Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli akikabidhi tuzo
kwa mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Rais ya mzalishaji bora wa mwaka 2015,
kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin wakati wa hafla ya
kutoa tuzo kwa washindi iliyofanyika jijini katika hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam . Wengine ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wenye Viwanda
Tanzania (CTI), Dk. Samwel Nyantahe ( wa pili kulia) na kushoto ni
Waziri wa Biashara ,Viwanda na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
Rais
John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha
wafanyabiashara wenye viwanda na watendaji wa makampuni ambayo
yameshinda tuzo mbalimbali katika kipindi cha mwaka huu
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin (wa nne mstari wa mbele kutoka
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa kampuni hiyo
waliohudhuria hafla ya kukabidhiwa tuzo.
…………………………………………………………………………………………………………………
Kampuni ya TBL Group imeibuka
mshindi wa kwanza wa tuzo ya Rais ya mzalishaji bora kwa kipindi cha
mwaka 2015,vilevile imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la
uzalishaji wa vinywaji ambapo imetunukiwa tuzo kwa ushindi huo.
Tuzo ya mzalishaji bora hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI na hafla
ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali imefanyika leo jijini Dar es
salaam katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo mgeni wa
heshima aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Mheshimiwa John Magufuli.
Akiongea baada ya hafla hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin,alisema ushindi huu ni
zawadi kwa wafanyakazi wote wa kampuni kwa kuwa jitihada za kila mmoja
ndizo zimepelekea mafanikio haya kupatikana.
“Kwetu TBL Grop tunayo furaha
kwa kushinda tuzo hizi tulizofanikiwa kuzinyakua siku ya leo,haya kwetu
ni mafanikio makubwa na tumefurahi kuona mchango wa uwekezaji wetu
unatambuliwa na tunaendelea kuwa washindi wa tuzo mbalimbali
zinazotolewa na taasisi mbalimbali”.Alisema Jarrin.
Alisema TBL Group itaendelea
kufanya uwekezaji zaidi nchini na kuchangia kukua kwa uchumi wa taifa
ikiwemo kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza tatizo la ajira
nchini ambapo mbali na kutoa ajira kwenye viwanda vyake na mtandao wa
wafanyabiashara inaoshirikiana nao tayari imeanzisha miradi ya
kuwasaidia wakulima ambayo tayari imeanza kuonyesha mafanikio kwa
kubadilisha maisha ya wakulima kuwa bora.
“Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kufanya kazi kwa
karibu na wawekezaji na nina imani tutaendelea kushirikiana ili kuweza
kupata mafanikio zaidi katika siku za usoni”.Alisema.
Kampuni ya TBL Group imeibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya
Rais ya mzalishaji bora kwa kipindi cha mwaka 2015,vilevile imeibuka
mshindi wa kwanza katika kundi la uzalishaji wa vinywaji ambapo
imetunukiwa tuzo kwa ushindi huo.
Tuzo ya mzalishaji bora hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI na hafla
ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali imefanyika leo jijini Dar es
salaam katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo mgeni wa
heshima aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Mheshimiwa John Magufuli.
Akiongea baada ya hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TBL
Group,Roberto Jarrin,alisema ushindi huu ni zawadi kwa wafanyakazi wote
wa kampuni kwa kuwa jitihada za kila mmoja ndizo zimepelekea mafanikio
haya kupatikana.
“Kwetu TBL Grop tunayo furaha kwa kushinda tuzo hizi
tulizofanikiwa kuzinyakua siku ya leo,haya kwetu ni mafanikio makubwa na
tumefurahi kuona mchango wa uwekezaji wetu unatambuliwa na tunaendelea
kuwa washindi wa tuzo mbalimbali zinazotolewa na taasisi
mbalimbali”.Alisema Jarrin.
Alisema TBL Group itaendelea kufanya uwekezaji zaidi nchini
na kuchangia kukua kwa uchumi wa taifa ikiwemo kuunga mkono jitihada za
serikali za kupunguza tatizo la ajira nchini ambapo mbali na kutoa
ajira kwenye viwanda vyake na mtandao wa wafanyabiashara inaoshirikiana
nao tayari imeanzisha miradi ya kuwasaidia wakulima ambayo tayari
imeanza kuonyesha mafanikio kwa kubadilisha maisha ya wakulima kuwa
bora.
“Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kufanya kazi kwa
karibu na wawekezaji na nina imani tutaendelea kushirikiana ili kuweza
kupata mafanikio zaidi katika siku za usoni”.Alisema.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO VYA HABARI
…………………….
JESHI
LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATU [3] WANAOJIHUSIHA NA
BIASHARA ZA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI NA WENGINE [7]
WANAOTUHUMIWA KULETA FUJO.
KWAMBA
MNAMO TAREHE 30.05.2016 MAJIRA YA SAA 14:00hrs KATIKA MAENEO YA MIHAMA –
MNARANI KATA YA KITANGIRI WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA,
ASKARI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA RAYMOND MONGESA MIAKA 18 MKAZI WA
MNARANI AKIWA NA MISOKOTO 30 PAMOJA NA KILO 10 ZA BHANGI, NA MWENZAKE
DIONIZI ELIAS MIAKA 27 MIHAMA AKIWA NA MSOKOTO 01 WA BHANGI KITENDO
AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA ZA NCHI.
AIDHA
BAADA YA KUWAKAMATA WATUHUMIWA HAO ASKARI WALIENDELEA NA DORIA PAMOJA
NA MISAKO YA KUWASAKA WAHALIFU AMBAPO NASIBU ABDUL NA WENZAKE 07
WALIKAMATWA WAKIFANYA FUJO NA KUBUGUDHI ABIRIA KATIKA MAENEO YA MECCO
STAND, PAMOJA NA MATHIAS MSUKUMA MIAKA 30 MKAZI WA NYAKATO SOKONI
ALIEKAMATWA NA MISOKOTO 20 YA BHANGI.
WATUHUMIWA
WOTE WAPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI DHIDI YA UHALIFU WA
KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA BHANGI ILI KUWEZA KUKAMATA WAHUSIKA
WENGINE ZAIDI WANAOSHIRIKIANANAO KATIKA BIASHARA HIYO, PINDI UCHUNGUZI
UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU MASHITAKA YANAYOWAKABILI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HASWA VIJANA
KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU ZA MADAWA YA KULEVYA KAMA BHANGI
NA ZINGINE KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA ZA NCHI, KWANI JESHI
LA POLISI TUMEJIPANGA KUHAKIKISHA TUNAKAMATA WAHALIFU WA AINA KAMA HIYO
KATIKA SEHEMU ZOTE ZA MKOA WA MWANZA, HIVYO TUNAOMBA WANANCHI WATUPE
USHIRIKIANO WA KWA KUTUPA TAARIFA MAPEMA ZA UHALIFU NA WAHALIFU ILI
TUWEZE KUWAKAMATA NA KUWAFIKISHA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
IMESAINIWA NA
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
RAIS UHURU KENYATTA AKUTANA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU RAILA ODINGA KATIKA IKULU YA NAIROBI
Rais wa Jahuri ya Kenya Mh. Uhuru
Kenyatta akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mh Raila Odinga
wakati alipomkaribisha Ikulu kwa Chakula cha Mchana na Mazungumzo katika
Ikulu ya Nairobi kwa mwaliko wa Ikulu ambapo viongozi wa Chama cha CORD
walialikwa kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe za siku ya Mdaraka
(Madaraka Day)inayotarajiwa kufanyika kesho mjini Nakuru nchini humo,
Kulia ni Makamu wa Rais wa Kenya Mh. William Ruto na Kushoto ni Gavana
Mosess Watangula.
Rais
wa Jahuri ya Kenya Mh. Uhuru Kenyatta kulia akiongozana na Waziri Mkuu
Mstaafu wa Kenya Mh Raila Odinga wakati Waziri Mkuu huyo mstaafu
alipoalikwa katika Ikulu ya Nairobi kwa chakula cha mchana na
maadhimisho ya Madaraka Day yanayotarajiwa kufanyika Kesho mjini Nakuru,
Kushoto ni Gavana Mosess Watangula.
Rais
wa Jahuri ya Kenya Mh. Uhuru Kenyatta akipozi kwa picha na Waziri Mkuu
Mstaafu wa Kenya Mh Raila Odinga wakati Waziri Mkuu huyo mstaafu
alipoalikwa katika Ikulu ya Nairobi kwa chakula cha mchana na
maadhimisho ya Madaraka (Madaraka Day) yanayotarajiwa kufanyika Kesho
mjini Nakuru, kulia ni Makamu wa Rais wa Kenya Mh. William Ruto na
Kushoto ni Gavana MOsess Watangula.
UCHAGUZI YANGA, MWISHO WA KUCHUKUA, KUREJESHA FOMU JUNI 6
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
iliyopewa jukumu la kusimamia uchaguzi wa Klabu ya Young Africans
imeridhishwa na mwenendo wa wanachama kwa namna wanavyochukua na
kurejesha fomu.
Katika kikao chake cha kufanya tathmini kilichoketi jioni ya leo Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Msomi Alloyce Komba kutokana na mipango yake, imesogeza mbele mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu mpaka Jumatatu Juni 6, 2016 saa 10:00 jioni. Isipokuwa Jumamosi na Jumapili ya Juni 4 na 5, 2016.
Hadi sasa wanachama tisa (9) wamechukua na kurejesha fomu. Wanachama hao ni Aaron Nyanda na Titus Osoro wanaowania nafasi ya makamu mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2010 inayotambulika serikalini hadi sasa.
Wengine ni Paschal Laizer, Edgar Chibula, Mohammed Mattaka, Mchafu Ahmed Chakoma, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ Omari Said kutoka Zanzibar ambao wanawania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji. Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Juni 25, 2016.
Fomu zinapatikana katika ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam. Vilevile utaratibu unafanyika ili fomu ziweze kupatikana katika tovuti ya shirikisho www.tff.or.tz
Fomu zinapatikana kwa gharama ya Sh 200,000 kwa nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti na Sh 100,000 kwa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji. Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni tarehe 6 Juni, 2016.

TANZANIA ELECTED CHAIR OF THE AFRICAN GEOLOGICAL BODY
The
Permanent Representative of Tanzania to the United Nations Economic
Commission for Africa (UNECA) and Ambassador of Tanzania to Ethiopia
H.E. Naimi Hamza Aziz Delivers her speech during the opening session of
the African Minerals and Geosciences Centre(AMGC) 36th Annual Meeting
hels at United Nations Economic Commission for Africa(UNECA), Conference
Centre in Addis Ababa Ethiopia
From Freddy Maro
Tanzania Embassy Addis Ababa Ethiopia.
May,31,2016.
Tanzania has been elected a Chair of the Governing Council of African Minerals and Geosciences Center (AMGC) during its 36th
annual meeting held at United Nations Economic Commission for Africa
(UNECA) conference Centre in Addis Ababa, Ethiopia over the weekend.
Tanzania was represented by The
Permanent Representative of Tanzania to the United Nations Economic
Commission for Africa (UNECA) and Ambassador of Tanzania to Ethiopia
H.E. Naimi Hamza Aziz who read the Member country’s statement on behalf
of Minister for Minerals and Energy Prof. Sospeter Muhongo.
In her speech, ambassador Naimi
urged Member States to consider the development of other strategic
minerals such as graphite; lithium and Rare Earth Elements (REEs) which
she said were not only economically viable but also important.
“The mining sector is seriously
affected by the drop of mineral prices in the global market especially
for precious and base metals which are mostly mined by our countries.
