Pages

Wednesday, June 29, 2016

MFUKO WA PENSHENI WA PPF KUTOA HUDUMA ZOTE KWA WATEJA WAKE VIWANJA VYA SABASABA 2016


MFUKO WA PENSHENI WA PPF KUTOA HUDUMA ZOTE KWA WATEJA WAKE VIWANJA VYA SABASABA 2016
Muonekano wa nje ya Jengo la PPF lililopo Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere jijini Dar esSalaam (Sabasaba).
 Maandalizi
 Afisa Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Tulla Mwigune (kulia) Afisa Michango wa Mfuko huo, Saluna Aziz Ally (katikati) na Afisa Michango Glory Maboya, wakijiandaa kuhudumia wateja leo asubuhi katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.
 Afisa Utafiti Neema Mjema (nyuma) na Mwanasheria wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Nyambilila Ndoboka, pia wakijiandaa kuweka mambo sawa kabla ya kuanza kupokea wateja katika Bandao lao la Maonesho kwenye Viwanja vya Sabasaba leo.
 Afisa Uwekezaji wa Mfuko huo, Jonas Mbwambo akiweka mambo sawa kabla ya kuanza kupokea wateja katika Banda lao namba 86 viwanja vya Saba saba.
 Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Pauline Msanga, akitoa maelezo kwa wananchi kuhusu Huduma za uendeshaji Mfuko huo, wakati walipotembelea katika Banda lao lililopo kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, leo. 
 Sehemu ya wananchi waliotembelea Banda la Mfuko wa Pensheni wa PPF wakipata elimu kuhusu Mafao yatolewayo na Mfuko huo na jinsi mwanachama anavyoweza kujiunga na kuchangia.
 Afisa Michango wa Mfuko huo, Saluna Aziz Ally, akimfafanulia mwanachama wake kuhusu uchangiaji wa michango ya Wanachama, 
 Afisa Huduma kwa Wateja, wa PPF Mwajuma Msina, akizungumza na Mwananchi aliyefika kutembelea Banda hilo wakati akimwelezea kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko huo.
  Afisa Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Tulla Mwigune (kulia) akifafanua jambo kwa mstaafu wa PPF.
    Mtaalamu wa Mifumo ya Habari wa Mfuko wa PPF, Isabela Ngalawa, akimwelekeza mmoja kati ya Wanachama wa Mfuko huo kuhusu 'PPF Taarifa Mobile Apps' ili mwanachama aweze kupata taarifa za michango yake kupitia simu yake ya mkononi.
 Afisa Huduma kwa Wateja, Mohamed Siaga, akizungumza na Mwananchi aliyefika katika Banda la PPF  kuhusu jinsi ya kujiunga na Mfumo wa 'Wote scheme kutoka sekta isiyo rasmi 
 Mmoja kati ya Wanasheria wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Nyambilila Ndoboka, akimwelekeza jambo mwanachama wa Mfuko huo kuhusu masuala ya Kisheria, wakati alipofika kutembelea Banda la Maonesho la PFF leo.
Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Temeke, Sostenes Lyimo (kushoto) akifafanua jambo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea Banda hilo.
Baadhi ya Wafanyakazi  wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya Banda lao Namba 86 lililopo katika Viwanja vya Sabasaba
MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA
B1 
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali ya Wabunge Leo Bungeni Mjini Dodoma kuhusu mpango wa Serikali wa kuimarisha Viwanda  vilivyopo hapa nchini na kujenga vipya katika Mikoa mbalimbali.
B2 
Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya ufundi Mhe. Dkt. Joyce Ndalichako akieleza juu ya mkakati wa Serikali kuimarisha vyuo vya Ufundi Stadi hapa nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni Mjini Dodoma.
B3 
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakiyembe akiteta jambo na Mbunge wa Korogwe Vijijini Mhe. Steven Ngonyani Bungeni Mjini Dodoma Leo.
B4 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango  akijibu hoja za wabunge kuhusu Muswada wa Marekebisha ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2016 Leo Bungeni Mjini Dodoma.
B5 
Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akitoa ufafanuzi kuhusu mikakati ya Serikali kuimarisha miundombinu ya Barabara hapa Nchini.
B6 
Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akitoa ufafanuzi kuhusu mikakati ya Serikali kuimarisha miundombinu ya Barabara hapa Nchini.
B8 
Mbunge Viti Maalum Mhe. Martha Mlata akichangia hoja wakati wa uwasilishwaji wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2016.
B7 
Baadhi ya Wabunge wakimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa katikati) mara baada ya kupitishwa kwa muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma.
(Picha zote na Frank Mvungi-Dodoma)

