Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu
wa nchi mbalimbali wanaoshiriki katika Mkutano wa TICAD 6 kwenye
Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyeatta (KICC) jijini Nairobi
Agosti 28, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
katika Mkutano wa TICAD 6 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano
cha Kenyatta (KICC) jijini Nairobi Agosti 28, 2016. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
katika Mkutano wa TICAD 6 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha
Kenyatta (KICC) jijini Nairobi Agosti 28, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akimsikiliza kwa
makini Bi. Rehema Kabuye (katikati) aliyekua akilia kwa uchungu,
akimsihi Waziri huyo wa Fedha na Mipango, amsaidie ili mume wake ambaye
ni Nahodha wa meli ya MV Liemba pamoja na wafanyakazi wengine wa Mamlaka
ya Huduma za meli mkoani Kigoma, walipwe mishahara yao ya miezi nane
ili kuwaondolea adha ya maisha inayowakabili wao na familia zao
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akionesha rundo la
makaratasi yaliyoandikwa hoja na kero mbalimbali za wafanyabiashara wa
mjini Kigoma, wakati wa mkutano kati yake na wafanyabiashara hao,
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na Askofu Dkt. Gerard Mpango, baada ya kumalizika
kwa mkutano wake na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mjini Kigoma,
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
BMU YATEKETEZA ZANA ZA UVUVI HARAMU MASANZA.
Na Shushu Joel, Rweyunga Blog - BUSEGA.
UONGOZI wa uangalizi wa mazingira ya mwalo katika kijiji cha Ijitu kata ya Kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu wameteketeza vyavu haramu aina ya makokolo kwa makusudi ya kuteketeza uvuvi haramu katika wilaya hiyo.
Akizungumza wakati wa uchomaji wa zana hizo Katibu wa Beach Management Unity( BMU) Adam Abel alisema kuwa makokolo ni nyavu ambazo ni hatari sana kwa mazalia ya viumbe viishivyo majini, kwani katika uvuvi wake ukokota kila kitu kilichoma ndani ya maji na hii inasababisha hasara kubwa kwa jamii husika na taifa kwa ujumla.
“Tumeamua kufanya hivi ili kuleta unafuu kwa wananchi na wavuvi wanatumia zana ambazo ni halali kwa jamii pia hii itaiongezea taifa pato kutokana na uzalishaji wa samaki wanaotakiwa kusafirishwa nje kuwa na tija na hata wale wadogo kukua bila kuwa na buguza ya aina yeyote ile”
Aliongeza kuwa makokolo yaliyochomwa ni mali ya Bi Yulitha Godfrey mkazi wa Bukome (37) ambaye alikuwa akifanya shughuli zake za uvuvi haramu katika maeneo mbali mbali ya ziwa victoria.
Aidha katibu huyo alisema kuwa anawataka wale wote wanaotumia zana za uvuvi haramu wazisalimishe wenyewe katika ofisi za BMU ili kuwapunguzia buguza viongozi wao wa serikali kwani wanapaswa kutambua kuwa sasa hivi ukikamatwa na zana hizo unataifishwa na kila kitu ambacho ulikuwa ukitumia katika kazi zako za uvuvi huo haramu.
Abel pia amempongeza diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya, Vumi Mgulila kwa ushirikiano ambao anawapatia katika kufanikisha agizo la Rais la kuteketeza zana haramu katika ziwa Victoria.
Kwa upande wake Yohana Peter ameupongeza uongozi huo kwa juhudi zake za kuhakikisha uvuvi haramu unatokomezwa katika wilaya ya Busega.
Aliongeza kuwa ili wafanikiwe zaidi, inawabidi wawashirikishe wananchi ili waweze kuwa wanawapa siri za wale wanaofanya uvuvi huo usiokubalika katika nchi.
Nyasato Maingu ni mfanya biashara mdogo wa samaki maarufu chinga ambaye ununua samaki kwa wavuvi na kisha kwenda kupima katika mizani anaeleza kuwa ni jambo la pongezi kwa Rais Magufuli kwa kutambua thamani ya ziwa pamoja na viumbe vilivyoma na hii itaifanya Tanzania kuongezeka kwa upatikanaji wa samaki kwa wingi kwani wale wadogo watakuwa hawavuliwi kiholela

RAPA DRAKE ABAINISHA KUWA ALIMZIMIA RIHANNA TANGU AKIWA NA MIAKA 22
Rapa Drake amebainisha mbele ya
dunia kuwa alikuwa anampenda Rihanna tangu akiwa na umri wa miaka 22,
kauli ambayo ameitoa wakati akimkabidhi Rihanna tuzo ya video ya
Michael Jackson ya Vanguard jana usiku.
Rapa huyo mwenye umri wa miaka 29,
ambaye amekuwa akihusishwa kimapenzi na mwanamuziki Rihanna,
amebainisha hilo wakati akiwa jukwani akiwa amevalia suti aina ya
tuxedo akiwa na tuzo hiyo mkononi.
