatia kuwa ni Sekta ambayo imebeba dhamana kubwa ya kutangaza Sanaa ndani na nje ya  nchi.



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu  wa kwanza kushoto akiangalia “honing machine” inayotumika kituoni hapo, kulia kwake ni ndugu Firmin Lyaruu na Meneja wa TEMESA Kilimanjaro Mhandisi Alfred Ng’hwani.

NA THERESIA MWAMI- TEMESA KILIMANJARO.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amewataka watendaji kuziba mianya ya uvujaji wa mapato, ili kuhakikisha Wakala unakusanya mapato iliyokusudia na kufanya matumizi stahiki kwa maendeleo ya Wakala.
Amesema hayo wakati akizungumza na  na watumishi wa kituo cha TEMESA Kilimanajaro alipotembelea na kujionea hali ilivyo katika kituo hicho na kuwahimiza watumishi wa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja na kutoa huduma zenye ubora. 
“Nawaomba muwe na  mbinu mbadala yakuzuia mianya ya uputevu wa mapato na  mzibane Taasisi mnazozidai  walipe madeni ili mapato yatakayokusanywa yasaidie kuboresha zaidi karakana zetu.” Alisisitiza Dkt. Mgwatu. 
Nao watumishi wa kituo cha TEMESA Kilimanjaro kwa nyakati tofauti, wamemuahakikishia mtendaji huyo kufanya kazi kwa kujituma na kuzidi kupambana kuipeleka mbele TEMESA ingawa kumekuwapo na  ukosefu wa vitendea kazi  kulingana na taaluma mbali mbali zilizopo kwenye kituo hicho.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yuko katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vilivyopo kanda ya Kaskazini kuangalia utendaji kazi wake na kuona changamoto zilizopo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa maendeleo ya Wakala huo.



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu akipata maelezo ya utendaji kutoka kwa Meneja wa TEMESA Kilimanjaro, Mhandisi Alfred Ng’hwani alipotembelea kituoni hapo.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wakwanza kulia), akiongea na watumishi wa TEMESA Kilimanjaro alipotembelea kituoni hapo

No comments:

Post a Comment