Baadhi ya washiriki wakijadiliana jambo baada ya kupata mafunzo juu ya uwekezaji katika miradi ya umma.
Naibu
Katibu Mtendaji –Uchumi jumla kutoka Tume ya Mipango Bi. Lorah Madete,
akiwaonyesha maafisa mipango kutoka mikoa ya Arusha, Tanga, na
Kilimanjaro mwongozo wa kusimamia uwekezaji wa miradi ya Umma.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mafunzo.
Mhandisi. Arnold Masaki moja ya wakufunzi akieleza jambo kwa washikiri wa mafunzo ya Uwekezaji katika miradi ya umma
MASHABIKI WAVAMIA UWANJANI NA KUMUANGUSHA NEYMAR MAZOEZINI
Mchezaji nyota wa timu ya Barcelona Neymar
amevamiwa na mashabiki akiwa mazoezini nchini Brazil wakati timu ya
taifa ikianza mazoezi, kujiandaa na mchezo dhidi ya Colombia.
Vijana wawili walivamia kiwanjani na
kumkumbatia kwa furaha kiasi ya kujikuta wakianguka chini na mchezaji
huyo ambaye alionekana kutokukerwa na kitendo hicho.
Neymar akianguka chini baada ya kukumbatiwa na mashaniki wawili
Walinzi na wasaidizi wa timu wakijaribu kuwaondoa mashabiki hao waliomuangusha Neymar
Kaimu Mkuu wa kitengo cha habari, elimu na mawasiliano
kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Eddah Katikiro (katikati),
akizungumza kwenye semina elekezi kuhusu uzinduzi wa Kondom mpya ya Zana
itakayokuwa ikitolewa bure na serikali kwa wananchi, iliyofanyika Jijini Mwanza
leo.
Na BMG
Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imewahimiza wananchi kuzingatia matumizi
sahihi na endelevu ya kondomu ili kujiepusha na mimba zisizotarajiwa pamoja na
magongwa ya kuambukiza ikiwemo virusi vya Ukimwi.
Kaimu Mkuu wa kitengo cha habari, elimu na
mawasiliano kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Eddah Katikiro, ametoa
rai hiyo hii leo Jijini Mwanza, kwenye semina elekezi kuhusu uzinduzi wa Kondom
mpya ya Zana itakayokuwa ikitolewa bure na serikali kwa wananchi.
Katikiro amesisitiza matumizi sahihi na endelevu ya
kondom ya Zana kwa wananchi walio kwenye mahusiano ya kimapenzi, yatasaidia
kupunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama virusi vya Ukimwi pamoja na
mimba zisizotarajiwa na kwamba aina hiyo ya kondom ni imara na yenye ubora.
Mratibu wa mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi,
mkoani Mwanza, Geofrey Mabu, amesema mkoa wa Mwanza umejipanga vyema ili
kuhakikisha kondom za Zana zinawafikiwa walengwa hususani kupatikana bure
katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye vituo vyote vya afya, maeneo ya starehe
pamoja na kwenye ofisi za serikali na binafsi.
Uzinduzi wa Zana Kondom
kitaifa ulifanyika mkoani Mbeya wiki iliyopita ambapo kwa mkoa wa Mwanza
uzinduzi utafanyika kesho Jijini Mwanza ambapo aina hiyo ya kondomu itakuwa
mbadala wa kondom za MSD zilizokuwa zikitolewa pia bure na Serikali lengo
likiwa ni kuhakikisha mapambano dhidi ya Ukimwi yanafanikiwa
Washirki wa semina hiyo
Wanasemina
Wanasemina
Mmoja wa washiriki wa semina akihojiwa na wanahabari
Mmoja wa washiriki wa semina akihojiwa na wanahabari
Picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment