Rais Dk.John Pombe Joseph
Magufuli akiwauliza Makatibu wakuu wa wizara mbalimbali na Manaibu
Katibu wakuu kama wameelewa na kukubali kusaini Kiapo cha Maadili katika
Utumishi wa Umma mara baada ya kusoma maelezo yaliyomo katika kiapo
hicho ambapo baada ya kuaapisha aliwauliza kama wanakubaliana na
masharti yaliyomo kwenye kiapo cha Maadili ya Utumishi wa Umma na kama
yupo ambaye hakuridhia masharti hayo aseme kabla ya kusaini kiapo hicho,
Hata hivyo Makatibu wote wamesaini katika kiapo hicho.(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-IKULU)
Profesa Elisante Ole Gabriel
Mollel (Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo,
Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi (Katibu Mkuu Maliasili na Utalii
kushoto wakila kiapo cha maadili ya utumishi Ikulu leo.
Baadhi ya Makatibu Wakuu na
Manaibu Katibu Wakuu wakila kiapo cha Maadili ya Utumishi mbele ya Rais
Dk. John Pombe Magufuli Ikulu leo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue akiwaongoza Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu kusoma
kiapo cha Maadili ya Utumishi kabla ya kusaini kiapo hicho.
Manaibu Katibu wakuu na Makatibu Wakuu wakisaini Kiapo hicho mara baada ua kusoma, kuelewa masharti yaliyomo na kuyakubali.
Waziri Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim
Majaliwa akitoa neno mara baada ya Makatibu hao kusaini kiapo cha
Maadili ya Utumishi Ikulu leo.
Baadhi ya Makatibu Wakuu wakisubiri kuapishwa.
Waziri wa Katiba na Sheria Dk.
Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mh.
Goerge Masaju huku Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyamnge
akifurahia kabla ya kuanza kwa hafla ya kuawaapisha Makatibu Wakuu.
Rais Dk. John Pombe Magufuli
akimkabidhi vitendea kazi mara baada ya kumuapisha Amon Mpanju (Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba ikulu leo.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mh. Amon Mpanju (Naibu Katibu Mkuu wizara ya Sheria na Katiba.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mh. James Dotto (Naibu Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango).
Rais Dk. John Pombe Magufuli akumiapisha Dkt. Paulina Pallangyo (Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini)
Rais Dk. John Pombe Magufuli
akimkabidhi vitendea kazi mara baada ya kumuapisha Profesa James Epifani
Mdoe (Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini)
Rais Dk. John Pombe Magufuli akumiapisha Profesa James Epifani Mdoe (Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini).
Rais Dk. John Pombe Magufuli
akimuapisha Immaculate Peter Ngwale kuwa (Naibu Katibu Mkuu)Wizara ya
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Deo Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu – Afya)
Rais Dk. John Pombe Magufuli akumiapisha Dkt. Mpoki Ulisubisya kuwa (Katibu Mkuu – Afya)
Rais Dk John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Laurian Ndumbaro kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
Rais Dk. John Pombe Magufuli
akimkabidhi Vitendea kazi Jaji Meja Jenerali Projest A. Rwegasira mara
baada ya kumuapisha kuwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani.
Jaji Meja Jenerali Projest A. Rwegasira akiapishwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa (Katibu Mkuu) Wizara ya Mambo ya Ndani.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akipiga saluti wakati wimbo wa taifa ulipokuwa ukipigwa .
Kutoka kulia ni Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri
Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa , Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na
Mwanasheria mkuu wa Serikali Mh. George Masaju.
Rais Dk. John Pombe Magufuli
akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano Ikulu tayari kwa kuwaapisha Makatibu
Wakuu na Mnaibu Katibu Wakuu leo, Kulia ni Balozi Ombeni Sefue Katibu
Mkuu Kiongozi.
Waziri wa Sheria na Katiba Mh.
Harrison Mwakyembe akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Majeshi Jenerali
Davis Mwamunyange wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na
Manaibu Katubu wakuu.
