Mama akifurahia mtoto baada ya kujifungua salama
Christian
Gaya, Majira
Jumanne 19 Julai 2016
Mmojawapo
wa wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii (mama mjamzito) akipatiwa huduma
kwenye hospitali ambazo zimeingia mkataba na mfuko ikiwa kama maandalizi
binafsi ya kujifungua, utayari wake kwa
matatizo yanayoweza kutokea katika ujauzito,
kujifungua na baada ya kujifungua.
Kutokana
na kanuni na haki za uzazi na utaratibu wa shirika la kazi duniani (ILO) lengo
la kubwa la kuwa na fao la uzazi ni kuhakikisha kuwa kazi za wanamke hawaingiliwi
na hali hatarishi ya afya ya wanamke pamoja na mtoto wake na kwamba shughuli za
kujifungua hazikwamishi shughuli zao za kiuchumi za kila siku pamoja na usalama
wa kazi zao iwe ya kujiajiri au kuajiriwa.
Kwa mara ya kwanza
katika karne, nguvu zaidi zimekuwa zikielekezwa
kwenye lengo la millennia ya maendeleo namba 5 yaani MDG 5, ambapo vifo
vya wanawake wenye mimba na watoto vimeweza kupungua mpaka kufikia asilimia 35.
Utafiti wa Shirika la
Afya Duniani, WHO, unaonesha ya kuwa wajawazito 303,000 kati ya milioni 130
wanaojifungua kila mwaka hufariki dunia kote ulimwenguni, watoto milioni 2.6
wakifariki dunia kabla ya kuzaliwa, na milioni 2.7 wakifariki dunia katika siku
28 baada na kuzaliwa.
Lakini kati ya nchi
zenye mapato ya chini kama Tanzania vyenye idadi kubwa ya vifo vya wajawazito
na watoto vimekuwa vikitofautiana sana na ni nchi 23 tu ambazo ziko kwenye
kundi la kufikisha asilimia 75 katika kupunguza vifo vya wajawazito na watoto
mpaka ilipofikia mwaka 2015.
Elementi
kuu za kinga za uzazi ni kama kupata likizo ya uzazi, kupata mafao taslimu ya
kuhakikisha kuwa mama anaweza kujikimu yeye pamoja na mtoto wake wakati akiwa
wa likizo ya uzazi, kuhakikisha kuwa anapatiwa matibabu kwa ajili ya kinga ya
afya ya ujauzito.
Mama
mjamzito au anayeyonyesha ana haki kupewa kinga ya kutofukuzwa na kubaguliwa na
kupewa kinga ya kwenda kunyonyesha mara tu baada ya kurudi kazini baada ya
kurudi likizo yake ya uzazi.
Kwa
hiyo kinga ya uzazi kwa akina mama lazima ichangie afya na ustawi wa wamama
pamoja na watoto wao na hivyo kutimiza malengo ya namba 4 na 5 ya maendeleo ya
millennia ya Tanzania kama mwanachama wa umoja wa mataifa, yanayotaka kupunguza
vifo vya watoto na kuboresha afya za wamama.
Wanawake
wengi wanakosa fursa ya kupatiwa malipo ya uzazi kabla ya kujifungua na hata
baada ya kujifungua. Na wanawake wengi zaidi wanatishiwa kufukuzwa kazi na hata
kubaguliwa eti kwa sababu ni mjamzito au atakuja apate mimba.
Kulea
watoto bila ya kuwaharibia wanawake fursa zao za haki za kushirikishwa kwenye
kazi za maendeleo ya kiuchumi inabaki kuwa ni changa moto kubwa wakati ubora na
uwezo nafuu wa mipangilio ya uangalizi wa mtoto haupo kwa mpana mkubwa kabisa.
Na inasekama karibu asilimia tisini na tisa ya wamama
duniani wanaopoteza maisha yao wakati wa kujifungua hutokea
Afrika na Tanzania ikiwa mojawapo.
Ingawa
vifo vya watoto wanaozaliwa kwa mwaka 1990 vilipungua kutoka 320 mpaka kufikia
250 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa wazima kwa mwaka 2008, lakini
angalau wanawake wapatao 343,000 wanaendelea kufa wakati wa ujauzito na wakati
wa kujifungua watoto kila mwaka. Kwa kila mwanamke anayekufa angalau kama 20
wanateseka na kusumbuka na maumivu makali au kupatwa na ulemavu.
