Pages

Sunday, November 22, 2015

VITANDA VYA MAGUFULI VYAWASILI HOSPITALI YA MUHIMBILI “HAPA KAZI TU”


MS1

Gari la mizigo la MSD likipakia vitanda hivyo na magodoro kwa ajili ya kupeleka kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo.
ms2 
Baadhi ya vitanda vikifungwa.
ms3index

NAIBU WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AWAANDALIA CHAKULA MADAKTARI KUTOKA HISPANIA

D1
Profesa Jose Pinquet kulia akitambulisha Timu ya Madaktari wanaotoa huduma za Matibabu ya Uti wa Mgongo na Ubongo katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja kwa Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo.
D2
Baadhi ya Madaktari wanaotoa huduma za Matibabu ya Uti wa Mgongo na Ubongo katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja wakipata Cahakula cha Usiku kilichoandaliwa ni Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo.
D3
Profesa Jose Pinquet akizungumza mara baada ya Chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili yao ambapo pia alishukuru mashirikiano wanayopewa na Madaktari Wazawa katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Ocean View.
D4
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Madaktari wa kujitolea kutoka Hispatinia mara baada ya Chakula cha usiku alichowaandalia kwa lengo la kuwashukuru kutokana na mchango wao mkubwa wanaoutoa katika sekta ya Afya Zanzibar, hafla hiyo ilifanyika Hoteli ya Ocean View.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

WANAHABARI WASISITIZWA KUFUATA SHERIA ZA HABARI ZIZLIZOPO HUKU TAASISI ZAKIHABARI ZIKIFUATILIA KUPATIKANA SHERIA BORA

c1
Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Dkt. Aboubakar Rajab akitoa hutuba ya ufunguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Ally Mwinyikai katika Mkutano Mkuu wa Wadau wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar ambapo alisitiza wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao. Kulia ni Katibu wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande Omar na kushoto ni Mwenyekiti wa ZPC Abdallah Mfaume.
c2
Katibu wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande akitoa Mada ya umuhimu wa kuzingatia Maadili kwa Wanahabari katika fani yao.
c3
Makamu wa Rais wa Chama cha Siasa ADA-TADEA akichangia katika Mkutano wa Wadau wa Mkutano wa Wadau wa ZPC uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar.
c4
Mkulima kutoka kikundi cha Ushirika cha Bambi Mwaka Saburi akichangia katika Mkutano wa Wadau wa ZPC uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar ambapo alishauri Wanahabari kuandika zaidi habari za Vijijini bada ya mijini pekee.
c5
Katibu wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) Faki Mjaka akisoma maazimio ya Mkutano wa Wadau wa ZPC uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar.
c6
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Zanzibar Press Club ZPC wakiwa katika Picha ya pamoja na Mgeni rasmi wa Mkutano huo Dkt. Aboubakar Rajab wakatikati waliokaa huko Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar 
…………………………………………………………………………………………
Na Maelezo Zanzibar
Wanahabari wametakiwa kuendelea kutii Sheria zilizopo zinazoongoza mwenendo wa utoaji wa habari nchini, huku Taasisi za kihabari zikiendelea kufuatilia upatikanaji wa sheria Bora za habari zinazoendana na wakati uliopo.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande Omar alipokuwa akiwasilisha Mada katika Mkutano Mkuu wa Wadau wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar ZPC uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar.
Amesema licha ya kuwepo kwa baadhi ya Sheria za habari zilizopitwa na wakati, ni vyema Wanahabari kuziheshimu na kuzitii huku juhudi mbalimbali zikifanywa na Wadau kuondoa Sheria hizo.
Chande amefahamisha kuwa Taasisi kama Vile Baraza la Habari Tanzania, Tume ya Utangazaji na Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar ZPC ni miongoni mwa Taasisi ambazo zinafanya kazi za kuwepo kwa Sheria zinaendana na wakati kwa maslahi mapana ya Taifa.
Aidha katika Mkutano huo uliojumuisha Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi maazimio mbalimbali yalipitishwa ikiwemo Wamiliki wa Vyombo vya Habari na Waaandishi kwa ujumla kuzingatia Weledi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Azimio jingine ni kuhakikisha kuwa Taasisi kama Vile Baraza la Habari Tanzania, Tume ya Utangazaji na Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar ZPC zinashiriki kikamilifu katika kuhamasisha upatikanaji wa Maslahi bora kwa Wanahabari ili kuwaepusha kupokea Zawadi kutoka Vyanzo vya habari ambazo hupelekea kukiuka maadili yao.
Aidha wameazimia kujiepusha na Ushabiki wa Kisiasa ili kuepuka upendeleo wa habari wanazojitoa kwa jamii.
Mmoja wa Wachangiaji kutoka Jumuiya ya Wakulima Mpwapwa amewaomba Waandishi wa habari kuandika pia habari za watu wa shamba badala ya kuandika habari zinazohusu watu wa mijini pekee.
Ametoa mfano kwamba katika uchaguzi Mkuu uliopita habari zilizoandikwa zilihusu Watu wa Mijini ambapo kwa  upande wa Vijijini Waandishi walishindwa kuonekana kwenda kuchukua habari.
Hata hivyo Washiriki wa Mkutano huo pia Waliafiki wazo hilo na kuazimia kufanya kazi kizalendo na kushirikisha makundi yote ya kijamii ikiwemo kuandika habari za Vijijini ili kuibua Fursa na changamoto zinazowakabili.
Akitoa hutuba ya Ufunguzi Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Dkt. Aboubakar Rajab kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Ally Mwinyikai alisisitiza wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao ili waheshimike katika jamii.
Amesema kukosekana kwa Maadili ya Habari hupelekea Migogoro mingi ikiwemo kuzalisha chuki na fitna miongoni mwa jamii husika.
Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar hufanya Mkutano Mkuu wa Wadau wake kila mwaka na kujadili mada kulingana na wakati husika ambapo katika Mkutano huo Walijadili umuhimu wa Waandishi kuzingatia Maadili katika kupatikana uchaguzi huru na Wahaki.

