Pages

Monday, September 26, 2016

CHINA DONATES US$200, 000 TO EAC FOR INTER-BURUNDI DIALOGUE


WANAWAKE WA MANCHESTER CITY WATWAA UBINGWA WA SUPA LIGI

MCHEZAJI NYOTA MKONGWE MAREKANI ARNOLD PALMER AFARIKI DUNIA

EALA JOINS PUSH FOR LEGISLATIVE POWERS AT ECOWAS PARLIAMENT

The Speaker of EALA, Rt Hon Daniel Fred Kidega (right) and the President of the ECOWAS Commission pay attention to the proceedings at the commencement of the 2nd Ordinary Session of ECOWAS Parliament in Abuja yesterday
A section of the ECOWAS Parliamentarians follow the proceedings yesterday
The EALA Speaker, Rt Hon Daniel Fred Kidega delivers his speech at the 2nd Ordinary Session of the ECOWAS Parliament in Abuja, Nigeria. The Speaker called for more legislative powers for ECOWAS Parliament.
The Speaker of EALA fields questions from the Nigeria Media. On right is the President of the Pan-African Parliament, H.E. Roger Nkodo Dang
The EALA Speaker, Rt Hon Daniel Fred Kidega says the time for the Economic Community of West African States’ (ECOWAS) Parliament to get Legislative powers is now, Such a move, Rt Hon Kidega notes would be a precursor to capacitate the Legislature to enact laws and respond to demands of the populace of the West African region. Consequently, the EALA Speaker is urging the 4th Legislature to up the push on the adoption and signing of the Supplementary Act on the Enhancement of powers of the said Parliament.

Rt Hon Daniel Fred Kidega made the remarks on September 22, 2016, as he delivered a solidarity message to the Assembly at the commencement of the 2nd Ordinary Session of the ECOWAS Parliament at the Parliamentary buildings in Garki, Abuja, Nigeria.

He further remarked that it was in the best interest of the bloc to speed up integration to realise the aspirations of the founding fathers of ECOWAS and those of its citizens.

“In order to realise integration to its fullest, this may perhaps be – an opportune moment for the ECOWAS Parliament to transform itself into a legislative body capacitating it to enact laws that can influence change and to respond to the demands of the populations”, the Speaker said.

“I recall with vigour the 3rd Legislature had sought the enhancement of its powers to include the power to legislate in co-decision with the Council of Ministers, representation, budget appropriation and confirmation of statutory appointees of the Community Institutions. 


The 4th Legislature continues with the spirited campaign for the adoption and signing of the Supplementary Act on the Enhancement of the Powers of the Parliament, which shall give ECOWAS Parliament the desired legislative powers, an initiative that EALA totally and fully supports”, the Speaker added

NAIBU WAZIRI MH.ANASTAZIA WAMBURA AMEWAAGIZA WASANII KUSAJILI KAZI ZAO BASATA.

bur1
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura akizungumza na Wasanii kuhusu umuhimu wa kusajili kazi zao wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza laTaifa la Sanaa (BASATA) pamoja na Kampuni ya Haak Neel Production lililofanyika Septemba 24 Jijini Dar es Salaam.
bur2
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Muingereza akitoa maelezo mafupi kuhusu siku ya Msanii Duniani wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza hilo pamoja na Kampuni ya Haak Neel Production lililofanyika Septemba 24 Jijini Dar es Salaam.
bur3
Mkurugenzi wa Kampuni ya Haak Neel Production Bw. Emmanueli Maendeka akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wa Kampuni yake katika uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa pamoja na Kampuni yake lililofayika Septemba 24 Jijini Dar es Salaam.
bur4
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura akiangalia baadhi ya kazi za Sanaa kutoka kwa Wasanii wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza la Taifa la Sanaa (BASATA)pamoja na Kampuni ya Haak Neel Production lililofanyika Septemba 24 Jijini Dar es Salaam.

WALIMU ARUSHA WALIPWA STAHIKI ZAO

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akiwa anaongea na waandishi wa habari ofisini kwake
Waandishi wa habari wakifatilia mkutano wa mkuu wa wilay

SERIKALI YATAKIWA KUANISHA KODI ZOTE ZA HIFADHI ZETU NA KUWEKA KATIKA MFUMO MMOJA ILI KUWEZA KUPUNGUZA USUMBUFU UNAOJITOKEZA MARA KWA MARA

 Mwenyekiti Wa chama cha wasafirishaji Wa utalii (TATO) wilbroad chambulo akichangia mada wakati wa mkutano
Mkutano uliandaliwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wa wadau wa utalii walikutana kujadili changamoto na Tathimini zinazokabili sekta hiyo .
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kushoto akiwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Fabian Daqarro wakifatilia mjadala uliokuwa ukiendelea

WEST HAM YAZIDI KUPOKEA VIPIGO KATIKA LIGI KUU YA UINGEREZA

MAONESHO YA UJASILIAMALI IRINGA YAFANA


Mkuu wa wialaya Mh Richard Kasesela akitoa hotuba wakati wa maonesho ya wajasiliamali aliyoyaandaa katika barabara ya Olofea Manispaa ya Iringa.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Amina Masenza amefungua maonesho ya wajasiliamali yalioandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela katika barabara ya Olofea Manispaa ya Iringa. 

