Mkuu wa Mkoa wa
Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe akifungua Mkutano wa wadau wa pamba
wenye dhamira ya kujadili maendeleo ya kilimo cha
zao la hilo katika mkoa wa Singida, Oktoba 31, 2016.
Wadaau wa kilimo cha Pamba Mkoa wa
Singida wakifuatilia kwa makini Mkutano wa kujadili namna bora ya
kuimarisha kilimo cha zao hilo katika Mkoa wa Singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa pamba Mkoa wa Singida
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Ikungi Bi Rustika Turuka akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa
kilimo cha Pamba Mkoa wa Singida
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe Elias Choro Tarimo akisisitiza jambo wakati wa Mkutano huo
Moja ya wakulima wa Kilimo cha pamba
Wilayani Ikungi Timoth S. Nkulu akimuomba Mkuu wa Wilaya kuzisimamia
Wilaya zote kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa uzalishaji wa kilimo hicho.
Wadau wa kilimo cha pamba wakihakiki maazimio waliyoyapitisha
NA MWANDISHI WETU
BODI ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza siku 90 kuanzia leo
(Jumatatu, Oktoba 31, 2016) kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo
2016/2017 kukata rufaa kwa njia ya mtandao ikiwa hawajaridhsihwa na matokeo ya
upangaji uliotangazwa hivi karibuni.
Serikali imetenga Tshs 483 bilioni
kwa ajili ya kutoa mikopo kwa jumla wanafunzi 119,012 – kati yao, wanafunzi
93,295 ni wanaondelea na masomo na wanafunzi 25,717 ni wa mwaka wa kwanza. Hadi
sasa, jumla ya wanafunzi 20,183 wa mwaka wa kwanza wameshapata mikopo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
leo (Jumatatu, Oktoba 31, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq
Badru, Bodi imeanza kupokea rufaa hizo kwa njia ya mtandao (Online Loan
Application and Management System) kuanzia leo (Oktoba 31, 2016) hadi Januari
31, 2017.
“Wanachotakiwa kufanya wanafunzi ni
kulipa Tshs 10,000.00 kwa njia ya M-Pesa na kuingia katika mtandao wetu wa http://olas.heslb.go.tz na kujaza fomu, kuichapa na
kuiwasilisha kwa Afisa Mikopo wa chuo chake ambaye atawasilisha kwetu fomu zote
za chuo chake kwa barua kwa ajili ya sisi kuzifanyia kazi,” amesema Bw. Badru.
No comments:
Post a Comment