Pages

Tuesday, November 24, 2015

MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA UONGOZI WA MTANDAO WA WANAWAKE TANZANIA.


MAK1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Uongozi wa Mtandao wa Wanawake Tanzania (WFT) wakati viongozi hao walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Nov 24, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR
MAK2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea baadhi ya Vipeperushi na Vitabu vya Mtandano wa Wanawake Tanzania (WFT) kutoka kwa mwenyekiti wa mtandao huo, Prof.Ruth Meena, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dares Salaam, leo Nov 24, 2015. Picha na OMR
MAK3 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mtandao wa Wanawake Tanzania (WFT) baada ya mazungumzo yao yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dares Salaam, leo Nov 24, 2015. Picha na OMR
……………………………………………………………………………………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na uongozi wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania (WFT) ambapo amezungumzia dhamira ya serikali katika kuyatafutia ufumbuzi matatizo mbali mbali yanayowakabili wanawake na watoto wa kike nchini.
Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais aliueleza ujumbe huo kuwa wakati wa kampeni aliahidi pamoja na kazi za kumsaidia Mhe. Rais bado kama mama atafuatilia kwa karibu utekelezaji wa ahadi ya kupatikana kwa maji safi na salama, kuboresha afya ya mama na mtoto, elimu na mazingira.
“Nilipokuwa kwenye kampeni nimejionea shida ya maji na wanawake ndiyo wanaopata tabu ya kutembea mwendo mrefu kutafuta maji. Kwa hiyo, pamoja na kazi zangu za kumsaidia Mhe. Rais nitasimamia miradi yote ya maji, alau tuhakikishe maji yanapatikana umbali wa mita 400 kutoka eneo wananchi wanakoishi au karibu zaidi”.
Alisema kinachofurahisha zaidi suala la maji liko kwenye Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na miradi mingi ikiwemo ya kuchimba visima virefu katika mikoa kama vile ya Singida na Dodoma iko kwenye mchakato na cha msingi ni kusimamia fedha zinatumika kuleta maji kama ilivyokusudiwa.
Kuhusu afya ya mama na mtoto alisema kazi hiyo ataianza hivi karibuni kwa kushirikiana na Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea haki za wanawake ili kupunguza vifo vinavyosababishwa na mimba za utotoni.
“Hili tutajitahidi kulipunguza kwa kiasi kikubwa na hasa baada ya serikali ya Awamu ya Nne kusema kwamba shule ya msingi ya lazima ni kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne”, alisema na kuongeza
“Katika kipindi hicho binti atakuwa amefikisha miaka 17, atakuwa tayari kukabiliana na mambo ya uzazi tofauti na ilivyo sasa ambapo anamaliza darasa la akiwa mdogo na matokeo yake anapata mimba katika umri mdogo. Mtusaidie kupiga debe huko nje utekelezaji uweze kufanikiwa.”
Hata hivyo, alisisitiza kusimamia suala la kuhakikisha zahanati, vituo vya afya na hospitali nchini zinakuwa na dawa na vifaa tiba vya kutosha katika wodi za wazazi kwa ajili ya kuhudumia akina mama na wananchi kwa ujumla ambao wengi wanaonekana ni watiifu kwa serikali yao.
Kwa upande wa elimu Mhe. Samia alisema atasimamia ujenzi wa mabweni kwa watoto wa kike na kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwa sababu uharibifu wa mazingira ndiyo umekuwa chanzo cha upungufu wa maji nchini.
Aidha aliuambia ujumbe huo kuwa hivi sasa tuna mpango wa kuimarisha utendaji serikalini kuanzia serikali kuu hadi serikali za mitaa ili kinachopatikana kidogo kimfikie kila mwananchi.
“Tutaendelea kuaihirisha sherehe ili fedha hizo ziweze kutumika kwa mambo ya kijamii. Kwa msimamo huu amabao Mhe. Rais ameanza nao labda watu wote tushirikiane kwa kutatua matatizo yetu kwa gharama nafuu kwa ufanisi mkubwa.”
Mapema akizungumza kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa Mtandao huo Prof Ruth Meena alimpongeza Mhe. Samia kwa kushika nafasi ya juu ya uongozi akiwa mwanamke wa kwanza kuweka historia katika Tanzania.
Alimweleza Mhe. Makamu wa Rais matarajio yao kwa serikali ya Awamu ya Tano kuwa itatetea misingi ya haki na usawa katika Nyanja zote.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam

Tamisemi yampongeza Waziri Mkuu

index2 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na baadhi ya vingozi na watendaji wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) alipotembelea Wizara hiyo kwa lengo la kuongea viongozi hao kuhusu utendaji kazi wenye tija kwa wananchi leo jijini Dar es salaam.
index1 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) akitoa taarifa fupi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa alipotembelea Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………….
Na Shamimu Nyaki-Maelezo
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imempongeza Mhe. Majaliwa Kassimu Majaliwa kwa kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Kumi na Mmoja wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na kuahidi kushirikiana naye kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yake.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa (TAMISEMI),Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Jumanne Sagini amewaagiza watumishi katika wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia maadili ya kazi pamoja na kujiepusha na tabia ya uzembe, uvivu na wizi katika maeneo yao ya kazi.
Katika halfa hiyo iliyofanyika kwenye, Ofisi za TAMISEMI amewasilisha majukumu ya ofisi na muundo uliopo katika ofisi ikiwa ni pamoja na idara na taasisi zilizopo katika wizara hiyo zitakazo kuwa chini ya Waziri Mkuu huyo.
Aidha TAMISEMI imemuhakikishia Waziri Mkuu kuwa itafanya naye kazi kwa kasi kubwa kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo katika ofisi hiyo ili kuleta mafanikio chanya ndani ya Serikali kwakuwa wizara hiyo ndio inayoshughulikia kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa sera za maendeleo kwa wananchi.
Akizungumzia kuhusu hotuba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa Bungeni hivi karibuni, Katibu Mkuu huyo amewaambia waandishi wa habari kuwa watasimamia na kutekeleza yote yalioainishwa na Mhe. Rais hasa kuhusu suala la elimu ya sekondari na msingi kwakuwa wao ndio watendaji na wasimamizi katika sekta ya hiyo.
Hata hivyo ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinasimamia ujenzi wa nyumba za waalimu,madarasa pamoja na maabara kwakuwa wao ndio wenye mamlaka ya kusimamia suala hilo katika utekelezaji wake.
“Wakurugenzi wa halmashauri wao ndio watekelezaji wakuu wa katika kusimamia ujenzi wa madarasa,nyumba za waalimu zenye heshima kwa waalimu”alisema Katibu Mkuu Sagini.
Aliongeza kuwa ushirikiano miongoni mwa wanyafakazi katika ofisi hiyo utamuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa urahisi na kasi kubwa katika kuwatumikia wananchi wa Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MADAI YA WAKULIMA WADOGO WA MIWA WA KILOMBERO KUKOSA SOKO

images 
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bibi Sophia Kaduma ameiagiza Bodi ya Sukari Tanzania, kushughulikia mara moja madai ya wakulima wadogo wa miwa (outgrowers) katika Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kilichopo Mkoani Morogoro yaliotokana na miwa yao kutonunuliwa na kiwanda.
Katika agizo hilo, Katibu Mkuu Bibi Sophia Kaduma ameiagiza Bodi ya Sukari Tanzania kukuta na Uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero na ule wa wakulima wadogo wa miwa ili kupata ufumbuzi wa kudumu kuhusu soko la miwa wanayozalisha.
Aidha, Katibu Mkuu ametoa muda wa siku saba kwa Bodi ya Sukari Tanzania iwe imetekeleza na kutoa taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo.
Agizo hilo limekuja kufuatia Serikali kupata taarifa kuwa Uongozi wa Kiwanda hicho umeshindwa kununua miwa ya wakulima hao licha ya makubaliano yao ya awali ya kuzalisha miwa na kukiuzia kiwanda kwa ajili ya kuzalisha sukari. Wakulima wamedai kuwa miwa hiyo, inakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16.
Bodi ya Sukari Tanzania imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Sukari Na. 26 ya mwaka 2001 kama ilivyorekebishwa mwaka 2009 na Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Mazao Na. 20 ya mwaka 2009 (Crop Laws (Miscellenous Amendments) Act).
Bodi ya Sukari Tanzania inajukumu pamoja na mambo mengine, kusimamia na kuratibu kilimo cha miwa na biashara ya sukari nchini, kusajili wakulima, wazalishaji wa sukari na wafanyabiashara wa sukari.
Aidha, Bodi ya Sukari ina dhamana ya kuhakikisha uwepo wa ushindani wa haki kwenye soko la miwa na biashara ya sukari nchini.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika
Kilimo Complex,
1 Mtaa wa Kilimo 15471
DAR ES SALAAM.