PICHA ZA KUMBUKUMBU BAADA YA RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KUZINDUA BUNGE DODOMA

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wabunge muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Spika Mstaafu Mhe Pius Msekwa huku Spika Mstaafu mwingine Mhe Anne Makinda akisubiri zamu yake muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na mmoja wa wabunge muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 201
6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Benjamin William Mkapa  muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi wakuu na wabunge muda  mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisikiliza kwa unyenyekevu mawaidha toka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein,  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe  Pandu Ameir Kificho  muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa wakijichanganya na wabunge kwenye mchapalo muda  mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Mhe Zitto Kabwe muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Mhe Anthony Diallo muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
14
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na  wabunge na wageni waalikwa kwenye mchapalo  muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015. Ni hapo alipoamuru kwamba zaidi ya shilingi milioni 200 zilizochangwa na wafadhili kwa ajili ya mchapalo huo zitumike kwa kununulia vitanda vya wagonja katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
17
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru Spika Job Ndugai  wakati anaondoka baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015. 
18
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru na kumkabidhi cheti Mkurugenzi Mkuu wa PSPF  Bw.Adam Mayingu kwa mchango wao  kwenye mchapalo  muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015. 
19
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru na kumkabidhi cheti mwakilishi wa Benki kwa mchango wao  kwenye mchapalo  muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015. 
21
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipozi na badhi ya mabalozi wa nchi za Kiafrika waliokaribishwa kwenye hafla ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015. 
Picha na Muhidin Issa Michuzi wa Ikulu