Ni
kweli ya kuwa idadi kubwa ya akina mama hawako katika mpango wa hifadhi ya
jamii hivyo wengi wamejiajiri wenyewe. Lakini hata idadi ndogo ya wanawake walioajiriwa
na kuwa wanachama wa mifuko hii ya pensheni hawajaweza hata kutumia fursa ya
fao la uzazi kabla ya kujifungua na baada ya kujifungua.
Kwa
kweli elimu ya juu ya fao hili la uzazi inahitajika sana, kwa sababu hata kama
wanawake wengi wamejiajiri wenyewe lakini wanaruhusiwa kujiunga, kwa mfano na
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF kwa mpango wa hiyari kwa kulipia
kadri ya uwezo wao kuanzia shilingi 20,000/= kwa kila mwezi ya mshahara wa kima
cha chini wa serikali na kufanya hivyo atakuwa na uwezo wa kupata mafao yote
yatolewayo na NSSF.
Na
kwa upande wa fao hili la uzazi mara nyingi wazazi wengi hawapata taarifa ya
kuwa anastahili kupata kabla ya kujifungua au baada ya kujifungua na kupita
muda wa ziada ambao ni miezi mitabu (3) au ndani ya siku tisini (90).
Dorca
Gikaro aliyekuwa wahi kuwa mwanachama wa mfuko NSSF Dar es Salaam, alipohojiwa
na Kituo cha HakiPensheni anasema alipata mafao ya uzazi karibu asilimia 100 ya
wastani ya mapato ya siku ambayo ni sawa na mafao ya muda wa wiki 12.
Anasema
tangia aanze na mimba ya mtoto wake kwanza aitwae neema alipata kwa awamu mbili
tofauti kwanza alipata mafao ya fedha taslimu wiki 4 kabla ya kujifungua na
awamu ya mwisho alipata baada ya wiki 8 baada ya kujifungua. Lakini ikumbukwe
ya kuwa mwanachama akitaka anaweza kuamua kulipwa kwa wiki zote 12 baada ya
kujifungua.
Dorca
mama mwenye watoto watatu kwa sasa anasema kuwa fedha ya awamu ya kwanza
ilimsaidia sana kwa ajili ya kujenga afya yake na ya kichanga tumboni.
Na
mafao ya awamu ya pili yaani baada ya kujifungua anasema ilimsaidia sana kujipatia
supu na mahitaji mengine ya muhimu kama mama mnyonyeshaji, kwani mtoto wake
alipata maziwa ya kutosha na yenye virutubisho vilivyo bora zaidi kwa mtoto
wake mchanga na kuimarisha zaidi afya ya mama.
Anasema
kuna wakati fulani mara tu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa uliokuwa umeambatana
na ujauzito wake, kama mwanachama, NSSF ilimtibu bure kwa gharama zao.
Bibi
Eunice Chiume ambaye ndiye Meneja mkuu wa uhusiano na masoko wa NSSF
alipohojiwa juu ya utaratibu wa utoaji wa huduma hii, anasema matibabu huanza
kutolewa baada ya wiki ya 24 ya ujauzito na huishia masaa 48 baada ya
kujifungua au siku 7 ikiwa nikujifungua kwa upasuaji.
Kutokana na Eunice NSSF inatoa huduma
yenye lengo maalumu na inayotolewa kwa wajawazito ikisisitiza juu ya afya wanawake kwa ujumla,
maandalizi binafsi ya kujifungua,
utayari wake kwa matatizo yanayoweza kutokea katika ujauzito, kujifungua na baada ya kujifungua.
NSSF inatoa huduma bure kwa mama
mwanachama aliyejiunga na mfuko kwa mfumo wa hiyari au lazima ili
kuwawezesha kuwa na afya ya kutosha
katika muda wote wa ujauzito, kujifungua, na baada ya kujifungua.
“Matibabu
haya hufanywa na hospitali ambazo zimeingia mkataba na Shirika wa kutibu
wanachama wa NSSF na unaruhusiwa kubadilisha hospitali nyingine pale unapoona
huduma zao haziridhishi au iko mbali na eneo la makazi yako” Eunice anakumbusha.
Christian Gaya ni
mwanzilishi wa Kituo cha HakiPensheni Tanzania, mshauri na mtaalamu wa masuala
ya pensheni. Kwa maelezo zaidi gayagmc@yahoo.com
Au kwa habari zaidi za kila siku juu ya HakiPensheni unaweza kutembelea tovuti www.hakipensheni.co,tz
au hakipensheni.blogspot.com Simu namba +255 655 13 13 41
No comments:
Post a Comment