Akifungu Maonyesho hayo, aliwaasa wana vikundi kuwa na umoja ili kufanikisha ndoto zao. Pia aliagiza benki ya Posta kuhakikisha wanawasaidia mikopo wajasiliamali hayo. 

Mapema akimkaribisha Mkuu wa mkoa , Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alimshukuru Mkuu wa mkoa kwa kukubali kuwa mgeni rasmi na kumuomba maonesho hayo yawe yanafanyika mara kwa mara ili wajasiliamali wapate soko na kujikwamua kwa uchumi. 

Meneja wa Benki ya Posta Mkoa wa Iringa Bwana Kayanda aliwambia wajasiliamali pesa ipo, ila wakopaji ndio hakuna hivyo anawakaribisha waje kukopa. 

Zaidi ya wajasiliamali 600 walipata mafunzo yaliyoandaliwa na Mh Kasesela hapo tarehe 18/8/16, na leo ilikuwa siku ya kuonyesha bidhaa hizo. 

Pia kilikuwepo kikundi ambacho kinatengeneza mipira ya kuchezea mpira wa miguu cha kata ya Ruaha.
Mkuu wa mkoa Bi Amina Msenza akipata maelezo kutoka kwa wajasiliamali baada ya ufunguzi wa amonyesho hayo.
Mkuu wa wilaya akicheza mpira uliotengenezwa na wajasiliamali wa Ruaha Iringa

CRISTIANO RONALDO ACHUKIZWA KUTOLEWA NJE WAKATI REAL MADRID IKITOKA SARE

RAIS DK. SHEIN AKUTANA NA MADAKTARI BINGWA WA UPASUAJI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Rais wa Taasisi ya Mendeleo ya Elimu inayohusiana na Mishipa ya fahamu,Uti wa Mgongo na Vichwa maji (NED) Dk.Jose Picer akiwa na Makamo wa Rais wa taasisi hiyo Dk.Mohamed Qureish walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.] 24/09/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Rais wa Taasisi ya Mendeleo ya Elimu inayohusiana na Mishipa ya fahamu,Uti wa Mgongo na Vichwa maji (NED) Dk.Jose Picer alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.] 24/09/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Rais wa Taasisi ya Mendeleo ya Elimu inayohusiana na Mishipa ya fahamu, Uti wa Mgongo na Vichwa maji (NED) Dk.Jose Picer (katikati) akiwa na Makamo wa Rais wa taasisi hiyo, Dk.Mohamed Qureish (kushoto) walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.] 24/09/2016.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imeokoa kiasi cha Tsh. Bilioni 9.7 kutokana na upasuaji wa maradhi ya mishipa ya fahamu, uti wa mgongo na vichwa maji uliofanywa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja tokea kuanzishwa kwa huduma hizo miaka miwili iliyopita.

Hayo yalielezwa leo Ikulu mjini Zanzibar katika mazungumzo yaliofanywa kati ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu inayohusiana na upasuaji wa Mishipa ya Fahamu, Uti wa mgongo na Vichwa maji (NED) Dk. Jose Picer akiwa na Makamo wa Rais wa Taasisi hiyo Dk. Mahmood Quiresh.

Katika mazungumzo hayo ambapo Madaktari hao bingwa walikuwa wameongozana na uongozi wa Wizara ya Afya chini ya Waziri wa Wizara hiyo Mahmoud Thabit Kombo, ambao walipongeza mashirikiano makubwa wanayoyapata katika kutekeleza shughuli zao hapa nchini.

Pamoja na hayo, madaktari hao walieleza kuwa miongoni mwa mafanikio makubwa yaliopatikana kutoka kwa Taasisi hiyo ni pamoja na kufanya upasuaji huo kwa wananchi wa Zanzibar wapatao 500 wakiwemo watoto, wanawake na watu wazima.

Madaktari hao walimueleza Dk. Shein kuwa gharama hizo ni kwa ajili ya taaluma na upasuaji mbali na gharama nyengine ambazo Serikali ingeweza kutumia katika usafirishaji, gharama za malazi na chakula kwa wagonjwa na wauguzi wao pale wanapowasafirisha kwenda nje ya nchi

No comments:

Post a Comment