TIGO Teams up with UNICEF, Champions Innovations for Tanzania’s Children

index
Tigo, under Millicom International Cellular (MIC) Tanzania Limited, has offered to support the children of Tanzania through four projects initiated and supported by UNICEF Tanzania.
From 2016 – 2018, financial and in-kind contributions worth about TZS $ 354,625,172 (USD $165,000) will be used to support the Under Five Birth Registration Initiative, the National Child Helpline, the ‘Tupime Watoto’ (HIV testing of children) initiative and UNICEF Tanzania’s Innovations Lab.
While signing the memorandum of understanding and handing over of contributions from TIGO to UNICEF, General Manager of Tigo, Mr. Diego Gutierrez said: “Our company is committed to helping children, families and communities in Tanzania. Through this initiative Tigo clearly demonstrates its Corporate Responsibility commitment of mobilizing community through the use of digital solutions. We are proud to be partnering with UNICEF and we will continue to work with UNICEF on other innovative and exciting projects to reach the most vulnerable children.”
While thanking Tigo, UNICEF Tanzania’s Representative, Dr. Jama Gulaid said: “This is not the first time Tigo has shown its commitment to improve the lives of the most disadvantaged. In the past two years, we have worked with Tigo and the Registration Insolvency & Trusteeship Agency (RITA) on an innovative campaign that helps children get birth certificates with minimum hassles.”
“The success of the birth certificate initiative in Mbeya inspired similar action in Mwanza Region. I commend Tigo for its readiness to engage in a public and private sector partnership for children in Tanzania” Dr. Gulaid added.
A name and nationality is every child’s right, enshrined in the Convention on the Rights of the Child. In Tanzania where only one in five children under the age of five is registered at birth, we have much work to do together – the government, private sector, communities and development partners”.
The Mobile birth registration (mBirth) is a tool that can help us. It is simple, affordable and accessible to many in Tanzania. The mBirth project has already been established in two regions – Mbeya and Mwanza – through funding donated by Canada through UNICEF and with assistance from Tigo, RITA and other partners.
The ‘Tupime Watoto’ project aims to expand HIV testing for children in Tanzania using mobile technology. The National Child Helpline was launched in 2013, with the aim to provide a response to child victims of violence and help them to access services. With Tigo’s support, UNICEF will be able to upgrade the National Child Helpline’s call centre to help in providing effective and timely responses to callers and improved access to services.

Mafundi wazishugulikia mashine za MRI na CT-SCAN Muhimbili.

images 
Na Raymond Mushumbusi -Maelezo
 
Mafundi kutoka kampuni ya Philips wanaendelea na matengenezo ya mashine za MRI na CT-SCAN katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zilizopata hitilafu za kiufundi hivi karibuni.
Akizungumza ofisini kwake leo hii Mkuu wa Idara ya Uhusiano Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Aminiel Buberwa Aligaesha amesema mafundi wapo katika eneo la kazi wakitengeneza hizo mashine ili ziweze kurudi katika hali yake ya kawaida.
“Tumepewa siku tatu kukamilisha ukarabati wa hizi mashine hivyo wananchi wawe na subira kwani mashine zikiwa tayari kwa matumizi tutatoa  taarifa” alisema Aligaesha.
Ameongeza kuwa wananchi wawape muda waweze kuzitengeneza mashine hizo ili ziweze kutengemaa kwa ajili ya kutoa huduma za MRI na CT-SCAN hospitalini hapo.
Mashine za MRI na CT-SCAN zilianza kufanya kazi  mara baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli kutembelea hospitali hiyo hivi karibuni na kuagiza kutengenezwa kwa mashine hizo na baadae kufanya kazi kwa muda wa siku kadhaa na kuharibika tena kutoka na hitilafu za kiufundi.
Wakati alipotembelea Hospital ya Taifa ya Muhimbili jana Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue aliagiza mashine hizo kutengenezwa,  ndani ya siku tatu  ziwe zimekamilika kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imekuwa ni kimbilio la wananchi wengi kupata huduma za afya hivyo serikali inapamabana kwa kila hali kuhakikisha huduma za MRI na CT-SCAN zinarudi katika hali yake ya kawaida hospitalini hapo.

CAF YAENDESHA SEMINA YA LESENI ZA VILABU

caflicence
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Yahya Mohamed leo amefungua semina ya mafunzo ya leseni za vilabu katika ukumbi wa mikutano wa Dar es salaam International Conference Centre (DICC) uliopo jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Yahya amesema imekua jambo jema kwa CAF kutupatia nafasi ya mafunzo ya leseni za vilabu hapa nyumbani, kwani viongozi wa vilabu wote wanapata nafasi ya kushiriki semina hii ya siku mbili kutoka kwa wakufunzui wa CAF.
“Uendeshaji wa mpira wa miguu duniani umebadilika, mabadiliko haya yapo katika nyanja zote za uongozi (utawala), miundombinu, kitu ambacho kwa sisi Tanania tumeshaanza kuendana na mabadiliko hayo, na sasa kupata kwetu semina hii kutawafanya viongozi wengi kufahamu umuhimu wa leseni za vilabu na kufanyia kazi mapungufu yaliyokuwepo” alisema Yahya.
Semina hiyo ya Leseni kwa Vilabu itakayofanyika kwa siku mbili inaedeshwa na wakufunzi watatu kutoka CAF ambao ni Dr. Bolaji Ojo Oba (Nigeria), Amanze Uchegbulanm (Nigeria) na Othman Mohamed kutoka nchini Sudan.
Agizo la CAF ni kuwa kila klabu inayoshiriki michuano ya kimataifa (Ligi ya Mabingwa, Kombe l Shirikisho) lazima iwe imepata leseni hiyo ambayo itaipa nafasi ya kushiriki michuano inayoandaliwa na CAF, na kwa klabu ambayo haitatimiza mahitaji ya kupata leseni hiyo haitaweza kushiriki michuano ya kimataifa.
Ili kupata leseni ya klabu, klabu inapaswa kutimiza vigezo vilvyowekwa ikiwemo masuala ya utawala, ripoti ya mapato na matumizi iliyokaguliwa, uwanja wa mazoezi nk.
Mmiliki mmoja wa klabu hatarusiwa kumiliki timu zaidi ya moja kwenye ligi moja, kila klabu lazima iwe na program za vijana na uwanja wa mazoezi.

Upendo Nkone naye achomoza Tamasha la Shukrani

maxresdefault 
MWIMBAJI maarufu wa muziki wa Injili Tanzania, Upendo Nkone naye amejitokeza kuwa mmoja wa waimbaji watakaofikisha ujumbe wa Shukrani kwa Mungu katika Sikukuu ya Krismasi kupitia tamasha linalotarajia kufanyika Desemba 25 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Kamati imefanikisha makubaliano na mwimbaji huyo.
Msama alisema Nkone anaungana na wenzake Rose Muhando, Ephraim Sekeleti sambamba na Kwaya ya Wakorintho wa pili.
“Kabla ya kukubaliana na Nkone, tulikuwa tumeshamalizana na wenzake Rose Muhando, Ephraim Sekeleti ambaye ni raia wa Zambia sambamba na Kwaya ya Wakorintho wa Pili yenye maskani yake Mafinga mkoani Iringa, bado tunaendelea na mawasiliano na waimbaji wengine ili kunogesha tamasha hilo lenye malengo mawili ambayo ni Shukrani kwa Mungu sambamba na Sherehe za kuzaliwa Masiha, Yesu Kristo,” alisema Msama.
Aidha Msama alisema Kamati yake imepanga kufikisha shukrani kwa Mungu kupitia waimbaji na viongozi wa dini na wa kada mbalimbali kama ilivyokuwa kwenye Tamasha la Kuombea Amani lililofanyika Oktoba 4 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambako mgeni rasmi alikuwa ni mke wa rais wa awamu ya nne, Salma Kikwete.
“Oktoba 4, tuliandaa Tamasha la kumbea amani uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 uwanja wa Taifa, hivyo ni nafasi yetu kumshukuru Mungu baaada ya kupitisha Tanzania kwenye uchaguzi ambao ulikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani,” alisema Msama.

