Pages

Wednesday, August 3, 2016

BancABC YAZINDUA HUDUMA MPYA YA “MKOPORAHISI”, MTEJA ANACHUKUA PESA NDANI YA SAA 48

H1

 

Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Rahisi, (Easy Banking), wa BancABC,Thompson Mwasikili, (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha benki hiyo, Joyce Malai,  wakati akizindua huduma mpya ya “Mkoporahisi”, makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Agosti 2, 2016. BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imerahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wateja wake ambapo mteja wa benki hiyo ambaye ni mtumishi wa serikali anaweza kupatiwa mkopo ndani ya masaa 48.
H2 
Na Mwandishi Wetu BANCABC ambayo ni sehemu ya Atlas Mara imerahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wateja wake kwani imeanza kutoa mikopo
ndani ya saa 48 kupitia huduma mpya ya ‘mkoporahisi’.
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 1, 2016, makao makuu ya benki hiyo, kwenye jingo la Uhuru Hights jijini Dares
Salaam, Mkuu wa kitengo cha Easy Banking wa BancABC, Thomson Mwasikili, (pichani juu), alisema
wameamua kuanzisha huduma hiyo ili kuwavutia wateja wengi zaidi kutoka sekta mbalimbali ikiwemo serekalini ili kuhakikisha wanapata huduma hii kwa haraka.
“Kwa kupitia huduma hii ya mkoporahisi tutahakikisha kuwa wateja wetu ambao ni waajiriwa wa Serikali, wanapata mikopo
yao ndani ya saa 48 kuanzia muda ambao maombi yaliwasilishwa..tutalisimamia hili na kuhakikisha linatekelezeka,” alisema Mwasikili.
Bw. Mwasikili alisema benki yake inatoa mikopo ya hadi  Tsh milioni 40 kwa riba ya kiwango cha chini
hadi asilimia 1.6 kwa mwezi ambayo ni miongoni mwa riba za chini kabisa katika soko la sasa.
“Waombaji wataweza kulipa mikopo yao kwa muda mrefu wa hadi miaka 6 na hakuna pingamizi kuhusu lini unaweza kuongeza
mkopo wako,” alisema na kuongeza kuwa muombaji ana uhuru wa kupata mkopo wa muda mfupi hata wa mwezi mmoja.
Kwa mujibu wa Mwasikili, tofauti na mikopo mingine, waombaji wana uhuru wa kuchagua matumizi ya fedha kwa mfano kulipia ada, kununua gari, kukarabati nyumba, kulipia kodi na kumaliza ujenzi na benki haitamlazimisha mkopaji matumizi ya mkopo wake.
Waombaji pia watapata fursa ya kuchanganya mikopo yao yote na kuwa na mkopo mmoja kwani BancABC inaweza kununua mikopo yote hiyo na kumpunguzia mteja usumbufu.
“Endapo muombaji wa mkopo atafariki, mkopo utafidiwa kupitia bima ya mikopo na fedha kiasi cha Tsh 500,000 taslimu
zitatolewa kugharamia mazishi,” alisema
“Tunatoa rai kwa wateja wetu wote na pia wale ambao hawana akaunti na benki yetu kuchangamkia huduma hii ya mkoporahisi kwani hii ndio benki pekee ambayo inakusogeza karibu na ndoto zako , pata
mikopo ndani ya saa 48,” alisema.
Atlas Mara iliorodheshwa katika soko la
hisa la London Disemba 2013. Atlas Mara ina lengo la kujitanua na kuwa kinara
katika masuala ya kifedha katika ukanda wa sub sahara kwa kutumia uzoefu wake
na uwezo wa kukuza mitaji. Malengo yake ni kuunganisha na kukuza uwezo wa
taasisi za kifedha na pia kuendeleza uchumi katika nchi ambazo inafanya
shughuli zake.

KATIBU MKUU WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS AZUNGUMZA NA WAANDHISHI WA VYOMBO VYA FM

01 
Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Nd,Salum Maulid Salum (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali vya Redio za FM kuhusu kongamano la Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora) linalotarajiwa kufanyika  Agosti 24 mwaka huu. 
02 
Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Nd,Salum Maulid Salum (wa pili kulia) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya Redio za  FM kuhusu kongamano la Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora) linalotarajiwa kufanyika  Agosti 24 mwaka huu (kushoto) Naibu Katibu wa Rais Nd,Marium Haji Mrisho na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Silima Kombo Haji.  
03 
Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Nd,Salum Maulid Salum (kulia) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya Redioza  FM kuhusu kongamano la Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora) linalotarajiwa kufanyika  Agosti 24 mwaka huu (kushoto)   Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Silima Kombo Haji.
[Picha na Ikulu.]

WAKALA WA UNUNUZI SERIKALINI GSPA KATIKA MAONYESHO YA NANENANE LINDI

gs1 
Meneja  masoko  na mauzo  wa  wakala wa ununuzi serikalini GPSA   Hamza hasani   (wa kwanza kushoto)   akitoa   maelezo  juu ya  huduma zinazotolewa  na  wakala hao  kwa  mteja  Bi NURU CHIWAMBA aliyetembelea  kwenye  banda  la  wakala  hao kwenye  maonyesho ya  nanenane viwanja vya  Ngongo  mkoani Lindi , (kulia  ni Huseni Athumani   Muhasibu wa GPSA  mkoa Lindi  na katika   Meneja wa GPSA  Mkoa wa Lindi  Mwakiselu  Mwambange )
gs2wafanyakazi wa wakala  wa wakala wa ununuzi serikalini GPSA   wakiwa kwenye banda  lao   lililopo  kwenye  viwanja vya  ngongo  mkoani  LINDI wakala  wa ununzi  serikalini  lengo kuu  na

Mashindano ya Olimpiki 2016 nchini Brazil, wawakilishi wa Tanzania kupeperusha bendera. DSTV, Bodi ya Utalii wajitokeza kuwapa nguvu.

oli2 
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikabidhi bendera kwa timu ya Tanzania inayoenda kushiriki katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 nchini Brazil  Agosti 1, 2016.
oli3Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Maharage Chande  akishukuru Serikali kwa fursa ya kuunga mkono jitihada za kuendeleza michezo wakati wa hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil  katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 nchini Brazil  Agosti 1, 2016.
oli4 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TTB Bw. Godfrey Tengeneza  akitoa nasaha zake kwa wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Olimpiki  kwenda kutangaza utalii wa Tanzania wakati wa hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil  katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 nchini Brazil  Agosti 1, 2016.
oli1 
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Zikiwa zimebaki siku chache kabla kuanza rasmi michezo ya 31 ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro nchini Brazil inayotarajiwa kuanza Ijumaa ya Agosti 4, 2016 katika mji wa Sao Paulo na Rio De Jeneiro nchini Brazil wawakilishi wa Tanzania katika michuano hiyo wamepata baraka zote kutoka kwa Serikali na kukabidhiwa bendera ya Taifa kabla ya kwenda kuipeperusha nchini Brazil.
Akikabidhi bendera kwa timu hiyo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura aliwataka washiriki wanaokwenda kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka huu huko Rio De Jeneiro nchini Brazil kujituma na kuhakikisha wanafanya vizuri ili warudi na medali.
Mhe. Annastazia Wambura alisema kuwa wanapokwenda kuiwakilisha waamini kuwa macho na masikio ya watanzania wote yapo kwao kwahiyo wajitahidi kadri ya uwezo wao kuweza kuhakikisha watakapokuwa wanarejea basi waje wakiwa wamevaa medali zao.
” Mnakwenda katika mashindano ya Olimpiki macho yote ya watanzania yapo kwenu tunategemea mkiwa mnarudi basi tutakuja kuwapokea mkiwa na medali zenu kifuani na hilo linawezekana kama mtajituma mkiwa na ari ya ushindi”.
Aidha  Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania , Filbert Bayi alisema kuwa kwa mwaka huu washiriki wamekaa kambi katika sehemu tofauti nchini na wengine wakiwa nje ya nchi na hilo limefanikisha kuweza kujifua vyema na kujiandaa ili kuweza kurejesha ushindi nyumbani.
Akizungumzia mara baada ya  kukabidhiwa bendera  Kocha wa timu ya kuogelea Bw. Alexandra Mwaipasi alisema kuwa wachezaji wake wameiva kwani mwanzoni walikuwa na changamoto ya kupata mabwawa yenye viwango vinavyoendana na mashindano hayo ili kwa matayarisho aliyowapatia wachezaji wake anahakika watarudi na medali.
Moja ya washiriki wa mchezo wa kuogelea katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 Magdalena Mosha alisema kuwa amejiandaa vizuri na anaamini kwa miaka aliyoshiriki kwenye mashindano ya Olimpiki ya Beijing na London yamempa uelewa zaidi wa nini anatakiwa kufanya na kuyafanyia kazi mazoezi aliyoyapata nchini Australia ili kurudi na ushindi.
Naye mmoja wa wawakilishi katika mchezo wa Judo, Adrew Thomas alisema amejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo na yuko tayari kuiwakilisha Tanzania na kuleta ushindi na pia kuitangaza Tanzania katika michezo na utalii uliopo kwa kuvitangaza vivutio vilivyopo nchini.
Kwa upande wake Sara Ramadhani ambaye ni mwakilishi mwanamke pekee katika mshindano hayo kwa wakimbiaji wa Marathon alisema yuko vizuri kuipeperusha bendera ya taifa na kuitangaza Tanzania kimataifa kwa kushindana na kushinda medali hivyo kuiletea sifa nchini.
Mmoja  wa wadhamini wa safari hiyo kampuni ya Multichoice Africa, imewataka washiriki hao kujituma zaidi kwani watanzania wote watakuwa wanawaangalia kupitia chaneli zao zinazopatikana kwenye kisimbuzi cha DSTV.
Katika mchango wao kwa wawakilishi hao Kampuni ya ving’amuzi  ya Dstv imetoa mchango wa kuwakutanisha pamoja kwa kuandaa hafla ya kuwaaga wawakilishi hao ikiwa ni moja ya kuwatia moyo waende kupambana na kushinda katika michezo mbalimbali na kuliletea sifa taifa.
Akizungumza kwa niaba ya kampuni hiyo Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania Maharage Chande alisema mwaka huu mashindano yote yatakuwa yakioneshwa  moja kwa moja kupitia channeli za Super Sport na itawapa fursa watanzania kuwashuhudia wawakilishi wao kwenye mashindano hayo makubwa duniani.
Bodi ya Utalii nayo haikuwa nyuma kuwapa nguvu na morali wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Olimpiki kwenda kufanya vizuri katika mashindano hayo na pia kutangaza vivutio vilivyopo nchini kwa mataifa mbalimbali yanayoshiriki mashindano hayo kwa kuwapatia vifurushi kwa ajili ya kusambaza ujumbe kuhusu utalii wa Tanzania.
Akitoa nasaha zake kwa wawakilishi hao  Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano TTB Bw. Godfrey Tengeneza aliwaasa wawakilishi hao kujituma kwa bidii na kutangaza nchi kupitia michezo na pia watumie fursa hiyo kutangaza vivutio vilivyopo Tanzania kwa kueneza habari kuhusu utalii Tanzania.
“Mtakapokuwa huko mbali na kushiriki katika michezo muitangaze nchi yetu kwa vivutio vilivyopo nchini ili tuzidi kupata watalii wengi kutoka duniani kote”.
Timu ya Tanzania inayoenda kushiriki mashindano ya 31 ya Olimpiki nchini Brazil  inawakilishwa na wachezaji saba ambao ni  waogeleaji wawili Magdalena Mosha anayeenda kwa mara ya tatu kwa upande wa wanawake huku Hilal Hilal akienda kwa mara ya kwanza kwa upande wa wanaume na wote watakuwa ni waogeleaji kwa umbali wa mita 50.
Wengine ni Fabian Joseph, Said Juma Makula na Alphonce Felix Simbu watakaokimbia marathon kwa wanaume na Sara Ramadhani ambaye ni mwanamke pekee anayeiwakilisha Tanzania katika mbio za marathon.
Na kwa upande wa mchezo wa Judo Tanzania itawakilishwa na Adrew Thomas Mulugu katika uzito wa kilogramu 73.
Katika mashindano ya Olimpiki mwaka huu takribani M yanatarajiwa kushindana katika michezo mbalimbali huku Marekani ikiongoza kuwa na wachezaji wengi zaidi katika mashindano hayo ikiwa na wachezaji 550 ikifuatiwa na Brazil iliyo na wachezaji 450 na China inayowakilishwa na wachezaji 380.               

