Pages

Tuesday, August 2, 2016

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, RAMO MAKANI AONGEA NA WANANCHI WA KONDOA VIJIJINI KUHUSU UTATUZI WA MGOGORO WA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kulia) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Keikei Wilayani Kondoa jana kwa ajili ya kusikiliza kero zao mbalimbali kuhusu Pori la Akiba Mkungunero. Wananchi hao wameiomba Serikali iwape maeneo kwa ajili ya Kilimo, Ufugaji na Makazi kutokana na uhaba wa ardhi katika maeneo hayo.

Naibu Waziri Makani aliwaomba wananchi hao kuwa na subira wakati huu Serikali inapoenda kushuulikia maombi yao ambapo tayari imeshaundwa tume ambayo ipo chini ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kukusanya takwimu mbali mbali ikiwemo mahitaji halisi ya ardhi na idadi ya watu ambapo zitatumika katika kutatua changamoto zilizopo.

Alieleza kuwa Serikali ya awamu ya tano imepanga kutatua kero mbalimbali za  wananchi ambapo tayari migogoro yote ya ardhi nchini imeshaorodheshwa kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu, ambapo kitaundwa kikosi kazi cha kitaifa kitakachohusisha Wizara ya Ardhi, Kilimo, Maliasili, Tamisemi, Sheria na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.

Eng. Makani alisema kuwa Tanzania bado ina maeneo mengi ambayo yanaweza kutumika kwa ajili ya kilimo na ufugaji, hivyo kumega hifadhi ili kukabiliana na tatizo uhaba wa ardhi itakuwa jambo la mwisho kufanyika baada ya maeneo mengine kuzingatiwa. Aliitaka tume iliyoundwa kukamilisha kazi yake haraka ili changamoto hiyo iweze kupatiwa ufumbuzi na mamlaka husika.

Pori la Akiba Mkungunero lilitangazwa rasmi na Tangazo la Serikali la mwaka 1996 na zoezi la kutafsiri mipaka husika likafanyika mwaka 2006. Tangu hapo ukaanza mgogoro kati ya wananchi na hifadhi kwa madai kuwa baadhi ya vitongoji vya vijiji vyao halali vipo ndani ya hifadhi hiyo. 
Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini, Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (kulia) ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango akizungumza na wananchi wa Jimbo lake wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika kijiji cha keikei Wilayani Kondoa.


 Dkt. Kijaji aliwasilisha kero na changamoto mbalimbali za wananchi wake, moja ikiwa ni uhaba wa maeneo kwa ajili ya kilimo na ufugaji,  maeneo ya vijiji halali vilivyopimwa kudaiwa kuwemo ndani ya hifadhi na mahusiano mabaya kati ya wananchi wake na watumishi wa Pori la Akiba Mkungunero.

Akijibu changamoto hizo, Naibu Waziri Makani aliahidi kuzifanyia kazi kwa mujibu wa sheria za nchi na taratibu zilizowekwa mara baada ya tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa kukamilisha kazi yake na kukabidhi taarifa na mapendekezo yake Wizarani.  Aliongeza kuwa kumega maeneo ya hifadhi haiwezi kuwa jibu pekee la changamoto zinazowakabili wananchi bali wanaweza kutumia maeneo madogo waliyonayo kwa kuweka mipango mizuri ikawa na tija zaidi kwa taifa na watu wake.
Mwananchi wa Kijiji cha Kisondoko, Khalifa Othman akiwasilisha kero zake wakati wa mkutano huo. Kilio chake kikubwa kilikuwa kupatiwa maeneo kwa ajili ya ufugaji na kilimo. Kulia aliyesimama ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Vijijini ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omari Kariati. Kushoto ni Naibu Waziri, Eng. Ramo Makani.
  Mkazi wa Kijiji cha Kisondoko Wilayani Kondoa akitoa kero zake kwenye Mkutano huo. Aliiomba Serikali kuzisaidia jamii za Wabarbaij na Wamang’ati kupata maeneo ya kulima na kufuga kwakuwa kwa sasa jamii hizo zimetengwa na hazina kabisa maeneo kwa ajili ya shughuli hizo, “Sisi Wamang’ati hatuna hata kipande cha ardhi na tukifa hatujui tutazikwa wapi” alieleza. 
 Naibu Waziri Makani akiendelea kuongoza mkutano huo. Alifikisha salam za Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa wananchi hao ambapo aliwataka, Kudumisha amani ya nchi yetu, kutumia amani hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuzalisha zaidi kukuza uchumi wa taifa letu. 
Baadhi ya wajumbe walioshiriki mkutano huo. (Picha na Hamza Temba – WMU)

DC TUNDURU JUMA HOMERA AWATIA MBARONI VIONGOZI 4 KWA TUHUMA ZA KUUZA VIWANJA.


Askari akiwa amewakamata Viongozi wawili wa Serikali ya Kijiji waliokuwa wakituhumiwa kwa ubadhirifu wa viwanja.

Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Ndugu Japhet Muogopeni Mnyagala akizungumza mbele ya Wananchi .

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera akizungumza na Wananchi wa Vitongoji vya FrankWeston na Umojavilivyokumbwa na mgogoro wa ardhi.
Mkuu wa Wilaya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera akimuagiza Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Ndugu Japhet Muogopeni Mnyagala kuchukua hatua stahiki kuhusiana na mgogoro wa Ardhi ndani ya Wilaya hiyo.

Wananchi wakimsikiza kwa makini Mhe DC. Juma Zuberi Homera .
 
Mkuu wa Wilaya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera, amewatia mbaroni Viongozi wanne wa Serikali ya vijiji kwa kosa la usimamizi mbovu wa ardhi katika Vitongoji vya Umoja na Frank Weston katika kata ya Nanjoka Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.
Akisoma taarifa mbele ya Mkuu wa Wilaya Bw. Yahaya

TUHUMA KUHUSU NGOs KUHAMASISHA VITENDO VYA USHOGA

logo 
Siku za hivi karibuni kumekuwepo na tuhuma za kuwepo kwa baadhi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) yanayojihusisha na kuhamasisha vitendo vya ushoga nchini. Tunapenda kuujulisha umma kuwa NGOs zinasajiliwa kutekeleza majukumu yanayokubalika kisheria na kwamba vitendo vya kuhamasisha ushoga si majukumu halali yanayopaswa kutekelezwa na NGOs. Tunazitaka NGOs kutekeleza majukumu yaliyo ndani ya usajili wao na kuepuka vitendo vya uvunjifu wa sheria. Aidha, tunazidi kusisitiza kuwa vitendo vya ushoga havikubaliki nchini kwani ni kinyume na mila, desturi na sheria za nchi. Ofisi ya Msajili inaomba wadau na umma kwa ujumla kutoa taarifa zitakazowezesha kuthibitisha tuhuma tajwa ili hatua stahiki dhidi ya NGOs husika zichukuliwe. Taarifa zinaweza kutolewa kupitia namba zifuatazo: 022 2110714/0222123143/ 0754391942/0715391942.
        M.S.Katemba
MSAJILI WA NGOs
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
01 Agosti, 2016

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO

RPC MSANGI 
MNAMO TAREHE 31.07.2016 MAJIRA YA SAA 5:10 ASUBUHI KATIKA MAENEO YA ILEMELA MLIMANI WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU WATATU AMBAO NI 1.BONIPHACE MASAMAKI MIAKA 47, 2. LINA COSMAS MIAKA 26 NA 3. ALI MOHAMED MIAKA 30 WOTE WAKAZI WA MTAA WA ILEMELA MLIMANI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUJIUNGANISHIA UMEME KINYEMELA KWENYE NYUMBA ZAO KINYUME NA SHERIA NA UTARATIBU ULIOWEKWA NA TANESCO.