CHAVITA YASIKITISHWA NA USHIRIKI MDOGO WA VIZIWI KATIKA UCHAGUZI MKUU

CH1
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA), Bw. Dickson Mveyange (kulia) akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu tathmini ya ushiriki wa Viziwi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Taifa Tanzania Bara uliofanyika 25 Oktoba, 2015. Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam 24 Novemba, 2015.
CHA2
Baadhi ya Waandishi wa Habari toka Vyombo mbalimbali wakifuatilia taarifa toka kwa Viongozi wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kuhusu tathmini ya ushiriki wa Viziwi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Taifa Tanzania Bara uliofanyika 25 Oktoba, 2015. Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam 24 Novemba, 2015.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)
……………………………………………………………………………………………………..
Na Zawadi Msalla
 
Chama Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA)   kimeeleza masikitiko yao juu ya ushiriki mbovu wa Viziwi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba  kote nchini.
 
Akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Habari-MAELEZO leo Mshauri Mwelekezi wa Elimu ya Uraia kwa Watu wenye Ulemavu Bw. Novat Rukwago amesema kuwa, licha ya jitihada mbalimbali ambazo walijaribu kuzifanya ili kuhakikisha viziwi kote nchini wanapata haki yao ya msingi na ya kikatiba ya kupiga kura bado ushiriki wao haukuridhisha.
 
Rukwago alizitaja changamoto mbalimbali zilizo jitokeza katika uchaguzi  huo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa wataalamu wa lugha za alama zinazotumiwa na viziwi katika kampeni mbalimbali za Vyama vya Siasa, hivyo sera na Ilani za vyama hivyo hazikuweza kujulikana kwa viziwi.
“Vyama vingi vilisema ni suala la rasilimali na ukosefu wa fedha za kuweka wataalamu hao, ingawa tuonavyo sisi ni kwamba walishindwa kutoa kipaumbele na si suala la fedha,” alisema Rukwago.
 
Aidha, Rukwago alisema CHAVITA kwa juhudi binafsi waliweza kutembea jumla ya mikoa 17 kote nchini na kufanikiwa kutoa elimu kwa baadhi ya viziwi ambapo jumla ya viziwi 2516 walijiandikisha, idadi hiyo ikiwa na wanaume 1256 na wanawake 1260. Waliopiga kura walikuwa ni 1807.
 
Aliongeza kwa kusema kuwa licha ya changamoto hizo pia mazingira ya kupigia kura hayakuwa rafiki kwa watu wenye uhitaji maalumu kwani hakukuwa na wataalamu wa lugha za alama  katika vituo vya kupigia kura.
 
Waliiomba Serikali kuzingatia umuhimu wa kuyapa kipaumbele makundi mbalimbali yenye uhitaji kwa chaguzi zijazo na kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya mawasiliano na vyama vya watu wenye uhitaji maalum mapema ili kuweza kushirikiana katika kuondoa changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi wa mwaka huu.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA TAMISEMI DAR

JAL1 
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI) , Jumanne Sajini baada ya kuwasili kwenye Ofisi ndogo ya TAMISEMI jijini Dar es salaam kuzungumza na watumishi Novemba 24, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JAL2 
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya Wakurugenzi baada ya kuwasili kwenye Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) jijini Dar es salaam kuzungumza na wafanyakazi Novemba 24, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JAL4 
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akizungumza na baadhi ya watumishi wa Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) jijini Dar es salaam Novemba 24, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JAL6 
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) jijini Dar es slaam baada ya kuzungumza nao Novemba 24, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

POP UP BONGO KUFANYIKA JUMAMOSI HII TRINITI OYSTERBAY DAR ES SALAAM

 
Nuya Essence
 
Founder of Branoz Collection Bahati Abraham with
customers
 
Secret Habits Seller servings customers
 
Pediah John, Founder of PSJ Brand with customers
copy
************************************************
Na Mwandishi Wetu
WASANII mbalimbali wa muziki na
maigizo pamoja na wadau wengine wa biashara watajumuika pamoja Triniti, Oyster
bay katika tamasha la biashara za bidhaa mbalimbali, Pop Up Bongo.
Tamasha hilo linalofanyika kila
baada ya miezi mitatu ni la siku moja na mwaka huu litafanyika tarehe 28 likiwa
chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Akizungumzia kuhusiana na tamasha
hilo mmoja kati ya waanzilishi wake, Natasha Stambuli alisema kuwa milango itafunguliwa
kuanzia saa mbili asubuhi na kuwa linatarajiwa kumalizika saa mbili usiku.
Alisema kuwa ikiwa ni kuelekea msimu
wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya tamasha hilo linawakutanisha watu
mbalimbali na wamiliki wa maduka na wafanyabiashara za aina mbalimbali.
Alikuwa inakuwa ni nafasi nzuri kwa
watu mbalimbali pia kukutana na mbali na kufanyika kwa biashara kwenye eneo
hilo lakini pia inakuwa ni fursa ya kuburudika kwa kuwa kutakuwa na muziki na
vinwaji hivyo kuongeza furaha kwa watakaojitokeza.
“Ni mwishoni mwa mwaka
tunaelekea na kama mnavyojua kunakuwa na mambo mbalimbali wakati tukielekea
kufunga mwaka vijana wanataka kujua wapi pa kununua bidhaa mbalimbali kama nguo
na vinginevyo na Pop Up bongo inawapatia fursa hiyo hapo Novemba 27″ alisema
Natasha.
Aliongeza kuwa “kwa mwaka huu
wasanii pia wapo ambao watafika kuonana nao wadau wengine wa bidhaa
zinazowahusu kama nguo na nyinginezo na hakuna kiingilio kabisa.
Alisema kuwa wafanyabiashara ambao
kwa mwaka huu wataonesha bidhaa zao ni pamoja na Secret Habits, KAYA African
Collection, Nuya’s Essence, HIGHSUPDSM, FT boutique, Branoz Collections, ATSU,
Dress Kitenge, American Nails na wengineo wengi.

Mbunge wa Chumbuni Mhe.Ussi Salum Pondeza HAMJAD Apokelea na Wapika Kura Wake

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe, Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kima taifa wa Abeid Amani Karume akitokea Dodoma kuhudhuria hafla ya kuapishwa iliofanyika wiki iliopita. 
Mhe Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akitabasamu wakati akiwasili uwanja wa ndege wa Zanzibar akitokea Bungeni Dodoma.na kupokelewa na Wananchi wa Jimbo lake. 
Mhe Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akipongezwa na Mke wakati alipofika kumpokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Dodoma kuhudhuria hafla ya kuapishwa wiki iliopita.
Mbunge wa Jimbo la VChumbuni Zanzibar akiwa na Mgombea Uwakilishi wa Jimbo hilo Miraji akimpongeza baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Bungeni Dodoma kuhudhuria hafla ya kuapishwa  iliofanyika wiki iliopita.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum AMJAD akisalimiana na wapiga kura wake waliofika uwanja wa ndege kumpokea baadha ya kuhudhuria hafla ya kuapishwa kuwa Mbunge wao. 
Wananchi wa Jimbo la Cumbuni Zanzibar wakimlaki Mbunge wao wakati akiwasili Zanzibar akitokea Dodoma kuhudhuria sherehe za kuapishwa zilizofanyika wiki iliopita Mjini Dodoma. 
Viongozi wa CCM Jimbo la Chumbuni wakimlaki Mbunge wao alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akitokea Dodoma kuhudhuria sherehe za kuapishwa zilizofanyika wiki iliopita Mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwa na Viongozi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar waliofika kumpokea uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar akitokea Mjini Dodoma kuhudhuria sherehe za kuapishwa wiki iliopita.
Imetayarishwa na OthmanMapara,Blogspot.
Zanzinews.com
Email othmanmaulid@gmail.com. 
 

RC KILIMANJARO,AMOSI MAKALA AKUTANA NA MAOFISA WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI KUZINGUMZIA JUU YA HOFU YA KIPINDUPINDU.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala akiwa katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi,kuzingumza na watendaji wa Afya na Mazingira.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala akifurahia jambo mara baada ya kukutana na watendaji wa Halmashauri kuzungumzia juu ya hofu ya Ugonjwa hatari wa Kipindupindu.kushoto kwake ni kaimu mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jeshi Lupembe. 
Baadhi ya watendaji.
Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Novatus Makunga akiwa na mmoja wa maofisa wakifuatilia maelelzo yaliyokuwa yakitolewa ofisini hapo.
 