MABONDIA TAMBA NA MWAKANSOPE KUPIGANA KESHO JUMAPILI MANZESE

Mabondia Ibrahimu Tamba kushoto akitunishiana misuli nas Baraka Mwakansope baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa utakaofanyika manzese frends corner siku ya jumapili . picha na SUPER D BOXING NEWS
……………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Ibrahimu Tamba wa Dar es salaam na Baraka Mwakansope wa Mbeya wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa kg 72 utakaofanyika katika ukumbi wa frends corner manzese mpambano uho wa raundi kumi utanza saa kumi za jioni
wakisindikizwa na mabondia mbalimbali ambapo bondia Pius Kazaula wa Morogoro atapambana na  Chisora Mawe na Vicent Mbilinyi atapambana na Said Tompoo wa Bagamoyo
na Julius Kisarawe atapambana na Ramadhani Kumbele mpambano wa ubingwa kg 51
na Mfaume Mfaume atamenyana na Mrisho Adam katika mpambano kg 63 raundi nne
Mohamed Kashinde atakabiliana na Twawabu Issa na Iddi Kayumba atamenyana na Manny Issa
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul ‘canelo’ alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila ‘Super D’ kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Dk.Ali Mohamed Shein ATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO MJINI UNGUJA

XX1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa  Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd,Mussa Awesu Bakari wakati alipokuwa akiangalia ramani ya Mradi wa ujenzi wa Ukuta wa Forodhani Mjini Unguja leo akiwa katika ziara maalum ya kutembelea maendeleo ya Miradi mbali mbali Mjini,
[Picha na Ikulu.]
XX2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimuuliza suala Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd,Mussa Awesu Bakari wakati alipokuwa akiangalia   Mradi wa ujenzi wa Ukuta wa Forodhani Mjini Unguja leo akiwa katika ziara maalum ya kutembelea maendeleo ya Miradi mbali mbali Mjini,
XX3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo ya ramani ya ujenzi wa Mtaro wa maji ya Mvua katika viwanja wa mnazi mmoja kutoka kwa Mhandisi wa Manispaa ya Zanzibar Mzee Khamis Juma wakati alipotembelea mradi huo wa ujenzi unaojengwa na kampuni ya CRJ kutokaChina,
XX4 XX5

WAZIRI MKUU MAJALIWA KWENYE HAFLA FUPI YA KUZINDUA BUNGE

X1 X2
Waziri  Mkuu,   Majaliwa Kassim Majaliwa  akizungumza na  Mke wa Rais Mstaafu wa  Awamu ya Nnne , Mama Salma Kikwete katika hafla fupi  iliyoyofanyika kwenye viwanja vya Bunge mjiniDodoma  baada ya Rais John Magufuli kuzindua Bunge Novemba 2015.
X3
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Kassim  wakizungumza na baadhi ya wabunge  na waalikwa waliohudhuria hafla fupi  iliyofanyika kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma  baada ya Rais John Magufuli kuzindua Bunge Novemba  20, 2015.
X4
Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na mbunge wa Mufindi, Cosato Chumi katika hafla  fupi ya kuzindua bunge iliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Novemba 20, 2015. Katkati ni Mbunge wa ROrya Lameck Airo.
X5
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na  Spika wa Bunge Job Ndugai (kushoto) , Mkewe Mary  (wapili kushoto) na  Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila  (wapili kulia) katika hafla ya  kuzindua Bunge iliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 20, 2015.
(Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)

HAFLA BAADA YA RAIS KULIHUTUBIA BUNGE MJINI DODOMA JANA

01
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Sophia Simba kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma, wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015.
02
Waziri Mkuu wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, akizungumza jambo na Rais staafu wa awamu ya sita wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
03
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
04
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
05
Rais Magufuli (katikati) akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar, Mohamed Ali Shein (kushoto) na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
06
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mbunge wa Shinyanga mjini, Stephen Masele, wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
07
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
08
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na mmoja kati ya wageni waalikwa wa Kimataifa, wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
09
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Vijana wa UVCCM, wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
010
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa, Spika wa Bunge, Job Ndugai na Katibu wake, baada ya hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Picha na OMR

No comments:

Post a Comment