Bunge limepitisha muswada wa marekebisha ya sheria ya ununuzi wa umma wa mwaka 2016

3 
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
——————–
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha muswada wa marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa Mwaka 2016 wenye lengo la kupunguza gharama na muda wa mchakato wa manunuzi Serikalini.
Marekebisho hayo yametokana na gharama kubwa ambayo Serikali imekuwa ikitumia kutokana na huduma na Bidhaa zinazonunuliwa na Serikali kuwa za juu ikilinganishwa na bei ya wastani ya soko.
“Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2016 una lengo la kuongeza ufanisi katika ununuzi wa Umma kwa kuondoa mapungufu yaliyopo katika Sheria ya sasa kwa kupunguza gharama na muda wa michakato ya ununuzi, kutoa upendeleo kwa kampuni za ndani, vikundi maalum, malighafi na bidhaa zinazozalishwa nchini pamoja na kuweka viwango mahsusi kwa bidhaa zitakazotumiwa na Serikali,” alifafanua Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju.
Mhe. Masaju ameendelea kwa kusema kuwa sheria hiyo imeweka kifungu cha dharura  ili kuwezesha vitu vya kuokoa uhai na vinginevyo kununuliwa kwa dharura pindi inapobidi.
Kwa upande wake Mbunge wa Babati Vijijini Mhe. Jitu Soni yeye ameiomba Serikali kuruhusu kununua vifaa tiba vilivyotumika ambavyo muda wake wa kutumia hauna mwisho, kwa mfano vitanda vya kujifungulia  ili kupunguza gharama ya kununua vitanda vipya na kuweza kununua vitanda vingi kwa wakati mmoja.
Aidha Mhe. Jitu ameiomba Serikali kuirudisha tena Sheria hiyo Bungeni baada ya mwaka mmoja ili kufanyiwa marekebisho na kuziba mianya yote ambayo itakuwa imebainika mara baada ya utekelezaji wake kuanza.
Muswada wa marekebisho ya sheria hiyo yanasubiri kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli ili kuanza utekelezaji wake.

Viwanda visivyo endelezwa kurudishwa kwa watanzania

W1 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage
—————————————————
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Viwanda vilivyobinafsishwa na Serikali ambavyo haviendelezwi kutwaliwa ili kutolewa kwa wawekezaji wenye uwezo wa kuviendesha.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini Mhe. Emmanuel Mwakasaka aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa juu ya mwekezaji wa kiwanda cha nyuzi Tabora kwa kushindwa kuendeleza kiwanda hicho.
“Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina inaendelea na tathmini ya viwanda vyote vilivyobinafsishwa na Serikali kikiwemo kiwanda cha nyuzi cha Tabora ili kujiridhisha kama wawekezaji wa viwanda hivyo wanatimiza matakwa ya mkataba na Serikali,” alifafanua Mhe. Mwijage.
Aliendelea kwa kusema kuwa, ikiwa viwanda hivyo vitabainika kubadilishwa matumizi yake au kutoendelezwa basi Serikali itavirudisha kwa watanzani ili viweze kuendelezwa.
Aidha Mhe. Mwijage amesema kuwa, kwa sasa mwitikio wa kuviendeleza viwanda ambavyo vilikuwa havizalishi ni mzuri kwani viwanda vingi vimeanza kufanya kazi lakini kwa wale ambao watashindwa kabisa  kuviendeleza basi viwanda hivyo vitarejeshwa kwa watanzania.
Vile vile Mhe. Mwijage amesema kuwa dhana ya Serikali ya awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda inaenda pamoja na kurejesha Serikalini viwanda vyote vilivyobinafsishwa lakini haviendelezwi ili vitolewe kwa wawekezaji wengine.
Sambamba na hayo Mhe. Mwijage amesema kuwa kufufua viwanda, hasa viwanda vya nguo ni pamoja na wakulima wa pamba kulima zao hilo kwa wingi kwa ajili ya uchakataji pamoja na kudhoofisha uingizaji wa nguo za mitumba nchini.
Wizara hiyo inaendelea na kushawishi wawekezaji mbalimbali ili kujenga viwanda vingi iwezekavyo kwa ajili ya uchakataji wa mazao yanayolimwa nchini pamoja na mifugo.