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizungumzia changamoto iliyojitokeza hivi karibuni ya kujaa kwa dampo la kutupa taka hali iliyosababisha mrundikano wa takataka katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi,Hapa alikuwa akitoa agizo taizo hilo kushughulikiwa mara moja.
Baada ya agizo hilo mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga alifanya ziara katika dampo lilopo Kaloleni kujinea tatizo lililosabaisha magari ya kubeba taka kushindwa kuendelea na zoezi hilo.
Katapila likijaribu kusawazisha takataka katika eneo hilo la dampo ili kurahisisha utupwaji wa taka katika eneo hilo.
Wakati zoezi la kurekebisha barabara katika eneo la dampo likiendelea,mmoja wa wananchi kkatika eneo hilo alikuwa na shughuli ya kujiokotea vitu ambayo anadhani vitamsadia katika kujipatia kipato.

WANAFUNZI WA UTURUKI NA BOSNIA WAFANYA ZIARA KATIKA KISIWA CHA TUMBATU ZANZIBAR.

BO1 
Wanafunzi kutoka Uturuki na Bosnia wakiwa katika Boti kuelekea katika kisiwa cha Tumbatu kwa ajili ya kuwatembelea wanafunzi wa madrasa na wananchi mbalimbali katika ziara yao ya siku mbili ili kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
BO5 
Wanafunzi kutoka Uturuki na Bosnia wakipata dua kwa Mzee wa Kisiwa cha Tumbatu na kutoa msaada wa chakula ikiwa pamoja na Mchele Unga wa ngano,Sukari na Mafuta ya kupikia  katika ziara yao ya siku mbili ya kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.
BO6 
Kiongozi wa Wanafunzi Omar akimkabidhi Mzee wa kijiji cha Tumbatu Msaada wa Chakula katika ziara yao ya siku mbili ya kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.
BO2 
Wanafunzi kutoka Uturuki na Bosnia wakiwa katika Kisiwa cha Tumbatu kwa ajili ya kuwatembelea wanafunzi wa madrasa na wananchi mbalimbali katika ziara yao ya siku mbili ya kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.
BO3 
Wanafunzi kutoka Uturuki na Bosnia wakiwasalimia wanafunzi wa madrasa na walimu waliokuja kuwa pokea katika Kisiwa cha Tumbatu katika ziara yao ya siku mbili ya kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar
BO4 
Wanafunzi kutoka Uturuki na Bosnia wakiwa katika picha ya pamoja na  wanafunzi wa madrasa na walimu  katika Kisiwa cha Tumbatu katika ziara yao ya siku mbili ya kujenga urafiki baina yao na watu wa Zanzibar.

UNDP YAKABIDHI MRADI WA DOLA ZA MAREKANI 150,000 WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI KIJIJI CHA CHAMWINO

