Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akifungua mkutano wa tano wa wadau wa Mfuko wa
Hifadhi za Jamii wa NSSF kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha
Arusha (AICC), Juni 2, 2015. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Felix Tibenda, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF ,Dr. Ramadhani Dau na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF Abubakari Rajab. (Picha na Ofisi
ya Wziri Mkuu).
Na
Queen Lema na Christian Gaya ARUSHA
MFUKO
wa hifadhi ya taifa ya jamii(NSSF)umefanikiwa kutoa kiasi cha Bilioni 55.6 kwa
wajasiriamali mbalimbali ambapo pia fedha hizo zimeweza kuwanufaisha wajasiriamali 7000
kutoka sehemu mbalimbali nchini.
hata
hivyo riba hiyo ilikuwa kati ya asilimia 9.3 hadi kufikia 10.7 ambapo kwa
taasisi nyingine za kifedha hufikia riba ya asilimia 15 mpaka 30 hali ambayo
nayo inachangia sana kuwadidimiza wajasiriamiali ambao wanategemea mikopo.
Akiongea
katika mkutano mkuu wa tano wa mwaka ambao uliwajumuisha wadau na wanachama wa
NSSF mkurugenzi mtendaji Dakt Ramadhani Dau alisema kuwa mikopo hiyo kwa
wajasiriamali ilitolewa kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita na mpaka sasa
wameshaweza kuwanufaisha wajasirimali wengi hapa nchini.
Dkt
Dau alifafanua kuwa kilichofanya mfuko huo kuweza kutoa mikopo kwa
wajasiriamali ni baada ya kuona kuwa kuna changamoto mbalimbali ambazo
zinawakabili wajasimali na kutokana na changamoto hizo zimesababisha washindwe
kufikia malengo yao mbalimbali.
Alidai
kuwa kwa sasa changamoto mojawapo ambayo inawakabili wajasiriamali hao ni
pamoja na ukosefu na upatikaji wa mitaji, kutokuwa na dhamana, kutozwa riba
kubwa, ukosefu wa elimu za biashara
pamoja na nidhamu na kudhubuti kuanza kufanya biashara hali ambayo kama
wajasiriamali wa sasa wataweza kutatuliwa hayo basi wataweza kufikia malengo
makubwa
Awali
akiongea kwa niaba ya serikali Waziri mkuu Mizengo Pinda alisema kuwa mfuko huo
wa NSSF umeweza kuwabeba wajasiriamali sana ingawaje pia mifuko ya hifadhi ya
jamii inahusika sana kuweza kulibeba taifa la Tanzania hasa kwenye sekta muhimu
hususani sekta ya ujasiriamali
“Kazi
iliyofanywa na NSSF tangia mwaka 1997 mpaka 2012 mpaka sasa ni kubwa sana na ya tija ambapo
imekuwa ni mchango mkubwa sana kwa uchumi wa taifa letu. nampokengeza sana Dakt
Ramadhani Dau kwani kwa kipindi chake NSSF imepata maendeleo makubwa sana na
mpaka sasa NSSF wamepata tuzo ya kimataifa ISO kwa kutoa huduma bora kwa
wanachama wake”.alisema Pinda
Pinda
alifafanua kuwa kwa pamoja na kuwa NSSF imeweza kuwasaidia wajasiriamali kwa
kiwango cha juu lakini bado kuna changamoto kuwa sekta ya ujasiriamali ni sekta
ya watu ambao wapo ovyo sana jambo ambalo halina ukweli kabisa.
“napenda
kuwasihi hata watumishi wa umma kuwa wasiridhike na kisha kuona ujasirimali ni
watu wa chini jiwekezeni hata huku acheni kunata na kama watu wote tutakuwa
wajasiriamali ni wazi kuwa wakati tutakapostaafu hatutaweza kupata
shida”aliongeza
No comments:
Post a Comment