Pages

Thursday, February 25, 2016

SERIKALI KUTOA MIKATABA MAALUM YA AJIRA SEKTA YA UJENZI

mal1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Amos Makala walipokutana mjini Moshi kwa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyo chini ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
mal2
Mkuu wa Wilaya ya Same Bw. Herman Kapufi akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wanaofanya kazi katika kampuni ya Dott Services Limited inayojenga barabara ya Same-Mkumbara Km 96. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
mal3
wafanyakazi  wa kampuni ya Dott Services Limited wakishangilia kwa furaha baada ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kumtaka mkandarasi kuwalipa madai yao yote ifikapo Februari 26, mwaka huu.
mal4
Muoneano wa Jengo la Kituo cha Forodha cha pamoja (One Stop Border Post) kwa upande wa Tanzania lililopo Holili.
mal5
Ujumbe wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ukielekea katika kituo cha pamoja cha forodha (One Stop Border Post) kwa upande wa Taveta nchini Kenya.
mal6
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipata ufafanuzi wa namna ya kituo cha pamoja cha Forodha  kinavyofanya kazi kutoka kwa Meneja Forodha kwa upande wa Taveta – Kenya Bw. Daniel Nyambaka.
mal7
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiagana na Meneja Forodha kwa upande wa Taveta – Kenya Bw. Daniel Nyambaka mara baada ya kukagua kituo hicho.
………………………………………………………………………………………………………

STATEMENT BY HEAD OF UN MISSION IN TANZANIA ON THE OCCASION OF THE 50TH ANNIVERSARY OF UNDP

Alvaro Rodriguez
UN Resident Coordinator in Tanzania and UNDP Resident Representative, Mr. Alvaro Rodriguez.
Today marks the 50th Anniversary of the United Nations Development Programme (UNDP). Founded in 1966, UNDP now works in some 170 countries and territories to help eradicate poverty and reduce inequalities and exclusion.

KLABU YA KIMATAIFA LIONS CLUB INTERNATIONAL YATOA MSAADA WA MADAWATI YA CHUMA SHINYANGA

Leo Februari 24,2016 ,Chama cha Kimataifa kinachotoa misaada mbalimbali ya Kijamii cha Lions Club International chenye makao yake makuu nchini Marekani kimetoa msaada wa madawati 165 yenye thamani ya shilingi milioni 18 katika shule ya msingi Town na Mwenge zilizopo katika manispaa ya Shinyanga ili kumaliza changamoto ya wanafunzi kukaa chini.
Pichani viongozi wa wilaya ya Shinyanga,wazazi na maafisa kutoka Lions Club International wakiongozwa na Gavana wa Lions Club katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini bwana Hyderali Gangji wakiwa katika shule ya msingi Town…Madawati hayo 165 yametolewa na Lions Club ya mkoa wa Mwanza.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama  Malunde ametuletea picha 30 kilichojiri mwanzo hadi mwisho
Hapa ni katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(katikati).Kushoto ni meya wa manispaa ya Shinyanga,ambaye pia ni diwani wa kata ya Shinyanga ilipo Shule ya Msingi Town na Mwenge akimtambulisha gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji na jinsi klabu hiyo inajihusisha na utoaji wa misaada kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji

Wanachama wa Lions Club International walioambatana na gavana

Kulia ni gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji akieleza namna klabu yake inavyofanya kazi katika nchi 210 duniani kote

Wanachama wa Lions Club International wakiwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga

Gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji alisema Lions Club International ina wanachama Milioni 1 na laki nne duniani kote na nchini Tanzania kuna vilabu 18 na nchini Uganda vilabu 24

Gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji alisema wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali mkoani Shinyanga ambapo mwaka jana walitoa msaada wa chakula kwa wahanga wa mvua ya Mwakata wilayani Kahama,pia chakula katika kituo cha walemavu wa ngozi cha Buhangija,kutoa madawati katika shule ya msingi Town na Mwenge

Miongoni mwa madawati ya chuma 165 yaliyotolewa na Lions Club International katika shule ya msingi Town na Mwenge katika manispaa ya Shinyanga

Hapa ni katika shule ya msingi Town katika manispaa ya Shinyanga ,aliyesimama ni mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Said Juma Issa akiwakaribisha viongozi mbalimbali waliofika katika shule wakati wa hafla fupi ya kukabidhi madawati 65 kwa shule hiyo na 100 katika shule ya msingi Mwenge

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Town wakiangalia madawati waliyopewa na Lions Club International

Kulia ni diwani wa kata ya Shinyanga mjini,ambaye pia ni meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam aliyefanya jitihada za kupatikana kwa madawati katika shule za kata yake,Town na Mwenge.Diwani huyo pia ni mwanachama wa Lions Club International

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Town Josephine Mabula akisoma risala kwa mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambapo alisema shule hiyo yenye wanafunzi 1104 sasa haina uhaba tena wa madawati baada ya kupokea kutoka Lions Club International
Continue reading →

Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano azungumza na wakala wa majengo (TBA)

nai1
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akiongea  na menejimenti ya  Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) alipowatembelea katika ofisi zao leo jijini Dar es Salaam, wakati wa   ziara ya kuzitambua tasisi zilizopo chini ya wizara yake  .
nai2
Wafanyakazi wa   Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)  wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani(hayupo katika picha) leo jijini Dar es Salaam, katika  ziara ya kuzitambua tasisi zilizopo chini ya wizara yake .
nai3
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi. Manase Ole Kujan katika ziara yake ya kuzitambua tasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kuangalia majukumu yanayotekelezwa na Taasisi hizo.
nai4
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani (Kushoto) akifafanua jambo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Mhandisi.Julius Mamilo(kulia) wakati ziara yake ya kuzitambua tasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kuangalia majukumu yanayotekelezwa na Taasisi hizo leo jinini Dar es Salaam.
nai5
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akiongea  wakati wa kikao na wafanyakazi wa   Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) alipowatembelea katika ofisi zao leo jijini Dar es Salaam, wakati wa  ziara ya kuzitambua tasisi zilizopo chini ya wizara yake  kushoto ni Mtendaji Mkuu  wa Wakala wa TBA Arch.Elius Mwakalinga .
nai6
Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani(Hayupo katika picha) Mamilo  katika ziara yake ya kuzitambua tasisi zilizo chini ya wizara

Tigo yafikisha upatikanaji wa huduma ya 4G LTE Moshi

Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata (katikati)  akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) katika uzinduzi wa huduma ya 4G LTE jijini Dodoma, kushoto ni Meneja wa huduma ya 4G LTE, Benedict Mponzi na kulia kwake ni Meneja Masoko wa kanda ya kaskazini  Kephar Kileo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo mjini Moshi.
Meneja wa huduma ya 4G LTE, Benedict Mponzi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katikati ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata na kulia kwake ni  Meneja Masoko wa kanda ya kaskazini  Kephar Kileo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo mjini Moshi.
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAMUAGA MWAKILISHI MKAZI WA UNHCR, JOYCE MENDS-COLE mwk1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (watatu kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (wapili kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (wapili kulia) wakielekea katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa ajili ya kumuaga Mwakilishi wa UNHCR nchini, iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mwk2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza katika hafla ya kumuaga  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (watatu kulia). Katika hotuba yake fupi, Waziri Kitwanga alimshukuru Mwakilishi huyo kwa ushirikiano wake mzuri kati ya Wizara na UNHCR, pia alimtakia safari njema na mafanikio mema arudipo nyumbani kwake. Joyce anatarajia kustaafu rasmi katika nafasi hiyo mwezi ujao. Wanne kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni, kushoto aliyekaa ni Katibu Mkuu, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mwk3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole, kwa ajili ya kumbukumbu yake kutokana na ushirikiano mzuri kati ya Shirika lake la UNHCR na Wizara. Hafla hiyo fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ilifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mwk4
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole akimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Wizara hiyo, kwa ushirikiano mkubwa waliompa wakati anaiongoza UNHCR. Pia katika hotuba yake, Joyce alimpongeza Rais John Magufuli kwa uongozi wake mzuri pamoja na ushirikiano mkubwa wanaoupata kutoka katika Serikali yake. Wakwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mbarak Abdulwakil ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, na Wanne kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrsion Mseke. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mwk5
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrsion Mseke akizungumza katika hafla ya kumuaga  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (watatu kulia). Katika hotuba yake, Mseke alimshukuru Joyce kwa ushirikiano wake mkubwa aliouonyesha wakati wa uongozi wake. Wapili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ambaye aliiongoza hafla fupi iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Wanne kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mbarak Abdulwakil ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mwk6
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kushoto) akimuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole mara baada ya kumaliza sherehe fupi iliyoandaliwa na Wizara ya kumuaga kiongozi huyo wa UNHCR. Hafla hiyo fupi ilifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Wizara akiwemo Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mwk7
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wanane kushoto), Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni (watano kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wasaba kushoto), Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais,

No comments:

Post a Comment