IMG_9773 
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo akikata utepe kuzindua Kisima cha maji safi na salama katika kijiji cha Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma mwishoni mwa juma lililopita.
Na Modewjiblog team, Chamwino
KIJIJI cha Manchali kilichopo wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, kimekabidhiwa mradi wa dola za Marekani 150,000 wenye lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mradi huo ulikabidhiwa kijiji hicho na Mratibu wa mashirika ya Umoja wa mataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodriguez.
Mradi huo umelenga kusaidia jamii inayoishi katika kijiji hicho kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mradi huo wa nishati ya jua umelenga kutatrua tatizo la nishati na kufanya matumizi bora ya ardhi na teknolojia ya maji.Mradi huo unasaidia familia 600.
Kwa uzoefu wa Tanzania na maeneo mengine duniani, familia maskini ndizo zinazopigika vibaya na mabadiliko hayo na ndio haizna uwezo wa kukabiliana nayo.
Kwa mradi huo wananchi wa Manchali wanatarajia kukabiliana vilivyo na mabadiliko ya Tabia nchi.
Akizungumza katika kijiji hicho cha Manchali, Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Bi. Awa Dabo alisema kwamba ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi uwezeshaji wananchi kiuchumi ni muhimu sana ili kufanya familia kustawi.
IMG_9772 
Kisima kilichozinduliwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo.
“Athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa watu maskini ni kubwa na ndio wanaoathirika zaidi” alisema Mkurugenzi Mkazi UNDP Bi. Dabo.
Aidha alisema kwamba anaishukuru serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuhangaikia suluhu ya watu kukubali kuwapo kwa mabadiliko ya tabia nchi na kufanya juhudi ya kukabili hali hiyo.
“Hii imo katika malengo ya maendeleo endelevu kwani malengo manne kati ya 17 yanahusiana na mabadiliko ya tabia nchi na kuhifadhi mazingira.kwa kutumia fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo, UNDP imefanikiwa kusaidia wananchi wa kijiji cha Manchali kufanyia kazi maeneo kadha muhimu ili kufanya uragibishi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, kuongeza kasi ya upoandaji wa miti na matumizi ya nishati jadidifu.” alisema.
Bi Dabo amesema kwamba mradi huo wa Manchali umekamilika ni mmoja wa mradi yenye mafanikio inayosimamiwa na UNDP.
Aliwapongeza wananchi wa Manchali kwa ushiriki wao na kuufanya mradi huo kuwa wakwao hali iliyosababisha kuwepo na matunda yenye tija katika kijiji hicho.
“Sisi UNDP kutokana na mafanikio haya tunaangalia maeneo mengine ya kufanya mradi kama huu” alisema Bi Dabo.
UZINDUZI-MRADI 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja waMataifa la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), kijijini humo.
Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez alisisitiza ushiriki wa wananchi katika kufaniukisha miradi na kusema kwamba mradi huo umefanikiwa kutoka na ushiriki wa wananchi na hasa kitendo chao cha kuufanya mradi huo kuwa mali yao.
Aliongeza kwamba kitendo cha kufanya mradi wao na kuwa viongozi wa maendeleo yao wao wenyewe kumefanya mradi uwe na tija kubwa kwao.
“Mradi huu umeleta maendeleo makubwa kwa wananchi wa hapa kutokana na wao kuanza kutumia nishati jadidifu, watoto wanakwenda shule na maeneo yameanza kurejewa na misitu.”
Mratibu huyo aliongeza kwamba mabadiliko ya tabia nchi ni ya kweli na wala si ya kuyafanyia mzaha, mashirika ya umoja wa mataifa na Umoja wenyewe wanatazama sana athari zake mbaya.
Alisema kijiji cha Manchali kimefanikiwa katika kuanza kukabili mabadiliko ya tabianchi kwa kubadili mambo yanayowazunguka na kurejesha uoto wa asili na kuacha kuharibu mazingira huku shughuli za maendeleo zikichukua sura mpya yenye kujali mabadiliko ya tabia nchi.
IMG_9802 
Bango la mradi uliozinduliwa na Bw. Alvaro Rodriguez.
IMG_9786 
Kutoka kushoto ni Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja waMataifa la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na viongozi wa kijiji wakiwakilisha wananchi ambao watanufaika na mradi huo.
IMG_9842 
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja waMataifa la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum katika picha ya pamoja.

BENKI YA STANDARD CHARTERED YATEUA MKURUGENZI WA KWANZA MTANZANIA

Sanjay - 3 
Sanjay Rughani (pichani) anakuwa Mtanzania wa kwanza kuiongoza benki ya Standard Chartered Tanzania akipokea uongozi wa benki hiyo kutoka kwa aliyekuwa mkurugenzi wake, Liz Lloyd, ambaye amerudi katika makao makuu ya benki hiyo, London, kuchukua nafasi ya Mshauri wa Kisheria wa benki hiyo.
Sanjay alijiunga na benki ya Standard Chartered Tanzania mwaka wa 1999 akiwa kama Meneja msaidizi wa kitengo cha Fedha. Baada ya miaka miwili Sanjay alipata cheo cha Meneja wa kitengo cha Fedha kwa Bara la Afrika, kazi ambayo aliifanya akiwa katika makao makuu ya benki hiyo, London. Alirudi nyumbani Tanzania mwaka wa 2002 na kupata cheo cha Mkuu wa Kitengo cha Fedha nchini Tanzania, kazi ambayo aliifanya hadi mwaka wa 2006.
Mwaka wa 2007, Sanjay alipata tena cheo kingine, wakati huu akihamishiwa Ghana, ambapo aliongoza Kitengo cha Fedha nchini humo huku pia akisimamia Afrika Magharibi, yaani Gambia, Cote d’ Ivoire na Sierra Leone, kazi ambayo aliifanya hadi Mei, 2013.
Juni, 2013 Sanjay alipandishwa tena cheo na kuwa Mkuu wa Operesheni za Kifedha na Mratibu wa Huduma za Kifedha kwa Bara la Afrika akiongoza kitengo hicho ambacho ni sehemu ya Kitengo Kikuu cha Fedha katika nchi kumi na tan

No comments:

Post a Comment