Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Nyanda za juu Kusini Jackson Kiswaga akipeana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dr Rehema Nchimbi mara baada ya kutoa hotuba wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya zoezi la usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa, uzinduzi huo ulifanyika jana mjini Iringa. |
Waziri wa Katiba na Sheria, Dr Harrison Mwakyembe akionesha mojawapo ya simu 800 zilizotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ili kufanikisha zoezi la usajili na utoaji wa vyeti kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, uzinduzi wa zoezi hilo kwa awamu ya tatu ulifanyika jana mjini Iringa. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza. |
|
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye akipokea zawadi ya jezi maalum kutoka kwa Mkurugenzi wa Klabu ya Soka ya
Seongnam Bw. Suk Hoon Lee kutoka Korea ya Kusini, jezi hiyo ni zawadi maalum
kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kutoka
kwa klabu hiyo Septemba 23,2016 jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA RAYMOND
MUSHUMBUSI-WHUSM)
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye akizungumza na ujumbe kutoka Korea ya Kusini ofisini kwake jijini Dar es
Salaam kuhusu uwekezaji katika sekta ya Habari, Michezo na Utengenezaji wa
Filamu nchini Septemba 23, 2016.
Katibu Mkuu Wizara wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel akitoa maelezo kuhusu sekta zilizopo katika Wizara hiyo
kwa ujumbe kutoka Korea ya Kusini katika kikao kilichojadili uwekezaji katika
sekta ya Habari, Michezo na utengenezaji wa Filamu nchini Septemba 23, 2016,
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Redio kutoka Shirika la
Utangazaji la Taifa (TBC) Bi Suzana Mungy akitoa maelezo ya utendaji wa Shirika
hilo na fursa zilizopo kwa wawekezaji kuwekeza katika sekta ya hiyo kwa ujumbe
kutoka Korea ya Kusini katika kikao kilichojadili uwekezaji katika sekta ya
Habari, Michezo na utengenezaji wa Filamu nchini Septemba 23, 2016.
Mkurugenzi wa Kampuni ya TCN Korea ya Kusini Bw. Soon Young-Soon
akimueleza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
na ujumbe wa Wizara(Hawapo pichani) kuhusu mpango wa Kampuni yake
kuwekeza katika Sekta ya Habari na utengenezaji wa Filamu katika kikao
kilichojadili uwekezaji katika sekta ya Habari, Michezo na utengenezaji wa
Filamu nchini Septemba 23, 2016.
Ujumbe kutoka Korea ya Kusini ukimsikiliza Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) katika
kikao kilichojadili uwekezaji katika sekta ya Habari, Michezo na utengenezaji
wa Filamu nchini Septemba 23, 2016 jijini Dar es Salaam.
Ujumbe kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
ukimsikiliza mmoja wa viongozi wa ujumbe kutoka Korea ya Kusini Bw. Soon
Young-Soon (Hayupo Pichani) katika kikao kilichojadili uwekezaji katika
sekta ya Habari, Michezo na utengenezaji wa Filamu nchini Septemba 23, 2016
jijini Dar es Salaam.
Ujumbe kutoka Korea ya Kusini ukimsikiliza Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) katika
kikao kilichojadili uwekezaji katika sekta ya Habari, Michezo na utengenezaji
wa Filamu nchini Septemba 23, 2016 jijini Dar es Salaam.
NA RAYMOND MUSHUMBUSI WHUSM
SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau kutoka Korea ya
Kusini wamekubaliana kushirikiana kuendeleza sekta za Habari, Michezo na filamu
kwa kuwekeza katika miundombinu na wataalamu.
Pande hizo mbili zimekubaliana kushirikiana katika sekta hizo
katika kikao kilichojumuisha ujumbe kutoka Kampuni ya TCN na Klabu ya Soka ya
Seongam kutoka Korea Kusini na ujumbe kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo walipokutana leo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amesema kuwa kuja kwa ujumbe
huo kutoka Korea ya Kusini ni fursa nzuri kwa Tanzania kuendeleza sekta za
Habari, Michezo na Filamu kupitia wadau mbalimbali na wawekezaji kutoka nje ya
nchi ambapo Serikali ipo tayari kushirikiana nao katika kuleta ufanisi na
maendeleo katika sekta hizo.
“Ni matumaini yangu kuwa mazungumzo haya yataleta matunda kwani
tayari tumeshazungumza nao kuhusu fursa zilizopo na kilichobaki ni wao
kutuandikia rasmi ili tuanze sasa mchakato na matunda yataanza kuonekana hivi
karibuni” Alisema Nnauye.
Aidha Mkurugenzi wa Klabu ya Soka ya Seongnam Bw. Suk Hoon Lee
kutoka Korea ya Kusini amesema klabu yake ipo tayari kuwekeza katika shule ya
michezo kwa vijana ili kuongeza kasi ya maendeleo ya soka kwa vijana.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TCN kutoka Korea ya Kusini Bw.
Soon Young-Soon alisisitiza kuwa kampuni yake imejiandaa kuja Tanzania kuwekeza
katika utengenezaji wa Filamu kwa kuleta wataalamu na kutengeneza miundombinu
ya kisasa katika utengenezaji wa filamu bora na utengenezaji wa vipindi
mbalimbali nchini.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Redio kutoka Shirika la
Utangazaji la Taifa (TBC) Suzana Mungy ameushukuru ujumbe kutoka Korea ya
Kusini na kuahidi kuwapa ushirikiano wataalamu kutoka Korea ya Kusini na
kuwakaribisha kuwekeza katika sekta ya Habari hasa utengenezaji wa vipindi
bora.
Korea ya Kusini ni moja ya nchi rafiki wa Tanzania na kwa miaka
mingi wamekuwa wakishirikiana katika sekta mbalimbali zikiwemo Habari, Michezo
Utamaduni na Sanaa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment