Na: Frank Shija, MAELEZO
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam
inakusudia kuruhusu baadhi ya maduka makubwa kutoa huduma zaidi ya muda
wa kawaida wa maduka kufungwa ili kutoa fursa kwa wafanyakazi kupata
huduma hiyo pindi wanapotoka makazini.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda alipomwakilisha Makamu wa Rais
kwenye hafla ya Futali iliyoandaliwa na Benki ya NMB jana jijini Dar es
Salaam.
Makonda alisema kuwa kusudio hilo
linatokana na changamoto ya upatikanaji wa nafasi ya kupata huduma hiyo
kwa wafanyakazi kwani uchelewa kutoka maofisini jambo lilalosababisha
baadhi ya wafanyabiashara kupeleka bidhaa zao huko huko ofisini.
Aliongeza kuwa amekusudia kufanya
mambo muhimu matatu katika kipindi hiki cha mwenzi mtukufu wa ramadhani
ambapo aliyataja mambo hayo kuwa ni kuongeza muda wa kufunga maduka
hasa yale makubwa (malls), kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika
maeneo ya umma na kupambana na watumiaji wa usafiri wa pikipiki
wanaokiuka sheria ya matumizi ya Kofia ngumu (helmet).
“Nimekusudia kufanya mambo muhimu
matatu ndani ya mwezi huu mtukufu wa ramadhan, niwadokeze tu kuwa mambo
hayo ni pamoja na kuongeza muda wa kufanya biashara kwa maduka makubwa (shopping malls),
kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya umma na kupambana na
wavunjifu wa sheria ya matumizi ya helmet.” Alisema Makonda.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania Bibi. Ineke Bussemaker alisema kuwa
wao kama Taasisi ya Kifedha imekuwa na desturi ya kuwajali wateja wao
hivyo wanatumia fursa hii kushiriki pamoja na wateja wao walio katika
mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ili kuwatia moyo wakustahilifunga
hiyo muhimu katika uislamu.
Aidha aliongeza kuwa NMB
itaendelea kushirikiana na jamii mbalimbali katika kuhakikisha inasaidia
pale panapohitajika msaada wao kama ambavyo wamekuwa wakitoa misaada
katika kuchangia huduma za kijamii kama vile madawati.
No comments:
Post a Comment