Kufuatia serikali kupitisha muswada wa ongezeko la VAT kwa watalii ambao wanakuja nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali, MO Blog imepata nafasi ya kufanya mahojiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Travel Partner, Erick Mashauri ili kujua ni kwa kiasi gani ongezeko hilo limeathiri biashara kwa makampuni yanayopeleka watalii mbugani na kwa sekta ya utalii kwa ujumla.
Mashauri alisema kuwa ongezeko la VAT kwa watalii limeathiri kwa kiasi kikubwa biashara zao kwani serikali ilifanya maamuzi ya haraka bila kuangalia athari ambazo zingejitokeza baada ya kupitisha muswada na haikuwashirikisha wao kama wadau wa karibu ambao wanafanya biashara ya kuwahudumia watalii wawapo nchini.
"Ongezeko la VAT ambalo serikali ilifanya limevuruga biashara ya utalii, ilisahau kama wageni hawa huwa wanafanya booking mwezi mmoja kabla ya safari, tukashangaa serikali inapeleka muswada haraka haraka bungeni na kuupitisha bila kuangali athari ambazo zitajitokeza,
"Baada ya kuongeza VAT ilibidi makampuni ya utalii yarudishe pesa kwa watalii na wengine wametaka kupelekana hata mahakamani kwani tayari wameshaingia mikataba alafu anakuja unaanza kumwambia tena inabidi alipie VAT, jambo ambalo nchi kama Kenya tayari wameitoa kwani waliona jinsi inavyoathiri utalii lakini hapa kwetu ndiyo tunaileta," alisema Mashauri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Travel Partner, Erick Mashauri akizungumza kuhusu ongezeko la VAT limevyoathiri biashara ya utalii kwa makampuni yanayowahudumia watalii wawapo nchini. (Picha zote zimepigwa na Rabi Hume, MO BLOG)
Mashauri alitumia fursa hiyo kuiomba serikali kupitia tena muswada huo na kuangali jinsi gani ongezeko la VAT linakavyoathiri biashara ya utalii nchini na ikiwezekana iitoe ili watalii wengi waje nchini na serikali iweze kupata pesa nyingi tofauti na sasa ambapo imeongeza VAT ambayo inachangia watalii kupungua.
"Serikali inasema bora waje watalii wachache lakini wanaolipa VAT, wakija watalii wa VIP au wa kawaida wote wanatoa pesa sawa na kwanza watalii wa VIP ambao wanawataka wao hata hoteli wanazotumia wakiwa hifadhi kama Serengeti sio za watanzania, zinamilikiwa na watu wa nje,
"Nafikiri serikali ipitie tena VAT na tozo inayofanywa na TANAPA kwani zote ni pesa za serikali, iangalie jinsi gani gharama hizo zinatuathiri, hakuna haja ya kuweka gharama kubwa hawa watu hawaondoki na hizo hifadhi, waweke gharama za kawaida ili watalii waje wengi zaidi," alisema Mashauri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Travel Partner, Erick Mashauri ameiomba serikali kupitia tena muswada wa VAT ili ikiwezekana itolewe kwani ongezeko hilo linaweza kusababisha idadi ya watalii wanaokuja nchini kupungua kwa kiasi kikubwa.
Aidha Mashauri aliishauri serikali kufanya mabadiliko ya matangazo ambayo imekuwa ikiyatumia kujitangaza kimataifa ya kutumia viwanja vya michezo kuwa njia hiyo haiwezi kusaidia kwa kiasi kikubwa kama inavyotarajia na badala yake itumie vyombo vya usafiri.
"Wanaokwenda mpirani wengi hawapendi utalii, njia rahisi ni kuingia mikataba na makampuni ya mabasi na treni, wakitangaza wale hapa tutawakimbia watalii, wanaingia mikataba mara moja na tangazo linakaa mwaka mzima, hebu fikiria mfano Uingereza kuna mabasi zaidi ya 300, kama tangazo kila siku likionwa na watu milioni moja tu kwa mwaka tutapata watalii wengi," alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Travel Partner, Erick Mashauri akielezea jinsi watalii wanavyonyang'anywa vinyago wanavyo nunua nchini na kuiomba serikali iliangalie jambo hilo na kuwaruhusu watalii kuondoka na vinyago hivyo kwani wao ndiyo wateja wakubwa wa biashara hiyo.
Pia Mashauri aliiomba serikali kuweka utaratibu wa watalii ambao wanakuja nchini kuruhusiwa kuondoka na vinyago ambavyo wamekuwa wakinunua nchini kwani hizo ndizo zawadi ambazo wanaweza kuzipata nchini na kuwapelekea ndugu zao katika nchi ambazo wametoka.
"Kuna tatizo kubwa la watalii kunyang'anywa vinyago wakifika uwanja wa ndege, hivi wanadhani hawa watalii zawadi gani wanaweza kuipata nchini tofauti na vinyago maana vingine ata kwao vipo, lakini watalii wakifika uwanja wa ndege wafanyakazi wa pale wanavichukua eti hawana kibali cha kuondoka navyo,
"Watalii wanakuwa wanaona nchi yetu hakuna mfumo wa kufanya kazi pamoja maana anayeuza vinyago amepewa leseni ya kuuza na mteja wa hivyo vinyago ni nani kama sio watalii, nadhani iliangalie jambo hilo kwakweli limekuwa likiwakera sana watalii pindi wanapokuwa wanarejea nchi walizotokea," alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Travel Partner, Erick Mashauri akizungumza na waandishi wa habari ambao walimtembelea ofisini kwake mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kuhusu Erick Mashauri amekuwa mmoja wa washindi wa tuzo za Top 100 kupitia kampuni yake ya Travel Partner ikishika nafasi ya 30 kati ya kampuni 100, amekuwa akifanya biashara ya kupeleka watalii katika hifadhi mbalimbali tangu mwaka 2007 na kupitia kampuni yake ametoa ajira rasmi kwa watanzania wasiopungua 90.
MAZISHI YA MWANDISHI ADOLPH SIMON KIVAMWO KATIKA PICHA
MWANDISHI wa habari marehemu Adolph
Simon Kivamwo,aliyefariki dunia wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka
48, amezikwa Septemba 25, 2016 kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar
es Salaam. Mamia ya wanahabari, Wafanyabiashara mashuhuri, viongozi wa
kisiasa, wananchi wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda, walifurika kwenye mazishi hayo yaliyotanguliwa na ibada ya
kuaga mwili wa marahemu iliyofanyika viwanja vya wazi, Leaders Club,
jijini Dar es Salaam. Marehemu alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda
mrefu maradhi ya Saratani ya Utumbo na ameacha mkecna watoto wanne.
Miongoni mwa watu mashuhuri waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi, Mbunge wa Kigoma mjini,
Zitto Kabwe, Mbunge wa Chalinze, Riziwani Kikwete, Mbunge wa Ubungo,
Saed Kubenea, na Mbunge wa Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji. Pia
wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini walishiriki
mazishi hayo
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth
Magufuli wakipeana mikono na waumini wengine katika kanisa la Anglikana la
Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam wakati wa Ibada ya Jumapili
kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26,
2016.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika Ibada ya Jumapili
kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26,
2016
Sehemu ya
waumini katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam
baada ya Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya
Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani
akiwasili nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere, Butiama Musoma akiwa ameambatana na watumishi wa NEC na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa ALAT
kutoka maeneo mbalimbali kuzuru kaburi
la Baba wa Taifa, Mwitongo wilayani Butiama. Tume ya Taifa ya Uchaguzi iko
mkoani Mara kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi.
Muongoza
wageni wa maeneo ya historia nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwitongo Butiama Bi.
Gaudensia Waziri akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima
Ramadhani (mwenye kofia) kuhusu Kaburi na historia ya Chifu Burito aliyekuwa chiefu
wa Kabila la Wazanaki.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani (Kushoto)
akisalimiana na Msemaji Mkuu na kiongozi wa familia ya Baba wa Taifa Chifu
Japhet Wanzagi (kulia) mara baada ya kuwasili eneo la Mwitongo wilayani
Butiama. Wa Pili kutoka Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Butiama Bi. Annarose
Nyamubi.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani akiwasha
mshumaa kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la
Mwitongo, Butiama. Wengine wanaoonekana na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa ALAT
na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Mwongoza
wageni na Mhifadhi wa Makumbusho ya Mwalimu Nyerere Butiama, Jacob Thomas akitoa
maelezo kuhusu picha za kumbukumbu za Baba wa Taifa kwa Mkurugenzi wa NEC Bw.
Kailima Ramadhani na watumishi wa NEC walioitembelea makumbusho hiyo eneo la
Mwitongo, Butiama –Musoma.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa NEC
waliotembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Mwitongo, Butiama.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi waandishi wa habari wa mkoa
wa Mara waliotembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere Mwitongo, Butiama. Watendaji wa NEC wako mkoani Mara kutoa elimu ya
mpiga kura kwa wananchi.
Na. Aron Msigwa –
NEC, Musoma.
Viongozi wa vyama vya
Siasa wametakiwa kuiga kwa vitendo uzalendo na moyo wa kujitoa aliokuwa nao Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere enzi za uhai wake ili
kuliwezesha Taifa kupiga hatua kimaendeleo.
Kauli hiyo imetolewa
na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima
Ramadhani mara baada kutembelea Kaburi na Makumbusho ya Baba wa
Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la Mwitongo wilayani Butiama.
Amesema
kuwa kumbukumbu
za Baba wa Taifa zilizohifadhiwa vizuri katika makumbusho hiyo zina
mambo mengi
ya kujifunza ambayo wanasiasa wanatakiwa kuyafanya kwa vitendo hasa
uzalendo kwa nchi, uvumilivu, upendo na moyo wa kujitoa kwa dhati
kuwatumikia
wananchi.
“Kupitia kumbukumbu
hizi sisi watumishi wa Tume tumejifunza ukomavu wa demokrasia aliokuwa nao
Mwalimu Nyerere akiwa ndani na nje ya Bara la Afrika, wengi wanadhani Demokrasia ni wakati wa
uchaguzi tu, kumbe demokrasia ni pamoja na kuheshimu watu wengine” Amesema
Kailima.
Ameeleza kuwa maisha
aliyoishi Baba wa Taifa ni mfano wa kuigwa na viongozi na watanzania wote hasa
pale alipojitofautisha na viongozi wengi wa Bara la Afrika alipoepuka tamaa ya madaraka
na mali kwa manufaa ya taifa.
“Sote ni mashahidi
kupitia kumbukumbu zake tumeona mahali alipokuwa anaishi mwalimu Nyerere kabla
hajajengewa nyumba na Jeshi, kama Rais
mstaafu wengi walitegemea asingeishi katika
eneo lile, kumbukumbu hii nzuri aliyoiacha inatufundisha watanzania kuwa
mwalimu aliitanguliza Tanzania mbele kuliko maslahi yake binafsi” Amesisitiza Kailima.
Bw. Kailima amebainisha
kuwa NEC itaendelea kumuemzi Baba wa Taifa kwa yale aliyoyafanya
na kuyasimamia kwa manufaa ya taifa huku akitoa wito kwa viongozi wa vyama vya Siasa wawe na kiasi na
waridhike na vile walivyonavyo.
“Suala la kuridhika na
kuwa na kiasi linapaswa kuzingatiwa, wanasiasa
wanapaswa kuwaheshimu wananchi wanaowachagua kupitia chaguzi mbalimbali,
matokeo yanapotoka kama ni sahihi basi
wanasiasa wakubaliane na maamuzi yao”
Ameainisha Kailima.
Kwa upande wake
Mhifadhi wa Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bw.
Jacob Thomas amesema kuwa watanzania
wanayo mengi ya kujifunza kupitia vitu alivyoviacha Baba wa Taifa ambavyo
vimehifadhiwa katika Makumbusho hiyo.
Amesema kuwa maisha
ya uadilifu aliyoishi enzi za uhai wake na mchango wake katika kuiletea
maendeleo Tanzania na Bara la Afrika vinapaswa kuenziwa kwa nguvu zote na
viongozi wa Tanzania.
“Ninyi mliopata nafasi
ya kuitembelea makumbusho hii mmejifunza vitu vingi kumhusu Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere kwamba alikuwa ni mtu wa namna gani kwa viwango vya Afrika na
dunia kutokana na kumbukumbu ya uadilifu aliyoiacha ndani na nje ya mipaka ya
Tanzania”
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey D.J Mwanri (Kulia)
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe akisoma Risala wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru
Baadhi ya wakuu wa Wilaya za mkoa wa Tabora wakiulaki mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili Mkoani humo
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey D.J Mwanri akisoma Risala wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru
Kutoka Kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi Bw Dandala Mzunguor, Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Fute Martin, Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe, na Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakijadili jambo muda mchache kabla ya
makabidhiano ya Mwenge wa uhuru
Kushoto
ni Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey D.J Mwanriakimkabidhi Mwenge wa Uhuru mkuu wa
Wilaya ya Igunga Mhe john Mwaipopo kwa ajili ya kushirikiana na
wakimbiza Mwenge Kitaifa kuukimbiza Wilayani humo
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji jumanne Mtaturu, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe,Mkuu
wa wilaya ya Iramba Emmanuel Uhahula, Mkuu wa wilaya ya Iramba, Injinia Masaka
John Masaka, Mkuu wa wilaya ya Singida Elias Choro Tarimo
Kutoka Kushoto ni Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew J. Mtigumwe, kulia ni Mkimbiza Mwenge Kitaifa George J. Mbijima
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akimuaga Mkimbiza
Mwenge Kitaifa lucia Vitalis kutoka Manyara mara baada ya kumaliza ziara
ya Mwenge katika Mkoa wa Singida na kuanza ziara Mkoani Tabora
Na Mathias Canal, Tabora
Mwenge wa Uhuru umewasili Mkoani Tabora ambapo unatarajiwa kuzindua
miradi 45 yenye thamani ya shilingi Bilioni ishirini na tatu, Milioni
nne, laki nne elfu na arobaini na saba mia tano sitini na sita
23,004,447,566/= ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 40% ukulinganisha
na miradi ya mwaka 2015 iliyokuwa na thamani ya shilingi 9,207,720,213.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha
Mgongolo, Kata ya Igunga, Wilayani Igunga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
D.J Mwanri amesema kuwa sera ya Vijana Tanzania ya Mwaka 2007 inatambua
kuwa vijana ni watu wote wenye umri wa miaka 15-35 ambapo kulingana na
sensa ya Mwaka 2012 inaonyesha kuwa Mkoa huo una jumla ya vijana 439,455
hivyo hekari 681 zimetengwa kwa ajili ya shughuli za vijana ili kukidhi
kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2016.
Mwanri alisema kuwa
Mwaka 2015 Mwenge wa Uhuru mkoani Tabora ulikimbizwa katika Halmashauri 7
zilizokuwepo ambapo Mwaka huu utakimbizwa katika Halmashauri 8 ambazo
ni Igunga, Nzega Mji, Tabora Vijijini (Uyui), Sikonge, Urambo, Kaliua,
Tabora Manispaa na Nzega Vijijini.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe
Aggrey Mwanri mara baada ya kukabidhiwa Mwenge huo naye amemkabidhi Mkuu
wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo ili aukimbize katika Miradi
iliyopangwa ukiwemo wa kuzindua Mradi wa maji Vijijini, Kufungua vyumba
viwili vya madarasa na choo cha matundu 10 katika Shule ya Sekondari
Mwayunge, Kuweka Jiwe la msingi katika Hoteli ya Mjasiriamali Zengo T.
Kija, Kuzindua mradi wa Kilimo cha bustani na Ufugaji wa samaki wa
kikundi cha Vijana cha Msongela, na Kuzindua zahanati ya Kijiji cha
Igogo.
Miradi mingine ambayo Mwenge wa Uhuru utazuru ni pamoja
na kugawa kadi za CHF kwa wanachama wapya, Kugawa vyandarua kwa wananchi
na baadaye utazuru katika Shule ya Sekondari Nanga.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa uongozi wa Mkoa wa Tabora, Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amewashukuru wananchi
wa Mkoa wa Singida kwa kujitokeza kwa wingi kutokana na juhudi na
ushiriki wao kwenye kuibua, Kutekeleza na Kusimamia miradi mbalimbali
ambapo pia amewataka wananchi hao kwa umoja wao kuitunza miradi hiyo.
Mtigumwe alisema kuwa tangu Mwenge wa Uhuru ulipokabidhiwa Mkoani
Singida ukitokea Mkoani Dodoma Septemba 17, 2016 umepita kwenye miradi
61yenye thamani ya Shilingi 14,266,628,518 iliyopo katika Halmashauri
saba ambayo ni pamoja na Mradi wa elimu, Afya, Maji, Barabara, Biashara,
Mazingira, Kilimo, Mifugo, Ushirika na programu mbalimbali za mapambano
dhidi ya Rushwa, Dawa za Kulevya, Ukimwi na Malaria.
Mtigumwe
alisema kuwa mbali na Mwenge wa Uhuru kupita kwenye Miradi mbalimbali
Mkoani Singida Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa amewaongoza wakimbiza
Mwenge wenzake kitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2016 ambao ni
"Vijana ni nguvu kazi ya Taifa, Washirikishwe na kuwezeshwa" Vile vile,
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa amesisitiza umuhimu wa vijana na
wananchi wote kwa ujumla kujiepusha na vitendo vya Rushwa, Dawa za
kulevya, Kuchukua hatua dhidi ya tabia hatarishi zinazoweza kuchochea
maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi na kutokomeza kabisa ugonjwa wa
Malaria.
Na Mathias Canal, Dodoma
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya wananchi (FDC)-CHISALU amekalia kuti kavu mara baada ya kubainika kuwa ameruhusu udahili wa wanafunzi wanaosoma fani ya utaalamu wa Kilimo na Mifugo ilihali chuo hicho ni maalumu kwa ajili ya mafunzo ya utaalamu wa Maendeleo ya jamii (Community Development).
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe Jabir Shekimweri amemsimamisha kazi Mkuu huyo kutokana na kupokea malalamiko ya baadhi ya wanafunzi chuoni hapo ambapo malalaniko yao yamekuwa na hoja za msingi zilizopelekea kuibuka kwa kadhia mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho.
Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa
(katikati) akiingia kwenye ukumbi wa Nyantale kwa ajili ya kufungua semina ya
ujasiriamali ya wanawake eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.
Wanawake wa Jimbo la Segerea wakiwa kwenye semina ya
ujasiriamali ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Wanawake wa Jimbo la Segerea wakiwa kwenye semina ya
ujasiriamali ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Ofisi ya Jimbo la
Segerea,Jacqueline,akizungumza na akinamama wa jimbo hilo kwenye semina ya
ujasiriamali.
Mkufunzi wa Elimu ya Utunzaji wa Fedha kutoka Benki ya
Equity,Daudi Mwashilindi,akitoa mada ya utunzaji wa fedha na mpangilio wa
mapato na matumizi jinsi inavyosaidia kwa wajasiriamali kukua kibiashara kwenye
semina hiyo.
Meneja wa Kanda ya Temeke wa Mfuko wa Pensheni wa
PPF,Erica Sendegeya,akizungumza na wanawake wajasiriamali umuhimu na faida ya
kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kwenye semina hiyo.
Mkufunzi wa Kujitegemea,Albert Magonga,akitoa mojawapo ya mada ya kuwawezesha
wanawake wajasiriamali kukua kiuchumi kupitia biashara zao.
Mkufunzi wa Elimu ya Utunzaji wa Fedha kutoka
Benki ya Equity,Daudi Mwashilindi,akitoa mada ya utunzaji wa fedha na mpangilio
wa mapato na matumizi
Mama mjasiriamali akichangia mada katika semina hiyo
Semina ikiendelea.
Wanawake wajasiriamali wa Jimbo la Segerea wakisikiliza
kwa makini wakufunzi waliokuwa wakizungumza kwenye semina ya ujasiriamali ya
kuwainua kiuchumi wanawake.
(PICHA ZOTE na SHUNDA BLOG )
Mwenyekiti wa Vikundi vya Wanawake Wajasiriamali wa Jimbo
la Segerea,Salma Fumbwe,akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la
Segerea,Bonnah Kaluwa (kushoto) katika semina ya ujasiriamali ya wanawake
iliyofanyika ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima,jijini Dar es Salaam,leo.
Kauli Mbiu ni Mwanamke Simama Inuka Piga Kazi”.
Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah
Kaluwa,akizungumza na wakinamama wajasiriamali wa jimbo lake kwenye semina ya
ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale,Tabata Bima
jijini Dar es Salaam leo.
Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah
Kaluwa,akizungumza na wakinamama wajasiriamali wa jimbo lake kwenye semina ya
ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale,Tabata Bima
jijini Dar es Salaam leo.
Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah
Kaluwa,akizungumza na wakinamama wajasiriamali wa jimbo lake kwenye semina ya
ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale,Tabata Bima
jijini Dar es Salaam leo.
Na Elisa Shunda
WANAWAKE washauriwa kutenganisha fedha ya msingi wa
biashara na fedha ya matumizi mbalimbali ya nyumbani ili kuboresha na kusonga
mbele kiuchumi tofauti na wakichanganya watakuwa wanadumaza biashara zao na
matokeo yake kupata hasara inayopelekea kusimamisha biashara anayoifanya.
Hayo yamezungumzwa na wakufunzi mbalimbali waliokuwa
wakitoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake kwenye semina yenye ujumbe wa kauli
mbiu ya Mwanamke Simama Inuka Piga Kazi iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la
Segerea,Bonnah Kaluwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata
Bima jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza kwenye semina hiyo mbunge wa jimbo
hilo,Bonnah Kaluwa,alisema kuwa ameamua kuandaa semina ya ujasiriamali ya
wanawake kwa ajili ya kuwapatia elimu mbambali za ujasiriamali pamoja na elimu
ya utunzaji wa fedha za biashara kwenye sehemu yenye uhakika pasipokuwa na
shaka wala wizi kwa kuwaletea benki ya Equity na Mfuko wa hifadhi ya Jamii ya
PPF ambao watawasaidia kuwahifadhia fedha zao pamoja na kuwapatia bima ya afya
na fao la kustaafu endapo watakidhi vigezo.