MKANDARASI APEWA WIKI MBILI KURUDISHA VIFAA NA KUENDELEA NA UJENZI

1 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa kiwanja cha ndege cha Rukwa Bw. Sandali Kaisi (kushoto) kuhusu uboreshwaji wa kiwanja hicho wakati alipotembelea kiwanja hicho.
2 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili Kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa kiwanja cha ndege cha Rukwa Bw. Sandali Kaisi (wa kwanza kushoto) wakati alipokagua kiwanja hicho.
3 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi anayejenga barabara ya Sumbawanga Mjini-Chala- Kanazi yenye urefu wa KM 75 alipokagua ujenzi wa barabara hiyo.
4Mkandarasi anayejenga barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni yenye urefu wa KM 76.6 akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipokagua ujenzi huo. Katikati ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina.

MAKALA KUHUSU FALSAFA, DHANA NA UMUHIMU WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVUTZFalsafa ya Mwenge wa Uhuru
Historia ya nchi yetu ni pana na ya kuvutia kwa namna ya pekee ukilinganisha na nchi nyingi za Afrika na Duniani kote. Upekee huu unatokana na uwezo wa kujenga hoja na uadilifu wa viongozi wetu, hasa mwasisi wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipochaguliwa kuwa mjumbe kwenye Baraza la kikoloni la kutunga Sheria (Tanganyika Legislative Council) mwaka 1958.
Kwa kuwa Mwalimu alikuwa na ndoto ya kuiona Tanganyika na Afrika iliyo huru, mwaka 1958 katika hotuba yake ya kwanza alitamka maneno ya kifalsafa kwa wajumbe na Spika wa Baraza la kikoloni la kutunga Sheria kwa kusema “Sisi tunataka Uhuru wa Tanganyika, Mkitupatia tutauwasha Mwenge wa Uhuru na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike ndani na nje na mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki na heshima palipojaa dharau”.
1 
Maneno haya aliyarudia tena mwaka 1959 alipohutubia kikao cha 35 cha Baraza la Umoja wa Mataifa kama Mbunge mwakilishi pekee wa Tanganyika.
Falsafa hiyo ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilikuwa ni kiashiria kikubwa kwa Waingereza kwamba watu wa Tanganyika wamechoka kutawaliwa. Siku Tanganyika ilipopata Uhuru tarehe 09 Desemba, 1961. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliuwasha Mwenge wa Uhuru na akamkabidhi Luteni Alexander Ngwebe Nyirenda na kikosi cha Vijana wenzake wakaupeleka Mwenge wa Uhuru juu ya Mlima Kilimanjaro.
Mwalimu wakati akitoa hotuba ya siku ya Uhuru; aliwatangazia Watanganyika, Afrika na Dunia kwa ujumla kwa kusema                               “Sisi tumekwisha uwasha Mwenge wa Uhuru na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike ndani na nje ya mipaka yetu, ulete matumaini pale ambapo hakuna  matumaini, ulete upendo mahali penye chuki na heshima mahali palipo jaa dharau”
2 
Luteni Alexander Nyirenda akipandisha Bendera na Mwenge wa uhuru juu ya mlima Kilimanjaro usiku wa kuamkia tarehe 9 december, 1961
Baada  ya  Uhuru wa Tanganyika na kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru,  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na viongozi wenzake wa awamu ya kwanza walielekeza juhudi zao katika kuwaunganisha Watanzania na kuweka misingi imara ya kulijenga taifa huru la Tanganyika; kudumisha amani, upendo, umoja, mshikamano na kuweka sera za kukabili  maadui ujinga, umaskini na maradhi.

WAKUU WA IDARA WILAYANI IKUNGI, MAAFISA TARAFA, WATENDAJI WA KATA, VIJIJI NA WENYEVITI WA VIJIJI WAFUNDWA

B1 
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwasilisha mtazamo wa namna ambavyo anataka Wilaya hiyo iwe.
B4Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ikungi Rustika Turuka aliyesimama akizungumza na Wakuu wa Idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Vijiji, na Wenyeviti wa Vijiji wakati wa kikao hicho cha kazi.
B2 
Wakuu wa Idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Vijiji, na Wenyeviti wa Vijiji wakifatilia mafunzo kutoka kwa wawasilishaji
B3 
Kutoka Kushoto ni Mustafa Mtopo kaimu Afisa usalama wa Taifa Wilaya ya Ikungi, Fortunatus Ndalama Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Ikungi, Dijovson Ntangeki Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ikungi Rustika Turuka, na Mkuu wa poiisi Wilaya ya Ikungi Milton Nkyalu wakifatilia mafunzo kutoka kwa wawasilishaji waliotoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo.
…………………………………………………………………………………………..
Na Mathias Canal, Singida
Wakuu wa Idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji 101 vilivyopo Wilayani Ikungi Mkoani Singida hii leo wamepatiwa mafunzo ya kutambua mipaka ya majukumu yao kiutendaji katika kikao cha kazi kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Ikungi.
Mafunzo hayo yameandaliwa na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kutokana na kubainika kuwa asilimia kubwa ya watendaji hususani wenyeviti wa vijiji na vitongoji wamekuwa wakiingilia katika majukumu ya kiutendaji.
Akifungua mafunzo hayo yaliyodumu kwa zaidi ya masaa matano yaliyojikita zaidi kutoa ufafanuzi juu ya majukumu ya watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Vijiji, Mkuu wa Wilaya hiyo Miraji Jumanne Mtaturu amebainisha kuwa pamoja na mafunzo kwa ajili ya ufahamu wa majukumu ya watendaji hao lakini amesema kuwa Wilaya ya Ikungi ipo nyuma kielimu kutokana na shule kuwa mbali na maeneo ya watu, wanafunzi wa kike kuachishwa shule na kuolewa, baadhi ya viongozi na wataalamu kutotimiza wajibu wao na wakati mwingine uzembe wa baadhi ya watumishi wa serikali katika kutatua kadhia za wananchi.
Pamoja na hayo pia DC Mtaturu amesema kuwa kuna baaadhi ya maeneo kuna shule ambazo zina majengo mazuri na Hosteli kwa ajili ya wanafunzi lakini wazazi wanakataa kuwapeleka wanafunzi shuleni ikiwa ni pamoja na shule ya Sekondari Mkinya iliyopo Kata ya Dung’unyi, Shule ya Sekondari Mtunduru, Shule ya Sekondari Mwaru na Wembere , huku shule ya Sekondari Issuna ikiwa na Majengo na Hosteli nzuri lakini wanafunzi wanaosoma hapo ni wale wanaotoka Wilaya nyingine huku wenyeji wakiwa wamejichimbia ndani.
Dc Mtaturu amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa kushirikiana na Polisi kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua baadhi ya Watendaji wa Kata, Waratibu wa elimu wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Vijiji wanaoshirikiana na baadhi ya wazazi kuwaachisha wanafunzi shule ili wakaolewe ambapo amebaini kuwa katika Kata ya Mwaru na baadhi ya Kata zinazozunguka katika Kata hiyo viongozi wake kwa kushirikiana na Waratibu elimu Kata wamekuwa wakifanya biashara ya kuruhusu wanafunzi kuolewa kwa kupewa Ng’ombe.
Hata hivyo pia amewaagiza Watendaji wa Kata ya Makilawa na Iyumbu kumpatia taarifa ya kamati ya maendeleo ya Kata (WDC) ili kubaini mpango wa mikakati katika kujenga shule za Sekondari katika Kata hizo mbili ambazo zimesalia ilihali Kata 28 tayari zina shule za sekondari kati ya Kata 30 zilizopo katika Wilaya hiyo.
Katika shule 28 ni shule 3 tu zenye maabara, shule ya Sekondari ya Puma na Wembere ambao nao walijenga maabara baada ya kupata msaada kutoka Benki ya dunia Mwaka 2013, shule ya Sekondari Mkinya ina maabara 2 ambazo zilijengwa kwa msaada wa SADC mwaka 2009 hivyo kupelekea Wilaya nzima ya Ikungi kuwa na Maabara 4 pekee zilizojengwa kwa msaada wa wahisani ambapo hakuna hata maabara moja iliyojengwa na wananchi ikakamilika kutokana na zuio la kuchangia walilolipata wananchi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu.
Sawia na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya amewaagiza Watendaji wa Kata na Vijiji kwa kushirikiana na Wabunge, Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji kuwaelimisha wananchi kukaa vikao na kupitisha maadhimio ya kuendelea kuchangisha michango ya ujenzi wa maabara kwa mujibu wa waraka wa Elimu namba 6 wa mwaka 2015 wa elimu msingi bila malipo.
Hata hivyo agizo limetolewa pia kwa Wazazi/Walezi pamoja na wanafunzi wenyewe kuchukuliwa hatua kali za kisheria kutokana na utoro wa wanafunzi shuleni jambo ambalo linapelekea kuwa na ufaulu duni wa wanafunzi Wilayani humo.
Dc Mtaturu pia amemuagiza Afisa Mtendaji wa Katana Afisa Mtendaji wa Tarafa kutumia siku 14 kuhakikisha madawati yanafika katika shule zenye uhaba wa madawati ili kuondokana na adha ambayo inaendelea kuwakumba wanafunzi shuleni ilihali madawati tayari yamepatikana.
Aidha ndani ya siku tano viongozi hao wameagizwa kuhakikisha kuwa Masoko pamoja na stendi zinaenda katika maeneo yaliyopangiwa ili ushuru upatikane kwa wakati na kwa kiasi kilichokusudiwa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka amewashukuru Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Vijiji kwa kujitokeza kwa wingi katika mafunzo hayo jambo ambalo limeonyesha kuwa wananchi hao wana imani na serikali ya awamu ya nne hivyo amewaomba kuachana na siasa na kufanya kazi kwa moyo na nguvu zaidi.
Amewataka viongozi wote wa ngazi ya Wilaya, Tarafa, Kata, Vijiji na vitongoji kutekeleza maagizo yote yanayotolewa na serikali kwa haraka na kwa ukamilifu.
Turuka amesema kuwa kila kiongozi anapaswa Kutatua kero za wananchi kwa kutenda haki, kutofanya kazi kwa mazoea, kutoa majawabu sahihi ya wananchi na kama hawafahamu wanapaswa kuuliza sehemu husika ili kutozungumza jambo wasilokuwa na uhakika nalo.
Kupitia kikao hicho kilichoitishwa na mkuu huyo wa Wilaya kilichokuwa na dhumuni la kufahamiana na kukumbushana majukumu na wajibu wa viongozi na kueleza mtazamo wa Ikungi mpya inavyotakiwa kuwa Afisa utumishi wa Wilaya sawia na Mkuu wa Polisi Wilaya wamepewa nafasi ya kuelezea majukumu na wajibu wa kila mmoja katika maeneo yao.
Kwa upande wao baadhi ya Watendaji wa Kata, Vijiji na wenyeviti wa vijiji 101 vilivyopo Wilayani humo wamesema kuwa mafunzo waliyoyapata watayatumia vyema kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi na kuwaelimisha zaidi ili kutambua mipaka yao na majukumu yao katika kuishauri serikali.
Aidha Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji wote ambao hawajahudhuria kikao hicho cha kazi wametakiwa kuandika barua za maelezo kwanini wameshindwa kuhudhuria na zimetakiwa kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ikungi hadi kufikia tarehe 10 ya mwezi huu wa nane.