WAZIRI MKUU AWAPONGEZA MAKATIBU WAKUU NA NAIBU KATIBU WAKUU
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewapongeza Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu,
mara baada ya kuapishwa Ikulu leo jijini Dar es Salaam.
Ametoa pongezi hizo wakati
Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu wakiwa wametia saini hati ya ahadi
ya uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya waandishi wa habari.
Waziri Mkuu Majaliwa pia amewataka
viongozi hao, kuwa waaminifu, kuwajibika na kutoa taarifa ya utendaji
kwa wananchi. Aidha, alisema kuwa, viongozi wengine watakao apa mbele ya
Kamishna wa Tume ya Maadili ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa
Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri, ikiwa ni hatua ya Serikali
kudhibiti na kufuatilia matumizi ya rasilimali fedha.
“Wakuu wa Wilaya watahakikisha
fedha zilizoenda katika Halmashauri zao lazima zitumike katika shughuli
zilizokusudiwa” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu alitoa wito kwa
watanzania kuendelea kuwa na imani na Serikali ya Awamu ya Tano, kwakuwa
itatimiza ahadi zote ambazo Mheshimiwa Rais na Makamu wa Rais walizitoa
wakati wa Kampeni.
Makatibu Wakuu na Naibu Katibu
Wakuu hao, wameapishwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli, ambapo
shughuli hiyo ilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia
Suluhu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mke wa Mheshimiwa Rais
mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI
S.L.P 3021
1141O DAR ES SALAAM
IJUMAA, JANUARI 1, 2016.
VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUWAOMBEA WATU WABADILI TABIA MBAYA MFANO WIZI, UVUVI NA UZEMBE
Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akipongezana na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye wakati wa mkesha maalum wa
kuombea taifa uliofanyika uwanja wa Taifa usiku wa kuamkia leo.
………………………………………………………………………………………………………..
Na Magreth Kinabo – MAELEZO
Viongozi wa dini nchini
wametakiwa kuwaombea watu wenye nia mbaya na Taifa la Tanzania ili
waweze kuwa raia wema na kuachana na tabia za kutaka rushwa, uvivu,
uzembe na matumizi ya dawa za kulevyia.
Kauli hiyo imetolewa leo na
Mgeni rasmi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli katika maombi maalum ya kuliombea dua
Taifa na viongozi, ambaye ni Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, William Lukuvi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dares
Salaam.
“Tabia hizi zimeota mizizi
zinahitaji maombi. Tunao uwezo wa kumwuunga mkono Rais. Kila mtu anao
mchango wa kumsaidia Rais anayoyafanya mfano katika vijiji kutumbua
majibu madogo,” alisema Lukuvi .
Aliongeza kwamba viongozi hao
wanapaswa kuelimisha jamii jinsi ya kufanya kazi kwa bidii, hivyo
wasiache kusisitiza juu ya suala hilo, likiwemo suala la, amani upendo
umoja na mshikamano.
“ Misingi hii ya, upendo,
umoja na mshikamano ilianzishwa na Serikali zilizopita na Serikali ya
Awamu ya Tano itaendelea kuhimiza juu ya misingi hii, bila ya kujali
dini , rangi, kabila, itikadi na eneo analotoka mtu,” alisisitiza.
Alisema uhuru wa kuabudu utaendelea kuwepo, ila kwa kuzingatia sheria zilizopo.
Aidha Waziri Lukuvi alisema Serikali itaendelea kutoa fursa sawa za kiuchumi na kijamii kwa wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Jumuiya wa Makanisa ya Pentekoste, ambaye pia ni Askofu wa Huduma ya
Tanzania Fellowship Churches (TFC), Askofu Godfrey Malassy alisema
wao kama viongozi wa dini wako pamoja na Rais John Pombe Magufuli, hivyo
hawatamwacha pekee yake katika mapambano hayo hadi Tanzania
itakapokuwa mahali penye neema pa kuishi.
Askofu Malassy aliongeza kwamba ni wajibu wa Watanzania kuomba ili kuweza kuleta mabadiliko katika Taifa letu.
Alisema madhuni ya maombi hayo
ni kumwombea Rais Magufuli aweze kuendelea kuliongoza Taifa ili liweze
kuwa na maendeleo ya ustawi wa watu wote na liendane na kasi ya kauli
mbiu ya ‘Hapa Kazi tu!.
Askofu huyo alisema mauzo ya
kitabu cha ijue siri ya amani na sadaka zitakazotokana na mkesha huo
zitatumika kuelimisha jamii ya ya umuhimu wa amani, kuendelea kutoa
huduma hiyo kwene mikoa ambayo hawajaifikia na kugusa jamii yenye
mahitaji maalum hasa wakina mama na watoto kwa kusaidia kutoa huduma ya
nishati ya umeme.
RAIS MAGUFULI AMJULIA HALI MUADHAMA KADINALI POLYCARP PENGO ANAYEFANYIWA UCHUNGUZI WA AFYA YAKE MUHIMBILI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli
wakimjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es salaam
katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika hospitali ya
Taifa ya Muhimbili leo January 1, 2016. Kardinali Pengo alilazwa
hospitalini hapo jana jioni kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya
yake.
PICHA NA IKULU
MKESHA WA MWAKA MPYA
Mmoja ya wanamaombi akiongoza sala
za maombi katika ibada ya mkesha maalum wa kuliombea dua taifa na
viongozi iliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dares Salaam leo.
Meza kuu akiwemo mgeni rasmi
ambaye alikuwa Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam
Lukuvi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli wakiwa katika maombi maalum ya kuliombea dua taifa
na viongozi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dares Salaam
leo.
Baadhi ya wananchi wakitoa sadaka
kwa ajili ya maombi hayo, ambayo itatumika kusaidia watu wenye mahitaji
maalum ambao wakina mama na watoto na kuendeleza mikesha hiyo.
Bandi ya polisi ikiongoza wibo wa Taifa.
Mama mmoja akiwa na mwanae akiwa katika maombi hayo.
Mgeni rasmi kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika
maombi maalum ya kuliombea dua taifa na viongozi Waziri Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (katikati) yaliyofanyika kwenye
Uwanja wa Uhuru jijini Dares Salaam leo akipeana mkono wa heri ya
kuingia mwaka mpya wa 2016 na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nnauye .
(Picha zote na Magreth Kinabo – Maelezo)
BONANZA LA MAZOEZI YA VIUNGO KITAIFA-LAFANA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza Matembezi
ya wanamichezo katika Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika
leo kwa kuwanzia Uwanja wa Tumbaku Mjini Unguja na kumalizia Uwanja wa
Amaan Studium.
[Picha zote na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza Matembezi
ya wanamichezo katika Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika
leo kwa kuwanzia Uwanja wa Tumbaku Mjini Unguja na kumalizia Uwanja wa
Amaan Studium.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanamichezo
wa Vikundi mbali mbali kama ishara ya kuyapokea maandamano ya vikundi
hivyo katika kilele cha Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa
lililofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Wamamichezo wa Vikundi vya mazoezi
wakipita mbele ya jukwaa kubwa Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja
katika kilele cha Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika leo
ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Wamamichezo wa Vikundi vya mazoezi
wakipita mbele ya jukwaa kubwa Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja
katika kilele cha matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa
yaliyofanyika leo ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Wanakikundi cha Amakweli Fitness
Club ya Welezo Grinada wakibeba bango la Chama cha Mchezo wa Maziezi ya
Vuingo Zanzibar (ZABESA) linalosema “JIKINGE DHIDI YA MARADHI YA
KISUKARI PRESHA NA SARATANI KWA KUFANYA MAZOEZI”wakipita mbele ya mgeni
rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi ya Bonanza la
mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium
Mjini Unguja.