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam YASHIRIKI MAONESHO YA SABASABA

1 
Mtendaji Mkuu wa Mahakama  Tanzania Bw. Hussein Kattanga akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Bi. Mary Shirima wakati wa maonyesho ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijin Dar es Salaam
3Wanausalama wakiimarisha ulinzi katika viwanja vya sabasaba ili wafanyabiashara na wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa amani.
4Mwanafunzi kutoka chuo cha VETA wa pili kutoka kulia akiwaelekeza baadhi ya wananchi ubunifu wa kutengeneza boti itakayokuwa inatembea barabarani kwa kuendeshwa na dereva mpaka baharini
Picha na Benjamin Sawe

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) LAANZA KUTOA HUDUMA KATIKA MAONESHO YA 40 YA KIMATAIFA ya SABASABA

1 2 
Banda  la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) likiwa katika  Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara, yanayofanyika kila mwaka katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba  jijini Dar es salaam tayari limeanza rasmi kutoa huduma zake katika viwanja hivyo.
3 
Afisa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Bi Edith Nguruwe akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda la (NHC) kuhusina na huduma zinazotolewa na Shirika hilo.
4 
Afisa Mauzo Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Emmanuel Limo (kushoto), akimuelezea Wananchi Kuhusiana na mradi wa SAFARI CITY  uliopo Arusha alipotembelea banda hilo katika maonesho ya Sabasaba.
5 
Afisa biashara (NHC), Clara Lubanga akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa Wananchi aliotembelea banda hilo kuhusiana uzwaji wa nyumba (katikati), Afisa Mauzo wa (NHC), Joseph Haule.
6 
Afisa Mauzo (NHC), Jasson Ipyana akimuelezea mwananchi kuhusina na miradi ya nyumba ya bei nafuu ilioko nchini.
7 
Bw: Klison Sanane (kushoto), akifafanua miradi mbalimbali ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
8 
Aika Swai (kushoto), akielezea kuhusiana na utaratibu wa unaoutumika katika ununuzi wa  nyumba za  (NHC) huku baadhi ya wadau kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakimsikiliza kwa umakini.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG.

Rais Magufuli Awataka wakuu wa Wilaya na mikoa kuchapa kazi.

index 
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli amewataka wakuu wa wilaya na mikoa kuchapa kazi kwa bidii kwani viongozi hao ndio wawakilishi wa wananchi wa vijijini.
Mhe.Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akizungumza wakati wakuu wa wilaya na mikoa walipokuwa Ikulu wakila kiapo cha maadili ya viongozi kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa mikoa yao.
Rais Magufuli pia amewataka viongozi hao kufanya kazi na kutimiza majukumu yao kwani wananchi wana changamoto nyingi,na wao waende kutatua matatizo ya wananchi walio maskini.
Aidha amewataka viongozi hao kutokuwa chanzo cha kutengeneza matatizo katika jamii na hivyo wasimamie haki na ukweli,wasiwe wala rushwa,wazingatie maadili na kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi za vyama zao,dini au kabila uku akiwataka kutekeleza waliyohaidi kwenye ilani ya chama cha mapinduzi.
Pia amewataka viongozi hao kuweke mkazo katika kutatua kero za wananchi na kuwataka kutimiza kwa vitendo kwa kushirikiana na viongozi watakaowakuta katika maeneo yao waliyopangiwa.
Hata hivyo amewataka viongozi hao kusimamia mapato ya Serikali katika miradi yote kwenye maeneo yao ili kuhakikisha serikali inapata kodi ambayo itasaidia katika maendeleo ya Taifa hili.

Makamu wa Rais awataka wakuu wa wilaya na mikoa kukamilisha zoezi la madawati kabla ya June 30.

index
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu amewataka wakuu wa wilaya na mikoa kuhakikisha wanamaliza zoezi la upatikanaji wa madawati kwa shule za msingi na sekondari.
Mhe. Suluhu ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati wakuu wa wilaya na mikoa walipokuwa Ikulu wakila kiapo cha maadili ya viongozi kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa mikoa yao.
Aidha amewaagiza viongozi hao kusoma alama za nyakati kwa kuangalia makosa ya waliokuwepo kabla yao ili kuhakikisha hawarudii makosa yaleyale.
Mhe.Suluhu pia amesema kuwa Serikali haitaki kusikia wananchi wanalia njaa na hivyo wakuu wa wilaya wahakikishe chakula kinapatikana katika maeneo yao kwani hilo ni jukumu lao.
Aliongeza kuwa wakuu wa wilaya wana majukumu makubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za muhimu katika maeneo yao kwani wananchi wana mategemeo makubwa juu yao.
Aidha ameagiza wakuu wa Wilaya hao kufanya kazi karibu na Maafisa Tarafa ili kujua kero za wananchi na kuzifanyia kazi kwa kasi ili wananchi wafaidike na maendeleo yawafikie kwa haraka.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene  ivi karibuni aliwaagiza wakua wa wilaya na mikoa kuhakikisha wanatimiza agizo la Rais John Pombe Magufuli kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakayekaa chini kwa uhaba wa madawati kufikia June 30,2016.

Waziri Mkuu ahagiza wakuu wa Wilaya na Mikoa kutembelea Vijijini ili kujua matatizo ya wananchi.

index 
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameagiza wakuu wa wilaya na mikoa kufanya ziara katika maeneo yao hasa vijijini ili kujua matatizo ya wananchi wao kwa ukaribu na kuyapatia ufumbuzi.
Mhe.Majaliwa ameyasema hayo leo hii Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wakuu wa wilaya na mikoa walipokuwa Ikulu wakila kiapo cha maadili ya viongozi kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa mikoa yao.
Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa  wakuu wa mikoa na wilaya waache kukaa maofisini mwao badala yake watembelee wananchi na hasa wale wa hali ya chini ili kujua matatizo yao ya Ardhi na kupatia ufumbuzi migogoro ya wafugaji na wakulima.
Pia Mhe.Majaliwa amewasisitiza wakuu hao kutambua kwamba majukumu waliyonayo ni makubwa na wananchi wana mategemeo makubwa juu yao na hivyo ni  budi wakatekeleza wajibu wao na kuhakikisha watanzania wanapata huduma zote za muhimu kwa kutumia elimu, uwezo, uadilifu, uaminifu na uwajibikaji walionao ili kufanikisha maendeleo kwa wananchi.
Aliongeza kuwa wakuu hao wana jukumu kubwa la kusimamia pesa za serikali pesa za miradi zinakokwenda katika halmashauri za wilaya zao na kukazia kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa yeyote ambaye hatofanya kazi zake kikamilifu.
Waziri mkuu amewaagiza wakuu wa Mikoa kushirikiana kwa karibu na wakuu wa Wilaya ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya maeneo yao kwani wananchi wana kiu ya maendeleo katika maeneo yao.

No comments:

Post a Comment