Balozi
wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke akiongea na waandishi wa habari na
Wadau wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) hawapo
pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho
ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto ,
Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando akiongea na waandishi wa habari
na Wadau wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH)
hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika
Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Balozi
wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke kulia akikata utepe kuashilia kuanza
rasmi kwa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni
10 mwaka huu jijini Dar es salaam na wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa
Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto ,
Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando.
Mshauri
wa ufundi kutoka Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH)
Dkt. Baltazar Ngoli wa kwanza kulia akitoa maelekezo ya picha kwa
Balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke wa pili kulia pamoja na
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia
na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando wa tatu kulia
wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya
Taifa jijini Dar es salaam.
Wadau
mbalimbali wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH)
wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya
Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt.
Margaret Mbando hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha
yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es
salaam.
Picha zote na Ally Daud-Maelezo
……………………………………………………………………………………………………………………..
Na Ally Daud- maelezo
Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama vinazidi kupungua kutoka siku hadi siku katika kufikia malengo ya milenia .
Akizungumza hayo katika hafla
fupi ya kuzindua maonesho ya picha Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya
Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt.
Margaret Mbando amesema kuwa Tanzania imepiga hatua katika kufikia
malengo ya milenia kwa kupunguza Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na
wakina mama.
“Tumefanikiwa kupunguza Idadi ya
vifo kwa watoto wachanga na wakina mama ili kufikia malengo ya milenia
kwa upande wa afya kupitia mfumo wa kujiunga na bima ya afya kwa jamii”
alisema Dkt. Mbando.
Mbali na hayo Dkt Mbando amesema
kuwa amewakaribisha wananchi wote hususani wakazi wa Dar es salaam
kuudhuria maonesho hayo yaliyofunguliwa leo yenye kauli mbiu ya “Huduma
Bora kwa Afya Bora”yatayofikia kilele mpaka Juni 10 mwaka huu ili kupata
ujumbe zaidi kupitia picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini.
Aidha ameipongeza Serikali ya
Ujerumani kupitia ubalozi wake kwa kushirikiana vizuri na Serikali ya
Tanzania na kukubaliana kupata msaada wa Euro milioni 47 kwa muda wa
miaka mitatu ijayo katika kuinua sekta ya Afya.
Kwa upande wa balozi wa Ujerumani
Mhe. Egon Kochanke amesema kuwa mchango wa Serikali ya ujerumani kwa
sekta ya afya Tanzania utaendelea kuwa sehemu ya mpango wa ushirikiano
wa nchi mbili ili kuinua sekta hiyo nchini.
BUNGE LAENDELEA NA KIKAO CHAKE MJINI DODOMA LEO
Baadhi
ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakitoka nje ya
ukumbi wa Bunge mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha
maswali na majibu na uchangiaji wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya
Wizara Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi leo mjini Dodoma.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter
Mavunde ambaye akiwasalimia kwa furaha wanafunzi wa Chuo cha Ufundi
Stadi (VETA) Dodoma leo kwenye viwanja vya Bunge.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter
Mavunde akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi -VETA mkoa wa Dodoma
nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju (katikati) akizungumza na viongozi
wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) waliolitembelea
Bunge mjini Dodoma.
akiwasisitiza
jambo viongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU)
alipokutana nao nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
Waziri
wa Elimu,Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako (kushoto)
akimweleza jambo Rais wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
(MoCU) Bw. Frank Nkya (kulia) nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma
Waziri wa Elimu,Sayansi
na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako (kulia)akijadiliana jambo
na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe.
Angella Kairuki (kushoto) nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi wa Chuo cha Ufundi -VETA mkoa wa Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.PICHA/Aron Msigwa-MAELEZO.
wanafunzi wa Chuo cha Ufundi -VETA mkoa wa Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.PICHA/Aron Msigwa-MAELEZO.
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Mwanza Alhaji Ferej awaongoza waaumini wa dini ya kiisilamu katika dua yakuwaombea waliowawa katika msikiti wa R Rahman Ibanda.
Mohamed
Taqi Khan (20) raia wa Jamhuri ya Watu wa Iran akionyesha uwezo na
kipaji chake cha kuhifadhi Quraan tukufu katika uwanja wa shule ya
Msingi Mbugani katika Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza.Ana uwezo wa
kutumia njia 52 kuelezea Quraan.Waliomshikia vinasa sauti (Microphone)
kulia ni Sheikh Ramadhan Hashimu na kushoto ni Mohamed Naqi Taqi.
Mohamed
Naqi Khan (20) akionyesha kipaji na uwezo wake wa kuelezea Quraan
ambayo ameihifadhi kichwani akiwa na umri wa miaka 10, miaka saba baada
ya wazazi wake kufariki dunia na antumia njia 52 kuelezea Quraan hiyo.
Hapa akionyesha kipaji chake hicho kwenye uwanja wa Shule ya Msingi
Mbugani Jijini Mwanza na kutokana na kipaji chake hicho amekuwa kivutio
kwa maelfu ya waumini wa dini ya Kiislamu akiwa ameendesha vipindi zaidi
2000 katika nchi za Kiislamu katika miji mbalimbali.
KATIBU
wa Bakwata wa Mkoa wa Mwanza Mohamed Salum Balla akizungumza baada ya
dua maalumu ya kuwaombea waumini wa dini ya kiislamu waliouawa wakiswali
katika msikiti wa R Rahman Ibanda Relini.Dua hiyo ilisomwa katika
Uwanja wa shule ya Msingi Mbugani jijini Mwanza juzi na kuhudhuriwa na
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Alhaji Salum Ferej wa pili kulia kwa
Balla wa pili ni Sheikh Hassan Kabeke ambaye ni Mwenyekiti mwenza wa
Amani na wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa wa Bodi ya wadhamini ya
TIC Dk. Mohamed Kanju .