MO Dewji amwaga Simba Mil. 100 za usajili, kutumia zaidi ya Bilioni

Hatimaye ahadi ya shabiki wa Simba, ambaye ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji amekamilisha ahadi aliyoisema kabla ya mkutano mkuu wa Simba kwa kukabidhi Milioni 100 kwa uongozi wa Simba kwa ajili ya kufanya usajili.
MO amekabidhi pesa hizo baada ya kueleza mipango yake kwa Simba ya kuwa kama wanachama wa Simba wataridhia kufanya mabadiliko basi atachangia pesa ya usajili jambo ambalo katika mkutano wake wa Jumatatu na waandishi wa habari kuwa ahadi yake ni kweli na ataikamilisha kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Akizungumza baada ya kupokea cheki kutoka kwa MO, Rais wa Simba, Evans Aveva, amemshukuru MO kwa msaada huo na sasa wanasimba watatembea kwa kujiamini kwani wamepata pesa ya kufanya usajili.
“Nakushukuru MO kwa msaada ambao umetupatia tunaamini ni mapenzi ambayo unayo kwa Simba ndiyo umefanya uwe tayari kutoa pesa hizi na sisi tunaamini zitaweza kutusaidia kupiga hatua na hata tuweze kutembea kifua mbele,” alisema Aveva.
Aidha Aveva alisema kiasi hicho cha pesa bado hakijatosha kwa kufanya usajili ambao wamepanga kuufanya lakini kitawasaidia kupiga hatua ya kufanya usajili ambapo kwa msimu huu wamepanga bajeti ya Milioni 400 lakini pia kumtaja mchezaji wa Ivory Coast ambaye wanataka kumsajili ni Fredrick Blagnon.
Kwa uapnde wa MO alisema ametoa msaada huo kama sehemu ya ahadi aliyoitoa kabla ya mkutano mkuu na hakuna makubaliano yoyote lakini pia kuwapa ahadi mashabiki wa Simba kuwa kama akipata nafasi ataweka bajeti zaidi ya Bilioni 1 kwa mwaka kwa ajili ya usajili.
Chanzo Mo Blog

Kampeni ya “Nunua, Uza, Shinda na Konyagi yazindi kupamba moto

index 
Mawakala na baadhi ya maofisa wa Konyagi wakiwa wamesimama kando ya moja linalowaniwa kwenye promosheni hii kubwa.
………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Kampeni ya mawakala wa kuuza vinywaji vya Kampuni ya Tanzania Distilleriers Limited (TDL) inayojulikana kama “Nunua, Uza, Shinda na Konyagi ambayo itawezesha washindi kujipatia malori ya usambazaji bidhaa inazidi kupamba moto.
Baadhi ya  mawakala wa kampuni hiyo kutoka mikoa mbalimbali  wanaendelea na mikakati mizito ya usambazaji vinywaji ili kufikia lengo la kuingia kwenye droo kila mmoja akiwa amepania kujishindia lori la zawadi ya kampeni hii.
Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group,George Kavishe, amesema kuwa baada ya kukamilika zoezi la uzinduzi kila kanda ambao umekuwa na mafanikio na kuwashirikisha mawakala wanaouza bidhaa za kampuni hivi sasa kazi kubwa imebaki kwao kufanya mauzo na kufikia viwango vya kuingia kwenye droo ya kupata washindi.
“Dhumuni kuu la kampuni yetu ya TDL kubuni kampeni hii ni  kuwainua wasambazaji wa biashara zetu. Tutaweza kufikia lengo hili kwani washindi wawili katika kampeni hii watajishidia magari mapya mawili ya usambazaji aina ya Eicher  yenye uzito wa tani 3 pia tunazo zawadi mbalimbali ambazo zimetengwa kwa ajili ya kuongeza motisha kwao katika kipindi hiki cha kampeni”alisema
Alisema kampeni itadumu kwa kipindi cha wiki 12 na wasambazaji wanaoshiriki wamewekewa viwango vya mauzo; na washiriki wote watakaofikia vigezo wataingia kwenye droo kubwa ya kupata mshindi mwezi Oktoba mwaka huu . “Tunaamini kabisa kampeni hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao watoongezea chachu ya manunuzi ya bidhaa zetu”.Alisema.
Baadhi ya mawakala wamepongeza jitihada za kampuni kutenga zawadi kubwa za promosheni ambazo zitawawezesha washindi kurahisisha biashara zao badala ya zawadi ndogondogo  zisizoweza kumwinua kimaisha mshiriki.
Mmoja wa wauzaji wa bidhaa ya Konyagi kanda ya Ziwa aliyejitambulisha kama John Masanja amesema kuwa japo sio mawakala wote watapata malori lakini watakaobahatika kushinda watakuwa wamepata zawadi ya uhakika na inayofanikisha biashara kukua. “Kampeni hii ya Konyagi ni kubwa cha muhimu ni kukidhi vigezo vya kuingia kwenye droo ya kumpata mshindi “.Alisema.

Mpango wa Urasimishaji Makazi Holela Jijini Dar waanza kutekelezwa

koc1 
Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji makazi holela toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Betha Mlonda akifafanua kwa waandishi wa Habari kuhusu mpango wa urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholea katika Jiji la Dar es saaam ambao umeanza kutekelzwa katika eneo la Kimara Jijini humo .kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari- Maelezo Bi Fatma Salum na kushoto ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bw. Hassan Mabuye.
koc2 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  na Vyombo vya Habari leo Jijini Dar es salaam.
koc3 
Moja ya eneo lenye makazi holela katika Jiji la Dar es salaam.
koc4 
Mmoja wa Wataalamu wa  upimaji Ardhi akiweka alama katika eneo lililorasimishwa.
………………………………………………………………………………………….
Fatma Salum-Maelezo
Serikali imeanza kutekeleza mpango wa kutambua, kupanga na kupima vipande vya ardhi na kuweka huduma za jamii kama miundombinu ya barabara na mitaro ya maji ya mvua ili kuboresha mazingira ya makazi na kuongeza usalama wa miliki kwa kutoa hatimiliki.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji Makazi Holela kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi. Bertha Mlonda wakati wa mkutano na vyombo vya habari.
Akifafanua Mlonda alisema kuwa mpango huo unatekezwa kwa kushirikiana na Halmashuri zote za Jiji la Dar es salaam na tayari zoezi limeanza katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ambapo wananchi wameonyesha mwitikio mkubwa kwa kuunga mkono juhudi hizo za Serikali .
Akizungumzia vigezo vinavyofuatwa katika urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholela, Mlonda alibainisha kuwa ni pamoja na eneo husika liwe limetengwa kwa ajili ya matumizi ya makazi katika Mpango wa Jumla wa Jiji (Master Plan).
“Mpango huu ni shirikishi, wananchi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana na wataalamu kubainisha mahitaji ya huduma za jamii na miundombinu na siyo makazi holela yote yana sifa ya kurasimishwa. “Alisisitiza Mlonda.
Aidha, alisema kuwa eneo husika ni lazima liwe na idadi kubwa ya watu wanaoishi katika eneo hilo ambao hawana uthibitisho wa uhalali wa kumiliki ardhi hata kama wanalipia ada.
Kigezo kingine ni kuwepo kwa ongezeko kubwa la ujenzi wa nyumba katika eneo husika na idadi kubwa ya wakazi ambao wameishi katika eneo hilo kwa kipindi kirefu.
“Kuna maeneo mengi ambayo wamiliki wanaendelea kuuza mashamba au viwanja vyao na ujenzi wa nyumba mpya kwa ajili ya makazi na biashara unaendelea kwa kasi kubwa; ndio maana tumeona ni vyema tukaanza utaratibu huu wa kurasimisha ili watu wamiliki hayo maeneo kihalali.” Alifafanua Mlonda.
Pia idadi kubwa ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Asasi za Kijamii wamehamasika na wako tayari kushiriki katika mipango ya urasimishaji kwa kuchangia gharama za kupanga, kupima na kumilikisha.
Mlonda alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na viongozi wao wa Serikali za Mitaa kutatua migogoro ya mipaka na kutoa ardhi kwa ajili ya barabara kwani ndio msingi wa ufanisi katika zoezi la urasimishaji makazi.
Makazi holela ni makazi ambayo yamejengwa bila kufuata Sheria, kanuni na taratibu za Mipangomiji. Ujenzi mijini unaongozwa na Sheria ya Mipangomiji namba 8 ya mwaka 2007 na ile ya Serikali za Mitaa sehemu ya mamlaka za miji ya mwaka 1982. ambazo zinaelekeza kupata kibali cha ujenzi kabla ya kujenga nyumba.