The decline of mineral price has resulted to low exploration activities
to Member States especially my country, which has led to the decline of
income to the centre (AMGC),” she said.
The Tanzania Permanent Rep.
further advised the African Minerals and Geo-Sciences Center(AMGC) to be
more creative and diversify its economic activities for its future and
sustainability.
In order for Member States to
catch up with fast growing technologies, the Ambassador said it was high
time for AMGC to invest in Research and Development (R&D), in which
the findings would be shared with Member States for optimal utilization
of mineral rich resources found in the continent.
She said that Member States
should endeavor to make AMGC a truly Pan African Center of Excellence
and to achieve this more needs be done in terms of marketing, which
would increase the center’s visibility and capability and promote the
tremendous work it does.
“It is therefore crucial that
Member States pay their respective annual contributions to the center,
in order to allow it to operate more efficiently and effectively and
successfully implement its programs and activities,” She emphasized.
Ambassador Naimi said Tanzania
was very proud to host the AMGC and stands committed to continue to
honor and fulfill its obligation which aims inter alia, to facilitate
and ensure that the center fulfills its mission and mandate to serve all
African countries.
In his opening speech the
outgoing AMGC chairman who is also The Ethiopian Minister of Mines,
Petroleum and Natural Gas H.E. Tolesa Shagi said Ethiopia and many
African countries were adopting effective mineral management policies
and strategies for the exploitation of mineral resources which were
vital in boosting economic growth.
“The Mining sector in Ethiopia is
providing support for the development of small and medium scale and
artisanal mining enterprises and encourage greater participation of
women in mining activities as a strategy for enhancing the development
impact of mineral resources,” he said.
The Minister highlighted
challenges facing mining industry in Ethiopia and Africa in general
including shortage of capacity in negotiating, administering and
monitoring the mining contracts as well as lack of sufficient
geo-science information.
He said for African countries to
overcome the challenges facing the mining industry they should opt for
coordinated efforts as envisaged in the Africa Mining Vision (AMV) that
was adopted by African Heads of States in February 2009, the long term
goal of the vision is to create a Transparent Equitable and optimal
exploitation of mineral resources to underpin broad-based sustainable
growth and socio-economic development.
Speaking during the same
occasion, the Deputy Executive Secretary and Chief Economist of ECA said
that the Economic Commission for Africa(ECA) was acutely aware of the
strategic importance of the AMGC as a partner to African Countries to
collectively implement a transformative agenda for mineral resources
development which would be instrumental for sustainable development.
African Minerals and Geosciences
Centre (AMGC) formerly known as the Southern and Eastern African Mineral
Centre (SEAMIC) started as a sub-regional development Centre for
Eastern and Southern African nations namely, Angola, Comoros, Ethiopia,
Mozambique, Tanzania and Uganda.
The Centre is located in Kunduchi Dar es Salaam Region, Tanzania.
NHIF YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WAKAZI WA JIJI LA TANGA KWENYE MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA.
AFISA UHAMASISHAJI WANACHAMA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA(NHIF) VISTUS TILUSASILA KUSHOTO AKITOA ELIMU KUHUSU MFUKO HUO KWA MKAZI WA JIJI LA TANGA. |
UPIMAJI WA WANANCHI UKIENDELEA KWENYE BANDA LA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA |
YALIYOJIRI KWENYE KIKAO CHA 33 CHA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wakielekea ndani ya Ukumbi wa Bunge
leo kusikiliza Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
leo kusikiliza Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Elimu,
Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Mbunge wa
Afrika Mashariki Mhe. Shy-Rose Bhanji nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Mbunge wa
Afrika Mashariki Mhe. Shy-Rose Bhanji nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi akichangia kuhusu Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Mawaziri wakifuatilia michango mbalimbali ya wabunge wakati wa mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa leo mjini Dodoma.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvu akizungumza
na Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mh. Peter Msigwa mara baada ya kikao
cha bunge kuahirishwa mchana leo, Kushoto anayecheka ni Mh. Balozi
Augustino Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Kikanda na Kimataifa.
WAAMUZI WA TAIFA STARS V MISRI
Waamuzi wanne kutoka Gabon, ndio watakochezesha mchezo wa
kimataifa kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Mapharao wa Misri
utakaofanyika Jumamosi Juni 4, 2016 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo utakaoanza saa 10.00 jioni ni wa kutafuta nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Gabon ambako mwamuzi wa kati atakuwa ni Meye Bastrel atakayesaidiwa na Mihundou Ganther na Vinga Theophile wakati Mwamuzi wa akiba (mezani) atakuwa Otogo Eric.
Wakati waamuzi wote wanatoka Gabon, Kamishna wa mchezo huo ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.
Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa Shirikisho Soka la Tanzania (TFF) kuipokea timu ya taifa ya Misri inayotarajiwa kuingia kesho Juni mosi, 2016 ambako wataweka kambi kambi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, Dar es Salaam.
Taifa Stars imeweka kambi Hoteli Urban Rose ambayo pia iko katikati ya jiji la Dar es Salaam tangu iliporejea kutoka Kenya jana Mei 30,2016 ambako ilicheza timu ya Taifa ya Kenya maarufu kama Harambee Stars. Katika mchezo huo uliofanyika Jumapili Mei 29, mwaka huu timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Serikali kuanzisha benki ya maendeleo ya viwanda nchini.
Na Lilian Lundo-MAELEZO
Serikali ya awamu ta Tano
imedhamiria kuifanya sekta ya Viwanda nchini kuchangia pato la taifa kwa
asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka asilimia 7.3 ya sasa
Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya
utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo
Jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema kuwa jambo
hilo linawezekana hasa kwa kuzingatia nchi yetu ina rasilimali
zinazohitajika katika kujenga uchumi wa viwanda.