“Wakinamama nimefurahi kwa jinsi mlivyojitokeza kwenye
semina hii natumaini tukimaliza hapa kila mmoja wetu atakuwa amepata elimu ya
kutosha kuhusiana na masuala ya ujasiriamali likiwemo la kutofautisha fedha ya
matumizi ya nyumbani na fedha ya biashara kwa kuwa ukipata elimu ya
kutenganisha vitu hivyo utaendelea kwenye biashara yako huwezi kutoa fedha ya
biashara kununua chakula au kumsomesha mtoto lazima utayumba hivyo ni bora kila
mtu ategeshe sikio lake vizuri kusikiliza elimu itakayotolewa hapa ambayo
itatufumbua kutofautisha masuala ya nyumbani na biashara ambayo itatusaidia
sana kufikia kwenye malengo yetu” Alisema Kaluwa
Aidha akitoa elimu ya ujasiriamali kwenye semina
hiyo,mkufunzi wa kujitegemea,Albert Magonga,alisema kuwa huwezi kuwa
mjasiriamali halafu huweki mazingira ya kuonyesha bidhaa zako kwa majirani yako
wanaokuzunguka na pia ni vyema mjasiriamali kuwa mbunifu wa kutambua eneo
unaloishi ni kitu gani ambacho ni adimu ili uanzishe upate wateja wako ambao
watanunua biashara yako kutokana na jinsi unavyokiandaa.
Naye Mkufunzi wa utunzaji wa fedha kutoka benki ya
Equity,Daudi Mwashilindi,alisema kuwa watu wengi wanaokopa fedha katika taasisi
mbalimbali nchini wana mapungufu ya kutokuwa na elimu ya fedha jinsi ya
kuitumia akatolea mfano benki yao wanakopesha hadi maprofesa ambao wanaaminika
wana upeo mkubwa wa kufikiri lakini kutokana na kutokuwa na elimu ya fedha
wanashindwa kutumia vizuri fedha walizokopa mwisho wanauza nyumba yake ili
kurudisha kiasi cha fedha walizomkopesha.
“Unapotaka kwenda kukopa katika taasisi yoyote ya fedha
ni lazima uwe na elimu ya matumizi ya fedha la sivyo utaishia pabaya kwa mfano
benki yetu ya Equity tunakopesha hadi maprofesa ambao tunaamini wana upeo
mkubwa wa akili ila kutokana na kutokuwa na elimu ya utunzaji na utumiaji wa
fedha wanashindwa kurudisha fedha zetu tunauza nyumba yake kwa ajili ya
kurudisha kiasi cha fedha tulizomkodisha,hivyo ninyi leo mnapata elimu ya kujua
bajeti yako na mapangilio wa mapato na matumaini ikiwemo na daftari la biashara
zako ili kujua mahesabu yako” alisema Mwashilindi.
Akaongeza kwa kusema mjasiriamali bora anapaswa kupata
taarifa sahihi kutoka kwenye vyombo vya habari ni fursa kwake akatolea mfano
ukipata taarifa ya habari kuwa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa mwezi wa kumi
kutakuwa na joto kali wewe kama mfanyabiashara kutokana na taarifa hiyo lazima
apange biashara ya kuuza vitu vinavyoendana na kipindi hicho kwa kufanya
biashara kama Soda,Maji na Juice.
Kwa
upande wake Meneja wa Kanda ya Temeke wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,
Erica Sendegeya,aliwashauri akinamama wajasiriamali kujiunga na
mfuko huo utakaowasaidia mambo mbalimbali ikiwemo la masuala ya afya kwa
kupata
vitambulisho vya NHIF kwa bei nafuu na kuwaambia mfuko wa PPF ukichangia
kwa
takribani miaka 15 kwa kila mwezi shilingi 20000 unaingizwa kwenye fao
la
pensheni hivyo aliwataka wakinamama hao kujiunga na mfuko huo.