Katibu
wa Bakwata wa Mkoa wa Mwanza Mohamed Salum Balla akizungumza baada ya
dua maalumu ya kuwaombea waumini wa dini ya kiislamu waliouawa wakiswali
katika msikiti wa R Rahman Ibanda Relini.Dua hiyo ilisomwa katika
Uwanja wa shule ya Msingi Mbugani jijini Mwanza juzi na kuhudhuriwa na
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Alhaji Salum Ferej wa pili kulia kwa
Balla wa pili ni Sheikh Hassan Kabeke ambaye ni Mwenyekiti mwenza wa
Amani na wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa wa Bodi ya wadhamini ya
TIC Dk. Mohamed Kanju ,Alhaji Sibtain Meghjee ambaye ni Mwenyekiti wa
Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania, wa kwanza kulia.
Picha zote na Baltazar Mashaka
Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi wanakuwa na miundombinu iliyobora-Profesa Mbarawa
Na Betrice Lyimo-MAELEZO
…………………………………
Serikali kwa kushirikiana na
Kampuni ya Mabey Bridge ya nchini Uingereza wamejipanga kikamilifu
kujenga barabara tatu za juu (Fly Overs) na barabara nne za
watembea kwa lengo la kupunguza msongamano wa foleni jijini Dar es
Salaam.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati wa
mazungumzo hayo na kampuni ya Mabey Bridge ya Uingereza kwa ajili
ya ujenzi wa barabara hizo nchini.
Profesa Mbarawa alisema kuwa
barabara hizo zitajengwa hasa maeneo ambayo yana msongamano mkubwa
wa magari ikiwa ni pamoja na eneo la barabara ya Mwenge.
“Serikali imejipanga kikamilifu
kuhakikisha wananchi wanakuwa na miundombinu iliyobora hasa katika
upande wa barabara za magari na barabara za waenda kwa miguu ili
kuwarahisishia wananchi kuwahi kuwajibika katika maeneo yao ya kazi”.
Mbali na hayo, Waziri Mbarawa
alifanya ziara ya kushtukiza katika Daraja la Nyerere lililopo maeneo
ya Kigamboni kwa lengo la kutaka kujua maendeleo ya daraja hilo na
kumtaka msimamizi wa daraja hilo kuandaa kadi maalumu au
kitambulisho zitakazotumika kwa lengo la kupunguza msongamano wakati
wa kulipia tozo.
vilevile Waziri
aliwataka wananchi kuwa waangalifu na miundombinu ya daraja hilo
na endapo kuna mtu atakaye bainika kuharibu atachukuliwa hatua
kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kulipa faini za gharama ya juu.
“kuanzia sasa kunatakiwa kuwepo
na faini kali kwa mtu yeyote atakaye haribu miundombinu ya daraja
hili kwa lengo la kulifanya daraja lidumi kwa muda mrefu” alisisitiza
Waziri Mbarawa
Kwa upande wake Msimamizi
Mkuu wa daraja la Nyerere, Gerald Sondo alisema wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ya madereva wa daladala kushindwa kutumia
daraja hilo na kudai kuwa tozo ni kubwa.
Vilevile Waziri huyo alifanya
ziara katika eneo la ujenzi wa mtambo wa Mafuta kutoka kwenye meli
kabla ya kuingia kwenye matanki (Flow Meter) kuona maendeleo ya
ukarabati wa mtambo hio uliyoharibika hivi karibuni kutokana na mvua
kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kumtaka mkandarasi
kuhakikisha eneo hilo linazungishiwa ukuta ili kuziba mitambo
hiyo.
Klabu ya Mwalimu Nyerere yazinduliwa jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
wa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezi Bi
Liliani Beleko akiongea na wanafunzi wa shule ya Msingi ya Mwalimu
Nyerere Magomeni wakati wa uzinduzi wa klabu ya Mwalimu Nyerere chini
ya Taasisi ya Ariseamka Afrika leo jijini Dar es Salaam,kulia kwake ni
Msaidizi Maalum wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Bw. Gallus
Abedi na kulia ni Mwanzilishi wa Taasisi ya Ariseamka Afrika Bi.Kulthum
Maabad.
Msaidizi
Maalum wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Bw. Gallus Abedi
akionyesha moja ya kitabu ambacho kiliandikikwa na Baba wa Taifa Mwalimu
Nyerere wakati wa sherehe za uzinduzi wa klabu ya Mwalimu Nyerere chini
ya Taasisi ya Ariseamka Afrika itakayokuwa ikiwafundisha wanafunzi
historia ya viongozi mbalimbali wa Afrika,lugha,uongozi na sanaa,kulia
ni Afisa Elimu Vifaa naTakwimu Manispaa ya Kinondoni Bi. Sion Nnko na
kushoto ni Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezi Bi Liliani Beleko
Mwanzilishi
wa Taasisi ya Ariseamka Afrika Bi.Kulthum Maabad akionyesha kipeperushi
chenye taarifa za wapigania uhuru wa Afrika katika sherehe za uzinduzi
wa klabu ya Mwalimu Nyerere chini ya Taasisi ya Ariseamka Afrika
itakayokuwa ikiwafundisha wanafunzi historia ya viongozi mbalimbali wa
Afrika,lugha,uongozi na sanaa katika kilele cha kuazimisha wiki ya
ukombozi wa Afrika leo jijini Dar es Salaam,kushoto kwake ni Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi ya Mwalimu Nyerere Magomeni Bw.Odas Bambaza.