“Nafahamu kwamba tunakila aina ya
rasilimali inayowezesha uwepo wa viwanda hapa nchini ikiwemo umeme wa
kutosha pamoja na malighafi zake na kwa maana hiyo serikali ya awamu ya
tano imepanga kuifanya sekta ya viwanda kuchangia pato la taifa kwa
asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka 7.3 ya sasa”. Alisema Rais
Magufuli.
Aidha Dkt. Magufuli aliwatoa
wasiwasi wadau hao kuhusu uwepo wa soko la uhakika kwa bidhaa
zitakazozalishwa kwani Tanzania imezungukwa na nchi zenye uhitaji wa
bidhaa mbalimbali na pia ni Mwanachama wa jumuiya mbalimbali ndani na
nje ya Afrika.
Naye Waziri wa Viwanda, Biashara
na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage aliwataka wamiliki wa Viwanda Nchini
kuunganisha nguvu katika uanzishaji na uendelezaji wa viwanda nchini ili
kuongeza upatikanaji wa bidhaa nchini hali itakayopelekea kukuza uchumi
wa nchi na kuongeza ajira kwa watanzania.
UZINDUZI WA MRADI WA USAID WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA MKOANI MARA
Mkuu
wa Wilaya ya Serengeti, Ally Maftah akizindua mradi wa Uboreshaji wa
mifumo ya sekta za Umma (PS3 Mkoani Mara leo. Maftah alizindua mradi huo
kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo. PS3 inatekelezwa
katika mikoa 13 ya Tanzania Bara kupitia Halamshauri 97 chini ya
ufadhili wa Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID).
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa
Mradi wa PS3, Mtaalam wa Fedha wa mradi huo, Abdul Kitula akizungumza
ambapo alisema kuwa PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya
Tanzania kwa ajili ya kuimarisha
mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji.
mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji.
Kaimu Katiobu Tawala Mkoa wa Mara, Eldom Anyosisye akizungumza.
Baadhi ya washiriki ambao ni Wakurugenzi na watendaji wengine kutoka Mara wakifuatilia uzinduzi huo.
Mtaalam
kutoka TMA, Paul Chikira ambae ni mmoja wa wawezeshaji akifuatilia
tukio hilo la uzinduzi wa mradi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Mkuu wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Felix Lyniva akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi
Washiriki wakipitia nyaraka wakati wa uwasilishaji mada.
Mtaalam wa masuala ya Rasilimali watu kutoka Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Remmy Moshi akiwasilisha mada.
Mtaalam wa Mawasiliano na Takwimu wa Mradi wa PS3, Desideri Wengaa akitoa mada juu ya mawasiliano na utoaji takwimu sahihi.
Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wakifuatilia mada katika uzinduzi huo.
Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wakifuatilia mada katika uzinduzi huo.
MKE WA RAIS MAMA JANETH AWATAKA WATANZANIA KUWASAIDIA WAZEE NA WATU WENYE ULEMAVU.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkaribisha Mke wa Waziri Mkuu Mama
Marry Majaliwa Ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam. Mama
Majaliwa alifika Ofisini hapo ili kujionea shughuli mbalimbali
zinazofanywa na mke wa Rais.
Mke
wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
Magogoni jijini Dar es Salaam.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akimuonesha Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry
Majaliwa mafuta maalumu yanayotumiwa watu wenye ulemavu wa ngozi Albino
ambayo atayagawa hivi karibuni kwa baadhi walemavu wa ngozi katika
maeneo mbalimbali nchini. Pia Mke wa Rais mama Janeth amewaomba
watanzania kuwajali Wazee na watu wenye ulemavu wa ngozi. PICHA NA IKULU
LUHWAVI AKAGUA JENGO LA MIKUTANO LA CCM DODOMA LEO
Luhwavi akitazama hali ya maua kwenye bustani za jengo la ukumbi huo |
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akihoji kuhusu hali ya bustani zinazozunguka jengo hilo |
Luhwavi akielekeza namna ya kuboreshwa bustani zinazozunguka jengo la ukumbi huo |
Luhwavi akiingia ndai ya ukumbi wa jengo hilo kuona hali halisi |
Bendera ya Taifa na bendera ya CCM zikipepea kwenye jengo hilo la Mikutano la CCM, kama ilivyo kawaida. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO |
Katibu Mkuu Wizara ya Afya azindua Baraza la Wafanyakazi Muhimbili
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki
Ulisubisya akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MNH) LEO. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamedi
Janabi, Katibu wa baraza hilo, Dk Kissa Mwambene. Kushoto ni Mwenyekiti
wa baraza hilo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru na Mkurugenzi wa Rasilimali
Watu wa MNH, Makwaia Makani.PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI (MNH)
Wajumbe
wa Baraza la Wafanyakazi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakipiga
makofi wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto
na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya wakizungumza na wajumbe wa baraza hilo
Leo kwenye hospitali hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa
Lawrence Museru akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi LEO
kabla ya kupiga kura za kuwachagua viongozi wapya wa baraza hilo.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani wa
hospitali hiyo.
Wajumbe
wa Baraza la Wafanyakazi la MNH wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru katika kikao hicho.
Wajumbe wakipiga kura LEO za kuwachagua viongozi wapya wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali hiyo.
Dk Kissa Mwambene akiwashukuru wajumbe baada ya kumchagua Leo kuwa Katibu wa baraza hilo.
Wakili Eneza Msuya akiwashukuru LEO wajumbe baada ya kumchagua kuwa Katibu Msaidizi wa baraza hilo.
Kutoka
kushoto ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa hospitali hiyo, Dk Kissa
Mwambene, Mwenyekiti wa baraza hilo, Profesa Lawrence Museru, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki
Ulisubisya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI), Profesa Mohamedi Janabi, Katibu Msaidizi wa baraza hilo,
Wakili Eneza Msuya na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia
Makani.
………………………………………………………………………………………………….