Soma hapa walichoandika wadau wa Simba baada ya MO Dewji kuitaka Simba SC

Chanzo Mo Blog
Baada ya juzi na jana kuendelea kuripotiwa habari za timu ya Soka ya Simba Sc kutaka mabadiliko ya kimfumo wa uendeshaji wa timu hiyo huku Mfanyabiashara mkubwa hapa Nchini, Mh. Mohammed Dewji ‘MO’ kutangaza dau la kuwekeza katika klabu hiyo ya Bilioni 20,  baadhi ya wadau wa soka wakiwemo viongozi wakubwa kabisa hapa nchini wamefunguka kwenye mitandao yao ya kijamii na kuandika haya:
Nape Nnauye:   Ambaye nii Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia ukurasa wake wa twitter ameandika:
“Uamuzi wa Wanachama Simba SC kuifanya club kampuni,ukisimamiwa vizuri utakuwa na tija.Utaondoa ushabiki bila tija! Shabikia kwa kununua hisa”.
Mh.-Nape-Nnauye-2
Nape miongoni mwa mashabaki wa Klabu ya Simba Sc
Zitto Kabwe: Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma
“Naunga mkono Mwana Simba mwenzetu kuwekeza ndani ya Simba. Hata hivyo Wanachama wengine wawe na 60% ya Hisa”
14 (1)
Zitto Kabwe ambaye ni miongoni mwa mashabiki wa Simba Sc mwenye kutaka mabadiliko ya klabu yake hiyo
Wengine waliandika:

Sarcastic Chimbo Chi  @Monotata

????????????????????????????????????