WAZIRI MKUU AKATAA KUPOKEA MADAWATI YALIYOTOLEWA NA TFS

MAJALIWA 
Asema huu si wakati wa kupokea vitu vibovu
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekataa kupokea msaada wa madawati uliotolewa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) baada ya kubaini yametengenezwa chini ya kiwango.
“Ofisa Elimu njoo kagua haya madawati yaliyo mazuri nitayapokea na yaliyobaki yarudishwe karakana yakatengenezwe upya huu si wakati wa kupokea vitu vibovu,“ amesema.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Agosti 02, 2016) wakati alipowasili katika kiwanja cha Mabau, Mtibwa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi ambapo alikabidhiwa madawati hayo na Meneja wa TFS
Alisema anatambua dhamira ya TFS ya kuunga mkono jitihada za Serikali za kumaliza tatizo la upungufu wa madawati lakini hawezi kupokea kupokea madawati yaliyotengenezwa chini ya kiwango.
Baada ya Ofisa Elimu (Msingi) wa Wilaya ya Mvomero, Michael Ligola kukagua madawati 102 yaliyoletwa uwanjani hapo madawati 84 yalibainika kuwa ni mabovu na 14 tu ndiyo yalikuwa mazima.
Waziri Mkuu alisema hawezi kupokea madawati hayo yaliyotolewa na Meneja wa Msitu wa Mtibwa, Hamza Kateti na kuuagiza uongozi wa wilaya ufuatilie suala hilo kwa kuwa walitakiwa kuyakagua kabla ya yeye kukabidhiwa.
Katika hatua nyingine aliwasisitiza wazazi na walezi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule na atakayeshindwa atachukuliwa hatua kali za kisheria.
“Serikali imewapunguzia mzigo kwa kuwaondolea michango na ada hivyo tumieni fursa hiyo kwa kuwapeleka shule watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule na wasimamie masomo yao,” alisema.
Awali mbunge wa jimbo la Mvomero, Saddiq Murad alisema miongoni mwa changamoto kubwa inayoikabili wilaya hiyo ni pamoja na wafugaji kuingiza mifugo katika mashamba hivyo amemuomba Waziri Mkuu kuingilia kati suala hilo.
Akizungumzia namna Serikali ilivyojipanga kutatua changamoto ya migogoro baina ya wafugaji na wakulima Waziri Mkuu alisema wafugaji wenye mifugo mingi watahamishiwa katika vitalu vinavyomilikiwa na ranchi za Taifa na wenye mifugo michache watatengewa maeneo katika vijiji.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, AGOSTI 02, 2016.

Ilala yashiriki maonyesho ya Nanenane yanayofanyika mkoani Morogoro

mj1 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema (kulia) akiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Charles Kuyeko (kushoto) wakihojiwa na mwandishi wa habari katika ufunguzi wa Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) iliyofanyika jana tarehe 01.08.2016 mkoani Morogoro.Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
mj3 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema (kulia) akiongea na baadhi ya Madiwani wa Manispaa hiyo katika ufunguzi wa Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) iliyofanyika jana tarehe 01.08.2016 mkoani Morogoro.
mj4Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Msongela Palela (wa pili kushoto) akipata maelezo ya namna ya upandikizaji wa mbegu za samaki kwa njia za kisasa  toka kwa Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Msongo Songoro (kulia)  katika ufunguzi wa Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) iliyofanyika jana tarehe 01.08.2016 mkoani Morogoro.
mje5 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando (kulia) wakijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Msongela Palela (kushoto) alipotembelea banda la maonyesho la Manispaa hiyo katika ufunguzi wa Sikukuu ya Wakulima (Nanenane)  iliyofanyika jana tarehe 01.08.2016 mkoani Morogoro.

DC ILALA,SOPHIA MJEMA AZINDUA UWANJA WA NETIBOLI NA KIKAPU SHULE YA JANGWANI

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akifunga goli wakati wa uzinduzi wa
uwanja wa Netiboli na Mpira wa Kikapu wa Shule ya Sekondari ya Jangwani
uliojengwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo
kupitia kampeni yake ya “Be Kidotified”.  Mjema alizindua uwanja huo leo
katika hafla fupi iliyofanyika katika shule hiy.Kushoto ni Jokate
akishuhudia tukio hilo.
PICHA NA MICHUZI JR
 Mkuu wa  Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto) akitoa hotuba yake
katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli
uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo (kushoto). Wa pili kushoto ni
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez
akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule Msaidizi wa
shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo (Kushoto)
akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa uwanja alioujenga kupitia
kampeni yake ya “Be Kidotified” uliomgharimu kiasi cha Sh Milioni 50. Wa
pili kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara
Gonzalez akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule
Msaidizi wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa. 
Mrembo wa zamani wa Tanzania, Faraja Kota akizungumza mbele ya Wanafunzi
katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli
uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo.
 
 Mandhari ya uwanja wa Mpira wa Kikapu na Netiboli wa shule ya Sekondari ya
Jangwani uliojengwa na Mrembo, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya
“Be Kidotified”.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala pichani kati Mh.Sophia Mjema akiwasili kwenye hafla
fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa Netiboli na Kikapu wa shule ya
Jangwani leo jijini Dar,Pichani kulia ni Katibu Tawala wilaya ya
Ilala.Ndugu Edward Mpogolo na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya Kidoti, Jokate Mwegelo.
……………………………………………………….
 Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema alisema kuwa
amefurahishwa na mpango huo wa Jokate kwa kusaidiana na Mo Dewji
Foundation na kuwaomba kuuendeleza kwa shule nyingineza jijini.
Mjema alisema kuwa Dar es Salaam kuna shule nyingi na angependa kuona hata
shule za Chanika zinafaidika na kampeni ya “Be Kidotified”. Alisema kuwa
amefarijika sana kuona shule aliyosoma yeye kufaidika kwa mradi huo na
kuwaomba wanafunzi na walimu kuutumia uwanja huo kama fursa ya
kuendeleza michezo na taaluma.
Wakati huo huo Mrembo mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya kuchangia
jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified” amejenga uwanja
utakaotumika kwa ajili ya michezo ya mpira wa kikapu na Pete (netiboli)
kwa Shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani. 
Uwanja huo ulizinduliwa jijini leo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye shule
hiyo na kuhudhuriwa na wanafunzi, walimu na viongozi mbalimbali wa
serikali. Ujenzi wa uwanja huo umemgharimu Jokate kiasi cha Shilingi
milioni 50. Akizungumza katika uzinduzi huo, Jokate alisema kuwa ameamua kuonyesha mfano kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo ya
michezo nchini hasa kwa katika shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya
sekta hiyo hapa nchini. Mbali ya michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha
zaidi na maendeleo ya elimu hapa nchini. 
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ya Tanzania imeadhimia kuondoa
changamoto nyingi katika elimu na yeye kuamua kuanzia katika masuala ya
michezo ambayo uchangia ufaulu darasani na kuibua vipaji ambavyo
vitamwezesha mshiriki kupata ajira. 
Alisema kuwa moja ya changamoto kubwa zinazorudisha nyuma maendeleo ya michezo
nchini ni ukosefu wa viwanja bora ambavyo ukwamisha wachezaji chipukizi
kuonyesha vipaji vyao ipasavyo. 
Kwa mujibu waJokate, alipokuwa anasoma, alikutana na changamoto hizo,
lakini alipiga moyo konde na kujihusisha na shughuli mbalimbali za nje
ya darasa ikiwa pamoja na michezo na kujifunza mengi. 
“Mimi ni mjasiriamali mchanga sana hapa nchini, nimehamasisha kwa kile kidogo
nilichonacho na kwa msaada wa wadhamini niliyotafuta kuhitimisha ujenzi
wa uwanja huu ambao utatumika si kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya
Jangwani pekee, bali hata kwa mechi za shule nyingine, ” 
“Nawapongeza wadhamini walioniunga mkono katika mpango huu kama Mo Dewji Foundation,
na wadau ambao walikuwa nyuma yangu katika kuhakikisha kampeni ya ‘Be
Kidotified’ inaanza kwa mafanikio makubwa na kuendelea kwa shule
nyingine za hapa jijini,” alisema Jokate. 
Alisema kuwa chapa ya Kidoti ni miongoni mwa chama zinazoongoza hapa nchini
katika mitindo, urembo na burudani kabla ya kuamua kupanua wigo kwa
upande wa michezo tofauti na mpira wa miguu. 
Alifafanua kuwa alianza kwa kuanzisha kampuni ya Kidoti (Kidoti Company) na
kuchangia katika soko la ajira nchini na baadaye kuanzisha “kidoti
brand’ akiwa na lengo la kuhamasisha vijana kujihusisha katika shughuli
mbalimbali za ujasiriamali ili kuweza kukabiliana na maisha ya kila
siku.

MIKATABA YA WACHEZAJI VPL, FDL

images 
Shirikisho la Mpira wa MiguuTanzania (TFF) linapenda kuzikumbusha timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwamba hatutatoa leseni ya mchezaji yeyote ambaye timu haikuleta mkataba wakati wa maombi ya usajili, hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 68 vipengele vya 1, 2, 3 na 8 ya Ligi Kuu ya Tanzania toleo la 2016/2017.
Kila timu inatakiwa kuleta nakala tatu za mkataba wa mchezaji, ili kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji iweze kupitia na TFF iweze kuidhinisha mikataba hiyo. Baada ya hapo timu na mchezaji, watakuja kuchukulia mikataba hiyo hapa TFF. Na kumbuka kanuni ya 68(8) inataka kulipia kiasi cha sh 50,000 kwa kila mkataba wa mchezaji.
Ni matarajio yetu kuwa kila klabu itatimiza wajibu wake ili kuondoa migogoro kati ya timu na mchezaji na mchezaji na timu. Tunategemea kupata ushirikiano.
Kadhalika, kwa mujibu wa kanuni 67 vipengele vya 1, 2, 3 na 8 ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania ya StarTimes, Shirikisho la Mpira wa MiguuTanzania (TFF) linakumbusha kwamba halitatoa leseni ya mchezaji yeyote ambaye timu haikuleta mkataba wakati wa maombi ya usajili.
Kila timu inatakiwa kuleta nakala tatu za mkataba wa mchezaji, ili kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji iweze kupitia na TFF iweze kuidhinisha mikataba hiyo. Baada ya hapo timu na mchezaji mtakuja kuchukulia mikataba hiyo hapa TFF. Na kumbuka kanuni ya 67(8) inataka kulipia kiasi cha sh 25,000 kwa kila mkataba wa mchezaji.
Pia katika hili tunategemea kila timu itatimiza wajibu wake ili kuondoa migogoro kati ya timu na mchezaji na mchezaji na timu.

NAIBU WAZIRI SULEIMANI JAFFO AHIMIZA USAFI KWENYE MAJIJI,AKAGUA MAGARI MAALUMU JIJINI ARUSHA

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kusimamia na kutumia mitambo na magari ya kisasa ya kukusanya Taka ngumu kwenye majiji na halmashauri zilizopo kwenye mpango wa kuendeleza miji kimkakati unaosimamiwa na Ofisi ya Rais kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia,kushoto ni Mratibu wa Mradi huo,Mhandisi Davis Shemangale na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mrisho Gambo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya usimamizi miundombinu ya ukusanyaji Taka ngumu wakimsikiliza Naibu Waziri,Suleimani Jaffo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo(aliyevaa tai nyekundu) akiwa ujumbe ofisi yake na watumishi  wa halmashauri ya Jiji la Arusha wakati akikagua eneo lililotengwa kwaajili ya kuchomea taka ngumu lilipo Dampo Kuu jijini humo katika mpango wa kuendeleza miji kimkakati unaosimamiwa na Ofisi ya Rais 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo akikagua Dampo la Jiji la Arusha liliboreshwa miundombinu yake  kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mrisho Gambo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Sehemu ya magari maalumu yatakayohusika kukusanya Taka ngumu kutoka mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha.
Naibu Waziri Jaffo alitaka mitambo hiyo itumike kwa malengo yaliyokusudiwa na kufanyiwa matengenezo kila mara ili iwe endelevu na kuongeza kuwa serikali imeshaweka mikakati ya miji yote kuwa misafi.