Katibu Mkuu Wizara ya Afya ,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya
ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuboresha maslahi ya
watumishi wake na kuendelea kuweka miundombinu bora ya kiutendaji.
Akizindua Baraza la Wafanyakazi
la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dk. Ulisubisya amesema hatua
hiyo ni ya kupongezwa kwani inampa motisha mtumishi kufanya kazi kwa
bidii.
“Nimefarijika sana kuoana
suala la maslahi ya watumishi linapewa kipaumbele hapa MNH kwa kweli
mnastahili pongezi na taasisi nyingine hazina budi kuiga mfano huu,
lakini napenda kusisitiza kuwa kila mtumishi ni vema akanufaika na
maboresho haya amesema,” Dk Ulisubisya.
Akizungumza kabla ya uzinduzi
wa baraza hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amesema hivi sasa hospitali hiyo
imeongeza mapato yake kutoka Shilingi Bilioni 2 hadi kufikia Bilioni 4.
Pia amesema katika kuendelea
kuboresha huduma za matibabu MNH ina mpango wa kuongeza ICU ya watoto
wadogo pamoja na ICU ya kina mama wenye matatizo ya uzazi ili kuokoa
maisha ya mama na mtoto .
Kwa mujibu wa Profesa Museru
Hospitali hiyo ipo katika hatua za mwisho za kupata mkopo kutoka Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkopo ambao utasaidia kupanua huduma
za afya ikiwamo kununua vifaa tiba vya upasuaji.
Katika kikao, wajumbe wa Baraza
la Wafanyakazi wamemchagua Dk. Kissa Mwambene kuwa Katibu wa Baraza
hilo pamoja na Eneza Msuya kuwa Katibu Msaidizi.
Serikali kuanzisha benki ya maendeleo ya viwanda nchini
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua
nembo mpya ya Tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa Viwanda PMAYA The President’s Manufacure of the Year pamoja na Mwenyekiti wa Wenyeviwanda Tanzania CTI Dkt. Samwel Nyantahe katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU / HASSAN SILAYO-MAELEZO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na wadau mbalimbali wa CTI na kutoka Sekta ya Viwanda nchini kabla ya
kutoa Tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2015 katika
Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Leodgar Tenga
mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rais.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
baadhi ya Wadau wa Viwanda nchi mara baada ya kumalizika kwa hafla hio
ya utoaji Tuzo za Rais.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia
na Waziri wa Nishati na Madini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais
kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es
Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea
baadhi ya mabanda ya bidhaa zinazotoka viwandani wakati wa hafla ya
utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo
Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akiongea na
wadau wa sekta ya Viwanda wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa
wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 na kuwataka kuunganisha
nguvu katika uanzishaji na uendelezaji wa viwanda nchini ili kuongeza
upatikanaji wa bidhaa nchini hali itakayopelekea kukuza uchumi wa nchi
na kuongeza ajira kwa watanzania.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua
nembo ya shirikisho la viwanda nchini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za
Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es
Salaam kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles
Mwijage, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda
Tanzania (CTI) Leodger Tenga na wa pili ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda nchini Tanzania (CTI)Dr.Samuel Nyantahe.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na
wadau wa sekta ya viwanda nchini(hawapo pichani) na kuwaahidi kuwaunga
mkono katika harakati za kuendeleza sekta ya viwanda ikiwamo kuanzisha
banki ya maendeleo ya viwanda nchini itakayosaidia kutoa mikopo yenye
riba nafuu kwa wale wenye nia ya kuanzisha viwanda.
Wadau
wa Sekta ya Viwanda nchini wakimsilkiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya utoaji tuzo za
Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es
Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo
kwa washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa
mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo
kwa washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa
mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora
wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
Zanzibar yaadhimisha siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani
Mwakilishi
wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Zanzibar Dkt. Ghirmany akitoa taarifa
ya Shirika hilo kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Wizara
ya Afya Zanzibar.
Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.
………………………………………………………………………………………………….
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Inakadiriwa zaidi ya watu milioni
sita duniani kote hupoteza maisha kila mwaka kutokana na athari za
matumizi ya tumbaku na wanaoathirika zaidi ni vijana wenye umri wa miaka
30 hadi 39.
Akizungumza na waandishi wa
habari katika Ukumbi wa Wizara ya Afya kwenye maadhimisho ya siku ya
kupinga matumizi ya tumbaku Duniani, Meneja wa Kitengo cha maradhi
yasiyoambukiza Zanzibar ndugu Omar Mwalimu Omar amesema mbali na
kusababisha vifo, matumizi ya tumbaku yamekuwa chanzo kikubwa cha
maradhi.
Amesema tafiti zilizofanyika
zimeonyesha kuwa matumizi ya tumbaku yanachangia kwa asilimia 71 kupata
saratani ya mapafu, asilimia 42 magonjwa ya njia za hewa na asilimia
kumi magonjwa ya moyo.
Ndugu Omar amesema pamoja na kuwa
Zanzibar haizalishi tumbaku na haina viwanda vya sigara, bado matumizi
ya bidhaa hizo ni ya kiwango cha juu.
Ameongeza kuwa kwa mujibu wa
utafiti uliofanywa na Wizara ya Afya mwaka 2011ulionyesha asilimia 7.3
ya wazanzibari kati ya miaka 25 hadi 64 ni watumiaji wa sigara na
asilimia 4.1 wanatumia tumbaku kwa njia za kunusa na kuvuwata.
Meneja wa Kitengo cha maradhi
yasiyoambukiza amezitaja athari nyengine zinazotokana na matumizi ya
tumbaku ni kuanguka kwa uchumi wa nchi.
“Kama nilivyotangulia kusema,
rika linaloathirika zaidi ni vijana wa miaka 30 hadi 39 ni wazi kuwa
nchi zinapoteza nguvu kazi ambayo ipo katika umri wa kuongeza kipato cha
nchi,” alisisitiza Ndugu Omar.
