Pages

Tuesday, March 1, 2016

Ministry tasks PwC with search for new KAA boss

Former Kenya Airports Authority (KAA) boss Lucy Mbugua leaves the Ethics and Anti-Corruption Commission. She was pusheed out of office over a Sh11million bus leasing scandal. FILE PHOTO | BILLY MUTAI |
Former Kenya Airports Authority (KAA) boss Lucy Mbugua leaves the Ethics and Anti-Corruption Commission. She was pushed out of office over a Sh11million bus leasing scandal. FILE PHOTO | BILLY MUTAI |  NATION MEDIA GROUP


By BRIAN NGUGI
More by this Author
The government has stepped up the search for a new Kenya Airports Authority (KAA) chief ...
executive two months after it annulled an initial recruitment process citing interference.
Kenya Airports Authority, (KAA) said on Monday in a notice that it is seeking a competent chief executive to drive its mandate. The right candidate should be holders of Bachelor’s degree from a recognized institution of higher learning, KAA said.
KAA has tasked advisory firm PricewaterhouseCoopers to steer the process.
On January 21, Transport Cabinet Secretary James Macharia cancelled the previous recruitment process citing interference.
Mr Macharia consequently directed that the process be initiated afresh with immediate effect by a “reputable and competent professional firm”.
The KAA board had taken up the process, following the KAA management’s alleged bungling of the procurement of a recruitment agency.
The board fired three of its senior officials — including managing director Lucy Mbugua, general manager for finance John Thumbi and acting airport engineer Christopher Warutere — on June 27 last year over allegations of improprieties in procuring airport buses.
Mbugua was also being probed for her alleged role in a controversial duty-free shops tender.

Profesa MAYUNGA HABIBU NKUNYA ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC)


maxresdefaultWaziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kwa Mamlaka aliyopewa amemteua Profesa MAYUNGA HABIBU NKUNYA kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kuanzia Februari 17, 2016.
Uteuzi huo ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 17 Februari, 2016 hadi 16 Februari, 2019.
Kabla ya uteuzi huo Profesa Nkunya alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Programu ya Mapitio ya Mfumo wa Taifa wa Ubunifu (National Innovation System Review Programme).
Uteuzi huo unafuatia kumalizika kwa muda wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo.  
Taarifa hii imetolewa na,
Eng. Joseph M. Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI),
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
01 Machi, 2016

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA IDARA YA HABARI MAELEZO

download (2)
Gazeti la Dira ya Mtanzania, Toleo Na.404 la Februari, 29 – Machi 6, 2016 liliandika taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho “Uchafu wa Ombeni Sefue Ikulu”.  Taarifa hiyo, ambayo ni muendelezo wa makala nyingine kwenye toleo la gazeti hilo la wiki iliyopita, ilimtuhumu Katibu Mkuu Kiongozi kushawishi juu ya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa MSD pamoja na Kampuni za “CRJE” na “UGG” kupewa tenda ya kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma, Daraja la Kigamboni na Reli ya Dar es Salaam – Kigali. Taarifa zote hizi ni za uongo na za kupotosha wananchi.  
Kuhusu uteuzi wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD,
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, hakuhusika kwa namna yoyote kushawishi uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa MSD. Uteuzi huo ulitekelezwa kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa. Nafasi hiyo ilitangazwa na Bodi tarehe 20 Novemba, 2013. Usaili ulifanywa na kampuni huru iliyopewa jukumu hilo na Bodi. Mapendekezo ya majina matatu yalipelekwa kwa Mhe. Rais na Waziri wa Afya, kwa ajili ya uteuzi. Balozi Sefue alikuwa hamjui aliyeteuliwa na wala hakuwahi kuwa na uhusiano naye. Alichofanya Balozi Sefue ni kutangaza tu uteuzi baada ya Rais kuteua. Gazeti hilo pia limeandika uwongo kuwa MSD haijawahi kuongozwa na Mkurugenzi Mkuu asiye Mfamasia.  Tangu MSD ianzishwe mwaka 1993 hadi sasa, ni Mkurugenzi Mkuu mmoja tu, Rino Meyers (1996-1999), ndiye  alikuwa Mfamasia. Wakurugenzi wengine kama  Peter Mellon (1993-1995), Jay Drosin (2001-2004) na Joseph Mgaya (2004-2013) hawakuwa Wafamasia.
Kuhusu Kampuni ya CRJE kuhusishwa na Balozi Ombeni Y. Sefue
Suala la kumhusisha Katibu Mkuu Kiongozi na kampuni hii nalo ni uzushi na uongo wa kupindukia. Wakati kampuni hii ikipewa tenda ya kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma mwezi Oktoba 2007, Balozi Ombeni Y. Sefue hakuwa Katibu Mkuu Kiongozi; alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani. Kadhalika mchakato wa kumpata mkandarasi wa daraja la Kigamboni, ulipoanza mwezi Machi, 2011, Balozi Sefue hakuwa Katibu Mkuu Kiongozi; alikuwa Balozi wa Tanzania, Umoja wa Mataifa, New York. Hata mkataba wa ujenzi wa Daraja hilo uliposainiwa tarehe 9 Januari, 2012, Balozi Sefue alikuwa na wiki moja tu ya kuwa Katibu Mkuu Kiongozi kufuatia kuteuliwa tarehe 30 Disemba, 2011. Aidha, Kampuni iliyoshinda tenda hiyo wala siyo CRJE kama ilivyoandikwa na gazeti hilo bali ni China Major Bridges Engineering Company (BCEC) kwa kushirikiana na Kampuni ya China Railway Construction (CRCEG).
Kuhusu tuhuma kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Chapuo Kampuni ya UGG:

MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA (TCAA), HAMZA JOHARI.AANZA KAZI RASMI.

JOH1
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari   (katikati) akimsikiliza kwa makini Mwanasheria wa Mamlaka hiyo , Vallery Chamulungu  wakati alipokuwa akimkaribisha rasmi ofsini hapo.
JOH2
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA).Hamza Johari  (watatu kushoto) akimsikiliza kwa makini Mwanasheria wa Mamlaka hiyo , Vallery Chamulungu (watatu kutoka kulia) wakati alipokuwa akimkaribisha rasmi ofisini Makao Makuu ya TCAA, Banana Ukonga Dar es Salaam. Wengini ni maofsa wa mamlaka hiyo.
JOH3
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  Hamza Johari (KUSHOTO)akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uongozaji ndege na Huduma za ufundi  , Bw. Nyello Abeid ,wakati wa kumkalibisha  rasmi  kuanza kazi TCAA.
JOH4
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari akiwa katika kikao na menejimenti ya Mamlaka hiyo mara baada ya kukaribishwa rasmi kuanza kazi   Makao Makuu ya TCAA, Banana Ukonga Dar es Salaam.
JOH6
.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari akiwa rasmi  ofini kwake kuanza majukumu yake kama Mkurugenzi Mkuu TCAA  ,baada ya kukaribishwa rasmi TCAA.
JOH8
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari akipokea  Shada la maua kutoka kwa  mmoja wa wafanyaakzi wa Mamlaka hiyo ,Evelyne Ngachengo ,wakati alipokuwaakikaribishwa na wafanyakazi wenzake rasmi kuanza kazi ,rasmi ofisini Makao Makuu ya TCAA, Banana Ukonga Dar es Salaam.

WANAFUNZI WA SHULE YA NAMABENGO SEKONDARI WAANDAMANA KUPINGA VITENDO VYA KIKATILI WANAVYOTENDEWA NA MWALIM MKUU MSAIDIZI SHULENI HAPO

 Mwanafunzi wa shule ya SEKONDARI NAMABENGO ambaye hakufahamika jina akionyesha kidonda anachouguza kutokana na fimbo ambazo wanapigwa na mwalim mkuu msaidizi wa shule hiyo SHAIB CHAMPUNGA.
 Wanafunzi wa shule ya sekondari namabengo wakiwa wamekaa na kumsikiliza afisa elimu wa wilaya hiyo ambaye hayupo pichani .

MAHAKAMA YA TANZANIA YAKUTANA NA WADAU JIJINI DAR ES SALAAM, YASISITIZA UTOAJI WA HAKI KWA WAKATI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU.

MAHM1
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi  Februari 1 hadi 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja,  jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu Mahakama Kuu, Solanus Nyimbi na Kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufaa,  John Lugalema Kahyoza
MAHM2
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi  Februari 1 hadi 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja,  jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu Mahakama Kuu, Solanus Nyimbi na Kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufaa,  John Lugalema Kahyoza
MAHM3
Washiriki wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi  Februari 1 hadi 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja, wakifuatilia kikao hicho leo jijini Dar es salaam.
MAHM4
Mmoja wa washiriki wa kikao hicho akichangia.
…………………………………………………………………………………………………….

DK. KIGWANGALLA AAGIZA KUFUNGWA CHUMBA CHA UPASUAJI CHA HOSPITALI YA SANITAS YA MIKOCHENI

Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa mara moja Chumba cha upasuaji cha hospitali ya Sanitas ya Mikocheni Jijini Dar es Salaam baada ya kubaini kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo mfumo na ramani yake kimefungwa kwa kutokidhi vigezo vya kimataifa vya namna chumba hicho kinavyotakiwa kuwa.
dk kigwa
Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata maelezo machache kutoka kwa Meneja uendeshaji wa Hospitali ya Sanitas, Bi. Gean Cabral wakati walipowasilia katika ziara hiyo..
dk hk 888
Dk Kigwangalla akikagua baaadhi ya sehemu katika hospitali hiyo.
dk hk55
Dk. Kigwangalla akizungumza na baadhi ya wagonjwa (hawapo pichani) namna Serikali ya Rais Magufuli inavyofanya kazi kwa kusimamia haki na usawa ikiwemo kufika katika maeneo yenye kero na kuchukua hatua ilikumuokoa Mwananchi katika kupata haki yake na huduma bora anayostahiki.
Kigwangalla akitoa maagizo
Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo kwa Meneja uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral
dk hkna
Dk. Kigwangalla akimuonesha moja ya ‘karatasi’ iliyoandikwa ujumbe mbalimbali dhidi ya madai kutoka kwa wafanyakazi wa Hospitali hiyo.
dk kigwa
Meneja Uendeshaji wa Hospitali hiyo Bi. Gean Cabral akifafanua jambo pamoja na Naibu Waziri wakati wa ziara hiyo..
dk hk iio
Dk Kigwangalla akiangalia namna hali ya Maabara ya Hospitali hiyo licha ya kuwa na vifaa vya kutosha, lakini imeshindwa kuweka mpangilio mzuri unaotakiwa kutumika katika mahabara. ikiwemo suala la usafi
dk hk67
Naibu Waziriwa Afya, Dk. Kigwangalla (kushoto), Msajili wa Hospitali Binafsi pamoja na maafisa wengine akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Aziz (kulia) wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kumalizika kwa ziara hiyo ya kushtukiza kuangalia namna ya uendeshaji katika huduma za Sekta za Afya, zikiwemo za Serikali na zile za watu binafsi. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

UNCDF YAWAKUTANISHA WATAALAMU WA FEDHA KUTOKA NCHI MBALIMBALI KUJADILI JINSI YA KULETA MAENDELEO KWA KUTUMIA VYANZO VYA NDANI

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha wa Umoja wa Mataifa (UNDCF), David Jackson, (kulia), akitoa mada kwenye mkutano wa siku mbili wa wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016. 
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Benki ya TIB, Jaffer Machano, akitoa mada kwenye mkutano wa siku mbili wa Wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016.
 Mtoa Mada, Suzane Ngane kutoka Cameroun,  akitoa mada kwenye mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT), Habraham Shemumoyo, kitoa mada kwenye mkutano wa siku mbili wa Wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani uliofanyika jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016. 

HALI YA UNYONYESHAJI WATOTO NCHINI SIO NZURI

Imeelezwa kuwa wastani wa unyonyeshaji kwa watoto walio chini ya miezi sita nchini sio mzuri na hivyo kuwa na uwezekano wa watoto kudhoofika kwa kukosa maziwa ya mama ambayo yanakuwa na virutibisho muhimu kwa ukuaji ya mtoto.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF ili kujadili jinsi uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kusaidia maendeleo kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.

DSC_0599
Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman akitoa neno la ufunguzi katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF ili kujadili jinsi uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kusaidia maendeleo kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.(Picha zote na Rabi Hume wa Modewjiblog)
DSC_0630
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF akielezea hali ya unyonyeshaji kwa watoto ilivyo nchini.
DSC_0622
Baadhi ya wadau wa sekta ya afya waliohudhuria katia warsha hiyo wakifatilia kwa makini ripoti zilizokuwa zikitolewa.
DSC_0654
Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin akielezea kuhusu makala za The Lancet juu ya uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama jinsi kunavyoweza kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.
DSC_0655
Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin akiwaonyesha wahudhuriaji wa warsha hiyo ripoti ya utafiti uliofanywa na jarida la The Lancet linalohusika na kuandika habari za afya.
DSC_0661
Viongozi wa Taasisi mbalimbali waliofika katika warsha hiyo wakifatilia ripoti ya utafiti uliofanywa na jarida la The Lancet. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Vicent Assey, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu,Obey Assery Nkya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda na Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman.
DSC_0665
Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Obey Assery Nkya akielezea hatua ambazo serikali imechukua ili kupunguza idadi ya kina mama ambao hawanyonyeshi watoto.
DSC_0674
Viongozi wa Taasisi mbalimbali waliofika katika warsha hiyo wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wadau wa sekta ya afya na waandishi wa habari. Wa kwanza kulia ni Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin, Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Vicent Assey, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu,Obey Assery Nkya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda na Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman.
DSC_0696
Mkuu wa kitengo cha fedha na malipo nchini kutoka Benki ya Dunia, Douglas Pearce akiuliza swali katika warsha hiyo.
DSC_0711
Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman akitoa neno la shukrani kuashiria kumalizika kwa warsha hiyo.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI AZINDUA MRADI WA MAJI KILIMANJARO

LW1Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga akizungumza mbele ya Waziri wa Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge, viongozi na wananchi wa Longuo, Wilayani Moshi.
LW2Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akimtwika maji mama katika Kijiji cha Longuo, Wilayani Moshi mara baada ya kuzindua mradi wa maji kijijini hapo.
LW3Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga (kulia) na wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA).
LW4Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiwa na viongozi na wataalamu aliombatana nao kwenye ziara yake kwenye chanzo cha maji cha Midawe, kilichopo kwenye Mto Nduruma, katika Kijiji cha Bangata, kilichopo Kata ya Bangata, Wilayani Arumeru
LW5Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA), Inj. Ruth Koya akimuonyesha Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge moja ya miradi ya maji inayotekelezwa na mamlaka hiyo, Kata ya Moshono, Wilayani Arumeru.
………………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge amezindua mradi wa maji wa Longuo, katika Kijiji cha Longuo, Wilaya ya Moshi mwishoni mwa wiki katika ziara yake mkoani Kilimanjaro. Mradi huo unaohudumia vijiji vya Longuo na Kariwa, umekuwa faraja kubwa kwa wananchi, ambao kwa muda mrefu walikuwa na tatizo la kupata huduma ya majisafi na salama na kusababisha hatari ya magonjwa ya milipuko kwa wananchi.
Mhe. Lwenge, amefurahishwa na utekelezaji wa mradi huo ambao umechukua siku themanini tu kukamilika, na kuipongeza Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Moshi (MUWSA) kwa usimamizi mzuri wa mradi huo. Pia, alitembelea chanzo cha maji, chemchemi ya Kisimeni iliyopo Kata ya Uru Kusini ambayo inachangia uzalishaji wa maji katika Wilaya ya Moshi.
Vilevile, Mhe. Lwenge alitembelea miradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA). Katika ziara yake hiyo mkoani Arusha, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, aliweza kufika kwenye chanzo cha maji cha Midawe, kilichopo kwenye Mto Nduruma, katika Kijiji cha Bangata, kilichopo Kata ya Bangata, Wilayani Arumeru ambao unachangia asilimia ishirini ya uzalishaji maji kwa Jiji la Arusha.
Pia, alifika kwenye chanzo cha maji cha chemchemi ya Machare, iliyopo Kata ya Moshono, Wilayani Arumeru iliyovamiwa na wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu kinyume na sheria na kuhatarisha uzalishaji wa maji ya kutosha kwa ajili ya kuhudumia mji wa Arusha.

SPIKA WA BUNGE MH. JOB NDUGAI AKUTANA NA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI LEO

J1
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Job Ndugai akizungumza na wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) hawapo pichani kutoka Tanzania wakati walipomtembelea katika ofisi zake zilizopo jijini Dar es salaam na kumpa salaam maalum za kumpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwake na watanzania na kuwa Rais wa Tanzania awamu ya Tano ikiwa ni pamoja na kupongeza utendaji kazi wake kwa ujumla wake.(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
J2
Baadhi ya wabunge wa bunge la Afrika Mashariki waliomtembelea Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai kutoka kulia ni Mh. Adam Kimbisa, Mh. Shy Rose Banjhi na Mh. Abdallah Mwinyi wakizungumza na Spika wa Bunge.
J3
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Job Ndugai kulia akizungumza na wabunge hao.
J5
Mkurugenzi wa Mhusiano ya Kimataifa ofisi ya Bunge Bw. Josey Mwakasyuka akijitambulisha katika mkutano huo.
J7
Mh. Shy Rose Banjhi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na Spika
wa Bunge Mh. Job Ndugai kushoto ni Afisa habari wa Bunge Bw. Owen Mwandumbya

No comments:

Post a Comment