Dr Ramadhani Dau Mkurugenzi Mkuu wa NSSF
Christian Gaya Majira Jumamosi Juni 06, 2015
Kuanza
mwaka ujao wa fedha shirika la taifa la hifadhi ya jamii litaanza kutoa mikopo
kwa wanachama wake kupitia kwa waajiri wake. haya yalisemwa na mkurugenzi wa
uwekezaji na miradi ndugu Yacoub Kidula
wakati akiwasilisha mada yake juu ya hifadhi ya jamii na ujasiriamali katika
mkutano mkuu wa wadau uliofanyika Ukumbi wa Simba Hall AICC-Arusha
ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.
Mizengo Kayanza Peter Pinda. Kidula alisema mpaka sasa NSSF
imetoa mikopo ya riba nafuu kwa wanachama wake ambao wengi wao ni wajasiriamali
ipatayo thamani ya shiilingi bilioni 55.6 za kitanzania kwa wanachama wapatao
6,920 kwa kupitia SACCOS 159, AMCOS 11na MFIs 2
.
Haya
yalifafanuliwa zaidi na mkurugenzi mkuu wa NSSF Dakt Ramadhani Dau wakati alipokuwa
akitoa risala yake kwa wanachama na
wadau mbalimbali waliohudhuria wapatao
zaidi ya 1000 katika mkutano huo mkuu wa 2015 ya kwamba mikopo inayotolewa NSSF
kwa ajili ya ujasiamali ni ya masharti nafuu sana, muda mrefu wa marejesho na
riba za chini kabisa ukilinganisha na hali ya soko.
“Muda
wa marejesho ya mikopo hii ni kati ya miaka miwili na mitano wakati riba ni
kati ya asilimia 9.32 na 10.68 kwa mwaka ukilinganisha na viwango vya riba
sokoni vya kati ya asilimia 15 had 30” alisema Dakt Dau
“
Kwa sasa tumeamua kutoa mikopo ya riba nafuu kwa wanachama wetu kupitia waajiri
wao ili kuwafikia wengi zaidi kuliko kupitishia kwenye SACCOS ambapo wengi wa wanachama
sio wanachama wa SACCOS na hivyo kuwarahisishia wa kupata mikopo kwa muda mfupi
zaidi, kujenga mshikamano zaidi sehemu za kazi, na kuwasaidia waajiri kuongeza
uzalishaji wenye tija zaidi, kuwapunguzia ukali wa maisha wanachama na hivyo
kupunguza umasikini kama sio kuondoa kabisa, ili mradi mwajiri akubali kutoa
dhamana kwa kila mwanachama atakayehitaji kupata mkopo kutoka NSSF”alisema
Kidula.
Kuhusu
masharti ya mwanachama kupata mkopo Yacoub alisema mwajiri anatakiwa kuwa
mchangiaji hai wa muda wa miaka mitatu (3) na kwa upande wa mwanachama atatakiwa
awe mchangiaji hai wa mfuko wa NSSF kwa muda wa miezi sita ( 6)
Alisema
kuanzia mwaka ujao wa fedha watatumia mawakala mbalimbali watakaotumika
kuwaandikisha wanachama kutoka katika sekta isiyo rasmi na walioko ughaibuni
yaani diaspora
Naye Bibi Delifina Masika
ambaye ni meneja mkuu wa mkoa wa Arusha alisema wakati alipokuwa akisoma
taarifa juu ya NSSF mfuko bora kwa hifadhi ya jamii Tanzania ya kuwa ukubwa na
idadi wa wanachama wa NSSF katika soko la sekta ya hifadhi ya jamii kulingana
na utafiti uliofanywa hivi karibuni inaonesha ya kuwa mpaka sasa NSSF inachukua
asilimia 53 wakati mifuko mingine inagawana asilimia 47 zilizobaki
“Kima cha chini cha
pensheni kwa wastaafu wa NSSF ni shilingi 80,000/- kwa mwezi wakati kima cha
juu cha pensheni kwa wastaafu wa NSSF ni shilingi milioni 10,685,000/- hivyo shirika
lina uwezo wa kujiendesha na kulipa mafao kwa wanachama wake kwa miaka saba (7)
bila kukusanya michango hivyo basi NSSF ni Shirika IMARA kwani mpaka kuishia
Juni 2014 mfuko ulikuwa na thamani ya shilingi trilioni 2.6 na kufikia mpaka
Juni 2015 mfuko unakadiriwa kuwa na thamani ya shilingi trilioni 3” Masika alifafanua.
Mwisho
No comments:
Post a Comment