Amekiri kuwa katika vita vya
kupambana na matumizi ya tumbaku kumejitokeza changamoto ya viwanda
vinavyotengeneza bidhaa za tumbaku kuwa na nguvu kubwa ya kifedha na
matumizi ya tumbaku imekuwa moja kati ya starehe hususan katika jamii ya
vijana.
Amewataka waandishi wa habari
kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Wizara ya Afya ya kudhibiti
matumizi ya tumbaku kwa kuitanabahisha jamii juu ya athari zinazotokana
na tumbaku.
Akizungumza katika mkutano huo,
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) aliepo Zanzibar Dkt.
Ghirmany amesema Umoja wa Mataifa umepanga kila ifikapo tarehe 31 Mei ya
kila mwaka iwe ni siku ya kupinga matumizi ya bidhaa zinazotokana na
tumbaku ili kuitanabahisha jamii juu ya athari inayotokana na tumbaku.
Ameishauri Serikali kuandaa
kanuni ya matumizi ya tumbaku ili sheria iliyotungwa ya kudhibiti
uvutaji wa sigara katika maeneo ya wazi iweze kufanya kazi.
Ujumbe wa mwaka huu katika
kuadhimisha siku ya kupinga matumizi ya tumbaku Duniani ni ‘kuwa tayari
kuondosha vivutio katika paketi za kuhifadhia sigara’.
SERIKALI ITAHAKIKISHA INAENDELEA KULINDA RASILIMALI ZA NCHI IKIWEMO URITHI WA DUNIA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa
……………………………………………………………………………………………..
Woinde shizza,Arusha
SERIKALI ya awamu ya tano imesema kuwa itaendeleza jitihada za
kutunza na kulinda urithi wa dunia ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi
wanaoishi maeneo ya uhifadhi ili watanzania wote waweze kunufaikana
rasilimali za nchi .
Hayo yalisemwa na waziri mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akifungua
mkutano wa kulinda urithi wa dunia wa Afrika kama nyenzo ya maendeleo
endelevu unaoendelea jijini Arusha
Majaliwa alisema kuwa rasilimali zilizopo ni za watanzania na ili
kuhakikisha kuwa wananufaika nazo serikali itahakikisha inatunza na
kulinda uhifadhi ili yawe endelevu na kusaidia vizazi vijavyo.
Alisema kuwa Tanzania ni moja ya nchi tajiri yenye urithi na hivyo ili
kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika haswa waishio maeneo ya uhifadhi
serikali itatoa elimu ya kutosha ili waepuke kuchangia uharibifu wa mazingira
unaotokea kwenye hifadhi za taifa .
“Rasilimali hizi ni zetu na hivyo hata wanaoishi maeneo ya hifadhi
watusaidie kwa wale wanaoingilia na kuharibu kwani hata hizo mali
asili zinatusaidia sote na ndiyo sababu tumewekea mikakati ya kutunza maeneo
hayo ili yawe endelevu’alisema
Kwa upande wake mwenyekiti wa mkutano huo ambaye ni Katibu Mkuu Wizara
ya Mali asili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi Alisema kuwa
madhumuni ya mkutano huo ni kutambua changamoto na mambo ambayo
yanatishia na kuathiri uhifadhi bora wa maeneo ya urithi wa dunia
katika afrika .
Aidha mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa kupitia upya shughuli
zinazotekelezwa katika eneo la urithi wa dunia na kuangalia mchango wa
miradi ya jamii za kiafrika na kuandaa muelekeo wa miaka kumi ijayo.
Milanzi alisema kuwa mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa kushawishi
wanawake kuongeza ushiriki wao katika miradi inayoendana na uhifadhi
wa urithi na maendeleo endelevu pamoja kuchunguza jinsi mitafaruku
inayotokea kwenye maeneo ya urithi wa dunia kutokana na makundi ya
kigaidi na kutunza amani utamaduni na uridhi asilia.
Aliongeza kuwa pia mkutano huo umejikita kwenye sera ya UNESCO ya
mwaka 2015 inayohusu kujumuisha maendeleo endelevu kwenye mkataba wa
uridhi wa dunia.
“mkutano huo pamoja na matokeao tegemewa kisayansi, pia utakuwa na
manufaa kwa taifa na sio tu kuitangaza Tanzania kutalii na kisasa bali
pia ni fursa muhimu ya kiuchumi kutokana na idadi ya wageni watakao
huthudhuria mkutano huu pamoja na kuanzisha mitandao wa kitaaluma na
kujenga mitaji wa kijamii”alisema Malinzi
Aidha pia mara baada ya mkutano huu na kupata muafaka wa yote kutakuwa
na tamko lililotokana na majadiliano yaliyokuwa yakifanyika siku zote
za mkutano na tamko hili linatarajiwa kutolewa katika hifadhi ya taifa
ya Ngorongoro

SERIKALI YAITAKA RITA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU UMUHIMU KUANDIKA WOSIA WA MIRATHI
Na Mahmoud Ahmad Arusha.
SERIKALI imeitaka
wakala wa usajili,Ufilisi na Udhamini, RITA, kuhakikisha inatoa elimu ya
kutosha kwa wananchi kuelewa umuhimu wa kuandika wosia na mirathi ,ili
kuondoa migogoro kwa familia wakati wa kugawa mirathi ya marehemu.
Rai hiyo imetolewa jana
na mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu, alipokuwa akifungua
kampeni ya siku NNe ya kisheria inayotolewa bure na RITA, kuhusu
kuandika mirathi na wosia na kuwaelekeza eneo salama la kuhifadhi wosia
ukisha andikwa na mhusika ili kuondoa migogoro mingi kwa familia pindi
mhusika anapofariki dunia.
