Mkuu
wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw.
James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sababu za ushiriki
wa Mfuko katika maonyesho ya biashara ya kimataifa (Saba Saba 2016).
Afisa
Mifumo ya kompyuta kutoka Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Yohana Nyabili
akitoa maelezo kwa mwanachama wa Mfuko pamoja na kumpatia taarifa ya
michango yake mara baada ya mwanachama huyo kutembelea banda ya Mfuko
kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa (Saba Saba 2016).
Mgeni
rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi
akifungua kongamano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ofisi
za ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki na wadau wengine katika
kongamano hilo.
Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak akizungumza kwenye kongamano hilo.
Pichani
juu na chini ni sehemu ya washiriki kutoka sekta binafsi, serikalini
pamoja na taasisi mbalimbali walioshiriki kwenye kongamano hilo.
KONGAMANO LA KUBADILISHANA UZOEFU WA MAFUNZO YA TAALUMA UFARANSA NA TANZANIA LAFANYIKA DAR
KONGAMANO
kubwa la aina yake limefanyika mjini Dar es salaam ambapo washiriki
walizungumzia namna ya kuendeleza rasilimali watu katika eneo la
utaalamu na taaluma katika shughuli mbalimbali za uendelezaji wa
makampuni na viwanda.
Kongamano hilo ambalo lilihudhuria na watu wenye kariba kubwa katika masuala ya viwanda na biashara akiwemo Dkt. Reginald Mengi ambaye ni Mwenyekiti wa makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF);na Balozi wa Ufaransa nchini Malika Berak liliangalia uhaba wa wataalamu na namna ya kuuondoa uhaba huo wakati taifa linaelekea katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda.
Wengine waliokuwepo katika kongamano hilo Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero na maofisa wa serikali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akikaribisha washiriki na wadau wengine alisema kwamba mafunzo hayo yaliyoratibiwa kwa pamoja katika wataalamu wa Ufaransa, ESRF na Benki ya Maendeleo ya Afrika yamelenga kudadavua tatizo lililopo na kulipatia ufumbuzi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida (katikati) akisalimiana na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya
Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi (kulia) alipowasili katika
ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Ufaransa
nchini, Mh. Malika Berak.
Kongamano hilo ambalo lilihudhuria na watu wenye kariba kubwa katika masuala ya viwanda na biashara akiwemo Dkt. Reginald Mengi ambaye ni Mwenyekiti wa makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF);na Balozi wa Ufaransa nchini Malika Berak liliangalia uhaba wa wataalamu na namna ya kuuondoa uhaba huo wakati taifa linaelekea katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda.
Wengine waliokuwepo katika kongamano hilo Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero na maofisa wa serikali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akikaribisha washiriki na wadau wengine alisema kwamba mafunzo hayo yaliyoratibiwa kwa pamoja katika wataalamu wa Ufaransa, ESRF na Benki ya Maendeleo ya Afrika yamelenga kudadavua tatizo lililopo na kulipatia ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment