Wabunge
Mhe. Anna Abdalla (kushoto) na Mhe. Ester Bulaya wakiaga mwili wa
marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye viwanja
vya bunge leo mjini Dodoma.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa (kulia)
akizungumza jambo na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu kwenye
viwanja vya bunge leo mjini Dodoma wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa
marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa.
Mbunge
wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu (kulia) akizungumza jambo na
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai
leo mjini Dodoma kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen
Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni
waliofika kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa
aliyekuwa mbunge wa Ukonga iliyofanyika leo katika viwanja vya bunge
mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wabunge Wanawake Mhe. Anna Abdallah akimfariji mume wa
marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa mbunge wa Ukonga aliyefariki usiku wa
kuamkia Juni 2 nyumbani kwake mjini Dodoma.
Waheshimiwa
Wabunge na baadhi ya watu mbalimbali waliofika kwenye viwanja vya bunge
leo mjini Dodoma kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen
Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga.
Mwili
wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga ukiwasili
kwenye viwanja vya bunge leo mjini Dodoma kwa ajili ya kuagwa.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai
akitoa salam za bunge kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe.
Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga iliyofanyika leo katika
viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Mchungaji
Mshana Samweli wa KKKT Jimbo la Dodoma akitoa neno kwenye shughuli ya
kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa leo mjini Dodoma.
Baadhi
ya Wabunge wakiwa kwenye hali ya majonzi mara baada ya kuwasili kwa
mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye
viwanja vya bunge mjini Dodoma leo.
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Martha Mlata akiimba kwa hisia wimbo wa
maombolezo kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen
Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga iliyofanyika leo katika viwanja vya
bunge mjini Dodoma.
Baadhi ya
wabunge wakitoa pole kwa wanafamilia wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa
aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye viwanja vya bunge leo mjini Dodoma.PICHA ZOTE NA FATMA SALUM – MAELEZO
No comments:
Post a Comment