Afisa
Elimu, Vifaa na Takwimu Manispaa ya Kinondoni Bi. Sion Nnko akiongea na
wanafunzi wa shule ya Msingi Mwalimu Nyerere ya magomeni
(hawapokatikapicha) wakati wa sherehe za uzinduzi wa klabu ya Mwalimu
Nyerere chini ya Taasisi ya Ariseamka Afrika itakayokuwa ikiwafundisha
wanafunzi historia ya viongozi mbalimbali wa Afrika,lugha,uongozi na
sanaa ,katika kilele cha kuazimisha wiki ya ukombozi wa Afrika leo
jijini Dar es Salaam ,wa kwanza kushoto ni Msaidizi Maalum wa
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Bw. Gallus Abedi na Mkurugenzi
wa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezi Bi
Liliani Beleko.
Msaidizi
Maalum wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Bw. Gallus Abedi
(kushoto) akikabidhi vitabu kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya
Mwalimu Nyerere Magomeni Bw.Odas Bambaza,kwa ajili ya wanafunzi
kujisomea na kuijua kiundani historia ya nchi katika sherehe za uzinduzi
wa ya klabu Mwalimu Nyerere chini ya Taasisi ya Ariseamka Afrika
itakayokuwa ikiwafundisha wanafunzi historia ya viongozi mbalimbali wa
Afrika,lugha,uongozi na sanaa ,katika kilele cha kuazimisha wiki ya
ukombozi wa Afrika leo jijini Dar es Salaam,katika ni Afisa Elimu,
Vifaa na Takwimu Manispaa ya Kinondoni Bi. Sion Nnko
Mkurugenzi
wa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezi Bi
Liliani Beleko(wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na
wageni waalikwa wakati wa sherehe za uzinduzi wa klabu ya Mwalimu
Nyerere chini ya Taasisi ya Ariseamka Afrika itakayokuwa ikiwafundisha
wanafunzi historia ya viongozi mbalimbali wa Afrika,lugha,uongozi na
sanaa ,katika kilele cha kuazimisha wiki ya ukombozi wa Afrika leo
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezi Bi
Liliani Beleko(katikati) ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwa katika picha
ya pamoja na wageni waalikwa wakati wa sherehe za uzinduzi wa klabu ya
Mwalimu Nyerere chini ya Taasisi ya Ariseamka Afrika itakayokuwa
ikiwafundisha wanafunzi historia ya viongozi mbalimbali wa
Afrika,lugha,uongozi na sanaa ,katika kilele cha kuazimisha wiki ya
ukombozi wa Afrika leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Lorietha
Laurence-WHUSM)
SERIKALI YANUNUA VIFAA VYA KUPIMA UBORA WA MAJENGO BILA KUYAHARIBU
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw. Elius Mwakalinga akitoa
ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu kutekelezwa kwa mpango wa
Serikali wa kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanapata makazi bora
ambapo wakala huo unajenga nyumba 10,000 ili kutimiza azma hiyo. Kulia
ni Mkurugenzi wa Milki Bw. Baltazar Kimangano na kushoto ni Mkurugenzi
wa Ushauri Bw. Edwin Nnunduma.
Mhandisi
Ujenzi kitengo cha Upimaji na Ukaguzi Majengo toka Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) wakwanza kulia Bi Khadija Salum akionesha kwa waandishi
wa Habari sehemu ya vifaa vilivyonunuliwa na wakala huo kwa ajili ya
kupima ubora wa majengo yaliyokwisha jengwa na yale yanayoendelea
kujengwa ili kuhakikisha kuwa Serikali inakuwa na majengo yenye ubora
kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa.
( Picha na Habari na Frank Mvungi ).
………………………………………………………………………………………………….
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali kupitia wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) imenunua vifaa vya kupima Ubora wa Majengo bila
kuyaharibu (Non destructive Testing equipments) .
Hayo yamesemwa Leo Jijini Dar es
salaam na Mtendaji Mkuu waTBA Bw. Elius Mwakalinga wakati wa mkutano na
vyombo vya Habari uliolenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa na wakala huo.
Akifafanua Mwakalinga amesema kuwa
wakala huo umenunua vifaa vya kisasa ili kuwezesha ukaguzi wa ubora wa
Majengo ya Serikali ili kuwa na majengo yenye Ubora unaotakiwa.
“Lengo la kununua vifaa hivi ni
kuhakikisha kuwa majengo yote ya Serikali yanakuwa na ubora kwa kuwa
tutayapima yaliyopo na yale yanayojengwa ili tuweze kuchukua hatua pale
inapodi” alisisitiza Mwakalinga.
Akieleza umuhimu wa vifaa hivyo
Mwakalinga amesema kuwa hakutakuwa na wasiwasi tena kuhusu uwezekano wa
wakandarasi kudanganya wakati wa ujenzi.
Aidha vifaa hivyo vitawezesha
Wakala kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika majengo ya Serikali ili
kubaini hali ya ubora wa majengo hayo ambapo gharama ndogo za ada ya
ushauri zitatozwa kwa Taasisi husika.
Vifaa hivi ni kama Rebund hammer
inayotumika kupima uimara wa zege iliyokauka, cover meter kwa ajili ya
kupima ukubwa wa nondo na umbali uliowekwa.
Akitaja vifaa vingine Mwakalinga
amesema kuwa ni “Utrasonic system/testing device” kwa ajili ya kupima
muonekano wa ndani ya zege iliyokauka.
Mbali ya jukumu la kuhakiki ubora
wa majengo ya Serikali, Wakala umeendelea na mpango wa ujenzi wa nyumba
zinazouzwa kwa gharama nafuu kwa watumishi wa umma ambapo mpango wa
wakala huo ni kujenga nyumba elfu kumi katika maeneo mbalimbali hapa
nchini.
Waziri Profesa Makame Atembelea daraja la Nyerere na Kituo cha kupimia mafuta yaingiayo nchini kuona Maendeleo
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa akiongea na wawakilishi wa kampuni ya Mabey
Bridge kutoka Marekani(hawapo pichani) na wadau wengine wa Ujenzi leo
kuhusu mpango wa kujenga fly overs takribani tatu katika jiji la Dar es
salaamu kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji.
