Pages

Sunday, January 3, 2016

Uzinduzi wa Sherehe za Mapinduzi kwa Usafi wa Mazingira Kitaifa

uc1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizoa taka katika zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
uc2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akibeba taka katika zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
uc3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumzaa na wananchi baada ya kumalizika kwa  zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
uc4
Baahi ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wakitandaza kifusi kwa kukiweka sawa katika zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
uc5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiteta  akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B.Unguja Ayoub Maohammed Mahmoud wakati zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
uc6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifanya mahojiano na waandishi wa Habari leo baada ya kumalizika zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]

WATAALAM WATEMBELEA VYANZO VYA MAJI YA MABWAWA YA KUZALISHA UMEME


Wataalam kutoka Wizara za Nishati na Madini,Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ,Wizara ya maji, na Umwagiliaji , Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco )pamoja na Watalamu wa bonde la mto Rufiji walitembelea  vyanzo vya maji vinavyotiririsha  maji katika mito mikubwa inayomwaga maji katika  mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji ya  Mtera, Kihansi na Kidatu ili kuangalia uharibifu wa vyanzo hivyo vya maji na kuchukua hatua za kuzuia uharibifu huo
Wataalam hao waliunganisha nguvu ya pamoja ili kurejesha utunzaji na usalama wa  vyanzo hivyo  ili viwe katika hali yake ya awali kutokana na kuathiriwa na shughuli za kibinadamu zinazoendelea na kusababisha kukauka kwa maji na kusababisha upungufu mkubwa katika mabwawa ya kuzalisha umeme tofauti na  ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
VY1
Muonekano wa Bwawa la Kihansi kwa sasa ambalo pia limepunguza uzalishaji wa umeme wa maji kutokana na kupungua kwa kina cha maji.
VY2
Timu ya wataalamu  kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi ,Wizara ya maji, na umwagiliaji , Shirika l Umeme Tanzania (Tanesco )pamoja na Watalamu wa bonde la mto Rufiji waliotembelea  vyanzo vya maji vinavyotiririsha  maji katika Mabwawa ya kuzalisha umeme wakiendelea na ukaguzi wao .
VY3
Eneo lenye  chanzo cha cha maji pamoja cha mto  Mbalo mto huu  hutumiwa kwa shughuli za kibinadamu na kusababisha upotevu wa maji yanayoingia katika  katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji
VY4
Moja ya sehemu ya mashine ama mtambo inayotumika kuzalisha umeme wa maji katika vituo vya Kihansi, Kitadu na Mtera.
VY5
Mashine inayotumika kuondoa  taka  kama vile magogo na nyingine za
namna hiyo katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji.
22709f7d-3f87-4d0f-b925-e712ddfa6542
Baadhi ya wajumbe wa Timu ya kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi ,Wizara ya maji, na umwagiliaji , Shirika l Umeme Tanzania (Tanesco )pamoja na Watalamu wa bonde la mto Rufiji wakipata maelezo ya namna ambavyo umeme wa maji huzalishwa katika kituo cha Kihansi .

WAZIRI MKUU KUANZA ZIARA MKOANI RUVUMA

maj2
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa   anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma, ambapo atawasili mkoani  hapo  leo saa tisa alasiri.
Baada ya Waziri Mkuu kuwasili Uwanja wa Ndege wa Songea, atapokelewa na viongozi wa Chama na Serikali, pia atakwenda Ikulu kupokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Ruvuma.
Aidha, siku ya jumatatu  atakuwa na shughuli za kufungua  tawi la Benki ya Posta mjini Songea, kukagua  maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula  (NFRA) kanda ya Songea na kukagua  makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Siku inafuata atatembelea na kukagua Hospitali ya Rufaa ya mkoa, na baadaye kuzungumza na watumishi wa hospitali  hiyo.
Siku ya nne ya ziara yaani jumatano, Waziri Mkuu atafanya majumuisho ya ziara mkoani humo, kabla ya kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na kurejea Dar es Salaam.

DKT. KIGWANGALA AMJULIA HALI MWADHAMA KARDINALI PENGO.

Dkt. Kigwangala amtembelea na kumjulia hali Kadinali Pengo.

HAMI
Na Benedict Liwenga-Maelezo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala leo amemtembelea na kumjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Kadinali Polycarp Pengo aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Akiongelea kuhusu hali ya Kadinali Pengo, Mhe. Kigwangala alisema kuwa Kadinali Pengo yuko salama katika mikono ya madaktari wa taasisi hiyo na hali yake inaendelea vizuri ambapo ameweza kuongea nae ana kwa ana kiasi cha kuweza kukaa na kuongea.
‘’Manzoni alilazwa katika Hospitali ya TMJ iliyopo hapa jijini Dar es Salaam, lakini ikaonekana ni vema akiletwa hapa kwenye Hospitali yetu hii ya juu kabisa ya matibabu ya moyo (Tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete), hivyo napenda kuwapa taarifa Watanzania kwamba yuko salama kabisa katika mikono ya madaktari wetu na hali yake inaendelea vizuri.’’
Awali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli akiongozana na Mkewe mama Janeth Magufuli walienda pia kumjulia hali Kadinali Pengo katika taasisi hiyo na kumtakia afya njema ili aweze kuendelea na shughuli zake za kiroho.
Kadinali Pengo alifikishwa katika taasisi hiyo ya moyo kwa ajili ya kuchunguzwa afya yake ambapo afya yake kwa sasa imezidi kuimarika.

BALOZI SEIF ALI IDI: SHEREHE ZA MIAKA 52 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ZIPO KAMA KAWAIDA.

id01
Balozi Seif Ali Iddi akinukuu kifungu cha Katiba ya Zanzibar kinachomruhusu Dkt. Ali Muhamed Shein kuendelea kuiongoza Zanzibar mpaka atakapoapishwa Rais mwengine.
id1
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu  maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kufikia miaka 52 Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
id2
Baadhi ya Waandishi  wa habari waliohudhuria mkutano wa  Makamu wa Pili wa Rais w Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakifuatiliia mkutano huo uliofanyika  Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
……………………………………………………………………………………………….
Na Khadija Khamis – Maelezo  
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuwa Maadhimisho ya Shereha za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar yapo kama kawaida na yanatarajiwa kuanza  rasmi tarehe 3.12.2016  kwa kazi za usafi  wa mazingira katika maeneo mbali mbali  ya makaazi pamoja na sehemu za kutolea huduma za kijamii kama vile Hospitali Sokoni  na maeneo mengine.
Kauli hiyo imetolewa  na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Alisema ingawa zoezi  la usafi hufanyika kila tunapoanza maadhimisho ya  Sherehe za Mapinduzi  lakini kwa muda huu wananchi  wanapaswa kuchukuwa  juhudi maalum ili kuhakikisha kuwa maeneo yote yanakuwa safi   muda wote kwa vile  hivi sasa  nchi inakabiliwa  na tatizo kubwa la kuenea kwa maradhi ya kipindupindu.
“Zoezi la usafi  wa mazingira litakuwa la lazima na kutaandaliwa utaratibu maalum kwa kila Mamlaka za Mikoa ,Wilaya Baraza la Manispaa Mabaraza ya Miji na Halmashauri za wilaya kuratibu zoezi  la usafi na viongozi Wakuu  wa Kitaifa wataungana nasi katika katika maeneo watakayopangiwa, “Alisisistiza.
Amesema  mbali na usafi wa mazingira, katika maadhimisho ya mwaka huu kutakuwa na shughuli mbali mbali zikiwemo ujenzi wa Taifa ,uwekaji wa  mawe ya msingi  na ufunguzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na burudani na michezo na kilele cha maadhimisho hayo itakuwa siku ya Jumanne katika Kiwanja cha Amaani.
“Kama  kawaida kila ifikapo tarehe 12 Januari ya kila mwaka nchi yetu huadhimisha sherehe za Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964,  kwa mwaka 2016 tutakuwa tunatimiza miaka 52 tangu viongozi na wazee wetu walivyokomboa nchi yetu,”  alisema Balozi  Seif Ali Iddi.
 Alikumbusha kuwa mafanikio na maendeleo  yaliyopatikana  Zanzibar  yanatokana   na imani na jitihada kubwa za viongozi ambao ni wanamapinduzi chini ya uongozi wa Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume aliyeweka msingi imara wa mashirikiano .
Alisema siku ya kilele cha maadhimisho hayo  katika Uwanja wa Amaani  kutakuwa na Gwaride la  Vikosi  vya Ulinzina Usalama , Burudani ya Ngoma za Utamaduni  pamoja na Maandamano ya Wananchi wa Mikoa Mitano ya Zanzibar.
Makamo wa Pili  Balozi Seif Ali Iddi alisema kuwa sherehe hizo zitahudhuriwa na Viongozi mbali mbali  wa Serikali na vyama vya siasa kutoka Zanzibar na  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Amewataka  wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mpinduzi ya Zanzibar na amewahakikishia  Serikali imejipanga kikamilifu kuona kunakuwa na hali ya utulivu na usalama mkubwa katika maeneo yote ya Zanzibar wakati  wa maadhimisho hayo.

Rangers kushuka dimbani kesho

rangers
Mwandishi Wetu
LIGI Daraja la kwanza inaendelea kesho kwa michezo miwili huku timu ya Friends Rangers ikishuka kwenye Uwanja wa mabatini Mlandizi kuvaana na timu ya KMC.
Ofisa Habari wa klabu ya Friends Rangers, Asha Kigundula, alisema kuwa wanatambua ugumu wa mechi hiyo lakini lengo lao ni kushinda na kupata pointi tatu.
Kigundula alisema anatambua kama wapinzani wao wamejipanga kushinda, lakini nao wapo kwa lengo la kufanya vizuri na kuondoka na pointi tatu.
Alisema wao hawajataka tamaa wana amini bado wana nafasi ya kupigania kupanda daraja na kucheza ligi kuu msimu ujao.
“Mechi ngumu sana lakini tumejipanga kushinda mchezo wetu huu, tunatambua uzuri wa KMC lakini nasi tuko vizuri kama tulivyowatoa kwenye michuano ya FA Cup.
Alisema kuwa wapo katika nafasi nzuri ya kupigana na kufanikiwa kuvuka vizingiti wanavyowekewa na baadhi ya wadau wengi.
Wakati huo huo mechi nyingine ya ligi hiyo itakuwa kati ya Africa Lyon dhidi ya Kiluvya United mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Karume.

TIMUATIMUA YATUA KWA KIGOGO WA MNADA WA PUGU,MWIGULU ASHIRIKIANA NA MAWAZIRI 3 KUTATUA KERO MACHINJIO YA PUGU


Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mh:Simbachawene wakiwasili kwenye eneo la machinjio ya Vingunguti kwaajili ya kutoa majawabu kutokana na kero mbalimbali zinazowakabili wadau wa machinjio hayo.
Mwigulu Nchemba akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh:Simbachawene wakikagua eneo la machinjio ya Vingunguti kabla ya kuzungumza na wadau wa eneo hilo pamoja na uongozi wake.
Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na Mh:Simbachawene wakielekea kuzungumza na wananchi wanaotumia Machinjio ya vingunguti.
Mawaziri kutoka kulia ni Naibu waziri wa Afya Mh:Kigwangallah,Wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Segerea Mh:Bonah,Watatu kutoka kulia ni Mh:Simbachawene na wa mwisho kushoto ni Mh:Mwigulu Nchemba wakijadiliana jambo.
Mkutano ukiendelea wa kutoa majawabu kuhusu changamoto za Machinjioya Vingunguti.
Mh:Simbachawene akiwaagiza watumishi wote wa Machinjio ya Vingunguti kuripoti ofisini kwake Jumanne wakiwa na mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.
Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi(Wadau) wa machinjio ya Vingunguti kuhusu hatua za kinidhamu alizozichukua kwa Mkuu wa mnada wa pugu inakotoka mifugo kabla ya kufika Machinjio ya Vingunguti kwa upotevu wa mamilioni ya shilingi ya kodi za serikali.
Mawaziri wakiagana na wananchi mara baada ya mkutano wa kutatua kero zao za Machinjio kumalizika.
Furaha ya Wananchi mara baada ya kutatuliwa kero zao kwa hatua za awali,wananchi wanasukuma gari la Mh:Mwigulu Nchemba kama ishara ya kukubali hatua alizochukua.
 ……………………………………………………………………………………………………………………………………….
Ile kauli ya HAPA KAZI TU imeendelea kutumika vizuri kwa mawaziri wa Mh:Rais John  Pombe Magufuli mara baada ya tukio la mawaziri watatu kufika eneo la Machinjio ya Vingunguti kwaajili ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wanaotumia eneo hilo kwa shughuli za kuchinja mifugo.
Awali,Mh.Mwigulu Nchemba alifanya ziara ya kushitukiza usiku wa tar 01/01/2016 katika machinjio hayo na kukutana na madudu ya kutafunwa kwa fedha za ushuru unaokusanywa kwenye mifugo,lakini pia hali ya mazingira ya kutoridhisha ya Machinjio hayo.
Hii leo mapema majira ya saa 3:asubuhi,Mwigulu Nchemba anarejea tena kwenye machinjio hayo akiwa ameongozana na mawaziri wawili ambao ni Mh:Simbachawene(TAMISEMI) na Mh:Kigwangallah(AFYA) ambao wote wanagushwa na machinjio hayo.
Mara baada ya kusikiliza kero na maoni ya pande zote mbili,Mawaziri hao waliamua kuchua hatua zifuatazo kwa wahusika.
Mwigulu Nchemba ameagiza Mkuu wa mnada na watumishi waliokuwa zamu tar 24/12/2015 na tar 01/01/2016 watafute kazi nyingine kuanzia sasa,Vilevile wahakikishe jumatatu wanafika ofisi ya Katibu Mkuu wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.
Pili,Mwigulu Nchemba ameagiza kuanzia sasa amesitisha ukusanyaji wa ushuru kwenye eneo la mnada wa pugu,badala ya hapo makusanyo yote yatafanyika eneo la machinjio la Vingunguti kwa kutumia mashine za kielektroniki za EFD.
Tatu,Mwigulu Nchemba ameagiza wananchi(wadau) kuanzia leo waanze kutumia eneo lililokuwa limetengwa kwaajili ya kutunzia nyama,Eneo hilo awali lilisitishwa bila sababu maalum na umeme ukakatwa.
Mwigulu Nchemba ameagiza umeme urudishwe hii leo na wananchi waanze kutumia eneo hilo.
Wakati huohuo,Waziri wa TAMISEMI Mh:Simbachawene ameagiza watumishi wote wa machinjio hayo kujitathimini na kufika Jumanne waripoti ofisini kwake wakiwa na mkurugenzi kwaajili ya hatua Zaidi.
Simbachawene ameenda mbali Zaidi kwa kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha fedha zinazokusanywa kwenye machinjio hayo zinatumika haraka kujenga miundombinu ya eneo hilo ilikuendana na wingi wa watu wanaotumia machinjio hayo.
Kwa upande wa Afya,Naibu waziri wa Afya Mh.Kingwangallah ameagiza daktari wa machinjio hayo Ndg.Juma aache kutoa huduma eneo hilo hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo,Pia upimaji wa afya kwa wanaotumia machinjio hayo uwe wa bure na Uongozi wa machinjio utenge ofisi maalu ya kupima watu hao.

Picha/Maelezo na Festo Sanga

BALOZI OMBENI SEFUE AFUNGUA SEMINA ELEKEZI KWA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU KATIBU WAKUU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

OBN1
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu wakati akifungua Semina Elekezi kwa Makatibu hao Ikulu jijini Dar es Salaam
OBN2
Baadhi ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
OBN3
Baadhi ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
OBN4
Baadhi ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
OBN5
Baadhi ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………………………………..
Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kutoka wizara zote za serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekutana hii leo (02 Januari, 2016) katika ukumbi wa Mikutano wa Ikulu Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kupata semina elekezi iliyoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Akizungumza kabla ya kuanza kwa mada zilizoandaliwa katika semina hiyo, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, amesema semina hiyo ni ya kikazi zaidi na kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu hao ambao waliapishwa jana wanatekeleza wajibu wa kusimamia utendaji kazi wa serikali vizuri.
Balozi Sefue ameelekeza kuwa kila Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu anapaswa kutambua kuwa nafasi yake ni ya maamuzi, hivyo serikali inatarajia kuona kuwa daima anafanya maamuzi kwa usahihi na kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazomuongoza katika majukumu yake.
Aidha, ameonya kuwa serikali ya awamu ya tano inawatarajia viongozi hao kuwa watakuwa wasimamizi wazuri wa fedha za umma na kwamba haitarajii kuwepo kwa hati za ukaguzi wa mahesabu zenye kasoro.
Balozi Sefue ameongeza kuwa Makatibu Wakuu hao na Naibu Makatibu Wakuu ni mamlaka ya nidhamu katika wizara zao, hivyo Serikali haitarajii kuona wanakua na kigugumizi katika kuchukua hatua dhidi ya watumishi watakaokuwa na makosa, na akakumbusha kuwa haikubaliki kwa mtumishi aliyefanya makosa katika sehemu moja ya kazi, kuhamishiwa katika sehemu nyingine badala ya kuchukuliwa hatua palepale alipo.
Semina hii elekezi imefanyika kwa siku moja.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
DAR ES SALAAM
02 Desemba, 2016

IRENTE VIEW POINT LUSHOTO TANGA, MOJA YA KIVUTIO AMBACHO WATU WENGI HAWAJAKITAMBUA.

Hapa ndipo kileleni na Mwonekano wa Irente 
 Hii ni Miamba mikubwa iliyopo Irente na moja ya kivutio kikubwa katika eneo hili kwa upande kwa Kushoto.
Eneo hili wakazi wa Irente wanaliita Pango ambapo watu wengi wanapenda kupigia picha
Hii ni njia ya kuelekea Pangoni 
Ukiwa Juu ndani ya Pango utaona hivi 
Mmoja wa walinzi akiandika akiwakatia risiti wageni mbalimbali waliotembelea eneo hilo.
 Mmoja wa wandishi wa Blogs za Mikoa Fredy Tony akiwa amefika kujionea eneo hilo.
 
Watu wengi wamekuwa na utaratibu wa kukalili kuwa wanapoambiwa kwenda kufanya utalii basi mawazo yanahamia katika hifadhi za taifa au Fukwe za Bahari, wakati kuna utalii wa kupanda milima,utalii wa uwindaji utalii wa picha, utalii wa kiutamaduni,Utalii wa Ikolojia,utalii wa fukwe,Michezo ya kwenye maji, utalii wa mali kale,utalii wa mikutano,utalii wa matibabu,utalii wa mashambani na utalii wa jiji.
 
Irente View Point inapatikana katika kijiji cha Irente kilichopo wilayani lushoto mkoani Tanga, eneo hili liligunduliwa na wazee wa kale ambao walikuwa wakifika hapo kwa ajili ya kuomba na kufanya matambiko na wengine walikuwa wakifika katika eneo hilo kwaajili ya kufanya ibada hasa wakati wa sikukuu za Christmas
 
Eneo hili lina urefu wa Mita 1500 kutoka usawa wa Bahari , ukiwa juu unaweza kuona maeneo mbalimbali vizuri bila usumbufu wowote, pia watalii wengi wamekuwa wakifika eneo hilo kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri, kuona Mandhari nzuri hasa wakati wa asubuhi na jioni.
 
Jinsi ya kufikia ikiwa unatokea upande wowote, fika hadi Mombo, panda daladala Tsh 3,000 mpaka Lushoto mjini baada ya hapo unaweza panda Boda boda Tsh 3,000 au ukachukua Tax Tsh 10,000 , kiingilio ni Tsh 2,000. (Imeandaliwa na Fredy A. Njeje 0765056399)
 
 
 
 
 
 
 
 
 

WANANCHI WASHIRIKI UKARABATI WA BARABARA YA MUTURU KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA TARIME.

Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Chira Kata ya Kenyamanyoro katika Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara wakishiriki zoezi la ukarabati mdogo wa barabara ya Muturu (Remaghinga) iliyopo Mtaa wa Buguti Kata ya Rebu ambayo inayotegemewa na Wakazi Kata zote mbili za Kenyamanyori na Rebu hatika halmashauri hiyo.
 
Zoezi hilo limefanyika leo Januari 02,2016 ambapo wananchi hao walikuwa wakifanya ukarabati wa kujaza moramu katika maeneo yaliyochimbika kutokana na maji ya mvua pamoja na kuchimba mitaro kwa ajili ya kupitisha maji wakati wa mvua.
 
“Hii barabara ni kama imesahaulika na Halmashauri ingawaje ni mhimu sana kwani tegemeo kwa wananchi pamoja na shughuli mbalimbali kama vile ujenzi kwa kuwa hapo ng’ambo kuna shughuli za uchimbaji wa mawe hivyo malori huwa yanapita hapa kwa ajili ya kwenda kufuata mawe hayo kwa ajili ya ujenzi katika maeneo mbalimbali ya mji”. Alibainisha mmoja wa wananchi hao na kuongeza kuwa imekuwa kawaida yao kufanya ukarabati wa aina hiyo pindi barabara hiyo inapoharibika.
 
Hatua ya Wananchi hao inapaswa kuigwa na wanajamii wengine pamoja na viongozi wenye dhamana ya kuwasimamia katika masuala ya maendeleo wakiwemo watendaji na wenyeviti wa serikali za mitaa kwani maendeleo yanapatikana haraka zaidi ikiwa wanajamii watashiriki ipasavyo katika shughuli zao za kimaendeleo badala ya kuishia kulalamika mitaani.
Na:George Binagi-GB Pazzo @Binagi Media Group
Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Chira katika Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara wakishiriki zoezi la ukarabati mdogo wa barabara ya Muturu (Remaghinga) inayotegemewa na Wakati Kata za Kenyamanyori na Rebu hatika halmashauri hiyo.
Hii ndiyo dhana halisi ya Maendeleo
Wanajamii wajiwekee utaratibu wa kutatua kero mbalimbali za kimaendelo katika maeneo/mitaa yao
Wanajamii wajiwekee utaratibu wa kutatua kero mbalimbali za kimaendelo katika maeneo/mitaa yao
Maendeleo yanaanza na kila mmoja katika jamii
Kulalamika mitaani si suluhisho la utatuzi wa kero mbalimbali katika jamii
George Binagi-GB Pazzo ambae ni Mwanahabari na Mmiliki wa Mtandao wa Binagi Media Group (Mwenye jembe) nae alishiriki zoezi hilo
George Binagi-GB Pazzo ambae ni Mwanahabari na Mmiliki wa Mtandao wa Binagi Media Group (Mwenye jembe) nae alishiriki zoezi hilo
Barabara ya Muturu (Remaghinga) ni tegemeo kwa wananchi wa kila rika wakiwemo watoto 
Hakika barabara hii imeharibika sana na inahitaji ushirikiano zaidi ili kuweza kurejea katika hali nzuri
Picha hii inaonesha baadhi ya makazi ya watu wanaotegemea barabara hiyo ya Muturu (Remaghinga) ambapo imepigwa kutoka ng’ambo ya pili inakoelekea barabara hiyo.

No comments:

Post a Comment