Semina hiyo ya ujasiriliamali kwa wanawake wa jimbo la
Segerea itawezesha kuwapatia elimu ya utunzaji wa fedha akinamama zaidi ya 500
ambao wapo kwa kanda mbili ambapo mkutano huu wa mwanzo ulifanyika kwenye jimbo
hilo kwa kanda ya A ambapo baadae kanda B nao watapatiwa elimu hiyo kupitia
ufadhili wa benki ya Equity na Mfuko wa Hifadhi ya jamii kushirikiana na ofisi
ya jimbo la Segerea.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akilakiwa
na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipofika kwenye Ofisi ndogo za makao
makuu ya chama hicho mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam Septemba 24, 2016.(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiongozana na mgeni wake Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuelekea ofisini kwake
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai
akimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman
Kinana alipomtembelea na kuzungumza naye katika Ofisi Ndogo za
CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai
akiagana na Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka mara baada
ya kuzungumza na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana katika Ofisi
Ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam.
SHIRIKA
la Umeme Tanzania ( TANESCO) linapenda kuwataarifu wateja wake wa
Mkoa wa Dar es Salaam kuwa leo Jumamosi tarehe 24/09/2016 kumetokea hitilafu katika Kituo kikubwa cha kupooza na kusambaza Umeme cha Ubungo 220kV/ 132kV na kusababisha kukosekana Umeme kwenye maeneo ya jiji la Dar es Salaam yanayotegemea Vituo vya Kumduchi na Makumbusho.
Mkoa wa Dar es Salaam kuwa leo Jumamosi tarehe 24/09/2016 kumetokea hitilafu katika Kituo kikubwa cha kupooza na kusambaza Umeme cha Ubungo 220kV/ 132kV na kusababisha kukosekana Umeme kwenye maeneo ya jiji la Dar es Salaam yanayotegemea Vituo vya Kumduchi na Makumbusho.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu jijini
mapema leo, tayari hatua za kurekebisha hitilafu hiyo zinaendelea kuchukuliwa ambapo
mafundi wa TANESCO wanaendelea na kazi ya kurekebisha hitilafu hiyo na umeme
utarejea masaa machache yajayo.
Taarifa
hiyo inawaomba radhi wananchi kutokana na usumbufu wowote utakaojitokeza.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya wananchi (FDC)-CHISALU amekalia kuti kavu mara baada ya kubainika kuwa ameruhusu udahili wa wanafunzi wanaosoma fani ya utaalamu wa Kilimo na Mifugo ilihali chuo hicho ni maalumu kwa ajili ya mafunzo ya utaalamu wa Maendeleo ya jamii (Community Development).
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe Jabir Shekimweri amemsimamisha kazi Mkuu huyo kutokana na kupokea malalamiko ya baadhi ya wanafunzi chuoni hapo ambapo malalaniko yao yamekuwa na hoja za msingi zilizopelekea kuibuka kwa kadhia mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho.
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira
Mngalu akikabidhi mifuko ya saruji na vifaa mbalimbali kwa ajili ya
ujenzi wa vyoo kwa Bw.Herry Mjengelaungu Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo ya
Jamii Kisarawe katika hafla iliyofanyika chuoni hapo leo kutoka kushoto
ni Katibu Tawala wa wilaya ya Kisarawe Bw. Mtera Mwampamba na Mkuu wa
wilaya ya Kisarawe Bi. Happiness Saneda.
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira
Mngalu akizungumza na wakufunzi na wanafunzi wa Chuo Cha Maendeleo ya
Jamii Kisarawe kabla ya kukabidhi vifaa katika chuo hicho kulia ni Mkuu
wa wilaya ya Kisarawe Mh. Happiness Saneda.
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira
Mngalu akipiga picha na mkuu wa chuo hicho pamoja na wakufunzi mara
baada ya makabidhiano.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Pwani kupitia CCM Mh. Subira
Mngalu akizungumza na Mkuu wa wilaya hiyo Bi. Happiness Sanneda wakati
wakikagua maeneo ya chuo hicho kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Bw. Herry
Mjengelaungu.
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akikagua chumba cha kompyuta.
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo angalia.
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira
Mngalu akikagua mabweni ya chuo hicho kutoka kwa mkuu wa chuo Bw. Herry
Mjengelaungu.
...................................................................................
NA MWANDISHI WETU
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu(CCM) ametoa msaada
wa vifaa za ujenzi wa vyenye thamani ya sh. milioni moja kwa Chuo
Maendeleo ya Wananchi(FDC) Kata ya Kazimzumbwi, Kisarawe mkoani
Pwani.