TPA YATAKIWA KUPUNGUZA VIKAO

jez1 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mkoa wa Rukwa Arch. Deocles Alphonce wakati alipokagua ujenzi  wa ofisi za  Bonde la Ziwa Rukwa na Maabara zake zilizopo Sumbawanga Mjini.
jez2 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua nondo zilizosukwa kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Kalambo lililopo katika barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga yenye urefu wa KM 112, Mkoani Rukwa.
jez3 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga yenye urefu wa KM 112, Mkoani Rukwa.
jez4 
Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Nicholas O’Dwyer Eng. Farley Vicente akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu ujenzi wa barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga yenye urefu wa KM 112, Mkoani Rukwa.
jez5 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa China Railway 15 Bureau Group Corporation kutoka China Zhang Tonggang (mwenye sweta nyekundu) inayojenga barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga yenye urefu wa KM 112 kwa kiwango cha lami, Mkoani Rukwa.
jez6 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihakiki taarifa za mapato katika Bandari ya Kasanga iliyopo Mkoani Rukwa. Katikati ni Msimamizi wa bandari hiyo Bw. Seleman Kalugendo.
jez7 
Meneja wa Shirika la Posta Tanzania Bi. Zahara Sukeiman akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu huduma ya kutuma na kupokea Vifurushi wakati Waziri alipotembelea ofisini hapo.
jez8 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa Maelekezo kwa Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)  nyanda za juu kusini Bw. Peter Kaguru wakati alipotembelea ofisi hizo Mkoani Rukwa.
……………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kupunguza idadi ya vikao vya baraza visivyo na ulazima ili kuondokana na matumizi mabaya ya fedha na badala yake fedha hizo zielekezwe kwenye uendelezaji wa miundombinu ya  bandari za maziwa.
Ametoa agizo hilo mara baada ya kukagua shughuli za utendaji  wa bandari ya Kasanga iliyopo mkoani Rukwa inayohudumia mkoa wa Kigoma, nchi ya Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC)  ambapo amebaini mapungufu ya kiutendaji ikiwemo malipo yasiyotumia njia za kielektroniki na miundombinu isiyo rafiki katika kukidhi ushindani wa kibiashara katika bandari hiyo.
Waziri Mbarawa ameitaka TPA kuweka mfumo wa uendeshaji vikao kwa njia ya kieletroniki (video conference) kwa lengo la kudhibiti matumizi ya fedha nyingi zilizokuwa zikitumika katika uendeshaji wa vikao hivyo.
“Nataka TPA muanze kutumia video Conference katika vikao vyenu ili fedha zilizokuwa zikitumika zifanyie kazi nyingine za maendeleo ya Taifa”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Ameongeza kuwa TPA  imekuwa na wajibu mkubwa wa kuchangia pato la Taifa kupitia huduma za upakiaji na upakuaji wa mizigo hivyo wanapaswa kuanza kutumia mfumo wa kielekroniki katika ukusanyaji wa mapato katika bandari zote nchini ili kudhibiti upotevu wa mapato.
“Tukianzisha mfumo wa kielekroniki katika bandari hii tutakuwa na uwezo wa kufuatilia mapato yanayopatikana katika utoaji wa huduma na kujua kama malengo yamefikiwa”, amesema Prof. Mbarawa
Katika Hatua nyingine Profesa Mbarawa amekagua barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga Port yenye urefu wa KM 112 inayojengwa kwa kiwango cha Lami na kumtaka Mkandarasi wa barabara hiyo China Railway 15 Bureau Group Corporation kukamilisha ujenzi huo ifikapo Julai mwakani.
Amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutaunganisha mji wa  Sumbawanga na Bandari ya Kasanga na hivyo kurahisisha shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka bandarini hapo na hivyo kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
“Kukamilika kwa barabara hii kutawawezesha wananchi kusafirisha bidhaa zao, kutoka sehemu moja hadi nyingine na hivyo kukuza uchumi wao na kuongeza pato la Taifa”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Aidha Waziri Mbarawa amemuhimiza Mkandarasi huyo kujenga barabara hiyo kwa viwango vilivyopo katika mkataba na kuzingatia thamani ya fedha katika ujenzi huo ili kuwezesha barabara hiyo kudumu kwa muda mrefu.
Naye Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini, Mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo umekamilika kwa asilimia 62 ambapo kukamilika kwa ujenzi huo utatagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 133.
“Mpaka sasa Mkandarasi ameweza kukamilisha kujenga makalvati makubwa 11 kati ya 13, na makalvati ya kawaida 169 kati ya 241”, amesema Eng Mkina.
Waziri Prof. Mbarawa yupo katika ziara ya kukagua miradi ya miundombinu na kuangalia utendaji kazi wa taasisi zilizopo katika Mkoa wa Rukwa.

SAFARI YA MWISHO YA MZEE JOSEPH SENGA

Mwili ukiwasili katika Kijiji cha Shushi Wilaya ya Kwimba Mwanza kwa ajili ya taratibu za maziko.
Mama wa marehemu akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na ndugu.
 
Mama wa marehemu akisaidiwa kugusa mwili wa mwanae kwa mara ya mwisho kabla ya maziko.
Mke wa marehemu akigusa mwili wa mumewe kwa mara ya mwisho kabla ya maziko.
Waandishi wa habari wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Joseph Senga.
Mke wa marehemu Winfrida Senga akiweka shada la maua katika kaburi la mumewe, marehemu Joseph Senga.
Mtoto wa marehemu, Joel Senga akiweka shada la maua.
Continue reading →

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS TAMISEMI AZINDUA KISIMA KILICHOCHIMBWA NA TAASISI YA KIDINI JIJINI ARUSHA

 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleiman Jaffo akizungumza kwenye mkutano wahadhara
kwenye soko maarufu la Kwamrombo kabla ya kuzindua kisima cha maji kwaajili ya matumizi ya wafanyabiashara wa soko hilo kilichochimbwa na taasisi ya kidini ya Ansaar MuslimYouth Centre tawi la Arusha .
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleiman Jaffo akizindua kisima cha maji kwenye soko maarufu la Kwamrombo kwaajli ya matumizi ya wafanyabiashara wa soko hilo kilichochimbwa na
taasisi ya kidini ya Ansaar MuslimYouth Centre tawi la Arusha .


