Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
(kushoto) akiongoza na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida mara baada ya
kuwasili kwenye ofisi za ESRF kufungua warsha ya nafasi ya wazee katika
kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF
kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.
Mkurugenzi
Mkazi Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International),
Amleset Tewodros (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (wa
pili kulia) ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa
Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati). Wengine kushoto ni
Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya
Fedha na Mipango, Anna Mwasha na Mkurugenzi Mkazi Msaidizi wa Shirika la
kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International), Smart Daniel (wa
pili kushoto).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na washiriki wa warsha ya
nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age
International iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar
es Salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akifungua warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya
maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na
Shirika la Help Age International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano
wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Jukwaa la Wazee Tanzania, Samson Msemembo (85) akizungumzia
changamoto wanazokutana nazo wazee katika vituo vya huduma za afya kwa
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu (katikati), Kaimu Kamishna Ustawi wa Jamii Bw.Rabikira Mushi
kutoka Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
(kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi
na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida waliopo meza kuu.
Mtafiti
Mkuu Mshiriki kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) na
Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Oswald Mashindano akizungumzia
nafasi ya wazee katika sera ya kitaifa kwenye warsha kuhusu nafasi ya
wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age
International iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi
Mkazi Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International),
Amleset Tewodros akishiriki kutoa maoni kwenye warsha kuhusu nafasi ya
wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age
International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida akifafanua jambo kwenye warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza
malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa
kushirikiana na Shirika la Help Age International. Kushoto ni Mkurugenzi
Mkazi Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International),
Amleset Tewodros.
Mshauri
wa Masuala ya Ushirikiano wa Kanda ya Afrika Mashariki, Kati na
Magharibi wa Shirika la Help Age International, Roseline Kihumba
akizungumzia hali ya uzee na wazee duniani na ushirikishwaji wa wazee
katika maendeleo endelevu kwenye warsha ya nafasi ya wazee katika
kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF
kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.
Mkurugenzi
wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na
Mipango, Anna Mwasha akichangia mada kwenye warsha ya nafasi ya wazee
katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na
ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Uchambuzi wa Sera na Utafiti wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Mudith Cheyo akifafanua jambo kwa washiriki wa warsha kuhusu
nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age
International.
Mkurugenzi
wa Mtandao wa Watu Waishio na Virusi vya Ukimwi Tanzania (SHDEPHA),
Joseph Katto akizungumzia changamoto zinazowakabili wazee wanaoishi na
VVU katika kupata huduma mbalimbali nchini kwenye warsha kuhusu nafasi
ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age
International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar
es Salaam.
Sehemu
ya washiriki waliohudhuria warsha kuhusu nafasi ya wazee katika
kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF
kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International na kufanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mikutano wa ESRF
wakati wa warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya
maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na
Shirika la Help Age International
Picha ya pamoja
MKUU WA WILAYA YA KASULU AFUNGA MAFUNZO YA JKT MUJIBU WA SHERIA KAMBI YA MTABILA 825KJ KASULU-KIGOMA
Mkuu
wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akikagua gwaride
maalum la wahitimu wa mafunzo ya JKT yaliyofanyika katika kikosi cha
825 JK Mtibila ambapo vijana 1140 walifuzu na kumaliza mafunzo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akipokea heshima kutoka kwa wahitimu.
Wahitimu wakipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akizungumza na wahitimu hao wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akiangalia madawati yaliyotengenezwa na vijana hao wa JKT.
**************
Mkuu
wa Wilaya ya Kasulu Col Martin Eliah Mkisi katika hotuba yake,
amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya JKT Oparesheni Magufuli Kundi la
nne Kwa Mujibu wa sheria, kuiamini, kuitekeleza na kuiishi kaulimbiu ya
HAPA KAZI TU.
Amesema
vijana hao waliobahatika kupata mafunzo ya JKT katika kambi ya 825 KJ
Mtabila kuja na mbinu mbadala na mawazo chanya ktk kutatua changamoto
mbalimbali za maisha badala ya kulalamika.
Amewataka
kuwa kielelezo cha nidhamu na uzalendo ktk maisha yao ya vyuoni na
mahali pa kazi hapo baadaye kama walivyofundishwa na Wakufunzi Mahiri wa
JKT.
Aidha,
Col Mkisi amelipongeza JKT kwa kutekeleza wajibu wake adhimu wa kuwalea
na kuwafundisha vijana wa Tanzania, stadi za maisha, uzalenda na
ujasiliamali.Vijana wapatao 1140 walifuzu mafunzo hayo yaliyochukua
miezi mitatu.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Doto James kuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiwa katika picha ya pamoja
na Katibu Mkuu wa Fedha na Mipango Doto James mara baada ya kuapishwa.(PICHA NA IKULU)
Shindano la Ulimbwende la "Ozona Miss
Lake Zone 2016" linaloshirikisha Walimbwende 18 kutoka Mikoa ya Kanda ya
Ziwa limezinduliwa rasmi hii leo Jijini Mwanza.
Shindano hilo litakalofanyika jumamosi
Septemba 10,2016 katika Ukumbi wa Rock City Mall, limeandaliwa na Flora
Promotions na kupewa nguvu na wadhamini mbalimbali akiwemo mdhamini
mkuu, Kampuni ya vipodozi ya Ozona ambayo imetoa zawadi ya gari lenye
thamani ya shilingi Milioni 12 kwa mshindi wa kwanza.
Katika picha, kushoto ni Mkurugenzi wa
Kampuni ya Ozona, Dr.Thobias Mkina, akizungumza katika uzinduzi wa
shindano hilo ambapo kushoto ni Mkurugenzi wa Flora Promotions, Flora
Lauwo.
Na BMG
Wadau mbalimbali Ozona Miss Lake Zone wakiwa kwenye uzinduzi wa shindano hilo hii leo
Wadau mbalimbali Ozona Miss Lake Zone wakiwa kwenye uzinduzi wa shindano hilo hii leo
Mkurugenzi wa Flora Promotions, Flora Lauwo, akiteta jambo kwenye uzinduzi wa shindano la Ozona Miss Lake Zone 2016
Baadhi ya Washiriki wa Ozona Miss Lake Zone 2016

Mzee wa Masauti, Christian Bella pamoja
na Mchekeshaji Erick Omond wanatarajiwa kuungana na watumbuizaji wengine
pamoja na wadau wengine kwenye kufanikisha Usiku wa Ozona Miss Lake
Zone 2016.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiweka saini katika moja ya makubaliano yaliofanywa na nchi za SADC
kwenye mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika Lozitha,
Mbabane nchini Swaziland.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(katikati) akiwa kwenye mkutano wa 36 wa nchi 15 za SADC uliofanyika
mjini Mbabane Swaziland, kulia ni Makamu wa Rais wa nchi ya Angola Mhe.
Manuel Domingos Vicente na kushoto ni Waziri Mkuu wa Madagascar
Mhe.Mahafaly Solonandrasana Olivier.
Mwenyekiti wa SADC Mfalme Mswati wa III(kulia) akizungumza na Katibu Mkuu Mtendaji wa SADC Dr. Stergomena L. Tax wakati wa kuhitimisha mkutano wa 36 wa SADC mjini Mbabane,Swaziland.
Mwenyekiti wa SADC Mfalme Mswati wa III akihutubia wakati wa kufunga mkutano 36 wa SADC mjini Mbabane ,Swaziland.
............................................
No comments:
Post a Comment