Baadhi
ya washiriki wa Mkutano wa Kikanda wa Kimataifa wa Siku Mbili
unaohusiana na Sekta ya Mafuta na Gesi asilia wakimsikiliza Balozi Seif
wakati akiufungua Mkutano huo.
Baadhi
ya washiriki wa Mkutano wa Kikanda wa Kimataifa wa Siku Mbili
unaohusiana na Sekta ya Mafuta na Gesi asilia wakimsikiliza Balozi Seif
wakati akiufungua Mkutano huo.
Balozi
Seif akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano wa Kikanda wa
Kimataifa wa Siku Mbili unaohusiana na Sekta ya Mafuta na Gesi asilia.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema licha ya juhudi kubwa zinazochukuliwa na Mataifa na Taasisi za Kimataifa kuunga mkono miradi ya Kiuchumi inayoanzishwa na Serikali, lakini bado nguvu za pamoja kwa Taasisi za ndani zinahitajika katika kushirikiana na Serikali kiuendeleza miradi hiyo.
Alisema zipo jitihada zinazofanywa na Serikali kuandaa Sera,mipango na Mikakati ya kujiandaa na miradi mipya kama Mafuta na Gesi asilia ambayo kufanikiwa kwake mbali ya kuinua pato la Taifa lakini pia inaweza kutoa ajira kubwa itakayopunguza wimbi la Vijana wasiokuwa na kazi za kujikidhi kimaisha.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akiufungua Mkutano wa Kikanda wa Kimataifa wa Siku Mbili unaohusiana na Sekta ya Mafuta na Gesi asilia ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi na kufanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Park Hyatt Mjini Zanzibar.
Alisema ingawa usimamizi wa kuendesha miradi ya sekta ya Mafuta na gesi asilia hupangwa na kupewa dhamana wawekezaji kulingana na kiwango cha taaluma walichonacho, hata hivyo jukumu la kusimamia sera litabakia kuwa mikononi mwa wazalendo wenyewe ili kujilinda mapema na changamoto za kimazingira zisizoepukika katika kuendesha miradi hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema licha ya juhudi kubwa zinazochukuliwa na Mataifa na Taasisi za Kimataifa kuunga mkono miradi ya Kiuchumi inayoanzishwa na Serikali, lakini bado nguvu za pamoja kwa Taasisi za ndani zinahitajika katika kushirikiana na Serikali kiuendeleza miradi hiyo.
Alisema zipo jitihada zinazofanywa na Serikali kuandaa Sera,mipango na Mikakati ya kujiandaa na miradi mipya kama Mafuta na Gesi asilia ambayo kufanikiwa kwake mbali ya kuinua pato la Taifa lakini pia inaweza kutoa ajira kubwa itakayopunguza wimbi la Vijana wasiokuwa na kazi za kujikidhi kimaisha.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akiufungua Mkutano wa Kikanda wa Kimataifa wa Siku Mbili unaohusiana na Sekta ya Mafuta na Gesi asilia ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi na kufanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Park Hyatt Mjini Zanzibar.
Alisema ingawa usimamizi wa kuendesha miradi ya sekta ya Mafuta na gesi asilia hupangwa na kupewa dhamana wawekezaji kulingana na kiwango cha taaluma walichonacho, hata hivyo jukumu la kusimamia sera litabakia kuwa mikononi mwa wazalendo wenyewe ili kujilinda mapema na changamoto za kimazingira zisizoepukika katika kuendesha miradi hiyo.
DK. SHEIN AWAHAKIKISHIA WAZANZIBAR WATAENDELEA KUWA NA AFYA NJEMA, ELIMU BORA NA WAKIISHI KWA AMANI NA UTULIVU
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Mkuu wa Chuo
cha Taaluma ya Sayansi za Afya Mbweni Dr. Haji Mwita Haji
alipomuwakilisha Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein katika mahafali
ya Pili ya Chuo cha Madaktari Zanzibar na yale ya 23 ya Chuo cha
Taaluma za Sayanzi za Afya Mbweni.
Balozi
Seif akisalimiana na wahadhiri walioendesha mafunzo ya Udaktari
Zanzibar kutoka Chuo Kikuu cha Matanzas cha Nchini Jamuhuri ya Watu wa
Cuba Tawi la Zanzibar hapo katika viwanja vya chuo cha Taaluma ya
Sayansi za Afya Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Baadhi
ya wahitimu waliomaliza mafunzo ya Udaktari chuo cha Udaktari Zanzibar
wakila kiapo cha utii katika kukabiliana na majukumu yao
watakayopangiwa hapo baadaye.
Baadhi
ya wahitimu waliomaliza mafunzo ya Udaktari chuo cha Udaktari Zanzibar
wakila kiapo cha utii katika kukabiliana na majukumu yao
watakayopangiwa hapo baadaye.
