Pages

Thursday, July 28, 2016

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUJITAMBUA, NI BAADA YA RIPOTI YA LHRC KUONYESHA ASILIMIA 80 HAWANA MIKATABA YA KAZI


Kaimu Mkurugenzi na Sera wa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji, Alfred Mapunda akitoa hotuba katika uzinduzi wa ripoti ya haki za binadamu kibiashara ya mwaka 2015.
Mtafiti wa ripoti, Clarence Kipobota akizungumza kuhusu ripoti hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba akitoa ushauri kwa serikali.
Kaimu Mkurugenzi na Sera wa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji, Alfred Mapunda akikata utepe kuashirikia ufunguzi wa ripoti.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimefanya uzinduzi wa ripoti ya haki za binadamu kibiashara ya mwaka 2015 ambayo imeonyesha jinsi hali ilivyo kwa sekta tatu ambazo walizifanyia utafiti za sekta ya habari, sekta ya usafirishaji wa abiria na mizigo na kutizama hali ilivyo kwa wabeba mizigo wa mlima Kilimanjaro.


Akizungumza kuhusu sekta ya habari, mgeni rasmi katika uzinduzi wa ripoti hiyo, Kaimu Mkurugenzi na Sera wa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji, Alfred Mapunda alisema ripoti hiyo inawapa nafasi kama serikali kufahamu ni sekta zipi ambazo bado zinahitaji kufanyiwa kazi kutokana na mapungufu yaliyopo.

Alisema pamoja na kazi ambayo serikali imekuwa ikiifanya lakini kwa waandishi wa habari inabidi kufika hatua watambue haki zao za msingi kwa kuwabana mabosi zao ili waweze kuwa na mikataba ya kazi wanazofanya.

“Ripoti kwa upande wetu sisi inatupa mwanga wa kujua nini tunatakiwa kufanyia marejebisho maana kama imevyotolewa bado kuna maeneo yanaonekana kuwa na shida lakini tutakaa na kufanyia kazi.

KOCHA PEP GUARDIOLA APATA USHINDI WAKE WA KWANZA AKIWA NA MAN CITY

Kocha Pep Guardiola amepata ushindi wake wa kwanza akiwa na Manchester City baada ya kufikia hatua ya penati dhidi ya Borussia Dortmund katika mchezo uliochezwa nchini China.

Kipa wa Manchester City Angus Gunn, 20, aliokoa penati ya Mikel Morino na kuihakikishia ushindi wa penati 6-5 baada ya mchezo kuishia kwa sare ya 1-1 huko Shenzhen katika dimba la Longgang.
Katika mchezo huo mchezaji wa Dortmund Christian Pulisic, 17, alisawazisha katika dakika za mwisho, na kufanya matokeo kuwa moja kwa moja baada ya awali Sergio Aguero kuifungia goli la kwanza la mchezo huo.
      Kipa wa Manchester City Angus Gunn akipangua penati iliyoipa ushindi timu yake
   Wachezaji wa Manchester City wakifurahia ushindi baada ya kipa Gunn kupangua penati

No comments:

Post a Comment