Pages

Friday, June 5, 2015

Thamani ya mfuko wa NSSF yapanda kufikia sh trilion 2.76




Tathimini inaonesha mfuko utakuwa imara bila kuteteleka kwa muda wa miaka 50 ijayo.

 
Mkurugenzi wa fedha wa NSSF ndugu Ludovick Mrosso  alipokuwa Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mfuko akitoa maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni linalojengwa na NSSF kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa waziri wa ujenzi na miundo mbinu Mh.Dakt John Pombe Makufuli

Christian Gaya Arusha Alhamis Juni 4, 2015
Mkurugenzi wa fedha wa NSSF ndugu Ludovick Mrosso alisema ya kuwa thamani ya mfuko iliongezeka na kufikia shilingi milioni 2,759,555 mpaka mwezi Juni 2014 ukilinganisha na shilingi milioni 2,551,227 kutoka mwezi Juni 2013, sawa na ongezeko la shilingi 208,328 likiwa sawa na ongezeko la asilimia 8.17 kwa mwaka.


Alitaja ya kuwa vitega uchumi viliongezeka kutoka shilingi milioni 2,295,251 za kitanzania  kwa mwaka wa fedha 2012/2013 mpaka kufikia shilingi milioni 2,403.606 kwa mwaka wa fedha 2013/2014. Hii ikiwa sawa na ongezeko la asilimia la shilingi milioni 108,355 ambapo ni sawa na asilimia 4.72 ukilinganisha na mwaka 2012/2013. 

“Aidha lengo lilikuwa kufikia vitega uchumi vyenye thamani ya shilingi 2,484,533, hivyo lengo lilifikiwa kwa asilimia 96.70” Mrosso  aliyasema haya siku ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa wadau uliofanyika ndani ya ukumbi wa Simba Hall Arusha ulioanza tarehe 2-4 June, 2015

Alisema kwa ujumla kumekuwepo na ongezeko la uwekezaji kwenye nyanja mbalimbali isipokuwa kwenye dhamana za serikali, amana za mabenki ambazo zinaonesha kupungua. upungufu mkubwa katika amana za mabenki umetokana na amana zilizowekezwa mwaka uliopita kuiva ndani ya mwaka huu, na kuwa mwaka huu uwekezaji ulifanyika kidogo katika amana za kibenki kutokana na mahitaji makubwa ya fedha kwa ajili uwekezaji wa fedha vya muda mrefu

Akizungumzia rasilimali zingine Mroso alisema ziliongezeka kutoka shilingi milioni 255, 976 kwa mwaka 2013 na kufikia shilingi milioni 355,949 kwa mwaka 2014 ongezeko likiwa ni asilimia 39.06 wakati kwa upande wa rasilimali halisi ziliongezeka kutoka milioni 2,378,068 toka Juni 2013 na kufikia milioni 2,582,921 mwezi Juni 2014 likiwa sawa na ongezeko la shilingi milioni 204, 853 sawa na asilimia 8.61

“Pato kutokana na vitega uchumi kwa mwaka  2013/2014 lilifikia shilingi milioni 222.160 ukilinganisha na shilingi milioni 252.547 kwa mwaka 2012/2013 na pungufu ukiwa ni sawa na asilimia 12.03. aidha kulikuwa na ongezeko la thamani ya hisa za kampuni zilizosajiriwa katika soko la hisa la Dar es Salaam kwa kiasi cha shilingi milioni 29.490” mkurugenzi wa fedha alifafanua.

Akifafanua juu ya ukusanyaji wa michango Mrosso alisema ya kuwa mpaka kufikia mwaka 2013/2014 mfuko uliweza kukusanya shilingi milioni 548.472 ukilinganisha na shilingi milioni 476.107 mwaka 2012/2013. ongezeko hili lilikuwa sawa shilingi milioni 72.365 sawa na asilimia 15.20.  Wakati kwaupande wa mafao alisema ya kuwa  kwa mwaka 2013/2014  mfuko uliweza kulipa wanachama  kiasi cha milioni 344,787 ukilinganisha na shilingi milioni 228.049 mwaka 2012/2013, ongezeko likiwa ni shilingi milioni 116,738 sawa na asilimia 51.19

Kwa upande wa hali ya ukwasi na thamani ya mfuko wa NSSF mkurugenzi aliwaambia wadau ya kuwa hali ya ukwasi kwa ujumla kwa mwaka 2013/2014 ilikuwa nzuri kwa sababu mpaka ilipofikia tarehe 30 Juni 2014 shirika ilikuwa na shilingi milioni 59,890. Tathimini ya uimara (solvency) wa mfuko ilifanywa na bwana George Langi’s wa Canada kwa kipindi kilichoishia tarehe 30.06.2009 na inaonesha mfuko utakuwa imara bila kuteteleka kwa muda wa miaka 50 ijayo. Pia tathimini iliyofanywa na kampuni ya Genesis Solution ya Africa kusini inaonesha ya kuwa rasilimali kwa ajili ya kulipa mafao ni asilimia 75.5 na kwa wanachama kuendelea kuchangia asilimia 20 ya mshahara na hivyo mfuko uko imara kabisa kwa miaka mingi ijayo alisisitiza.

No comments:

Post a Comment