Mwakilishi
wa Chuo Kikuu cha Matanzas cha Nchini Jamuhuri ya Watu wa Cuba Dr.
Zailit Gonzalet Cruiz akimuhudhurisha Mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya
Udaktari katika chuo cha Udaktari Zanzibar.
MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA) YAONGEZA VYANZO VIWILI VYA MAJI .
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira
mjini Moshi,Prof Faustine Bee (kushoto) akimuongoza Waziri wa Maji na
Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge kuelekea katika chanz cha
Mkashilingi kilichopo wilyani Hai kwa ajili ya uzinduzi, kulia kwa
Waziri ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini
Moshi (MUWSA).Joyce Msiru.
Waziri
wa Maji na Uwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akizungumza wakati wa
uzinduzi wa chanzo cha maji cha Mkashilingi kilichopo wilayani Hai
mkoani Kilimanjaro.
TANZANIA YAWAKARIBISHA WAKOREA KUSINI KUWEKEZA SEKTA YA VIWANDA
Mkuu
wa kitengo cha utafutaji Rasilimali, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango,
Zanzibar, Sabra Issa Machano, akiwasilisha mada kuhusu fursa za
uwekezaji zinazopatikana Tanzania Zanzibar, wakati wa mkutano wa 5 wa
ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika
(KOAFEC), Jijini Seoul, Korea Kusini.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimpongeza Mkuu wa
kitengo cha utafutaji Rasilimali, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango,
Zanzibar, Sabra Issa Machano, baada ya akiwasilisha mada kuhusu fursa za
uwekezaji zinazopatikana Tanzania Zanzibar, wakati wa mkutano wa 5 wa
ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika
(KOAFEC), Jijini Seoul, Korea Kusini.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akifuatilia kwa
makini wakati Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji kutoka kituo cha
uwekezaji Tanzania-TIC, John Mnali, akiwasilisha mada kuhusu fursa za
uwekezaji zinazopatikana Tanzania, wakati wa mkutano wa 5 wa ushirikiano
wa kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini
Seoul, Korea Kusini. Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Utafutaji
Rasilimali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Zanzibar-Sabra Issa
Machano.
Mkurugenzi
wa Uhamasishaji uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC, John
Mnali (Katikati), akibadilishana mawasiliano na mmoja wa
wafanyabiashara walioonesha nia ya kuweka nchini Tanzania baada ya
Mkurugenzi huyo kuwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji
zinazopatikana Tanzania, wakati wa mkutano wa 5 wa ushirikiano wa
kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), Jijini
Seoul, Korea Kusini.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akibadilishana
mawasiliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MarineBio, Heo
Yun-Young, ambaye kampuni yake inataka kuwekeza kiwanda cha kusindika
zao la mwani linalopatikana katika Bahari Kuu ya Hindi nchini Tanzania.
DK. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
akitoa maelekezo wakati alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika
kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo
mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo Ikulu Mjini
Unguja,[Picha na Ikulu.] 27/10 /2016.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kulia) akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika kikao cha Mpango
kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza
ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo Ikulu Mjini Unguja
Baadhi
ya maafisa wa Vikosi vya SMZ wakiwa katika kikao cha Mpango kazi wa
mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya
Julai-Septemba 2016 cha Uongozi wa Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ,kilichofanyika leo Ikulu
Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Wakuu
wa Vikosi vya Ulinzi vya SMZ wakiwa katika kikao cha Mpango kazi wa
mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya
Julai-Septemba 2016 cha Uongozi wa Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ,kilichofanyika leo Ikulu
Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
MAJALIWA AKUTANA NA ASKOFU MKUU BEATUS KINYAIYA WA DODOMA
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la
Dodoma, Beatus Kinyaiya kabala ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri
Mkuu mjini Dodoma Oktoba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ABU DHABI YAAHIDI KUENDELEZA KUKUZA UHUSIANO NA TANZANIA KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail:
press@ikulu.go.tz
Tovuti :
www.ikulu.go.tz
Faksi:
255-22-2113425
|
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA
BARACK OBAMA,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Ikulu,
Dar es Salaam,
Mrithi
wa Mfalme wa Abu Dhabi na Kaimu Rais, Mtukufu Sheikh Mohamed bin
Zayed Al Nahyan amemuahidi Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John
Pombe Magufuli kuwa nchi hiyo imedhamiria kuendeleza na kukuza zaidi
uhusiano wake na Tanzania hususani katika utekelezaji wa miradi ya
maendeleo.
