fastjet,
shirika la ndege la bei nafuu Afrika limezifanya ndoto za
usafiri kuwa za kweli kwa abiria wake zaidi ya milioni mbili waliopaa
anga za Afrika tangu kuzinduliwa kwake Novemba 2012.
Ukiwa
kama mkakati wa kuhamasisha hata Watanzania wengi zaidi kusafiri,
fastjet imetangaza kwamba abiria yeyote anayenunua tiketi kuanzia
Jumanne Mei 31 ataingia kwenye bahati na nasibu ya kwanza ya aina
yake ijumulikanayo Big 10 draw ambapo washindi 10 watasafiri
bure katika njia yoyote ya fastjet katika mtandao wake barani Afrika.
Kwa
watu kumi watakaoshinda bahati nasibu hiyo shirika linawapa uwezo wa
kwenda katika mapumziko au kwenda katika safari ya manunuzi pamoja na
marafiki na familia jambo wamekuwa wakiliwazia kila mara.
Ama
kwa wajasiriamali wa Tanzania, safari hiyo inaweza kutumia kukuza
mahitaji ya biashara kwa kuokoa gharama za usafiri katika safari
nyingine kumi wanazozihitaji kusafiri.
“Ni
rahisi, lengo la fastjet ni kufanya uwezekano kwa wateja wengi
kusafiri, iwe ni kwa shughuli za biashara, kutembelea marafiki na
familia, au kufurahia burudani ya kusafiri,” alisema Meneja Mkuu wa
fastjet Tanzania John Corse.
Njia
ambazo zinahusiana kwa ajili hiyo ni safari za kutoka Dare es Salaam
kwenda Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Zanzibar, Nairobi, Entebbe, Lusaka,
Harare na Johannesburg hali kadhalika safari kati ya Kilimanjaro na
Harare.
Tiketi
zitakazonunuliwa Jumanne Mei 31, 20016 kwa njia za kimataifa na za
ndani zitawawezesha abiria wake kuingia katika bahati nasibu ya Big 10.
Washindi watatangazwa Juni 2016 na safari 10 za bure ni lazima
zifanyike kabla ya Desemba 11, 2016.
Ikitambuliwa
kama shirika la ndege la gharama nafuu Afrika, fastjet hivi sasa
inafanya safari ndani ya nchi 11 kwa wafanyabiashara, watali na familia
ambazo zimeipokea tozo lake la nauli nafuu na linalofikia kwa usafiri
wa anga.
“Usafiri
wa anga ni ufunguo unaoendelea kuhamasisha na kukuza uchumi wa
Tanzania kwa kuufanya uwe rahisi kwa familia, wafanya biashara na
watalii kumudu kusafiri,” alisema Corse na kuongeza, “tumezindua
punguzo hili la nauli hivyo kwamba hata wasafiri wanaweza kuzoea
usafiri wa anga wanaoumudu, iwe wanasafiri kwa ajili ya biashara au
mapumziko.”
Kukata tiketi kiunaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kupitia www.fastjet.com, kupitia wakala aliyethibitishwa au kwa kuwasiliana na na fastjet kupitia +255 784 108 900. Malipo pia yanaweza kufanyika kwa fedha taslimu, kwa njia ya mtandao kwa kutumia kadi au malipo kwa njia ya mitandao ya simu.
No comments:
Post a Comment