Mkuu huyo wa wilaya,
alisema,wananchi wengi hawana elimu juu ya wosia na mirathi hivyo RITA,
ambayo ni wakala wa serikali ina jukumu kubwa la kuhakikisha elimu
inawafikia wengi na hivyo kuwezesha wajane na watoto ambao ndio
waathirika kupata mirathi .
Alisema wosia unasaidia
kutatua migogoro ambayo ingelijitokeza wakati wa kugawa mirathi ya
marehemu na mtu kuandika wosia sio uchuro bali ni kuweka utaratibu wa
mali za muhusika zitakavyogawiwa pindi akisha fariki dunia.
Aliikumbusha jamii kuwa
msimamizi wa mirathi sio mrithi wa mali ya marehemu bali jukumuake ni
kukusanya mali yote na madeni yote ya marehemu na kusimamia ugawaji na
ulipaji wake na kamwe msimamizi yeyote asijihusishe na urithi .
Jamii nyingi zimekuwa
zikiingia kwenye migogoro ya kugawana mirathi kutokana na kutokuwa na
elimu ya kutosha ya kuandika wosia kabla ya kifo na matokeo yake
wanaoathirika ni wajane na watoto ambao hukosa haki yao .
Awali mratibu wa
kampeni hiyo,msajili na wosia kutoka makao makuu ya RITA, Augostino
Mbuya, alisema migogoro mingi imekuwa ikijitokeza kwenye familia wakati
wa kugawa mirathi kutokana na kutokuwepo kwa wosia ambao ni mwongozo wa
jinsi ya kuigawa mali ya marehemu kwa wahusika na matokeo yake watoto na
wajane hukosa haki yao ya kurithi.
Alisema kutokana na
hali hiyo RITA, ipo tayari kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma hiyo ya
kuandika wosia kutokana na wananchi wengi kutokuwa na elimu na kufahamu
wapi watapata huduma hiyo ya kuandika wosia na ugawaji wa mirathi za
marehemu
Mbuya,alisema mkakati
uliopo ni kusogeza huduma ya kuandika wosia na mirathi ngazi za mikoa na
wilaya pamoja na kuhakikisha wanakuwepo wanasheria wa kutosha lengo ni
kuiwezesha jamii kuondokana na migogoro ambayo inaweza kuepukwa wakati
wa kugawa mali za marehemu.
Alisema tangia
kuanzishwa kwa huduma hiyo ya Rita, imeweza kusajili wosia zaidi ya 300
na 30 kati yake zimeshachukuliwakwa utekelezaji .
Akisoma taarifa ya kazi
za Rita, msajili wa mirathi na wosia, kutoka makao makuu ya Rita,
Joseph Mwakatobe amesema mahakama kuu imeiteua RITA, kusimamia utatuzi
wa migogoro ya urithi na uandishi wa wosia lngo ni kuondoa migogoro
inayojitokeza pindi mtu anaofariki dunia.
Alisema Rita,
itaendesha kampeni hiyo ya kuhamasisha wananchi kuhusu kuandika mirathi
na wosia katika mkoa wote wa Arusha,ili kuwezesha wajane na watoto
wanapata haki yao ya kurithi mali za marehemu .
Aliongeza kuwa kuandka
wosia ni swala lahiari ya mtu,na Rita, imekuwa ikikumbana na changamoto
mbaimbali zkiwemo za kutokuwepo na wosia wakati wa mirathi .
Aliongeza kuwa mirathi
inatolewa kulingana na sheria za dini ya kiislamu, mila na sheria ya
India ya mwaka 1865 ambayo inahusisha makundi yote ambayo hayapo kwenye
makundi ya kidini na mila.
WAZIRI WA AFYA MHE.UMMY MWALIMU ATOA TAMKO KUHUSU SIKU YA KUPINGA MATUMIZI YA TUMBAKU DUNIANI, TAREHE 31 MEI 2016
Siku ya kupinga matumizi ya Tumbaku Duniani, huadhimishwa duniani kote kila mwaka tarehe 31 Mei.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya kupinga matumizi ya tumbaku mwaka 2016 ni “jiandae kwa pakiti zisizo na matangazo wala vivutio”
Kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha jamii juu ya kujiepusha au kujikinga na vivutio mbalimbali vya matangazo yanayo hamasisha matumizi ya sigara ambayo ina madhara mengi kiafya.
Tanzania kama zilivyo nchi nyingine duniani inaadhimisha siku hii, kwa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kutoa elimu ya umuhimu wa kuzuia na kujikinga na matumizi ya sigara na bidhaa za tumbaku.

Tafiti nyingi zinathibitisha
madhara yatokanayo na matumizi ya tumbaku ni pamoja na magonjwa
yasiyoambukiza kama vile saratani, magonjwa ya mishipa ya damu na moyo,
kiharusi, magonjwa ya njia ya hewa.
Tafiti pia zinaonyesha takriban watu 6,000,000 hupoteza maisha duniani kwa mwaka kwa utumiaji wa tumbaku na bidhaa zake.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani kwa mwaka 2016, inalenga kuelimisha na kuhamasisha jamii kuachana na matumizi ya tumbaku na kusisitiza kwa wazalishaji kutokuweka maandishi au nembo zinazovutia ili kuishawishi jamii kutumia bidhaa hizo. Aidha tumbaku imekuwa ikisababisha madhara kiafya kama vile magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza. Magonjwa hayo ni magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, saratani, ugonjwa wa kisukari na magonjwa ya njia ya hewa.
Mambo mengine yanayoongeza uwezekano wa kupata magonjwa yasiyoambukiza ni pamoja na ulaji usiofaa hasa matumizi ya chumvi kupita kiasi, kutofanya mazoezi, unywaji pombe kupita kiasi na msongo wa mawazo.

Ili kuzuia maradhi
yasiyoambukiza yatokanayo na matumizi ya tumbaku na bidhaa zake ni
muhimu kufuata kanuni za afya ambazo ni kutovuta sigara na kama wewe ni
mvutaji, kutovuta sigara hadharani maana madhara yake ni sawa hata kwa
mtu asiyevuta ambaye anapata moshi kutoka kwa mvutaji, kuendelea
kuielimisha jamii juu ya madhara mbalimbali yatokanayo na utumiaji wa
tumbaku hususani kwa vijana.
Serikali inaendelea na mkakati
wa tiba kwa watu wenye uraibu wa matumizi ya tumbaku, ikiwa na lengo
kupunguza matumizi hayo miongoni mwa jamii. Kuhakikisha pakiti za
tumbaku na bidhaa zake ziwe na tahadhari ya madhara ya utumiaji wa
tumbaku na bidhaa zake. Aidha, serikali, inaendelea kurekebisha sheria,
kanuni na taratibu za udhibiti wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatumia maadhimisho haya kuwa sehemu ya uhamasishaji kwa jamii kama ilivyo kwenye nchi zote duniani.
Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatumia maadhimisho haya kuwa sehemu ya uhamasishaji kwa jamii kama ilivyo kwenye nchi zote duniani.
TANROADS yakanusha kudaiwa fidia
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Wakala wa Barabara Tanzania
(TANROADS) wamekanusha kudaiwa fidia na wananchi wa Kijiji cha
Mazingira,Wilaya ya Handeni mkoani Tanga waliovunjiwa nyumba zao ili
kupisha ujenzi wa barabara.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Meneja wa TANROADS Mhandisi Alfred Ndumbaro alipokuwa
akiongea na mwandishi wa habari hii juu ya malalamiko ya wananchi wa
Kijiji hicho kuhusu kutolipwa fidia zao.
”Sheria iko wazi kuwa wanaojenga
karibu na barabara wakivunjiwa hawalipwi fidia yoyote lakini wale ambao
ujenzi wa barabara uliwafuata katika maeneo yao wana haki ya kulipwa
fidia”, alisema Mhandisi Ndumbaro.
Mhandisi Ndumbaro ameongeza kuwa
zoezi la malipo ya fidia kwa wanakijiji waliokuwa na uhalali wa malipo
hayo lilishakwisha zamani kwa hiyo, wanaodai sasa ni wale ambao nyumba
zao zilivunjwa kutokana na kujenga eneo la barabara.
Aidha, Mhandisi huyo ametoa rai
kwa wananchi kufuata sheria za ardhi ili kupata uhalali wa viwanja vyao
pamoja na kuepuka usumbufu na gharama za kuvunjiwa nyumba zao.
Nyumba hizo zilivunjwa ili
kupisha ujenzi wa barabara ya lami yenye Kilomita 54 kutoka Mkata hadi
Handeni iliyojengwa na Kampuni ya Synohydro Corporation Limited ya
China.
ZIARA YA RAIS KUTEMBELA SEHEMU ZILIZOHARIBIWA NA WAPINZANI (CUF)
Wanachama
cha Mapinduzi CCM Tawi la Tibirinzi Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini
Pemba wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein
(hayupo pichani) wakati alipotembelea tawi lao lililochomwa moto na
Wapinzani kwa sababu za kisiasa kuona hali ya uharibifu uliotokea,
[Picha na Ikulu.] 31/05/2016.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimianana Sheha wa Shehia ya
Maziwa Ngombe Bi,Asha Yussuf Hassan, aliyevunjiwa Nyumba yake na Wafuasi
wa Chama cha CUF hivi karibuni kwa sababu za kisiasa pamoja na kukatiwa
Migomba yeke wakati alipomtembelea leo kuangalia maafa hayo, [Picha na
Ikulu.]31/05/2016.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimianana Viongozi wa Chama
cha Mapinduzi Wilaya ya Micheweni wakati alipomtembea Sheha wa Shehia ya
Maziwa Ngombe Bi,Asha Yussuf Hassan, aliyevunjiwa Nyumba yake na
Wafuasi wa Chama cha CUF hivi karibuni kwa sababu za kisiasa pamoja na
kukatiwa Migomba yeke wakati alipomtembelea leo kuangalia maafa hayo,
[Picha na Ikulu.]31/05/2016.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo ya
ushuhuda kutoka kwa Sheha wa Shehia ya Maziwa Ngombe wilaya ya
Micheweni Pemba, Bi,Asha Yussuf Hassan (katikati) aliyevunjiwa Nyumba
yake na Wafuasi wa Chama cha CUF hivi karibuni kwa sababu za kisiasa
pamoja na kukatiwa Migomba yeke wakati alipomtembelea leo kuangalia
maafa hayo, [Picha na Ikulu.]31/05/2016.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na wanachama cha
Mapinduzi Tawi la Tibirinzi Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba
ambalo lilichomwa Moto na wapinzani hivi karibuni,akiwa katika ziara
maalum ya kutembelea maeneo mbali mbali yaliyopata matukio ya
kisiasa,[Picha na Ikulu.] 31/05/2016.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) alipokuwa
akizungumza na Wananchi wa Shehia ya Maziwa Ngombe wilaya ya Micheweni
Pemba leo wakati alipomtembelea Sheha wa Shehia hiyo Bi,Asha Yussuf
Hassan (katikati) aliyevunjiwa Nyumba yake na Wafuasi wa Chamacha CUF
hivi karibuni kwa sababu za kisiasa pamoja na kukata Migomba yeke,
[Picha na Ikulu.]31/05/2016.
Mkuu
wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe,Rasshid Hadid (wa pili
kulia) akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein
(katikati) wakati alipofika Kijiji cha Shengejuu shehia ya Pembeni
kutembelea ujenzi wa Nyumba ya Nd,Said Khamis Iliyobomolewa na Wafuasi
wa Chama cha CUF kwasababu za Kisiasa,(kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar Mhe,Vuai Ali Vuai,[Picha na Ikulu.]31/05/2016.
No comments:
Post a Comment