Katibu mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi)
Eng. Joseph Nyamhanga akifafanua jambo kuhusu mpango wa ujenzi wa
kujenga fly overs katika jiji la Dar es salaamu kwa lengo la kupunguza
msongamano wa magari katika jiji hilo kushoto ni muakilishi kutoka
Kampuni ya Kimarekani ya Mabey Bridge Bw. Darren Keep na kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
Msimamizi Mkuu wa Daraja la Nyerere Bw. Gerald Sondo akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo ya Daraja pamoja na changamoto
wanazozikabili, katika Ziara ya kushtukiza iliyofanya na Waziri huyo leo
jijini Dar es salaamu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Fundi mitambo Bw.
Simon Dotto kuhusu maendeleo ya ukarabati wa mtambo wa kupima mafuta
kutoka kwenye meli kabla ya kuingia kwenye matanki ambao uliharibika
hivi karibu kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wahudumu wa
kivuko cha Mv Magogoni kuhusu utaratibu wa ukatishaji tiketi katika
kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo na changamoto mbalimbali kutoka
kwa abiria wanaotumia kivuko cha Mv Magogoni leo jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Beatrice Lyimo)
ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE MNARA WA SIMU JIJINI MWANZA.
Kijana Mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya
kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.
Na BMG
kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.
Na BMG
Tukio
hilo limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia
kijana huo ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na
kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana.
Mashuhuda
wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema
huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha
ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na
kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa
akiyatumia.
Akizungumza
kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza,
mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, amsetoa rai kwa makampuni
yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa
hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema.
Baadhi
ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana
huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu “rukaa,
ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume” hali ambayo ilikuwa
ikimuongezea morari kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati
ya mnara huo.
Baada
ya kijana huyo kujirusha kutoka katikati ya mnara hadi chini, alipoteza
fahamu na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza,
Sekour Toure kwa ajili ya huduma ya kwanza.
CHUMBA CHA DEREVA TAX CHAZUA KIZAA ZAA MTAA WA MBEZI MTONI GOLD STAR, DAR
Wananchi na mwenye nyumba wakifungua mlango
Chupa zinazodaiwa kuwa na mikojo zikiwa zimetapakaa ndani ya chumba hicho.
Huyu Ndiye Dereva wa Tax Nyati anayedaiwa kumiliki chumba hicho.
………………………………………………………………………………………………………..
Na Ripota wa Sufianimafoto Blog,Dar
UKIHADITHIWA na kuonyeshwa chumba
cha Dereva Tax anayeonekana kitaani na katika kazi zake akiwa amepiga
pamba wala hutaamini masikio yako wala macho yako pindi utakapopata
bahati ya kufika na kushuhudia chumba hicho kilichopo maeneo ya Gold
Star Mtaa wa Mbezi Mtoni Bondeni jijini Dar es Salaam.
Mtandao huu ulipata fursa ya
kufika na kushuhudia yale yaliyokuwa yakisemwa na baadhi ya wakazi wa
mtaa huo jana majira ya saa tano usiku baada ya kutokea mtafaruku na
sintofahamu katika nyumba hiyo ya Mama Mwakajinga, anayoishi Dereva huyo
aliyejulikana kwa jina la Steven al-maarufu kama ‘NYATI’.
Akizungumza na mtandao huu wa
Sufianimafoto, Mama mwenye nyumba kuhusu tukio hilo, alisema kuwa siku
ya Mei 23, akiwa ameketi uwanji karibu kabisa na Chumba cha Jamaa huyo
huku akichambua mboga, alihisi harufu kali na mbaya iliyokuwa ikivuma
kutoka chumbani kwa Dereva huyo aliyepanga katika nyumba yake tangu
mwaka 2008 na kuona wadudu aina ya funza wakitoka chumba hicho kupitia
chini ya mlango.
Kesho yake Mei 24 Baada ya kuona
wadudu hao huku harufu ikizidi kuwa kali, alimuita jirani yake na
kumshirikisha jambo hilo huku wote wakishikwa na butwaa na kuwa na
mashaka na chumba hicho.
Mei 25 Mama mwenye nyumba aliamua
kwenda kwa Mjumbe wa eneo hilo Badili Makoye, kutoa taarifa juu ya
wasiwasi uliotanda katika nyumba hiyo na kuongozana na Viongozi wengine,
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Frank Kyaruzi, Wajumbe wengine
Abdalla Mlaliya na Matrida Paston, waliofika na kujionea hali halisi ya
chumba hicho.
Baada ya viongozi hao kufika
eneola tukio walimuamuru Mama mwenye nyumba kwenda kutoa taarifa kituo
cha Polisi. Mama huyo alitekeleza agizo na kwenda kuripoti Kituo cha
Mbezi Garden na kuongozana na Mkuu wa Kituo hicho na baadhi ya askari
hadi nyumbani na kukuta hali hiyo ya sintofahamu.
Walipofika eneo la tukio na
kushuhudia hali hiyo, Mkuu wa Kituo aliamuru mlango huo uvunjwe huku
wanachi na Viongozi wa Mtaa huo wakishuhudia na kuingia ndani ambako
walikuta Chumba kizima kikiwa kimejaa Chupa za Plastiki zilizojaa
mikojo, Mifuko ya Rambo ikiwa na Vinyesi, Feni moja iliyochomekwa kwenye
Soketi ya Umeme ukutani, Pakiti nyingi tupu za Sigara aina ya Embassy
na Kondomu zilizotumika na zisizotumika.
Baada ya zoezi hilo, Mwenyenyumba
alimpigia simu mpangaji wake na kumtaka kurejea nyumbani, lakini Dereva
huyo alijibu kuwa kwa muda huo alikuwa mbali maeneo ya Kunduchi na
kuahidi kuwagongea usiku pindi atakaporejea.
Hadi Mtandao huu unaondoka eneo
la tukio majira ya saa tano usiku bado wakazi wa maeneo hayo walikuwa
wamejazana nje ya Chumba hicho wakiendelea kumsubiri arudi ili kupata
ukweli kuhusu mambo waliyoyaona katika chumba chake.
Aidha Mama mwenye nyumba
aliuambia mtandao huu kuwa mpangaji wake huyo, tangu alipohamia katika
nyumba hiyo mwaka 2008, hakuwahi kumuona akiingia na mwanamke katika
chumba hicho, wala kumuona mgeni wa aina yeyote kwa Dereva huyo,jambo
lililomshangaza kukuta Kondom zilizotumika katika chumba hicho. Ama
kweli ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Filauun.
Hadi leo hii Mei 27, mtandao huu
umeshindwa kumpata dereva huyo baada ya kutompata hewani simu yake ikiwa
imezimwa tangu kutokea kwa tukio hilo.
Leo hii Mei 27, Mama mwenye
nyumba ameripoti kuwa mpangaji wake huyo,hajatokea nyumbani hapo tangu
kutokea kwa tukio hilo ambapo leo, amechukua uamuzi wakuwalipa vijana wa
mtaa huo ili wasafishe chumba hicho.
Tayari tumewalipa pesa vijana kiasi cha sh.200,000/= ili wafanya usafi na wameshamaliza na kwenda kufukia bonde la mto Mbezi.
WAZIRI MKUU AKAGUA UTENDAJI KAZI MABASI YA DART
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa
akiwaangalia Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa na Mzee David
Mwaibula walippkuwa wakisalimiana akiwa njiani kutoka Feri kwenda Kimara
katika usafiri wa mabasi ya Mwendokasi leo.
…………………………………………………………………………………………………………………
*Ataka watu walipe tiketi rasmi, wafuate taratibu
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amekagua utendaji kazi kwenye mabasi ya mwendokasi yanayotoa huduma
katika Jiji la Dar es Salaam na kubaini changamoto kadhaa ambazo amesema
zitarekebishwa kadri mradi unavyoendelea.
Waziri Mkuu ambaye alilipa nauli
na kupanda basi namba 23 lenye usajili namba T125 DGW kuanzia kituo cha
Ferry, Kivukoni, ametumia muda wa dakika 50 kufika Kimara mwisho kwa
kutumia usafiri huo.
Waziri Mkuu alipanda basi hilo
saa 3:30 asubuhi na lilianza safari saa 3:33 baada ya kusubiri wengine
wapande. Kwa wastani ililtumia kati ya dakika mbili hadi tatu kutoka
kituo kimoja hadi kingine. Basi hilo liliwasili Kimara Mwisho saa 4:23
asubuhi.
Akizungumza na waandishi wa
habari akiwa Kimara mwisho mara baada ya kumaliza ziara hiyo fupi ya
ukaguzi leo (Ijumaa, Mei 27, 2016), Waziri Mkuu alisema aliamua kufanya
ziara hiyo ya ghafla ili kuangalia matumizi ya njia za mabasi yakoje na
pia kuona abiria wanaelewa vizuri namna ya kuitumia huduma hiyo.
Amesema ameridhishwa na mradi
unavyofanya kazi ila ameelezwa kuna usumbufu kwenye mageti wakati abiria
wanapotaka kuthibitisha tiketi zao hasa wakati wa asubuhi kunapokuwa na
msongamano wa abiria. Pia alielezwa kwamba kuna baadhi ya abiria
wanakuja na tiketi za jana yake jambo ambalo linaleta usumbufu kwa
sababu hazitambuliki kwenye mfumo wao.
Kibiti kufanya kongamano la kuipokea Wilaya mpya kwa kushiriki shughuli mbalimbali za Maendeleo.
Na Daudi Manongi-MAELEZO
Viongozi wa umoja na wadau wa
maendeleo wilaya mpya ya kibiti (UWAWAMAKI) mkoani Pwani umepanga
kufanya kongamano la kuunga mkono tamko la Serikali ya awamu ya Tano ya
Mhe.John Pombe Magufuli kwa kuifanya Kibiti kuwa Miongoni mwa Wilaya
mpya siku ya jumapili tarehe 29 saa nne asubuhi kwenye ukumbi wa Shule
ya Sekondari TEDEO Temeke jijini Dar es Salaam.
Akiongea na waandishi wa Habari
leo jijini Dar es Salaam Katibu wa umoja huo Bw.Selemani Ndumbogani
amesema kuwa wanakibiti wamefarijika sana na kauli ya Serikali ya
Kuipatia Kibiti wilaya jambo ambalo lilikuwa kilio cha muda mrefu ikiwa
ni takribani zaidi ya miaka arobaini tangu uhuru na kuongezea kuwa
walikuwa mbali sana na huduma muhimu za Serikali.
Pia umoja huo umeomba wana jimbo
la kibiti hususani Rufiji kujitokeza kwa wingi kwenye kongamano hilo ili
liwe lenye mafanikio makubwa.
Miongoni mwa mambo yaliyoandaliwa
kufanywa ni pamoja na usafishaji wa mitaa,soko, maeneo ya standi ,eneo
litakalojengwa wilaya,na kuendesha dua kwa madhehebu mbalimbali ya dini
ili kuiombea kheri wilaya ya kibiti,Pia kuiombea nchi na Rais wetu wa
Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli na
Mhe.Kassim Majaliwa kuishi kwa amani na usalama katika kusimamia
shughuli za Taifa.
Mwaka huu mwezi Februari Rais wa
awamu ya tano Dr.John Pombe magufuli alitangaza kuipandisha adhi wilaya
hiyo mpya ya kibiti ambapo kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano
wa Tanzania ya mwaka 1977 imempa mamlaka rais ya kugawa nchi kwa kadri
ambavyo atakavyoona inafaa.
RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA NNE DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia
jambo wakati akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya
Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete wakifurahia
jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete wakifurahia
jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Picha na IKULU
NECTA SASA KUFUNGA MITIHANI KWA KUTUMIA MASHINE.
Na Fatma Salum-MAELEZO, Dodoma.
Baraza la Mitihani la Tanzania
(NECTA) limejipanga kuanza kufunga bahasha zenye karatasi za mitihani
kwa kutumia mashine maalum ili kuondokana na hatari ya kuvuja kwa
mitihani hiyo na gharama za ufungaji wa mitihani kwa kutumia mikono.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako wakati
akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara yake kwa mwaka
2016/2017, jana Bungeni Mjini Dodoma.
Prof. Ndalichako alisema kuwa
katika kuimarisha utendaji kazi wake NECTA itanunua mashine mbili za
kufunga mitihani (Auto Poly Wrapping and Packing Machine) ili kuimarisha
usalama wa mitihani kwa kupunguza watu wanaoshiriki kwenye maandalizi
ya mitihani hiyo.
“Katika mwaka 2016/2017 Baraza
litasimika mashine mbili za kufunga bahasha za mitihani hivyo kuondoa
hatari zinazoweza kujitokeza kwa kuwa idadi ya watu wanaofanya kazi hiyo
itapungua.” alisema Prof. Ndalichako.
Aidha, Prof. Ndalichako aliongeza
kuwa Baraza litaboresha mfumo wake wa ukusanyaji na uchakati takwimu na
kuweka Mfumo wa Kielektroniki wa kumtambua mwanafunzi kwa namba maalum
tangu anapoandikishwa shuleni hadi atakapomaliza mzunguko wa masomo
yake.
Alisema kuwa mfumo huo wa
utambuzi utaunganishwa nchi nzima ili kuwezesha kufuatilia maendeleo ya
mwanafunzi kwenye shule yoyote atakayoenda kusoma ndani ya nchi kwa kuwa
namba hiyo atakayopewa na Baraza ataitumia hata kwenye shule nyingine
atakazohamia.
“Wizara itaweka Mfumo wa
Kielektroniki wa ukusanyaji taarifa za wanafunzi chini ya Baraza la
Mitihani ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa hizo wakati wa mitihani
na utaratibu huu utapunguza matumizi makubwa ya fedha kupitia mfumo wa
TSM9.” alisema Prof. Ndalichako.
Pia alieleza kuwa katika
kufanikisha Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), mwaka wa fedha
uliopita Mamlaka ya Elimu Tanzania imechapisha vitabu 558,720 vya jinsi
ya kujibu mitihani ya Kidato cha Pili na Kidato cha Nne ili kuwawezesha
wanafunzi watahiniwa kujibu maswali vizuri katika mitihani yao hatimaye
kuongeza ufaulu.
RC aitaka NHIF kuwa wabunifu ili kuongeza wanachama
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Saidi
Meck Sadik ametoa rai kwa watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) kubuni mbinu mpya za kuwahudumia wanachama wao ili kuhamasisha
watanzania wengi kujiunga na mfuko huo.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa
Wilaya wa Siha Dkt. Charles Mlingwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa alipokuwa
akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa mfuko huo uliofanyika
Mkoani humo.
Mhe. Meck Sadik amesema kuwa
Baraza la wafanyakazi ndiyo chombo sahihi cha uwakilishi wa sauti za
watumishi katika kupanga malengo ya Taasisi pia ni chombo cha kutatua
migogoro ya kikazi na hivyo kumaliza mapema tofauti zinazojitokeza
katika sehemu za kazi kabla hazijaathiri utendaji.
“Kutokana na umuhimu wa huduma
zenu kwa umma, Baraza la Wafanyakazi la Mfuko wenu linatakiwa lichukue
sura mpya na kuwa ni mahali pa ubunifu na kisima cha kuibua mbinu mpya
za kuwahudumia vizuri wanachama wenu na kujua namna gani mtaendelea
kuwavutia Watanzania wengi zaidi kujiunga na Mfuko”,alisema Meck Sadik.
Mhe. Meck Sadik ameongeza kuwa
anawapongeza kwa ubunifu wao wa kubuni mipango mbalimbali ya uchangiaji
inayolenga kuwafikia watanzania wa makundi mbalimbali kulingana na hali
zao za vipato na uwezo wao wa kuchangia.
“Hali halisi ya uchumi wa
watanzania mnaifahamu, siyo watu wengi wenye uwezo wa kugharamia
matibabu kwa fedha taslimu hivyo, huduma za matibabu kupitia Mfuko huu
ni ukombozi mkubwa kwa kundi kubwa la watanzania”, alisema Meck Sadik.
Aidha, Mhe. Meck Sadik
amewakumbusha wajumbe wa Baraza hilo kuwa wao ni kiungo muhimu kati ya
wafanyakazi na uongozi wa Mfuko kwa hiyo, wana wajibu wa kuyaelewa
malengo ya Taisisi yao kiutendaji na kuyawasilisha kwa wafanyazi wenzao
wakiwa kama wamiliki wa kile walichokubaliana na uongozi kuwa ndiyo dira
na mwelekeo wa taasisi.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa NHIF, Bernald Konga amesema kuwa mfuko huo utaendelea
kushirikiana na Serikali, kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto ili kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la
upungufu wa dawa nchini.
“Tunajua kuwa upungufu wa dawa
katika vituo vya matibabu umekuwa ni mojawapo ya kero kubwa katika sekta
ya afya. Ili kuondokana na kero hiyo, Mfuko umeanza kuchukua hatua
mbalimbali za kukabiliana na upungufu huo kwa kuanzisha mpango maalumu
wa kutoa mikopo ya dawa kwa watoa huduma waliosajiliwa ili kuhakikisha
kuwa wanachama wetu na watanzania kwa ujumla wanapata dawa kila
wanapokwenda kupata huduma za matibabu”,alisema Konga.
Chimbuko la Mabaraza ya
Wafanyakazi linatokana na Agizo la Rais Na. 1 la mwaka 1970 lililoagiza
kuwa mahali popote penye wafanyakazi wa kudumu kumi na kuendelea
panatakiwa pawe na chombo cha kuwawakilisha.
WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA AKAGUA MRADI WA MABASI YA MWENDOKASI DART LEO
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza
na mwanafunzi Amina Abdallah wa darasa la sita katika shule ya msingi
ya Ukombozi jijini Dar es salaam ambaye amepanda basi la Mwendo Kasi
Ajentina na kushuka Manzese, Waziri Mkuu Majaliwa ametumia usafiri wa
DART leo kutoka Feri kwenda Kimara Mwisho wakati alipokagua miundombinu
ya usafiri huo ili kujionea mafanikio na changamoto mbalimbali
zinazojitokeza mara baada ya mradi huo kuanza mwezi mmoja sasa ili
ziweze kurekebishwa na kuuboresha zaidi.
Usafiri DART umekuwa mkombozi
kwa wasafiri wengi wa jiji la Dar es salaam wakati wanapotoka majumbani
mwao na kuelekea kazini na kurejea majumbani mwao,Katikati ni Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia
jambo wakati Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa akisamimiana na Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.
Baadhi ya abiria wakisafiri pamoja na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kwenye basi la DART.
Moja ya Basi likiwa katika ruti yake kutoka Kimara kuelekea Posta.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikagua
kituo cha Kimara Mwisho mara baada ya kuwasili kituoni hapo
Moja ya basi la Mwendo kasi likipakia abiria katika kituo cha Kimara Mwisho leo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza
na mwanafunziambaye jina lake halikufahamika mara moja wakati alipofika
kwenye kituo cha mabasi ya Mwendo kasi Kimara Mwisho leo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiuliza
swali kwa mmoja wa wafanyakazi wanaokatisha tiketi katika vituo hivyo
wakati alipokagua miundombinu ya DART leo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiangalia
utendaji kazi unavyoendelea ikiwa ni pamoja na kubaini changamoto
zinazojitokeza.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikaua kituo cha Kimara Mwisho.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia
jambo na Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa katikati ni Mzee David
Mwaibula.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kukagua miundombinu hiyo leo kulia
ni Mzee David Mwaibula na katikati ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama
Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga.
MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI, DODOMA.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni
Mbunge wa CCM Jimbo la Mtama akiwasili katika viwanja vya Bunge mjini
Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge hilo leo 27 Mei, 2016.
Mbunge
wa CHADEMA Jimbo la Mlimba, Mhe. Susan Kiwanga akiwasili katika viwanja
vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge hilo leo 27 Mei,
2016.
Mbunge
wa Viti Maalum CCM, Mhe. Martha Mlata (kushoto) akiwa ameongozana na
Mbunge mwenzie wakiingia ndani ya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao
vya Bunge hilo leo 27 Mei, 2016.
Mbunge
wa Mbozi Vwawa (CCM) Mhe. Josephat Hasunga kushoto) akiwa ameongozana na
Mbunge mwenzie wakiingia ndani ya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao
vya Bunge hilo leo 27 Mei, 2016.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akiwa ameongozana na Naibu
Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni wakiwasili
katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge hilo
leo 27 Mei, 2016.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akiwa
ameongozana na Mbunge mwenzie wakiwasili katika viwanja vya Bunge mjini
Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge hilo leo
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DODOMA.
Mshindi wa bahati nasibu ya Taifa kupatikana kesho
Mbunge
wa zamani jimbo la Nanyumbu Dastan Mkapa (kulia) akipewa maelezo namna
mshindi wa bahati nasibu ya Taifa atakavyopatikana mara baada ya kukata
tiketi ya mchezo huo katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma
jana baada ya kuzinduliwa rasmi ukataji tiketi za mchezo.
Mkurugenzi
wa Bodi ya michezo ya bahati nasibu ya Taifa ,Abbas Tarimba
akiwaelekeza wananchi jinsi mashine za mchezo huo zinavyofanya kazi.
Wakala
wa ukataji tiketi za mchezo wa bahati nasibu ya Taifa mjini Dodoma
Jamila Baduwel akitoa huduma hiyo kwa mmoja wa wananchi aliyetaka
kununua tiketi za kushiriki.
…………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Baada
ya kampuni ya Murhandizwa kutoka nchini Afrika ya Kusini ambayo
ilipewa leseni ya kuendesha mchezo wa bahati nasibu ya taifa kuanza
kuuza tiketi za mchezo huo wiki iliyopita ,leo (Jumamosi) ndio mchezo wa
kwanza utafanyika na mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100
atatangazwa.
Mwenyekiti
wa kampuni ya Gidani International ambayo ni kampuni mama ya kampuni ya
Murhandizwa,Prof .Bhongani Khumalo alisema kuwa michezo yote
itaendeshwa kwa utaalamu kwa kutumia teknolojia ya kisasa na kwa uwazi
vilevile kuanza kwa mchezo huo hapa nchini ni mwendelezo wa michezo
mingine mingi ya bahati nasibu itakayokuja baadaye.
“Kampuni
yetu inao uzoefu wa muda mrefu kuendesha michezo ya Bahati Nasibu na
tutahahakikisha watanzania wananufaika na mchezo huu pia tutachangia
pato la taifa kwa njia ya kodi kupitia mchezo huu.Aliongeza kuwa
uchezeshaji wa mchezo utakuwa wa wazi kupitia vyombo vya habari na
mshindi atakuwa anatangazwa na kupatiwa fedha zake mara moja bila kuwepo
urasimu wa aina yoyote.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubatisha ya
Taifa,Abbas Tarimba aliwataka watanzania kuchangamkia fursa hii kwa
kununua tiketi za kushiriki katika mchezo kutoka kwa mawakala
waliosambaa nchini kote ili waweze kujishindia zawadi ya mamilioni ya
fedha na kubadilisha maisha yao.
Tarimba
aliwataka wananchi wasiwe na hofu ya kushiriki kwenye mchezo kwa kuwa
unafanyika kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali
“Wananchi wasiwe na wasiwasi kushiriki kwenye mchezo huu kwa kuwa fedha
zao na kanuni za uendeshaji wa mchezo vinasimamiwa na serikali.
Alisema
ujio wa mchezo huu nchini mbali na kuwanufaisha washindi binafsi
utachangia kupanue wigo wa ajira kwa Watanzania wengi watakaosimamia
zoezi la ukatishaji tiketi katika vituo zaidi 20,000 vitakavyofunguliwa
Nchi nzima.
Tiketi
za mchezo huu zimeanza kuuzwa nchi nzima na wakati wa uzinduzi wa
huduma za kampuni mkoani Dodoma wananchi wengi walijitokeza kununua
tiketi za kushiriki na walishauri mtandao wa kuuza tiketi ufanyike
kupitia hata kwenye simu za mkononi ili kuwawezesha wananchi wengi
kushiriki kununua tiketi ambayo kila moja inauzwa shilingi 500/-
EAC TABLES USD 100 M BUDGET TO EALA
Hon Dr Susan Kolimba, Deputy Minister, Foreign Affairs and East African
Co-operation, Dr Susan Kolimba holds the Budget Speech. She is flanked by the EAC Secretary General, Hon Amb Liberat Mfumukeko
Co-operation, Dr Susan Kolimba holds the Budget Speech. She is flanked by the EAC Secretary General, Hon Amb Liberat Mfumukeko
The deputy Minister of Foreign Affairs and East African Co-operation, Hon
Dr Susan Kolimba presents the Budget Speech to the House. At back is the
EALA Speaker, Rt. Hon Daniel Fred Kidega.
Dr Susan Kolimba presents the Budget Speech to the House. At back is the
EALA Speaker, Rt. Hon Daniel Fred Kidega.
The EAC today presented Budget estimates for the Financial Year 2016/2017 totaling
$101,374,589 to the East African Legislative Assembly sitting in Arusha.
Deputy Minister for Foreign Affairs and East African Co-operation, Hon
Dr Susan Kolimba presented the Budget speech to an attentive House on
behalf of the substantive Minister and Chair of the EAC Council of
Ministers, Hon Dr. Augustine Mahiga.
The 2016/2017 Budget is a$101,374,589 to the East African Legislative Assembly sitting in Arusha.
Deputy Minister for Foreign Affairs and East African Co-operation, Hon
Dr Susan Kolimba presented the Budget speech to an attentive House on
behalf of the substantive Minister and Chair of the EAC Council of
Ministers, Hon Dr. Augustine Mahiga.
drop down from $110,660,098 Million presented to the House in the
previous Financial Year. The Budget prioritizes the full implementation
of the EAC Single Customs Territory, enhanced implementation of the EAC
Common Market Protocol especially additional commitments and
interconnectivity of border immigration systems and procedures across
Partner States and enhancement of productivity and value addition in key
productive sectors.
MATUKIO MBALIMBALI YA PSPF-INTER COLLEGE BONANZA
Picha
mbalimbali zikionyesha matukio mbalimbali yaliyojiri katika tukio la
PSPF INTER -COLLEGE BONANZA lililofanyika katika viwanja vya chuo cha
uhasibu jijini Arusha mwishoni mwa wikii liyopita ambalo lilikuwa na
lengo la kutoa elimu kwa wanachuo mbalimbali kuhusu mfuko wa hifadhi ya
jamii wa PSPF.
(picha na mahmoud ahmad,Arusha.
MULTICHOICE TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA AFRIKA.
Sehemu
ya Watendaji wakuu wa Kampuni ya MultiChoiche Tanzania wakiongozwa na
Mtendaji Mkuu wao, Francis Senguji (wa pili kushoto) wakiwa katika
tafrija ya kuadhimisha siku ya Afrika, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa
Hoteli ya New Afrika, Jijini Dar es salaam.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya MultiChoiche Tanzania, Furaha Samalu akizungumza
machache katika tafrija hiyo ya kuadhimisha siku ya Afrika, iliyofanyika
kwenye Ukumbi wa Hoteli ya New Afrika, Jijini Dar es salaam.
Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya MultiChoiche Tanzania, Francis Senguji akizungumza
machache katika tafrija hiyo ya kuadhimisha siku ya Afrika, iliyofanyika
kwenye Ukumbi wa Hoteli ya New Afrika, Jijini Dar es salaam. Kushoto ni
Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Furaha Samalu.
Burudani ya Kiafrika ikitolewa.
Mshehereshaji
katika Tafrija hiyo, Masoud Kipaya (kati) pamoja na Meneja Masoko wa
Kampuni ya MultiChoiche Tanzania, Furaha Samalu, wakimsikiliza Msanii wa
Muziki wa Kizazi kipya, Shilole wakati akimtangaza mmoja wa washindi wa
Dikoda ya DSTV Exprola.
Washindi
wa Dikoda za DSTV Exprola kwa usiku huo walikuwa ni Mmiliki Mwendeshaji
wa Libeneke la Full Shangwe Blog, John Bukuku na Mwanadada Latoya
aliewahi kuwa Mshiriki wa Shindano la Big Brother Afrika miaka ya nyuma.
No comments:
Post a Comment