PONDAMALI, MANYIKA DARASANI TFF

index 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limefanikiwa tena. Safari FIFA – Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu limeipa nafasi Tanzania kuwapa mafunzo ya juu ya ukocha wa makipa (Advanced Goalkeeping Coach Course) ikiandika historia kuwa nchi ya pili barani Afrika kwa makocha wa nafasi hiyo baada ya Botswana.
Makocha wa makipa 25 hususani wa wa timu za taifa, timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wanahudhuria kozi hiyo inayoongozwa na Alejandro Heredia ambaye ni Mkufunzi kutoka FIFA.
Makocha hao ni Peter Manyika (Taifa Stars ya Tanzania), Saleh Ahmed (Zanzibar Heroes); Muharami Mohammed (Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys); Mohammed Silima (Timu ya Taifa ya Vijana Zanzibar) na Elyutery Mhoery (Timu ya Taifa ya Wanawake – Twiga Stars) na msaidizi wake ambaye pia anachezea JKT Queens, Fatuma Omary.
Wengine ni makocha maarufu wa makipa wakiwamo Juma Pondamali (Young Africans); John Bosco (Majimaji ya Songea); Salimu Tupa (Tanga); Bakari Ali Hamadi (Wete Pemba – Zanzibar); Hafidh Muhidin Mcha (Mkoani Pemba – Zanzibar); Mussa Wanena (Kagera Sugar); Juma Bomba (African Lyon), Adam Abdallah Moshi (Simba SC), Idd Mwinchumu (Azam FC) na Hussein Tade (Seeb Club-Oman/Toto African)
Pia wamo Khalid Adams (Mwadui FC); Josia Steven (Mbeya City); Herry Boymanda (Tanzania Prisons); Emmanuel Mwansile (Polisi Morogoro); Ben Kalama (Stand United); Abdallah Said (JKT Ruvu); Patrick Mwangata (Mtibwa Sugar); Augustin Malindi (Mkoa wa Kigoma); Raphael Mpangala (Ndanda FC); Salimu Tupa (Tanga) na nAbdul Mgude (Coastal Union ya Tanga).
“Mjione kwamba mmepewa kipaumbele,” alisema Heredia akiwanoa makocha hao na kuongeza: “Kinachohitajika sasa ni juhudi tu. Kozi hii haijafanyika pengine hapa barani Afrika zaidi ya Botswana. Mjue kuwa mna bahati.”
Akitoa nasaha wakati wa ufunguzi wa kozi hiyo, Makamu Rais wa TFF, Wallace Karia aliishukuru FIFA na CAF kwa namna inavyoshirikiana na TFF katika kuwapa kozio nyingi za makocha wa timu kwa wachezaji wa mbele, makocha wa makipa na waamuzi wa madaraja tofauti.
“Hakuna kipindi TFF imepata kozi za makocha nyingi za makocha kama kipindi hiki cha uongozi wa Jamal Malinzi,” anasema Karia na kuongeza: “Tumetoka kwenye kozi ya makocha wa Daraja A sasa tuko kwenu. Lengo ni Tanzania kuwe na makipa wazuri. Ninyi mtaleta makipa wazuri. Na hii ni kwa manufaa ya sasa na baadaye kwa upende wetu, timu zetu na taifa kwa ujumla.”
Karia aliwatia hamasa makocha hao wanaoshiriki kozi hiyo kuwa, mara baada ya kozi hiyo ipo siku watakwenda kuwa wakufunzi nje ya mipaka ya nchi kadhalika makocha ambao wanaweza kupata kazi mahala popote duniani hasa ukizingatia walimu wa daraja lao wako Tanzania na Botswana tu.
Kadhalika, Makamu huyo wa Rais wa TFF alielezea kuwa mpira wa miguu una changamoto nyingi na nyingine husababishwa na watalaamu hao kubweteka kwa mafanikio. “Hili ni tatizo. Tubadilike kifikra na kivitendo. Msilaze damu, kuweni active (mahiri).”

SERIKALI ZETU ZINATAMBUA MCHANGO WA WANADIASPORA

index 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinatambua mchango mkubwa wa Wanadiaspora na ndio maana hutayarisha makongamano ambayo hutoa fursa ya kujadili masuala mbali mbali ya kimaendeleo kwa lengo la kuimarisha uchumi wa Tanzania na ustawi wa wananchi wake.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Salum Maulid Salum aliyasema hayo leo huko Ikulu Mjini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na waandishi wa Habari mbali mbali kutoka Redio za FM zinazofanya kazi zake hapa Zanzibar kuhusu Kongamano la Diapora la Tanzania linalotarajiwa kufanyika hapa Zanzibar mwaka huu.
Katika maelezo yake Katibu Mkuu huyo aliyekuwa pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Silima Kombo Haji, alisema kuwa kwa miaka miwili iliyopita makongamano hayo yamefanyika  Dar-es-Salam na kusisitiza kuwa mikutano iliyokwisha fanyika imeweza kuleta mafanikio makubwa.
Alisema kuwa Mkutano wa mwaka huu unatarajiwa kufanyika hapa Zanzibar kwa muda wa siku mbili kati ya tarehe 24 na 25 linatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli huko katika ukumbi wa hoteli ya  Zanzibar Beach Resort.
Katibu Mkuu huyo alisema kuwa mada mbali mbali zinatarajiwa kutolewa katika Kongamano hilo ambalo  kauli mbiu yake ya kila mwaka ni “Mtu kwao ndio Ngao’ ambapo pia, ujumbe mkubwa kwa mwaka huu ni “Mtizamo mpya wa Kuimarisha Utalii wa Tanzania na uekezaji”
Katika melezo yake Katibu Salum alisema kuwa tayari matayarisho ya kongamano huo yanaendelea vizuri na kueleza kuwa Wanadiaspora wamekuwa na mwamko mkubwa katika ushiriki ambapo kila mwaka idadi ya ushiriki wao imekuwa ikiongezeka huku akieleza kuwa vyombo vya habari zikiwemo Redio za FM, vina nafasi kubwa katika kuwaeleza wananchi juu ya mkutano huo.
Aidha, alisema kuwa miongoni mwa mafanikio yaliopatikana ni pamoja na Wanadiaspora wengi wa hapa nchini wameweza kutoa michango yao mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha mirado mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ya afya, elimu na mengineyo.
Katibu Mkuu huyo alitumia fursa hiyo kueleza juhudi za viongozi hapa nchin i katika kuhakikisha suala hilo linaimarika huku akitolea mfano juhudi za makusudi zinazochukuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika kuhakikisha ushirikiano kati ya Wanadiaspora na Serikali zote mbili unaimarika.
Nae Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Silima Kombo Haji aliwaeleza waandishi hao wa habari faida zinazopatikana kutokana na kuunganishwa kwa Wanadiaspora hapa nchini pamoja na changamoto zilizopo.
Balozi Silima alizitaja baadhi ya nchi zilizopo ndani na nje ya Afrika ambazo zimenufaika na zinazaendelea kunufaika kutokana na Wanadiaspora wa nchi zao zikiwemo Kenya, Ethiopia, Ghanam Idia, Pakistan, Ufilipino, Bangladesh na nyenginezo.
Sambamba na hayo, Balozi Silima alisema kuwa serikali zote mbili zimeweka mikakati maalum ya kuhakikisha Wanadiaspora wanapewa kipaumbele sambamba na kushirikishwa katika masuala mbali mbali ya maendeleo kwa nchi yao.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

WASANII, WATANGAZAJI NA WATU MAARUFU KUVUNA MAPESA KUTOKANA NA MITANDAO YAO YA JAMII

Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga alielezea machache mbele ya wageni na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo juu ya huduma mpya ya matangazo katika bara la Afrika utakaowanufaisha watangazaji, wasanii na watu maarufu uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel na Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa Binary, Eni Kihedu. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel (katikati) akimsifia msanii Diamond Platinumz kwa jinsi ambavyo amekuwa akiitanga Tanzania nje ya nchi kwa muziki wake.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabrielakimsifia Wema Sepetu jinsi ambavyo amekuwa akilitunza jina lake.
 Msanii Diamond Platinuz akitoa shukrani zake za pekee kwa niaba ya wasanii walihudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga (kushoto) akizunguza na Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel wakati wa uzinduzi wa huduma ya matangazo kutumia teknolojia ya kidigitali ambayo itawezesha watangazaji wa biashara kutangaza biashara zao kwa kuwatumia wasanii na watu maarufu katika jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni ni
Wageni waalikwa waliohudhuria shughuli hiyo.
Wasanii waliohudhuria shughuli hiyo.
Waandishi nao hawakuwa nyuma kufuatilia tukio.
Huduma ya matangazo kidigitali kwa kutumia wasanii na watu maarufu yaanzishwa nchini.
Kampuni inaoongozwa kwa kutoa huduma ya matangazo ya biashara nchini ya Aggrey & Clifford imezindua kitengo cha kutoa huduma ya matangazo kutumia teknolojia ya kidigitali ambayo itawezesha watangazaji wa biashara kutangaza biashara zao kwa kuwatumia wasanii na watu maarufu katika jamii ambayo itanufaisha pande zote zitazoshiriki kutumia huduma hii .
 
Huduma hii ya kisasa inayoendana na wakati wa sasa wa kizazi kipya inawezesha matangazo kuwafikia walengwa wengi na kwa haraka inasimamiwa na kampuni tanzu ya masuala ya huduma za matangazo ya biashara kwa kutumia teknolojia ya kidigitali ya Aggrey&Clifford inayojulikana kama Binary.
 
Uzinduzi wa kitengo hiki cha matangazo kwa kutumia teknolojia ya kisasa itakayoleta mapinduzi katika sekta ya matangazo ya biashara nchini umefanyika jana katika hoteli ya Hyatt Regency ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel na ilihudhuriwa na wataalamu wa masoko kutoka makampuni ya FMCG, huduma za mawasiliano,mabenki na taasisi mbalimbali za biashara ikiwemo wasanii na wanamichezo.
 
Kampuni ya Binary kwa kuanza tayari inashirikiana na wasanii na watu maarufu Zaidi zaidi ya 40 ambao miongoni mwao wapo wasanii wa filamu,wanamuziki,watangazaji maarufu wa redio na luninga. Kutokana na ushirikiano huu Binary itawatumia katika huduma za matangazo za wateja mbalimbali wanaotangaza huduma na bidhaa zao kidigitali ili kuwafikia watumiaji wa huduma/bidhaa wengi na kwa urahisi.
 
Huduma hii mpya ya matangazo katika bara la Afrika unanufaisha watangazaji kwa huduma zao kuwafikia wananchi ama wateja wengi kutumia umaarufu wa wasanii na watu maarufu ambao pia wananufaika kwa kupata mapato ya uhakika kutokana na kutumiwa kwao katika huduma ya matangazo na pia ina unafuu kulinganisha na njia nyingine za matangazo.
 
Profesa Elisante Ole Gabriel alisema kuwa serikali inao dhamira ya kuwasaidia wasanii wa tasnia mbalimbali na wanamichezo na alipongeza kuanzishwa kwa huduma hii nchini ambao itaongeza ajira na vipato vya wasanii wakati huohuo kunufaisha makampuni kwa njia ya matangazo ya biashara zao.
 
Naye Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa Binary, Eni Kihedu amesema “Huduma hii mpya ni jukwaa la aina yake lya matangazo ya baiashara kwa kuwa inawezesha matangazo kuwafikia walengwa kwa asilimia 100% kwa kulinganisha na kutangaza kwa kutumia magazeti na ama majarida na inaleta unafuu kwa watangazaji ambao kwa kutumia mtandao wasanii zaidi ya 40 ambao tunashirikiana nao kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii matangazo yataweza kuwafikia watumiaji wa bidhaa na huduma zaidi ya milioni 20 nchini na tunao uwezo wa kufikia watu wengi zaidi”.
 
Kuhusiana na huduma hii mpya ya matangazo itakavyonufaisha wasanii Kihedu alisema “Tunatumia fursa ya kutumia teknolojia ya digitali katika biashara ambayo itaongeza vipato vyao wakati huohuo vipaji vyao kuendelea kuonekana kwa watu wengi katika jamii na kuwawezesha kuwekeza zaidi kwenye fani yao na tasnia yao”
 
Aliongeza kuwa ushirikiano wa Binary na wasanii katika huduma za matangazo utafanyika kwa uwazi na kunufaisha pande zote na kutafanyika makubaliano maalumu ya malipo kutokana na viwango vinavyotozwa kwa kila tangazo litakalowekwa kwenye akaunti za mitandao yao ya kijamii na kulingana na wafuasi wanaotembelea akaunti zao.
 
“Viwango vya matangazo viko wazi kwa watangazaji na wasanii hivyo tunaamini kila upande utanufaika inavyostahili .Tunaamini njia hii ni jukwaa la aina yake kwa watangazaji kufikisha matangazo yao kwa wateja wanaowalenga kwa kuwa njia zilizokuwa zinatumika awali kutangaza hazina nafasi tena kutokana na mabadiliko ya tekonolojia“.Alisema

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI YAJIPANGA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA UFINYU WA BAJETI

muh
Hospitali ya Taifa Muhimbili imekuwa na mafanikio kadhaa katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Mafanikio haya ni pamoja na uwepo huduma ya uhakika ya tiba ya figo na kuchuja damu, ikiwa ni jumla ya mashine ambapo kwa sasa kuna mashine 17, kuboreshwa kwa huduma ya magonjwa ya matumbo na ini. Aidha tumeanza kwa muda kufanya upasuaji kwa njia ya hadubini (Laparascopic Surgery )hususani kwa magonjwa ya masikio, pua na koo, na katika eneo hili idara husika naongoza katika matumizi ya technologia hii mpya.  Tumeanza upasuaji wa macho kwa kutumia vifaa vya kisasa (retina surgery), kuimarisha huduma za Uuguzi (Super Specialists Nursing care in Critical Care, Mental Health). huduma nyingine zilizoboreshwa ni kupanua Idara ya Kinywa na Meno (Preventive Dentistry na Pediatric Dentistry). Kwa upande wa Maabara kuwa na vifaa vipya vya kisasa katika kuhakikisha huduma hiyo inatolewa kwa ubora wa hali wa ya juu. Kuna mashine mpya ya Architect Analyzer C4100 ambapo mashine moja inaweza kupima vipimo zaidi ya 1,200 kwa saa moja ili kupunguza muda wa wagonjwa kusubiri majibu kwa muda mrefu.  Uwepo wa famasi mbili zinazofanya kazi kwa saa 24  na kuhakikisha idara zote 18 za tiba zina watalaam wa ubingwa wa juu (superspecialist).
Pamoja na mafanikio haya, pia imekuwa inakabiliwa na changamoto mbalimbali za uendeshaji na katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa zinazojumuisha upungufu wa rasilimali fedha. Katika makala haya, Hospitali imejipanga kutekeleza yafuatayo ili kukabiliana na changamoto;
Kuongeza Mapato na Kupunguza Gharama za Uendeshaji.
Hospitali imejipanga katika kuongeza mapato na kupunguza matumizi ili kuongeza uwezo wake wa kujiendesha na kutoa huduma za ufanisi kwa wagonjwa.
Kuongeza Mapato
Hospitali imeweka mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato ikiwemo:-

CCM ZANZIBABAR YASISITIZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA DR.MAGUFULI.

index 
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewasisitiza watendaji wa  Chama na Jumuiya zake  kuharakisha zoezi la kuhorodhesha Mali za taasisi hizo ili kutekeleza kwa vitendo agizo la chama hicho.
Akizungumza na watendaji wa chama, jumuiya na watumishi wa  chama hicho wa ngazi mbali mbali , Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai huko afisi kuu ya CCM Kisiwanduzi Unguja.
Alifafanua kwamba hatua hiyo inatokana na agizo la Mwenyekiti mpya wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli aliyetaka mali za chama hicho kuhorodheshwa haraka kwa lengo la kuimarisha chama hicho.
Alisema kwamba CCM Zanzibar ilianza utaratibu wa kukagua mali zake kabla ya Mwenyekiti huyo kutoa agizo hivyo anatarajia kwamba watendaji hao watatekeleza kazi hiyo haraka na kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa ili kuepuka usumbufu usiokuwa wa lazima.
Alieleza kwamba licha ya Chama kupata ruzuku kutoka serikali bado kina wajibu wa kutumia rasilimali zake vizuri kuongeza vyanzo vya mapato ili kuongeza ufanisi wa kiutendaji ndani ya chama hicho.
Alisema hatua ya kuhorodhesha mali za chama hicho iambatane na kumaliza kasoro na mapungufu yaliyopo katika miradi ya chama na jumuiya hasa kupitia upya mikataba ya ukodishwa ili kuhakikisha inakidhi na kufuata utaratibu wa kisheria.
“ Nawakumbusha watendaji wenzangu wa CCM kwamba tujiandae vizuri kifikra kwa kuhakikisha tunafanya kazi kwa bidii kubwa na kuacha tabia za kufanya kazi kwa mazoea kwani huu ni wakati wa mabadiliko kwa kila sekta ndani ya chama chetu.
Pia mnajua kwamba chama chetu hivi karibuni kumefanyika Mkutano Mkuu Maalum na kumpata Mwenyekiti Mpya Dkt. Jonh Pombe Magufuli atakayesaidiana na Makamo Mwenyekiti wake Dkt. Shein kuhakikisha wanaendeleza kuimarisha na kukuza ustawi wa CCM, hivyo nasi ni lazima twende sambamba na kasi ya utendaji wao.”., alisema Vuai.

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YAANZISHA KIFURUSHI KIPYA MAHSUSI CHA MIITO NA DATA KATIKA TAMASHA LA FIESTA 2016

 Meneja Chapa wa Kampuni ya Simu ya Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Kampuni hiyo, Kijitonyama Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu kampuni hiyo kuanzisha kifurushi kipya mahsusi cha miito na data katika tamasha la Fiesta 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tamasha la Fiesta, Sebastian Maganga.
 Mwenyekiti wa Tamasha la Fiesta, Sebastian Maganga (kushoto), akizungumzia kukamilika kwa maandalizi ya tamasha hilo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 
Na Dotto Mwaibale
 
KAMPUNI ya simu ya Tigo  imetangaza vifurushi viwili vipya vya miito na data vinavyofahamika kama  ‘Vifurushi vya Fiesta’ (Fiesta packages) ambavyo vinalenga kuwanufaisha watega wote wa Tigo na wasio wakati wa tamasha la Fiesta 2016. 
 
Vifurushi hivi vya kuvutia vitakuwa vinapatikana kwa wateja wote watakaohudhuria matamasha  na hata wasio hudhuria.
 
Vifurushi vipya vitawawezesha  wateja  kuchagua kati ya data za GB 1 au visivyo na ukomo ambavyo vinajumuisha  dakika 490 Tigo kwenda Tigo, dakika 10 mitandao yote  na SMS 100 kwa shilingi 1000 wakati wale ambao sio wateja wa Tigo ambao wamenunua kadi ya simu ya 4G ya Tigo watapata dakika 60, sms 60 na MB 60 papo hapo pindi wanapojisajili na baadaye  kuchagua kati  ya data na kifurushi kisicho na ukomo.
 
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya Tigo, Meneja Chapa, William Mpinga alisema, “vifurushi hivi  vimekuwa ikiwa ni ahadi tulioyoitoa kwa wateja wetu  kuhusu ofa mbalimbali na promosheni  ambazo zitakuwepo  wakati wa msimu wa Fiesta 2016. Hali kadhalika tutaendelea na uanzishaji wa bidhaa na huduma za ubinifu  ili kukidhi mahitaji  ya wateja wetu na pia kutoa nafasi kwa wateja wapya.”
 
Mpinga alifafanua kuwa tamasha la Fiesta 2016 linawakaribisha Watanzania wote  na kuongeza kuwa pia tukio hilo litatoa shughuli zenye mabadiliko  kijamii.
 
Mpinga alisema, “Mwanzoni wa wiki iliyopita tulianzisha kauli mbiu ya tamasha la fiesta inayosema, “Fiesta 2016 Kwa Kishindo cha Tigo, Imooooo!” ambapo mantiki iliyopo katika kauli mbiu hii  ni kutoa bidhaa na huduma ambazo ni mahsusi kwa wateja wetu  katika kipindi cha tamasha.”
Mwenyekiti  wa Tamasha la Fiesta 2016, Sebastian Maganga  alisema, “ Tunafurahi sana kutangaza kwamba tamasha la Fiesta 2016 litaanza rasmi jijini Mwanza Agosti 20, 2016. Kwa hiyo wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake   watarajie kupata vifurushi hivi maalum pamoja na shughuli za kufurahisha  katika kipindi cha wiki nzima  kabla ya tamasha.”
 
Tamasha la Fiesta 2016  linaandaliwa kila mwaka na kampuni ya Prime Time Promotions, na hivi sasa ni mwaka wa 15 tangu kuanziswhwa kwake na  linatarajiwa   kujumuisha mikoa 15 ambayo ni pamoja na Mwanza, Kahama, Kagera, Musoma, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Mtwara, Iringa, Mbeya na Dar es Salaam.
 
Tamasha la Fiesta 2016 linafanyika kwa ushirikiano wa Prime Time Promotions na Tigo Tanzania ambayo ni mdhamini mkuu.  
 

TIMU TEULE ZA JESHI KUKABIDHIWA BENDERA KWA AJILI YA KUELEKEA RWANDA KESHO(LEO)

mkuu3Wanariadha wa Timu Teule ya JWTZ wakifanya mazoezi katika Kambi iliyoko Mbulu Mkoani Manyara.
Picha na Maktaba
…………………………………………………………………………………….
Na mwandishi wetu JWTZ
Timu teule za Jeshi la wananchi wa Tanazania zinazotarajiwa kushiriki mashindani ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki zinatarajiwa kukabidhiwa bendera ya Taifa Kesho(Leo) tayari kuelekea Kigali chini Rwanda kwa ajili ya mashindano hayo.
Kwa Mijubu wa Afisa habari wa Michezo  Kutoka makao Makuu ya Jeshi Luteni Selemani Semunyu alisema mkuu wa Operesheni na mafunzo Meja Jenerali Issa Nassoro ndiye anayetarajiwa kukabidhi bendera hiyo kwa Niaba ya Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.
Luteni Semunyu alisema kuwa Hatua hiyo inafikiwa baada ya Timu hizo kuweka kambio katika Visiwa vya Zanziba kwa Michezo minne huku Riadha wakiweka kambi Arusha kabla ya kambi hiyo kuhamishiwa mbulu Mkoani Manyara kutokan na haliya hewa.
Aliitaja Michezo hiyo kuwa mpira wa miguu,pete,Mikono,Kikapu na Riadha  ambapo wachezaji wako katia ari ya hali ya juu kutokana na wito wa mkuu wa majeshi kuwatak kurejesha hshima ya JWTZ katika Michezo.
ASlifafanua kuwa QWachezaji wa Timu hizo teule walipatikana baada ya kupitia hatua mbali mbali za mcvhujo kwa kuanzi na kombe la Mkuu wa majeshi ambalo lilishirikisha kuanzia ngazi ya Viko mpaka kamandi na hivyo kuibua vipaji.
Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki imekuwa ikifanyika kila mwaka kwa kuhama nchi wenyeji kutoka na utarativbu waliojipangia nchi wananchama ndio maan mwaka huu yanafanyika nchini Rwanda na Mwakani yatahamia katika nchi nyingine amabayo itatangazwa baada ya kumalizika mashindano haya.
Timu teule za Jeshi zinatarajia kuanza safari kuelekea Kigali nchini Rwanda Agosti nne siku moja baada ya kukabidhiwa bendera ili kuwahi ratiba ya kuanza mashindano hayo yanayotarajia kuanza Agosti saba na Kumalaizika Agosti 17.

MHE. KAIRUKI KATIKA KIKAO KAZI WATUMISHI KUJADILI MATUMIZI YA TEHAMA SERIKALI

SONY DSC
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (aliyeinua mkono) alipokuwa akifafanua jambo wakati wa kikao kazi na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais- Utumishi kuhusu utoaji huduma na matumizi ya TEHAMA katika Utumishi wa Umma  kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi leo, wa tatu kulia (mstari wa mbele) ni Naibu Katibu Mkuu Utumishi na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi.
SONY DSC
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akielekeza jambo kwa baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais Utumishi wakati wa kikao kazi kuhusu utoaji huduma na matumizi ya TEHAMA kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi leo.
SONY DSC
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimsikiliza Mkurugenzi wa TEHAMA katika Utumishi wa Umma, Bw. Priscus Kiwango  wakati wa kikao kazi kuhusu utoaji huduma na matumizi ya TEHAMA katika Utumishi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi leo.
SONY DSC
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakijadili kuhusu matumizi ya TEHAMA katika utoaji huduma Serikalini wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi leo.

RIDHIWANI:VIJANA WAJITAMBUE WAACHE KUTUMIWA /WACHANGAMKIE FURSA ZILIZOPO

index1 
Mbunge wa jimbo la  Chalinze Ridhiwani  Kikwete, akizungumza na vijana wa Chalinze Saccos iliyoanzishwa jimboni hapo ambapo Ridhiwani  ni mlezi wa saccos hiyo(Picha na Mwamvua Mwinyi)
index2 
Vijana wa Chalinze saccos wakiwa katika mkutano uliolenga kuzungumzia masuala mbalimbali ya saccos hiyo ambapo pia walimchagua mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kuwa mlezi wao.(Picha na Mwamvua Mwinyi) 
………………………………………………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
MBUNGE wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete amewataka vijana wajitambue na kuacha kutumiwa kama ngazi na baadhi ya watu kwa ajili ya maslahi yao binafsi na badala yake wajikite kwenye shughuli ndogondogo za kujiongezea kipato.
Aidha mbunge huyo amekubali kuwa mlezi wa Chalinze vijana saccos ambayo itakuwa mfuko wa kuwezesha vijana kiuchumi na kutambulishwa fursa mbalimbali za kimaendeleo.
Ridhiwani aliyasema hayo, kwa vijana mbalimbali mjini Chalinze katika mkutano wa kuchagua viongozi wa muda mfupi wa saccos hiyo na mlezi pamoja na kujadili masuala ya kimaendeleo .
Alisema vijana wabadilike kwa kuchangamkia fursa zilizopo sanjali na kujiajiri ili hali kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira.
Ridhiwani alisema ipo tabia kwa baadhi ya vijana ambao hushawishiwa kujiingiza kwenye mambo yasiyo na tija katika maisha yao kuliko kuwashawishi kuwajengea uwezo wa kuinua uchumi wao kimaisha.
Aliwaasa vijana kujitambua kwa kutumia fursa chache zilizopo ikiwemo kuanzisha vikundi vya kiujasiliamali,kutumia mafungu ya fedha zinazotengwa na halmashauri,licha kuwepo changamoto za mtaji .
Ridhiwani alisema yupo bega kwa bega na vijana hao bila kujali itikadi za kisiasa ambapo atahakikisha anawaonyesha fursa mbalimbali.
“Tatizo ni kwamba vijana hawajazitambua fursa ama kushindwa kuzitumia,kwa upande mmoja na kwa upande mwingine wale walioziona hawana uwezo wa kifedha ili kuzifikia”alisema Ridhiwani.
Ridhiwani alieleza kuwa ni imani yake  kama mlezi wa saccos hiyo kuwaonyesha fursa zilipo na kuzitumia huku akishirikiana nao kupata mitaji kwa kutumia wafadhili,halmashauri na taasisi zinazojishughulisha na masuala ya kusaidia vijana.
Hata hivyo Ridhiwani alisema ameshawezesha vijana wengi jimboni hapo kujikwamua kiuchumi lakini changamoto ipo kwenye kujitambua na kumtumia katika kumfikisha kijana husika katika hatua nzuri kimaisha.
Aliwaasa vijana kuwa na moyo wa kuwa na maendeleo pale wanapopata mtu wa kuwainua bila ya kufanya makosa ya kutumia nafasi wanayoipata na hatimae kujutia baadae.
Ridhiwani aliwataka vijana kujiunga makundi katika shughuli zao na kuacha ubinafsi ili kuweza kusaidiwa na kufikiwa kirahisi kuliko kuwa mmoja mmoja.
Kwa upande wa vijana hao wa halmashauri ya Mji wa Chalinze kwa ujumla wao walimchagua Ridhiwani kuwa mlezi wao .
Walisema wameamua kwa pamoja kuunga mkono hatua za serikali kuwezesha vijana kiuchumi kupitia vicoba na saccos.
“Tumeanzisha Chalinze vijana saccos,ambayo itakuwa mfuko wa kuwezesha vijana kiuchumi na kutambua fursa za kuzikimbilia ili kujikomboa katika kupiga vita umaskini’walisema.

MADIWANI MJI WA KIBAHA WAWAASA WATENDAJI/WATAALAMU WA HALMASHAURI KUSIMAMIA ILANI

index 
Madiwani mbalimbali wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, wakiwa katika kikao cha baraza la  madiwani ambacho kilijadili na kupitisha agenda ikiwemo taarifa ya maendeleo ya kata,kupokea taarifa ya mapato na matumizi ambapo waligomea kupitisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka jana  baada ya kubaini mapungufu makubwa.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
……………………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MADIWANI wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,wamewataka wataalamu na watendaji wa halmashauri hiyo kuwa makini katika kuandaa taarifa mbalimbali ikiwemo ya utekelezaji wa ilani ili kuondokana na usumbufu wa kufanya maboresho yasiyo ya lazima.
Wamesema taarifa ya utekelezaji wa ilani ya mwaka jana ambayo ilikuwa ikijadiliwa katika kikao cha madiwani kilichofanyika ,kujadili mambo ya maendeleo,ilani na mapato na matumizi ,ina mapungufu makubwa.
Aidha madiwani hao wamewaagiza wataalamu na watendaji hao kufanya maboresho na kuirekebisha taarifa hiyo ili mwezi ujao iweze kujadiliwa na kupitishwa rasmi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti madiwani hao walisema,agenda ya kupitia taarifa hiyo muhimu ya uchaguzi ya mwaka 2015 wameiahirisha kwa ajili ya maboresho kabla ya kwenda chama.
Walielezea kuwa ni ngumu kuikwepa ilani ya chama tawala kwa kukubali kufanyakazi za serikali pasipo kuifanyia kazi ilani hiyo ambayo utekelezaji wake unakwenda sambamba na serikali iliyo madarakani.
 Diwani wa kata ya Visiga ,Mbegu Legeza,alisema watendaji ,wataalamu wa serikali sambamba na halmashauri wanapaswa kusimamia kikamilifu  utekelezaji wa ilani .
“Tuliyoyaona kwenye taarifa ya ilani hii mengi yamechotwachotwa na kubambikwa huku miradi mingine ikiwa haijawekwa kwenye taarifa hiyo”
“Mambo mengi hayapo sawa ukisema mmekopesha vikundi lazima iainishwe kata ngapi wamepewa hizo fedha,makundi gani yamepokea fedha,kuna viwanda vimejengwa na kuwekezwa vingine vimeandikwa vingine havijaandikwa”
“Kuna vikundi vimefundishwa lakini diwani wa kata husika hajui na kwenye kabrasha imeandikwa kuna elimu imetolewa kwenye kata hiyo hapo ni lazima diwani husika akatae”alisema legeza.
Diwani wa kata ya Mailmoja ,Ramadhani Lutambi alieleza kuwa ,hali hiyo inaonyesha udhaifu mkubwa kwa wataalamu hao kwa kushindwa kufanya kazi zao kwa uhakika.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Leonard Mloe,alikiri kuwepo kwa mapungufu kwenye taarifa hiyo ambapo alisema agenda nyingine zilijadiliwa na kupitishwa bila tatizo.
Agenda zilizojadiliwa ilikuwa ni pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo robo ya nne april-juni  2016 ,taarifa ya maendeleo ya kata na kupokea taarifa ya mapato na matumizi.
Nae mwenyekiti wa CCM mji wa Kibaha ,Maulid Bundala, alitoa wito kwa baraza hilo kubadili utaratibu wa kupitia taarifa ya ilani kwenye baraza hilo kwa kutenganisha na kuichambua ilani hiyo kwenye vikao vingine ambavyo haviudhuliwi na viongozi wa vyama.
Alisema raha ya chakula usikione kikipikwa wala kuandaliwa hivyo ni vyema ukafanyika utaratibu mwingine wa kujadiliwa taarifa hiyo kwenye kikao cha madiwani pekee kabla ya baraza.
Hata hivyo Bundala alisema baada ya kujadiliwa taarifa hiyo ni lazima itafika katika chama hivyo hakuna sababu ya kujadiliwa wakati wao wakiwepo.
Alisema watendaji,watalaamu wa serikali na halmashauri hawawezi kukwepa ilani ya chama cha mapinduzi ,na kusema anaeona kichefuchefu kutekeleza ilani hiyo atoke nje wakati wa kuijadili.
“Itakuaje maziwa ya ng’ombe yawe mazuri halafu ng’ombe wake awe mbaya,serikali hii inaongozwa na CCM,sasa utakwepaje kuisimamia ilani ya chama tawala,jamani huu ni wakati wetu na ukifika wa chama kingine itasimamiwa ilani yao”alisema Bundala.
Bundala alieleza kuwa hata kama ni mkurugenzi ameajiliwa na serikali ambayo imenatekeleza ilani ya CCM hivyo kuna kila sababu ya watendaji wote kufanyakazi kwa moyo na kusimamia majukumu yao.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Lucy Kimoi alisema wamepokea ushauri na maagizo yote na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi.
Katika hatua nyingine halmashauri hiyo imekisia kukusanya kwa mwaka 2015/2016 bil 3.744 katika mapato yake ya ndani .
Robo ya nne inayoishia juni mwaka huu,imekusanya mil.732.102 na kufanya jumla ya mapato yaliyokusanywa julai /juni 2016 kuwa zaidi ya bil.2.910.866 sawa na asilimia 78 ya makisio.

