Pages

Friday, June 24, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA BALOZI WA NORWAY, FINLAND NA MJUMBE MAALUM KUTOKA OFISI YA WAZIRI MKUU WA MALAYSIA, IKULU

j1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Norway hapa nchini Hanne-Marie Kaarstand Ikulu jijini Dar es Salaam.
j2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Norway hapa nchini Hanne-Marie Kaarstand mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
j3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na balozi wa Norway hapa nchini Hanne-Marie Kaarstand watatu kutoka kushoto mara baada ya kumaliza mazungumzo  yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
j4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma barua ya pongezi iliyowasilishwa kwake na Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia Dato Sri Idris Jala ambaye ni Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Malaysia.
j5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia Dato Sri Idris Jala ambaye ni Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Malaysia mara baada ya kumkabidhi barua hiyo ya pongezi.
j6 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia Dato Sri Idris Jala ambaye ni Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Malaysia mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
j7 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Finland hapa nchini Pekka Hukka aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
j8 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Finland hapa nchini Pekka Hukka mara baada ya kumkabidhi Kitabu Ikulu jijini Dar es Salaam.
j9 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Finland hapa nchini Pekka Hukka mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU

Rais Dkt. Shein AFANYA uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .

RAIS WA ZANZIBAR
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
———————————
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Nd. Bakari Khamis Muhidin ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango ya Raslimaliwatu ni ndugu Khamis Haji Juma na Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Pemba Nugu Masoud Ali Mohamed.
Katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za Serikali Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ni Ndugu Daima Mohammed Mkalimoto.
Wizara ya Fedha na Mipango alieteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi ni Ndugu Ali Bakari Ishaka, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Barabara ni Ndugu Mwalim Ali Mwalim na Ofisa Mdhamini wa Wizara hiyo Pemba ni Ndugu Ibrahim Saleh Juma.
Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Kamishana wa Kazi ni Ndugu Fatma Iddi Ali, Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa wazee Ndugu Wahida Maabad Mohamed na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Ndugu Mwanaidi Mohamed Ali.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Wanawake na Watoto Ndugu Nasima Haji Choum na Ofisa Mdhamini, Wizara ya Kazi Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Pemba Ndugu Khadija Khamis Rajab.
Dkt. Fadhil Mohamed Abdullah anakuwa Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya katika Wizara ya Afya na Mkurugenzi wa Huduma za Hospitali ni Dkt. Mohammed Dahoma.
Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Naibu Katibu Mkuu (Mifugo na Uvuvi) ni Dkt. Islam Seif Salum.  Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti ni Ndugu Sheha Idrissa Hamad na Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi Ndugu Noah Saleh Said.
Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo ni Ndugu Mohamed Khamis Rashid, Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka Ndugu Yussuf Haji Kombo wakati Dkt. Bakari Saad Assed anakuwa Mkurugenzi wa Chuo cha Kilimo, Kizimbani.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, Kizimbani ni Dkt. Suleiman Shehe Mohammed, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Ndugu Mussa Aboud Jumbe, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mifugo Dkt. Yussuf Haji Khamis na Ofisa Mdhamini, Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Pemba ni Ndugu Sihaba Haji Vuai.
Katika Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Ndugu Hassan Abdalla Mitawi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu (Habari), Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti Ndugu Mahmoud Omar Hamad.
Ndugu Imane Duwe ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ZBC ni Nassra Mohammed Juma.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji ni Ndugu Rafii Haji Makame, Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali Ndugu Yussuf Khamis Yussuf, Mkurugenzi wa Habari (Maelezo) Ndugu Hassan Vuai.
Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari ni Chande Omar Omar na Ofisa Mdhamini, Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Pemba Ndugu Khatib Juma Mjaja.
Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi ni Ndugu Bimkubwa Abdi Nassib. Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti Ndugu Khatib Mohamed Khatib na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini ni Ndugu Abdalla Hussein Kombo.
Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Mkurugenzi wa Baraza la Mitihani katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ni Ndugu Zubeir Juma Khamis.
Ofisa Mdhamini Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Pemba ni Ndugu Juma Bakari Alawi na  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) ni Dkt. Said Seif Mzee.

WAZIRI MWIGULU AFUNGA MAFUNZO YA AWALI YA JESHI LA POLISI NA UHAMIAJI NAMBA 1/2015/2016, CCP MJINI MOSHI

g1 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimkabidhi zawadi mhitimu Irene Joji (kushoto) kwa kufanya vizuri katika masomo yake wakati wa mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji yaliyofanyika katika Chuo Cha Polisi (CCP) mjini Moshi. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo hayo ambayo yamefungwa rasmi na Waziri Nchemba mjini humo leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akikagua gadi ya wahitimu wa Jeshi la Polisi na Uhamiaji kabla ya kuyafunga mafunzo ya wahitimu hao wa mafunzo ya awali yaliyofanyika katika Chuo Cha Polisi (CCP) mjini Moshi. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo.
g3 
Wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi na Uhamiaji wakimuonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (hayupo pichani) jinsi miili yao ilivyokuwa imara kwa pikipiki kupita juu ya matumbo yao. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo hayo ambayo yamefungwa rasmi na Waziri Nchemba
g4 
Kikosi cha gwaride la heshima kikitoa heshima mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto jukwaa kuu) wakati wa sherehe yao ya kumaliza mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi na Uhamiaji, Chuo cha Polisi (CCP) mjini Moshi. Jumla ya wahitimu 3,904 walimaliza mafunzo
g5 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akisalimiana na Naibu Inspekta Jenerali  wa Polisi, Abdulrahman Kaniki wakati Waziri huyo alipokuwa anawasili katika viwanja vya Chuo Cha Polisi (CCP), mjini Moshi kwa ajili ya kufunga mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji, kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli na watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadick.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

MSWADA WA SHERIA YA MANUNUZI YA UMMA WA MWAKA 2106

IMG_20160624_151157_421 
Katika kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni ya 117(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari 2016; Kamati ya Bunge ya Bajeti imepanga kufanya mkutano wa kusikiliza maoni ya wadau wote wa masuala ya Ugavi (Public Hearing) kuhusu Muswada wa Sheria ya Manunuzi ya Umma wa Mwaka 2016 (Public Procurement Act 2016) kabla Muswada huo haujapitishwa na Bunge kuwa Sheria.
Mkutano huo wa kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) unatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu Juni 27, 2016 Bungeni Dodoma kuanzia saaTanoAsubuhi katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni – Dodoma.
Kwa kuzingatia umuhimu wa Muswada huo, Kamati inawaalika wadau wote kufika na kuwasilisha maoni yao mbele ya Kamati kabla kupelekwa katika hatua nyingine. Maoni ya wadau yanaweza pia kuwasilishwa kwa njia ya Posta au Barua pepe kwa anuani ifuatayo:
Katibuwa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
S.L.P. 941,
DODOMA
Baruapepe: cna@bunge.go.tz

PROF. MBARAWA AKAGUA UPANUZI WA UWANJA WA NDEGE DODOMA

1 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi Kampuni ya Chico, anayefanya upanuzi wa njia ya kuruka na kutua ndege katika Uwanja wa ndege wa Dodoma.
2 
Ujenzi wa Barabara ya Kuruka na kutua ndege katika Uwanja wa ndege wa Dodoma ukiendelea. Ujenzi huo kwa kiwango cha lami unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi miwili.
3 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Miradi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Eng. Mbila Mdemu ( wa pili kulia), wakati alipokagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma.
4 
Meneja wa Miradi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Eng. Mbila Mdemu, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alipokagua maendeleo ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma.
————————————————————-
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa miezi miwili kwa mkandarasi Chicco anaefanya upanuzi wa njia ya kuruka na kutua ndege katika uwanja wa ndege wa dodoma kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakamilika.
Akizungumza mara baada ya kukagua kazi ya upanuzi wa uwanja huo, Prof. Mbarawa amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha kuwa ujenzi wa uwanja huo unafanyika kwa kuzingatia viwango vilivyokubalika katika mkataba na kuukabidhi kwa wakati.
“Hakikisheni upanuzi huu unakamilika kwa wakati ili kuupa hadhi inayostahili uwanja wa ndege wa Dodoma,hasa mkizingatia umuhimu wake kitaifa’, amesema Prof. Mbarawa.
Naye Mkandarasi anaejenga uwanja huo amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa atahakikisha ujenzi wake unazingatia viwango na kuukabidhi katika muda uliokubalika kimkataba.
Zaidi ya shilingi bilioni 11.8  zinatarajiwa kutumia katika upanuzi huo na hivyo kuwezesha ndege nyingi zaidi kutumia uwanja huo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

No comments:

Post a Comment