Wananchi wakifurahia hotuba ya Naibu Waziri Jaffo ambaye alitumia mkutano huo kumwagiza Meneja wa Tanesco kuwaunganishia umeme mapema inavyowezekana.

SERIKALI YAWAJENGEA UWEZO WATENDAJI WAKE

1 
Mkurugenzi  wa Mikataba, Ofisi ya  Mwanasheria  Mkuu wa  Serikali Bi. Eveline Makala  akitoa neno la ukaribisho  kwa washiriki wa nafunzo (hawapo pichani) 
2 
Washiriki wa  mafunzo  wakifuatilia  Mada ya dhana ya ubia iliyokuwa  ikiwasilishwa  na Dkt  Frank  Mshiru kutoka Wizara ya  Fedha na Uchumi 
……………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania imeendelea kuwajengea uwezo watendaji wake ili kuwawezesha kuhakiki na kusimamia utekelezwaji wa miradi ya uwekezaji ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi (Public Private Partnership) katika sekta ya Nishati na madini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watendaji mbalimbali wa Serikali yanayofanyika kuanzia Agosti 1-4,2016 mkoani Tanga, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ndugu Gerson Mdemu ameeleza kuwa Serikali imechukua hatua hiyo ili kuondoa ombwe la uelewa wa watumishi wa umma kuhusu Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi ya mwaka 2010  (The Public Private Partnership Act).
Itakumbukwa kuwa, kabla ya mwaka 2010,hakukuwa na Sheria iliyosimamia huduma itolewayo na ubia kati ya Sekta ya umma na Sekta binafsi ingawa tayari kulikuwa na huduma ambazo zilikuwa zikitolewa kwa sura ya ubia kati ya mashirika ya dini na serikali au mashirika ya umma katika sekta ya afya,elimu na maji jambo ambalo lilipelekea Serikali kutumia gharama kubwa katika kuhakikisha kuwa miradi husika inatekelezwa ipasavyo.
Ili kuondokana na changamoto hiyo, Serikali ililazimika kurasimisha shughuli zilizokuwa zikifanywa na sekta binafsi katika utoaji wa huduma kwa umma kwa kutunga Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya umma na sekta binafsi kwa lengo la kutumia teknolojia na utaalamu wa sekta binafsi kutoa huduma yenye gharama nafuu kwa umma na kuhakikisha kuwa huduma inayotolewa na sekta binafsi inaendana na vigezo vilivyowekwa na Serikali.
Aidha Ndugu Mdemu alifafanua kuwa Sheria hii imeipa Sekta binafsi njia mbili za utoaji huduma ambazo ni  mosi, kujenga miundombinu mipya na bora na pili ni kumiliki miundombinu ya Serikali, kuiboresha na kuiendesha wakati wa kutoa huduma bora na kuikabidhi Serikalini baada ya muda wa mkataba kukamilika.
Vilevile Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametumia fursa hiyo kuzikumbusha taasisi za Serikali kuzingatia ushauri wa kisheria unaotolewa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika utekelezaji wa mikataba na majukumu mbalimbali kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 23 cha Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  ya mwaka 2005 (The Attorney General [Discharge of Duties] Act) ambacho kinaeleza kuwa ushauri unaotolewa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndio msimamo wa Serikali hadi utakapoondolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali mwenyewe au Mahakama.
“Kwa Mawakili wa Serikali,umuhimu wenu unatokana na nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama ilivyowekwa wazi Kikatiba. Mwanasheria yeyote wa Wizara,Taasisi,Mashirika ya Umma au Serikali za mitaa anayetoa ushauri wa kisheria katika eneo lake la kazi,kimsingi anafanya kazi kwa niaba ya Mwanasheria Mkuu” aliongeza Ndugu Mdemu.
Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Mhiru    alieleza kuwa washiriki watajengewa uwezo wa masuala muhimu ya kuzingatia wakati wa kuhakiki mikataba ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kuiwezesha nchi kupiga hatua katika ukuaji wa uchumi .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mikataba kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Bi Evelyne Makala alieleza kuwa sekta ya Nishati ni sekta ambayo ina mikataba mingi ya ubia na yenye maslahi makubwa kwa Taifa hivyo mafunzo haya yatasaidia katika kutoa mwongozo wa uhakiki na kusimamia miradi ya uwekezaji katika sekta ya Nishati na madini.
Mafunzo hayo amabayo yamefadhiliwa na Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) yameshirikikisha watendaji wa Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya Fedha na Mipango,Wizara ya Mambo ya Nje,Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kimataifa, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar,Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Jamhuri ya Muungano,na watumishi kutoka Ofisi za Mwanasheria Mkuu za Mikoa ya Pwani,Arusha,Morogoro,Tanga na Ofisi ya Wilaya ya Monduli.