Kikundi cha Mazoezi Mwera Fitness Club kikipita mbele ya mgeni rasmi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi wakati wa Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi wakati wa Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Kikundi cha Mazoezi Chumbuni Studio kikipita mbele ya mgeni rasmi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi wakati wa Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi wakati wa Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Kikundi cha Mazoezi kutoka
Kisiwani Pemba kikipita mbele mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
alipoyapokea matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa
lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Kikundi kutoka Dar es Salaam ni
miongoni mwa vikundi vilivyojumuika katika matembezi ya Bonanza la
mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium
Mjini Unguja ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Kikundi kutoka Dar es Salaam ni
miongoni mwa vikundi vilivyojumuika katika matembezi ya Bonanza la
mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium
Mjini Unguja ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Miongoni mwa Vikundi vya Mazoezi
hapa Mjini Unguja nacho kikionesha manjonjo ya aina ya mazoezi mbele ya
mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Mohamed Shein (hayupo pichani) katika kilele cha Bonanza la mazoezi ya
viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguj.
MKESHA WA MWAKA MPYA WAFANA DAR
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Wiliam Lukuvi kwa
niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe
Magufuli, akihutubia kwenye Mkesha Mkubwa Kitaifa,Dua Maalum ya
kuwaombea viongozi na Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini
Dar es salaam.
Mchungaji
Eden Godfrey akihubiri kwenye Mkesha Mkubwa Kitaifa, Dua maalum
uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Umati wa wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwenye ibada
maalum ya mkesha wa mwaka mpya uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.
Wananchi wakiwa kwenye maombi ya kuliombea Taifa Amani, na kuwaombea viongozi wake afya njema.
Mwalimu Teddy Kwilasa akitoa maombi maalum kwa Taifa kwenye mkesha wa mwaka mpya.
Wananchi wakiwa kwenye maombi mazito ya kuwaombea Viongozi wa Taifa letu
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (wa pili
kulia) akiwa pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Nnauye pamoja na wake zao wakiupokea mwaka kwenye Mkesha
Mkubwa Kitaifa, ambapo Taifa na Viongozi wake waliombewa.
Sehemu ya Vijana waliojitokeza kwenye mkesha mkubwa uliofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitoa salaam
maalum za kuwataka wazazi kuwafundisha watoto wao umuhimu wa amani ya
nchi wakati wa mkesha wa mkubwa kitaifa wa kuombea Taifa na Viongozi
wake dua maalum.
Bi. Christina Elias wa Aleluyah kwaya kutoka Tabata akiimba kwa hisia
kwenye mkesha mkubwa wa kitaifa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es
Salaam.
Viongozi wakiwa kwenye maombi maalum ambapo waliwakilisha Mawaziri wote nchini.
SALAMU YA MWAKA MPYA, 2016
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.
……………………………………………………………..
KAMANDA WA POLISI MKOA KAMISHNA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED ZAHORO MSANGI, ANAWATAKIA KHERI YA
MWAKA MPYA 2016 WAANDISHI WOTE WA HABARI. “NINASHUKURU KWA USHIRIKIANO
WENU KWA KIPINDI CHA MWAKA 2015 NA KUOMBA USHIRIKIANO ZAIDI KWA MWAKA
2016.
“TUSHEREHEKEE MWAKA MPYA, 2016 KWA AMANI NA UTULIVU” TUKUMBUKE “ULINZI NA USALAMA SIKU ZOTE UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”
AHASANTENI!!!
MWENYEKITI WA BODABODA MKOA WA MWANZA AWAOMBA RADHI WATANZANIA
Na”George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mwenyekiti wa Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoa wa Mwanza Makoye Kayanda Bunoro anawatakia Waendesha Pikipiki wote nchini Kheri ya Mwaka Mpya 2016 huku akiwasihi kutimiza majukumu yao kwa kufuata sheria na taratibu za Usalama barabarani bila shuruti.
Mwenyekiti wa Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoa wa Mwanza Makoye Kayanda Bunoro anawatakia Waendesha Pikipiki wote nchini Kheri ya Mwaka Mpya 2016 huku akiwasihi kutimiza majukumu yao kwa kufuata sheria na taratibu za Usalama barabarani bila shuruti.
“Tuache
Mchezo na Vyombo vya Moto, Tuvae Elmenti, tusibebe mishkaki (zaidi ya
abiria mmoja) tusiendeshe kwa mwendo kasi kwani ni hatari, tusitumie
pombe tukiwa kazini huku tikiwapenda abiria na kujiepusha na vitendo vya
uhalifu vya aina yoyote”. Anasema Bunoro.
Aidha
Bunoro amewaomba radhi wale wote waliopata usumbufu kwa namna moja ama
nyingine kutokana na kazi ya bodaboda na kwamba kusameheana ndilo jambo
la msingi huku akiwakumbusha bodaboda kujipanga katika majukumu yao ili
kuendana na kasi ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli ya “Hapa Kazi Tu”.
Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi
Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi
MATUKIO MAKUBWA YA MUZIKI WA DANSI NCHINI KWA MWAKA 2015
Tarehe 31-Jan-2015, BMM Classic Band, ilizinduliwa katika ukumbi wa BMM Mwenge, opposite TRA.
- Tarehe 21-Feb-2015, JJ Band yazinduliwa katika ukumbi wa. JJ Band ni bendi dada ya Skylight Band itakayokuwa inatumbuiza mjini Mwanza katika hotel ya Jembe ni Jembe Resort.
- Tarehe 06-Mar-2015 (Ijumaa), Ruby Band ilitambulishwa rasmi katika ukumbi wa Coco Beach Pub ambapo pia ilizindua video ya wimbo mpya wa “Noma”.
- Tarehe 18-Jul-2015 (Jumamosi), Stars Band yazinduliwa katika ukumbi wa Mzalendo Pub. Bendi hiyo inaongozwa na mwanamuziki Aneth Kushaba aka “AK47” aliyekuwa Skylight Band. Meneja wa bendi ni mpiga drums James Kibosho. Bendi hii inaundwa pia na mpiga solo Alain Kisomundele na Mao Santiago aliyekuwa Machozi Band.
- Dec-2015, bendi mpya itakayojumuisha Mule Mule FBI, Totoo Ze Bingwa, Alain Mulumba Kashama, Montana Amarula na Didi “Number” Kayembe (Numero) aka “Dume la Mende” ipo katika maandalizi ya kuundwa na kuzinduliwa huku Mule Mule FBI akiwa rais (prezidaa) wa bendi hiyo huku Losso Mukenga, mpiga solo wa Ally Kiba, akiipigia pia bendi hiyo.
UZINDUZI WA ALBUM MPYA
- Tarehe 27-Dec-2015, Milimani Park Orchestra “Sikinde-Ngoma ya Ukae”, ndani ya TCC Chang’ombe, yazindua album ya “Jinamizi la Talaka” sambamba na kufanya sherehe za miaka 37 tokea bendi ianzishwe mwaka 1978
KILI MUSIC AWARD
- Tarehe 23-Mar-2015, Kililimanjaro Music Award 2015 yazinduliwa rasmi
- Tarehe 25-Apr-2015, Academy ya Kili Music Award yakutana kuchagua majina ya washiriki wa kila kipengele.
- Tarehe 29-Apr-2015, majina ya washiriki wa kila kipengele yatangazwa rasmi
- Tarehe 13-Jun-2015 (Jumamosi), sherehe za washindi wa Kili
Music Award 2015 zilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City. Kulikuwa na
jumla ya vipengele (categories) 6 vya muziki wa dansi. Washindi walikuwa
kama ifuatavyo;
1. Bendi Bora ya Mwaka- FM Academia
- Mtunzi Bora wa Mwaka Bendi-Jose Mara (Mapacha Watatu)
- Rapa Bora wa Mwaka Bendi- Fergusson (Mashujaa Band)
- Wimbo wa Kiswahili Bendi- ”Wale Wale” (Vijana Ngwasuma)
- Mwimbaji Bora wa Kiume Bendi- Jose Mara (Mapacha Watatu)
- Mtayarishaji Bora wa Nyimbo Bendi-Amoroso Sound
No comments:
Post a Comment