Rihanna na Drake wakipozi pamoja baada ya kumpatia tuzo hiyo
Drake akimshika mkono mpenzi wake Rihanna wakiondoka jukwaani baada ya kumpatia tuzo
Rihanna akitumbuiza katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo za MTV
Rihanna alitumbuiza nyimbo mbalimbali katika tuzo hizo za MTV
Rihanna akitumbuiza katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo za MTV
Rihanna alitumbuiza nyimbo mbalimbali katika tuzo hizo za MTV
IVAN RAKITIC AIPATIA BARCELONA POINTI TATU MUHIMU
Mchezaji Ivan Rakitic ameipatia
Barcelona ushindi muhimu baada ya mshambuliaji Luis Suarez kushindwa
kuonyesha makali yake katika mchezo dhidi ya Athletic Bilbao.
Ivan Rakitic aliifungia Barcelona
goli pekee katika mchezo huo mnamo dakika 21, akiunganisha kwa kichwa
mpira wa krosi uliopingwa na Luis Suarez.
Luis Suarez akifanya vitu vyake licha ya kushindwa kufunga goli
Beki wa Athletic Bilbao akimshika jezi Lionel Messi ili asikatize na kuleta madhara
MATUKIO MKUTANO WA WAFANYABIASHARA KIGOMA NA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO
MANCHESTER CITY YAENDELEZA UBABE, MIDDLESBROUGH YATOKA SARE
Timu
ya Manchester City imeendeleza wimbi la ushindi na kuongoza Ligi Kuu
ya Uingereza kwa tofauti ya idadi ya magoli baada ya kuifunga West
Ham kwa magoli 3-1.
Katika
mchezo huo Manchester City walikuwa wa kwanza kufunga goli kupitia
kwa Raheem Starling na kisha baadaye Fernandinho aliongeza la pili
kwa mpira wa kichwa.
Michail
Antonio alipunguza tofauti ya magoli baada ya kuifungia West Ham
katika kipindi cha pili, kabla ya Sterling kufunga la tatu katika
dakika ya 90.
Fernandinho akiruka juu na kupiga mpira wa kichwa uliozaa goli la pili la Manchester City.
Timu
ya Middlesbrough imeendeleza rekodi yao ya kutofungwa katika Ligi Kuu
ya Uingereza baada ya kutoka sare tasa na timu ya West Brom hii leo.
Katika
mchezo huo beki wa kushoto Brendan Galloway alipata nafasi nzuri ya
kufunga katika kipindi cha kwanza baada ya kupanda mbele lakini kipa
wa Middlesbrough Brad Guzan alikuwa imara.
Kipa Brad Guzan akizuia mpira uliopigwa na James McClean
WEST HAM YANAMNASA MSHAMBULIAJI SIMONE ZAZA
Timu
ya West Ham ya Uingereza imeinasa saini ya mshambuliaji wa Italia
Simone Zaza akitokea Juventus kwa mkopo wa msimu mzima wa kiasi cha
paundi milioni 4.3.
Makubaliano
hayo ya kumtwaa Zaza yanaweza kuwa ya kudumu na kufikia ada ya paundi
milioni 17, na nyongeza ya milioni 2.5 kulingana na atakavyokuwa
anashuka dimbani.
Usajili
huo ni wa 11 kwa West Ham katika majira ya joto, na umefikisha kiasi
cha paundi milioni 60 zilizotumika kwa usajili.
UZINDUZI WA DR.AMON MKOGA FOUNDATION SOUTHERN SUN HOTEL TAREHE 25/8/2016
Pichani ni Mwenyekiti wa Dr.Amon Mkoga Foundation na Bw.Habibu Msammy (Mwenye miwani), mwakilishi wa Katibu mkuu wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo pembeni ni Bw.Basel Haydar na Meneja wa shirika la Ndege la Qatar nchini Tanzania ambao ni wadhamini wa kuu wa mradi wa madawati uitwao Simama kaa desk campaign ambao unaendeshwa na Taasisi hiyo.
Mradi huo mwenye lengo la kupunguza uhaba wa madawati unadhaminiwa pia na Halotel, Empress Furniture, TIRA, CBA Bank, Insignia,tayari mikoa ya Tabora na Pwani wameanza kufaidi matunda ya mradi huo
REAL MADRID IKIWA BILA RONALDO YAIFUNGA CELTA VIGO
Mjerumani
Toni Kroos ameifungia Real Madrid goli la ushindi dhidi ya Celta Vigo
katika mchezo uliomalizika kwa ushindi wa magoli 2-1.
Katika
mchezo huo, Alvaro Morata, aliipatia Real Madrid goli la kwanza mnamo
dakika ya 60, hata hivyo Fabian Orellana aliisawazishia Celta Vigo
kwa goli safi.
Toni
Kroos aliifanya Real Madrid iongoze kwa shuti la karibu katika dakika
ya 81 baada ya James Rodriguez aliyetokea benchi kutumia mwanya wa
makosa na kuchangia goli hilo.
Toni Kroos akiachia shuti lililoipa Real Madrid goli la ushindi
Mchezaji nyota wa Real Madrid Gareth Bale akiruka juu na kupiga mpira kwa kichwa
No comments:
Post a Comment