KAMPUNI YA OFF GRID YAJIBADILI JINA LA BIASHARA NA KUFUNGUA MADUKA MAPYA TANZANIA NA RWANDA

Mmoja wa viongozi wa Kampuni ya vifaa vya umeme wa jua ya Zola, akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo, jijini Arusha. 
Shughuli za uzinduzi wa duka hilo, jipya la vifaa vya umeme wa jua la Kampuni ya Zola, zikiendelea jijini Arusha. 
Wafanyakazi wa Kampuni ya vifaa vya umeme wa jua ya Zola wakishangilia mara baada ya kukatwa utepe wa kulizindua rasmi duka hilo, jipya jijini Arusha.

Ilala yawataka wafanyabiashara kuzingatia muda wa usafi

DC ILALA 
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaaam imewataka wafanyabiashara kuzingatia muda uliopangwa na Serikali kwa ajili ya usafi wa mazingira katika maeneo yao ya kazi unaofanywa kila ifikapo siku ya jumamosi.
Muda uliowekwa kwa ajili ya zoezi hilo ni kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 3:30 asubuhi, ambapo wafanyabiashara wote watapaswa kufungua maduka na masoko yao mara baada ya zoezi hilo kukamilika.
Hayo yamesemwa leo na Afisa wa Manispaa hiyo, David Langa wakati alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii kuhusu mwitikio wa wananchi juu ya zoezi la usafi wa mazingira unaofanyika kila jumamosi na kila mwisho wa mwezi.
“Nawaomba Wafanyabiashara wenye tabia ya kujichelewesha ili wafike baada ya muda wa usafi pamoja na wale wanaofungua biashara kabla ya muda uliopangwa na Serikali kuacha mara moja kwani  lengo la kubadili muda wa kufungua biashara ni kwa ajili ya kufanya usafi” alisema Langa.
Akifafanua zaidi Langa aliwatahadharisha wananchi wanaopenda kutupa taka hovyo kuacha mara moja kwani sheria ya afya na sheria ya mazingira inapinga suala hilo na kwa mujibu wa sheria hizo adhabu yake ni faini ya shilingi milioni moja au kifungo kisichozidi miaka 6.
Kwa mujibu wa Langa alisema kuwa, suala la usafi sio suala la Serikali pekee bali wananchi wanatakiwa walifanye kuwa ni sehemu ya kulinda afya zao, hivyo kila mmoja anapaswa kuzingatia usafi kwenye maeneo yanayomzunguka.
Aidha Langa alisema kila mwananchi anapaswa kuwa mlinzi wa mwenzie kwani zoezi la kulipishwa faini bado ni endelevu, mtu atakaemkamata mwenzie anatupa taka atapewa shilingi elfu 20 na aliyekamatwa atatoa faini ya shilingi elfu 70.

No comments:

Post a Comment