Tuzo aliyotunukiwa mkurugenzi mtendaji
wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016
jijini New York nchini Marekani katika hotel ya St. Regis, New York.
African Leadership hutoa tuzo katika kutambua michango unaotolewa na
viongozi wa bara la Afrika katika kuleta maendeleo na utendaji wa kazi
wenye ufanisi' katika kukuza uchumi kwa kusaidia kukuza na kuwainua
wawekezaji wazawa. African Leadership ilishawahi kutoa tuzo kama hilo
kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka April 9, 2014 katika hotel ya St
Regis ya Washington, DC. Picha na Vijimambo Blog/Kwanza Production, New
York.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB,
Dkt Charles Kimei akifuatilia hafla ya utoaji tuzo kwa viongozi wa
Afrika iliyofanyika siku ya Alhamisi Sepemba 22, 2016 katika hotel ya
St. Regis New York. Kulia ni Rais wa Burkina Faso, Mhe. Roch Marc
Christian Kabore.
Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akielezea mafanikio na
utendaji wa benki ya CRDB na jinsi gani inavyowawezesha wawekezaji
wazawa kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu katika kusaidia kuinua
uchumi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB,
Dkt Charles Kimei akitunukiwa tuzo na Rais wa Malawi, Mhe. Prof. Arthur
Peter Mutharika kulia ni fisrt lady Mke wa Rais wa malawi.
kushoto ni Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa akisalimiana na Rais wa Malawi Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika mara tu baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei kupokea tuzo iliyotolewa na African Leadership siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016 katika hotel ya St. Regis, New York. kulia ni fisrt lady Mke wa Rais wa malawi.
Picha ya pamoja.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa fedha
wa benki ya CRDB, Bwn. Frederick Nshekanabo, Mkurugenzi wa masoko,
utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei alipokua
akifanyiwa mahaojiano mara tu baada ya kupokea tuzo kutoka African
Leadership katika hotel ya St. Regis, New York siku ya Alhamisi Septemba
22, 2016.
Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma
kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa akifuatilia sherehe ya Tuzo
kutoka kwa African Leadership iliyofanyika katika hotel ya St. Regis,
New York siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016. Kulia ni Rais wa Burkina Faso, Mhe. Roch Marc Christian Kabore.
Hapa ni siku Balozi wa Nigeria nchini
Marekani Profesa Adebowele Adufye, alipomkabidhi aliyekuwa Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe Tuzo
la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la
Afrika kwa mwaka 2013 anayopokea kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania awamu ya nne Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
wakati huo katika sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St.
Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikata tiketi
ya mabasi ya Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo cha
Ubungo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusafiri na mabasi hayo kutoka
katika kituo hicho kuelekea Posta. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama
Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga naye akiwa mmoja wa
wasafiri wa mabasi hayo. Masauni aliyapanda basi la Mwendo kasi mara
baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo
kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha zote na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiigusisha
tiketi yake katika mashine ya Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT
katika Kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam ili mruhusu kuingia ndani
ya stendi hiyo kwa ajili ya kusafiri na mabasi hayo kutoka katika kituo
hicho kuelekea Posta. Mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika
Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa
abiria Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiingia ndani
ya Basi la Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo cha
Ubungo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusafiri na basi hilo kuelekea
katikati ya Jiji, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu
ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa ndani
ya moja ya mabasi ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi ya UDA-RT jijini Dar
es Salaam akitoka kituo cha Ubungo kuelekea katikati ya Jiji, baada ya
kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua
mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
KOCHA ARSENAL ARSENE WENGER KUTOSOMA KITABU CHA HASIMU WAKE JOSE MOURINHO
NAIBU WAZIRI MASAUNI APANDA MABASI YA MWENDO KASI, JIJINI DAR ES SALAAM
MAJALIWA APOKEA MISAADA
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni 16 kutoka kwa
Dkt. Ave Maria Semakafu (kulia), Berious Nyasebwa (wapili kushoto) na
Benjamin Thomson wote kutoka Group la Whats App la Leaders Forum ukiwa
ni mchango wa group hilo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani
Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar
es salaam Septemba 21, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwashukuru viongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya
ambao walitoa mchango wa shilingi milioni 10 kwa waathirika wa tetemeko
la ardhi mkoani Kagera, Septemba 22, 2016. Makabidhiano hayo yalifanyika
ofisini kwa Waziri Mkuu jijini .Kutoka kushoto ni Sheikh Tahir Mahmood
Chaundhry, Issa Mwakitalima, Khuram Shahzad na Jamil Mwanga. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mchango wa tani 40 za saruji zenye
thamani ya shilingi milioni 16.5 kutoka kwa Dhruv Jog na Lebulu Victor
(kulia) wote wa Kampuni ya ujenzi a Advent ukiwa ni mchango kwa
waahirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera Septemba 22, 2016.
Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es
salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 100 kutoka kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VODACOM TANZANIA, Bw. Ian Ferrao
(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Rosalynn Mworia ukiwa ni
mchango kwa waarhirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Ofisini kwake
jijini Dar es salaam Septemba 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
TUME YA MIPANGO YAENDESHA WARSHA KUJENGA UELEWA JUU YA MIPANGO YA MAENDELEO YA KIMATAIFA NA KIKANDA
Washiriki
wakipata ufafanuzi wa malengo ya warsha hiyo kutoka kwa Naibu Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa
na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe mara baada ya ufunguzi.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Innocent Shiyo (katikati)
kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya
kufungamanisha sera, mikakati na mipango ya maendeleo ya kitaifa na ile
ya kimataifa na kikanda iliyofanyika Septemba 22, 2016 katika ukumbi wa
kituo cha mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam. Kushoto
ni Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya
Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe na kulia
ni Bw. Maxwell Mkumba kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Nchi za Kusini
mwa Afrika (SADC).
Washiriki wakichukua hoja kutoka kwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango (hayupo pichani) katika warsha hiyo. (Picha zote na Adili Mhina)
No comments:
Post a Comment