MAALIM SEIF AZUNGUMZA NA WAZANIBARI BOSTON
Maalim Seif, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) alikamilisha ziara yake hiyo tarehe 30 Julai kwa kuzungumza na Wazanzibari kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Massachusetts.
Mgeni huyo rasmi alikaribishwa kwa risala ya Jumuiya ya Wazanzibari waishio katika jiji la Boston kulikofanyika mkutano huo, Bwana Mohammed Lali, iliyoelezea imani yao juu ya uongozi wa Maalim Seif katika mapambano ya kupigania haki sawa na demokrasia Visiwani Zanzibar.
Akijibu risala hiyo, Mwanasiasa huyo alielezea shukrani zake za dhati kwa imani ya Wazanzibari juu uongozi wake na kuwahakikishia kuwa haki yao itapatikana.
Madhumuni ya Ziara zake.
Maalim Seif, aliyekuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF katika uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana, alielezea lengo la mizunguko yake hiyo kuwa ni kukutana na viongozi wa ngazi za juu wa nchi na taasisi alizozitembelea ili kuwapa picha halisi ya hali ya mambo ilivyo huko Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika nyanja za demokrasia na haki za binadamu kufuatia uchaguzi huo.
"Tumekuwa tukiwasiliana ili kuwapa 'brief' (maelezo) ya hali halisi ilivyo" aligogoteza Maalim.Alisema kuwa nchi nyingi kwa kupitia Balozi zao zilikuwa zikitetea demokrasia, na wala siyo chama au kiongozi fulani.
"Nchi nyingi kwa kupitia Balozi zao zilikuwa zinatetea demokrasia, na wala siyo CUF wala Maalim Seif", alisema gwiji huyo wa siasa, na kuongeza kuwa,
"Msimamo huo ndio uliotusukuma kutembelea nchi hizi ili kuwapa 'utandu na ukoko', kwani kwa kufanya hivi tunapata nafasi ya kukutana na watunga sera wenyewe"Hii ni kutokana na kuwa Mabalozi wanafanya kazi kutokana na maagizo ya viongozi wa nchi zao, "na kama hamkujikaza swala hili linaweza kusahaulika", alisistiza.
Katika mkutano huo, mwanasiasa huyo mkongwe alielezea kwa mukhtasari juu ya historia ya migogoro visiwani Zanzibar kwa kusema kuwa migogoro visiwani humo ni tofauti na migogoro katika nchi nyengine ambako huwa inajikita katika misingi ya ukabila au udini. lakini swala la ukabila au udini haliko Zanzibar licha ya kuwa 97% ya watu wake ni Waislamu.
"Mgogoro zaidi ni wa kisiasa tangu zama hizo zinazoitwa za siasa", alifafanua mweledi huyo, na kuongeza: "Baada ya kuanzishwa kwa vyama vya ASP, ZNP na ZPP, siasa iliwagawa Wazanzibari na baadaye yakaja Mapinduzi ya mwaka 1964"
MKANDARASI APEWA WIKI MBILI KURUDISHA VIFAA NA KUENDELEA NA UJENZI SUMBAWANGA
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Mkandarasi anayejenga barabara ya Sumbawanga Mjini-Chala-
Kanazi yenye urefu wa KM 75 alipokagua ujenzi wa barabara hiyo.
Mkandarasi
anayejenga barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni yenye urefu wa KM 76.6
akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa wakati alipokagua ujenzi huo. Katikati ni Meneja wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina.
Mbunge
wa Jimbo la Nkasi kaskazini Mhe. Ally Kessy (mwenye kofia) akieleza
jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa wakati alipokagua miundombinu ya Bandari ya Kipili, Mkoa wa
Rukwa.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia)
akitoa maelekezo kwa Meneja wa kiwanja cha ndege cha Rukwa Bw. Sandali
Kaisi (kushoto) kuhusu uboreshwaji wa kiwanja hicho wakati alipotembelea
kiwanja hicho.
Meneja
wa kiwanja cha ndege cha Rukwa Bw. Sandali Kaisi (wa kwanza kushoto)
akitoa maelezo ya hali ya miundombinu kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia kwake) wakati Waziri
alipokagua kiwanja hicho.
WAKUU WA IDARA WILAYANI IKUNGI, MAAFISA TARAFA, WATENDAJI WA KATA, VIJIJI NA WENYEVITI WA VIJIJI WAFUNDWA
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwasilisha mtazamo wa namna ambavyo anataka Wilayahiyo iwe.
Wakuu wa
Idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Vijiji, na
Wenyeviti wa Vijiji wakifatilia mafunzo kutoka kwa wawasilishaji
Afisa
utumishi wa Wilaya ya Ikungi Evodius Buberwa akifafanua na kutofautisha
majukumu ya watendaji wote ngazi ya Wilaya, Tarafa, Kata na Vijiji
Mkuu wa
Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza umuhimu wa kuchangia
maabara kwa ajili ya kuwanusuru wanafunzi wanaotaka kusoma masomo ya
sayansi lakini kikwaza inakuwa maabara
Kutoka
Kushoto ni Mustafa Mtopo kaimu Afisa usalama wa Taifa Wilaya ya Ikungi,
Fortunatus Ndalama Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Ikungi, Dijovson Ntangeki
Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji
Jumanne Mtaturu, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ikungi
Rustika Turuka, na Mkuu wa poiisi Wilaya ya Ikungi Milton Nkyalu
wakifatilia mafunzo kutoka kwa wawasilishaji waliotoka ofisi ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ikungi Rustika Turuka aliyesimama
akizungumza na Wakuu wa Idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa
Kata, Vijiji, na Wenyeviti wa Vijiji wakati wa kikao hicho cha kazi.
WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA KATIKA KIWANDA CHA MTIBWA.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Meneja wa Kiwanda cha
sukari cha Kagera, Ashuwin Rana baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha
sukari cha Mtibwa baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha sukari cha
Mtibwa Agosti 2, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt.
Stephene Kebwe na wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Kagera
Sugar na Mtibwa Sugar, Seif Ali Seif .
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha
sukari cha Mtibwa kukagua uzalishaji wa sukari katika kiwanda hicho,
Agosti 2, 2016. Kulia ni mkewe Mary, wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa
wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe na Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa
Kiwanda cha sukari cha Kagera na Mtibwa, Seif Ali Seif . Kushoto ni
Kaimu Katibu wa CCM mkoa Wa Morogoro, Kulwa Solobi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la mtambo wa maji ya
kumwagilia katika shamba la miwa la kiwanda cha sukari cha Mtibwa
wakati alipokitembelea kiwanda hicho, Agosti 2, 2016. Kushoto ni mkewe
Mary na wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sukari cha
Kagera na Mtibwa, Seif Ali Seif .
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la mtambo wa maji ya kumwagilia
katika shamba la miwa la kiwanda cha sukari cha Mtibwa wakati
alipokitembelea kiwanda hicho, Agosti 2, 2016. Kushoto ni mkewe Mary
na wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera na
Mtibwa, Seif Ali Seif.
No comments:
Post a Comment