Mtukufu
Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan ametoa ahadi hiyo kupitia kwa
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi Bw. Mohamed Al
Suwaidi aliyekutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli leo tarehe
27 Oktoba 2016.
Mfuko
wa maendeleo wa Abu Dhabi unashirikiana na Tanzania katika
utekelezaji wa miradi mbalimbali na katika mazungumzo ya leo
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo ameonesha nia ya kushirikiana zaidi na
Tanzania katika maeneo ya ujenzi wa miundombinu ikiwemo reli na
barabara, usafiri wa anga na madini.
Pamoja
kumshukuru Mrithi wa Mfalme wa Abu Dhabi na Kaimu Rais Mtukufu Sheikh
Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Rais Magufuli ameialika nchi hiyo
kupitia mfuko wake wa Maendeleo na wadau wengine wa maendeleo kuja
kuwekeza hapa nchini katika miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa
bandari, ujenzi wa viwanda, kilimo, uvuvi, gesi na kushirikiana
katika ujenzi wa reli ya kati ambayo itazinufaisha nchi nyingine saba
za Afrika Mashariki na kati ambazo hazina bandari.
“Tanzania
imeamua kujenga reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge)
na tayari katika bajeti yetu tumetenga Shilingi Trilioni 1 kwa ajili
ya kuanza ujenzi, hivyo tunawakaribisha Mfuko wa Maendeleo wa Abu
Dhabi kushirikiana nasi, wapo wengi ambao wamejitokeza kushirikiana
nasi lakini na nyie pia tunawakaribisha, mnaweza kuchukua sehemu ya
reli na mkaijenga”
amesema Rais Magufuli.
Aidha,
Dkt. Magufuli ameutaka mfuko huo kufupisha muda unaotumika katika
mchakato wa kuanza utekelezaji wa miradi ili kuharakisha matokeo yake
na manufaa kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
27 Oktoba, 2016
REAL MADRID YAFANYA KUFURU KWA KUISHUSHIA MVUA YA MAGOLI LEONESA
Timu ya Real Madrid imeishushia
kipigo cha paka mwizi timu ndogo ya daraja la tatu ya Cultural
Leonesa kwa kuichakaza kwa magoli 7-1 katika mchezo wa kombe la Copa
del Rey.
Katika mchezo huo ambao Madrid
waliwapumzisha Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Karim Benzema,
walipata goli la kwanza baada ya mchezaji wa zamani wa West Brom beki
Gianni Zuiverloon, kujifunga
Magoli mengine ya Real Madrid
yalifungwa na Marco Asensio na Alvaro Morata waliofunga magoli mawili
na Nacho na Mariano walifunga moja kila mmoja.
Gianni Zuiverloon akiwa amempoteza mahesabu kipa wake na kujifunga
Marco Asensio akifunga goli la pili la Real Madrid
CHELSEA YAZAMA MBELE YA WEST HAM HUKU MASHABIKI WAKIPIGANA
Ugomvi baina ya mashabiki wa West
Ham na Chelsea umeibuka mwishoni mwa mchezo wao wa jana wa kombe la
EFL, ambao Chelsea walilala kwa magoli 2-1 kwenye dimba la London.
Chupa za plastiki na viti vilirushwa
na mashabiki mwishoni mwa mechi hiyo huku mamia ya mashabiki wakorofi
wakihusika na tukio hilo baya kutokea katika soka.
Katika mchezo huo Cheikhou Kouyate
alifunga kwa kichwa kabla ya mapumziko na kisha Edimilson Fernandes
akaongeza la pili kwa shuti la yadi 18 huku Gary Cahill akiifungia
Chelsea goli pekee katika dakika ya 90.
Kipa wa Chelsea akiruka bila ya mafanikio kuzuia mpira wa kichwa uliopigwa na Cheikhou Kouyate
Edimilson Fernandes akiachia shuti lililzaa goli la pili la West Ham
Mashabiki wakizozana punde tu baada ya kumalizika kwa mechi hiyo
JUAN MATA AIPELEKA MANCHESTER UNITED ROBO FAINALI KOMBE LA EFL
Juan Mata amefunga goli na kuipatia
ushindi Manchester United dhidi ya majirani zao Manchester United
katika mchezo wa kombe la EFL na kutinga hatua ya robo fainali.
Mhispania huyo aliachia shuti la
chini lililojaa wavuni akiunganisha mpira uliogongwa nyuma na Zlatan
Ibrahimovic na kujihakikishia kukutana na West Ham robo fainali.
Paul Pogba aligonga mwamba muda
mchache kabla ya kufungwa goli hilo, ambapo mpira katika mchezo huo
ulichangamka katika kipindi cha pili.
Juan Mata akiachia shuti lililomshinda kipa na kujaa wavuni
Kipa na wachezaji wa Manchester City wakiwa hoi baada ya kutinga goli hilo
No comments:
Post a Comment