Pia imekisia kutumia zaidi ya bil.31.836.942 kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi wa mji huo .
Katika utekelezaji wa shughuli zake kwa robo ya nne iliyoishia juni 2016 imetumia bil.5.950.420 na kufanya jumla ya matumizi kwa julai/juni  mwaka huu kufikia bil.21.614.164 sawa na asilimia 67 ya makisio.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AVITAKA VIWANDA VYA SUKARI KUZALISHA ASILIMIA 100 YA MAHITAJI IFIKAPO 2020

1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Meneja wa Kiwanda cha sukari cha Kagera,  Ashuwin  Rana baada ya kuwasili kwenye  kiwanda  cha sukari cha Mtibwa  baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha sukari cha Mtibwa Agosti 2, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe na wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Kagera Sugar na Mtibwa Sugar, Seif  Ali Seif .
2 






Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha sukari cha Mtibwa   kukagua uzalishaji  wa sukari katika kiwanda hicho, Agosti 2, 2016.   Kulia ni  mkewe Mary, wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe na Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha sukari cha Kagera na Mtibwa, Seif Ali Seif .  Kushoto ni Kaimu Katibu wa CCM mkoa Wa Morogoro, Kulwa Solobi.
3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la mtambo wa maji ya kumwagilia katika shamba la miwa la kiwanda cha sukari cha Mtibwa  wakati alipokitembelea kiwanda hicho, Agosti 2, 2016.  Kushoto ni  mkewe Mary na wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera na Mtibwa, Seif  Ali Seif .
4 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la mtambo wa maji ya kumwagilia katika shamba la miwa la kiwanda cha sukari cha Mtibwa  wakati alipokitembelea kiwanda hicho, Agosti 2, 2016.  Kushoto ni  mkewe Mary na wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera na Mtibwa, Seif  Ali Seif.
5 Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa na Mkewe Mary wakisalimiana  na wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa  wakati alipotembelea kiwanda hicho Agosti 2, 2016.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Stephene Kebwe.
6 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa wakati alipokitembelea kiwanda hicho Agosti 2, 2016.
(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amevitaka viwanda vya sukari nchini kuongeza mikakati ya uzalishaji zaidi ili mwaka 2020 Tanzania iwe imefikia kiwango cha kuzalisha asilimia 100 ya mahitaji yake.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Agosti 02, 2016) wakati alipotembelea kiwanda cha sukari cha Mtibwa kilichoko mkoani Morogoro ambapo amesisitiza viwanda vya ndani vizalishe zaidi ili kupunguza uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi.
Amesema Serikali imejikita katika kuimarisha na kulinda viwanda vya ndani nchini hivyo ni vema viwanda vya sukari vikaweka mikakati ya kuzalisha kwa wingi ili kuondokana na uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje.
“Kiwango cha mahitaji ya sukari nchini ni zaidi ya tani 400,000, nimeiagiza Bodi ya Sukari kukaa na wataalamu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kufanya utafiti ili tujue mahitaji halisi ya sukari,” alisema.
Waziri Mkuu amesema Serikali imeweka mkakati wa kulinda viwanda vya ndani kwa kuziongezea kodi bidhaa zinazotoka nje ambazo zinazalishwa na viwanda vya ndani ikiwemo sukari hivyo wenye viwanda hawana budi kuzalisha kwa wingi zaidi.
Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa viwanda vya sukari nchini kutoa motisha kwa wakulima wa nje kwa kununua miwa yao kwa bei nzuri na kuwalipa kwa wakati ili nao wanufaike na uwepo wa viwanda hivyo na kuwa walinzi wa uwekezaji huo.
Kwa upande wake Meneja Uhusiano Mwandamizi wa kiwanda hicho, Ibrahim Juma amesema kwa sasa kiwanda kinazalisha tani 20,000 kwa mwaka na wanatarajia kuongeza uzalishaji hadi kufikia tani 70,000 ifikapo mwaka 2021.
Juma alisema uzalishaji wa sukari kiwandani hapo ulipungua kutokana na uingizwaji wa sukari kutoka nje hivyo aliipongeza serikali kwa kudhibiti uingizwaji holela wa sukari kutoka nje jambo litakalosaidia ukuzaji wa viwanda vya ndani.
Meneja huyo alisema kuwa kwa sasa wameanza upanuzi wa mashamba kiwandani hapo ambapo wanatarajia kuongeza hekta 400,000 lengo likiwa ni kutimiza ndoto ya Serikali ya kuifanya Tanzania ijitosheleze katika uzalishaji wa sukari.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, AGOSTI 02, 2016.

WASIFU WA MAREHEMU KAMISHNA MSTAAFU WA MAGEREZA EGNO KAMILIUS KOMBA

           KAMISHNA MSTAAFU WA MAGEREZA MAREHEMU EGNO KAMILIUS KOMBA
  ………………………………………………………………………………….
Marehemu Kamishna Mstaafu wa Magereza EGNO KAMILIUS KOMBA alizaliwa tarehe 20 Oktoba,1947 katika Kijiji cha Mtungu – Kindimba Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.  Mwaka 1956 alijiunga na Elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Kindimba na kuhitimu elimu hiyo mwaka1959. Alijiunga na Shule ya Kati (Middle School) ya Litembo mwaka 1960 na kuhitimu mwaka 1963. Alijiunga na Shule ya Sekondari ya Kigonsera mwaka 1964 na kuhitimu Kidato cha Nne mwaka 1967.  Mwaka 1968 alijiunga na Shule ya Sekondari Karimjee iliyopo Mkoani Tanga na kuhitimu mwaka 1968.
Marehemu aliajiriwa na Jeshi la Magereza tarehe 02 Agosti, 1972 na kupelekwa kuhudhuria mafunzo ya awali ya Uaskari katika Chuo cha Usalama – Moshi. Marehemu alihitimu mafunzo hayo tarehe 30 Aprili, 1973 na kupangiwa kufanya kazi Gereza Malya, Mkoa wa Shinyanga.

Mwaka 1975 akiwa mwajiriwa wa Jeshi la Magereza, Kamishna mstaafu wa Magereza, Marehemu EGNO KAMILIUS KOMBA alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa ajili ya masomo ya Shahada ya Kwanza katika Uchumi  na kuhitimu mwaka 1978.
Marehemu akiwa Jeshini alitunukiwa vyeo mbalimbali kama ifuatavyo:-
Afisa Magereza  Daraja la III (PO III)​– ​30/04/1973 – 31/09/1973
Afisa Magereza  Daraja la I (PO I)​​- ​01/09/1973 – 31/06/1976
Afisa Magereza Mkuu (PPO)​-​01/07/1976 – 30/11/1978
Mrakibu Msaidizi wa Magereza (ASP)​- ​01/12/1978 – 31/09/1980
Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP)​ – ​01/10/1980 -31/12/1996
Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) ​- ​01/07/1984 -19/09/1989
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP)-20/09/1989-30/6/1996
Kamishna wa Magereza (CP)   ​- ​01/07/1996 – 30/06/2007 (Alipostaafu kwa umri Mkubwa).

Marehemu alifanya kazi katika vituo  vifuatavyo vya Magereza:-
Gereza Malya – Shinyanga ​- Tarehe 01/05/1973 – 12/05/1974
Makao  Makuu ya Magereza ​- Tarehe 13/05/1974 – 30/06/2007
​                          Katika utumishi wake Jeshini Marehemu pia alitunukiwa nishani mbalimbali kama ifuatavyo:-
Nishani ya Mstari wa Nyuma ya Vita vya Kagera,
Nishani ya Utumishi Mrefu Tanzania na,
Nishani ya Utumishi Uliotukuka.
Katika utendaji wake wa kazi, Marehemu alikuwa na uwezo mkubwa wa kujifunza, kutawala na kuyamudu majukumu yake ya kazi ipasavyo.  Viongozi na watumishi wa Jeshi la Magereza tunamlilia mno kwa Utumishi wake uliotukuka na hazina kubwa ya utendaji aliyoondoka nayo  kwani hata baada ya kustaafu katika Jeshi la Magereza bado alikuwa akitoa ushauri katika mambo mbalimbali ya Uendeshaji wa Jeshi la Magereza.
Kamishna Mstaafu wa Magereza EGNO KAMILIUS KOMBA alikuwa anasumbuliwa na Ugonjwa wa Moyo hadi umauti ulipomkuta mchana ya tarehe 31 Julai, 2016 nyumbani kwake Mvuti, Chanika Jijini Dar es Salaam. Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuzikwa kesho Agosti 3, 2016 Shambani kwake Mvuti, Jijini Dar es Salaam.
MWENYEZI MUNGU AIWEKE PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU EGNO KAMILIUS KOMBA, AMEN

MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII (SSRA) KATIKA MADHIMISHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA MKOANI LINDI

Mkuu wa Kitengocha uhusino na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika (katikati) akigawa baadhi ya vifaa vya uhamasishaji kwa wadau waliotembelea banda la SSRA katika maonesho ya sherehe za Wakulima katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi jana. Maadhimisho ya sikukuu hiyo, yatafanyika Agost 8, 2016.
Bi. Sarah Kibonde Msika (kulia) na Bw. Mathayo Mihayo (Kushoto) wakitoa maelezo mbalimbali ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi waliotembelea banda la SSRA katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi katika maonesho ya Nane nane.
Wananchi mbalimbali wakipata maelezo ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii kutoka kwa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) katika maonesho ya Nane nane.
Wananchi mbalimbali wakipata maelezo ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii kutoka kwa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) katika maonesho ya Nane nane mjini Lindi jana.
Mkulima akipokea vipeperushi na maelezo toka kwa Afisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. David Mathayo katika maonesho ya wakulima Nane nane mkoani Lindi jana.
Afisa Uhusiano na Uhamasishaji Bi. Agnes Lubuva akitoa malezo na vipeperushi kwa wageni waliotembelea banda la SSRA katika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi wakati wa maonesho ya Wakulima jana.

AMASHA LA MAADILI LILIVYO TIKISA DAR

tic1 
Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, akizungumza katika Tamasha la maadili kwa vijana  lililoandaliwa na Tumaini Media kupitia Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Kanisa Katoliki lililofanyika Katika uwanja wa Uhuru juzi
tic2
Umati wa wananchi uliohudhuria katika tamasha hilo.
tic4 
Aliyekuwa mgeni wa  heshima katika Tamasha la Maadili, Balozi Paul Rupia, akizungumza katika tamasha hilo lililoandaliwa na Tumaini Media kupitia Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Kanisa Katoliki lililofanyika Katika uwanja wa Uhuru juzi.
tic5 tic6 
Kwaya ya Mtakatifu Kizito wakitumbuizaatika Tamasha la maadili kwa vijana  lililoandaliwa na Tumaini Media kupitia Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Kanisa Katoliki lililofanyika Katika uwanja wa Uhuru juzi

No comments:

Post a Comment