Subira alimkabidhi msaada wa vifaa hivyo ambavyo ni
saruji,mchanga,mbao, matofali, nondo na kokoto kwa ajili ya kusaidia
ujenzi wa choo cha wavulana baada ya cha awali kubomoka na wanafunzi
kulazimika kutumia choo kimoja cha wasichana.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo jana, Subira alisema
anaamini ujenzi wa choo hicho utakamilika mapema kwa kuwa unafanywa na
nguvu kazi ya vijana wenyewe chini ya usimamizi wa wakufunzi wao.
Mbunge huyo alisema kwamba anatambua kwamba ana wajibu wa kuhakikisha
afya za vijana wanaosoma chuoni hapo zinakuwa salama hivyo ametoa kama
kiongozi na mzazi wa watoto hao.
Alisema aliguswa baada ya kutembelea chuo hicho mwezi mmoja uliopita
na kuona changamoto nyingi zinazowakabili wanafunzi na watumishi wa
chuo hicho ambapo alihidi kusaidia na kuhamasisha viongozi wengine
wafike chuoni hapo.
Subira alisema vyuo hivyo na vyuo vya ufundi vilivyopo chini ya VETA
ni muhimu hususan wakati huu ambao nchi inaelekea kwenye uchumi wa
viwanda,vyuo hivyo ndivyo vitakavyozalisha wataalamu watakaofanya kazi
kwenye viwanda.
Alisema vyuo hivyo ambavyo kwa Mkoa wa Pwani vipo Kibaha, Kisarawe na
Ikwiriri wilayani Rufiji, miundombinu yake ni chakavu na wanakabiliwa
na changamoto nyingi hivyo wakati serikali inaangalia namna, viongozi
na wadau wanapaswa kusaidia.
Mbunge huyo alimuomba Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happines Senada na
uongozi wa halmashauri kuwatumia vijana wa chuo hicho kuwapa kazi
hususan za ujenzi wa vyoo vya shule za msingi ili kusadia vyuo hivyo
na kwamba sheria ya manunuzi imeruhusu kutumia makundi maalumu ya
vijana na wanawake.
Awali akizungumza na wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho Mkuu wa
Wilaya, Happines alisema chuo hicho kina umuhimu mkubwa hivyo
atahakikisha changamoto zinazowakabili zinatatuliwa kwa kushirikiana
na wadau.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Heri Mjengelaungu, alisema chuo
hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo miundombinu chakavu,
tatizo la maji, umeme, vifaa vua kufundishia kwa vitendo , haina
magari.
Alimshukuru mbunge huyo kwa msaada wake wa vifaa vya ujenzi wa choo
hicho kwa kuwa hali ni mbaya hivyo watahakikisha kwa kushirikiana na
wanafunzi na wakufunzi choo hicho kinakamilika mapema zaidi kwa kuwa
shimo limeshachimbwa.
WAZIRI Mkuu wa zamani
wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CHADEMA, Edward Lowassa amewatembelea
wananchi wa mji wa Bukoba walioathirika na tetemeko la ardhi na kuwasihi
Watanzania kuwasaidia wananchi hao kama ilivyo desturi yetu.
Akizungumza na Mkuu wa
Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu) Salum Kijuu Septemba 10, 2016 alipofika
Ofisini kwake kumpa pole kufuatia tetemeko hilo lililotokea Septemba 10, 2016
na kuua watu 17. Lowassa alisema, amefika mkoani humo ili kutoa mkono wa pole
kufuatia maafa hayo na kumpapole Mkuu wa mkoa huo kwa niaba yawananchi wa mkoa
wa Kagera.
“Nawasihi watanzania wenzangu tuendelee
kujitolea kuwasaidia wahanga kama ilivyo desturi ya umoja wa kitaifa tulionao”.
Ameandika Lowassa katika ukurasa wake wa Tweeter.
Baada ya kuona hali
ilivyo sasa kwa baadhi ya wakazi wa mkoa huo kupoteza ndugu zao, nyumba na mali
zao kuharibika, Lowassa ametumia ukurasa wake wa Twitter kufikisha ujumbe kwa
jamii ya watanzania sehemu yoyote walipo duniani kote.
Ujumbe wa kwanza
Lowassa aliandika “Poleni ndugu zangu Wa Kagera na mlioathirika na tetemeko,
Tupeane nguvu ili tuvuke katika kipindi hiki kigumu pamoja”
Lowassa akizungumza na wakazi wa Hamugembe, baada ya kutembelea eneo hio lililoathirika sana na tetemeko hilo
No comments:
Post a Comment